Kikwete apokea Ripoti ya EPA ajiandaa kuhutubia Taifa!

Kikwete apokea Ripoti ya EPA ajiandaa kuhutubia Taifa!

...10. Maslahi ya wafanyakazi. Uliunda kamati kupitia maslahi ya wanafanyakazi. Mbona hatuoni mabadiliko?

11. Usalama wa chakula? Tueleze hatua gani unachukua tofauti na mkapa na waliokutangulia wengine. Si unajua chakula kitazidi kuwa haba duniani. Hivi hatuna uwezo wa kutoa trekta moja kila kata kwa kuanzia kama siyo kijiji chenye ardhi na hali ya hewa safi. Hatuoni kuwa kilimo kinaweza kutuokoa?

12. Bidhaa feki: vipi serikali imelala au?Mbona bidhaa feki zitatumaliza. Tueleze kwa nini zipo na hatua gani umechukua kama kiongozi wa nchi?

Hiyo ndo dazeni ya issues zangu ambazo ukizitolea maelezo kwa ufasaha wananchi tutakupa 5. Otherwise hotuba ikiwa kama ya mwisho wa mwezi uliopita utatuacha midomo wazi.
Nawasilisha ili wana Jf muongezee na hatimaye salva rweyemamu amfikishie ujumbe mh. Rais

Brilliant!! hili li-talii Kikwete lina kazi kweli!!?

13:Katiba: Bila kuzungumzia katiba utakuwa usanii tu maana suala la Zanzibar na mgombea binafsi yanahusishwa na katiba

14: Safari za nje zimegharimu kiasi gani? Aeleze ni masaa mangapi aliyokwisha travel so far, then azidishe mara $ 5000 (gharama ya Jet kuwa angani kwa lisaa limoja) = mabilioni mangapi ya walalahoi amepoteza kwa utalii wake wa kijinga?
 
Tatizo ninaloliona hapa ni watu kumu underrate Jakaya.Hivi kweli mnadhani hajui afanye nini kuhusu EPA?subirini.

Kama angekuwa anajua angeshachukua hatua toka mwaka jana.inawezekana bado anajifanya hajui.

mie nilishakubali yaishe siku nyingi na ndiyo maana sipendi watu waendelee kupiga domo,inabidi wajipange zaidi ili kuondoa watu wanaopenda kupiga domo bila kuchukua hatua
 
naamini kwamba uvumilivu wa wa-tz tunaouhubiri au hubiriwa utatakiwa uwe na mpaka,
hii ni big challenge kwa mheshimiwa kuona kwamba kila mpiga kura wake aliyekamilisha ile 80% na kutimiza kiu yake, basi ni vyema kwa imani hiyo naye i reflect back kwa kutuondolea kero hizo,ukianzia na hilo la EPA,Richmond,Nchi ndani ya nchi,malimbikizo ya ma-staffs na mengineyo. 2010 inaweza ikawa ni option tena kwake kama muda mrefu kwa wa-tz ku- suffer then at the end ndio actions against kero ndio zinaonyeshwa kutekelezwa. kwa kweli wa-tz wa leo sio wale wa kupiga vigelegele katika hotuba za wakubwa hata pasipo na points.alhamis tunaamini ndio speech italenga.
 
Tatizo ninaloliona hapa ni watu kumu underrate Jakaya.Hivi kweli mnadhani hajui afanye nini kuhusu EPA?subirini.

Mpaka hapo atakavyofanya hivyo anavyojua afanye. Lakini kwa sasa ukweli ndio huo.
 
Nadhani sasa hivi hana ujanja isipokuwa kuchukua hatua kwa sababu gia ya kwanza ya "
Ripoti ya EPA" tumeichomoa mapema na tumeshamwambia Rais wetu kuwa hiyo haingii aje na nyingine. Anachoweza kufanya ni kusimama kuongoza.

a. Wakati Rais anazungumza na kuelezea hatua zilizochukuliwa kuhusu EPA vikosi vya Polisi vitakuwa kwenye nyumba na maofisa watakaotajwa na watu kutiwa mbaroni kufikishwa mahakamani. Miongoni mwao ni Mramba na Yona

b. Kiwira itatangazwa kurudishwa serikali baadaya kuwepo "irregularities" katika mchakato wa upatikanaji wote.

c. Rais atakubali kujiuzulu kwa Mwanyika kama Mwanasheria Mkuu na atatumia nafasi hiyo kutangaja jina la Mwanasheria Mkuu mpya ambaye ataapishwa pia kama Mbunge. Edward Hosea kuondolewa kutoka nafasi yake ya sasa na kuhamishiwa idara nyingine (kusubiri kupangiwa kazi nyingine).

Kimsingi, my instincts zinanilazimisha kuamini kuwa Kikwete atakachofanya ni kwenda to the other extreme ambayo itakuwa ni Over Kill. Ile Ijumaa na mwishoni mwa Jumaa kutakuwa na shamrashamra za watu kufurahia "Kikwete afanya Kweli".

Lakini kubwa zaidi atakalofanya ambalo naamini linaweza kuwa na alama kubwa zaidi ya Urais wake ni suala la Zanzibar kujitangaza kuwa ni nchi nje ya Jamhuri ya Muungano. Nimeandika kwa kirefu kwenye gazeti moja la Jumatano na nitaandika pia kwenye jingine kufafanua uzito wa hili. Katika kushughulikia hili, Watakuwa wamepitia hukumu ya Mahakama ya Rufaa na kujua tatizo lilipo na hivyo sitoshangaa kabisa kama Rais Kikwete atafanya kile ambacho kingefanywa miaka mingi iliyopita, nayo ni kuanzisha Mjadala wa Katiba ili mara moja na daima kuondoa kasoro za Muungano.

Nje ya hapa; I dare say itakuwa ni kuundwa kwa Kamati nyingine kushughulikia jambo jingine.
 
Kikwete atakachofanya ni kwenda to the other extreme ambayo itakuwa ni Over Kill. Ile Ijumaa na mwishoni mwa Jumaa kutakuwa na shamrashamra za watu kufurahia "Kikwete afanya Kweli".

Unanilazimisha nikuamini hapo.....ila siku zote wewe ukiongea kitu lazima kitatokea tu kwa hili nakwamini mkuu ngoja tuvute subira tuone Mungwana atakacho amua.
 
Nadhani sasa hivi hana ujanja isipokuwa kuchukua hatua kwa sababu gia ya kwanza ya "
Ripoti ya EPA" tumeichomoa mapema na tumeshamwambia Rais wetu kuwa hiyo haingii aje na nyingine. Anachoweza kufanya ni kusimama kuongoza.

a. Wakati Rais anazungumza na kuelezea hatua zilizochukuliwa kuhusu EPA vikosi vya Polisi vitakuwa kwenye nyumba na maofisa watakaotajwa na watu kutiwa mbaroni kufikishwa mahakamani. Miongoni mwao ni Mramba na Yona

b. Kiwira itatangazwa kurudishwa serikali baadaya kuwepo "irregularities" katika mchakato wa upatikanaji wote.

c. Rais atakubali kujiuzulu kwa Mwanyika kama Mwanasheria Mkuu na atatumia nafasi hiyo kutangaja jina la Mwanasheria Mkuu mpya ambaye ataapishwa pia kama Mbunge. Edward Hosea kuondolewa kutoka nafasi yake ya sasa na kuhamishiwa idara nyingine (kusubiri kupangiwa kazi nyingine).

Kimsingi, my instincts zinanilazimisha kuamini kuwa Kikwete atakachofanya ni kwenda to the other extreme ambayo itakuwa ni Over Kill. Ile Ijumaa na mwishoni mwa Jumaa kutakuwa na shamrashamra za watu kufurahia "Kikwete afanya Kweli".

Lakini kubwa zaidi atakalofanya ambalo naamini linaweza kuwa na alama kubwa zaidi ya Urais wake ni suala la Zanzibar kujitangaza kuwa ni nchi nje ya Jamhuri ya Muungano. Nimeandika kwa kirefu kwenye gazeti moja la Jumatano na nitaandika pia kwenye jingine kufafanua uzito wa hili. Katika kushughulikia hili, Watakuwa wamepitia hukumu ya Mahakama ya Rufaa na kujua tatizo lilipo na hivyo sitoshangaa kabisa kama Rais Kikwete atafanya kile ambacho kingefanywa miaka mingi iliyopita, nayo ni kuanzisha Mjadala wa Katiba ili mara moja na daima kuondoa kasoro za Muungano.

Nje ya hapa; I dare say itakuwa ni kuundwa kwa Kamati nyingine kushughulikia jambo jingine.

Habari za uhakika ni kwamba taarifa hiyo imekabidhiwa bila ya kuwapo waandishi wa habari leo hii IKULU, kutokana na Rais kukabiliwa na majukumu mengine muhimu ndipo akalazimika kupokea kwa haraka taarifa hiyo bila kuwapo waandishi.
 
Nadhani sasa hivi hana ujanja isipokuwa kuchukua hatua kwa sababu gia ya kwanza ya "
Ripoti ya EPA" tumeichomoa mapema na tumeshamwambia Rais wetu kuwa hiyo haingii aje na nyingine. Anachoweza kufanya ni kusimama kuongoza.

a. Wakati Rais anazungumza na kuelezea hatua zilizochukuliwa kuhusu EPA vikosi vya Polisi vitakuwa kwenye nyumba na maofisa watakaotajwa na watu kutiwa mbaroni kufikishwa mahakamani. Miongoni mwao ni Mramba na Yona

b. Kiwira itatangazwa kurudishwa serikali baadaya kuwepo "irregularities" katika mchakato wa upatikanaji wote.

c. Rais atakubali kujiuzulu kwa Mwanyika kama Mwanasheria Mkuu na atatumia nafasi hiyo kutangaja jina la Mwanasheria Mkuu mpya ambaye ataapishwa pia kama Mbunge. Edward Hosea kuondolewa kutoka nafasi yake ya sasa na kuhamishiwa idara nyingine (kusubiri kupangiwa kazi nyingine).

Kimsingi, my instincts zinanilazimisha kuamini kuwa Kikwete atakachofanya ni kwenda to the other extreme ambayo itakuwa ni Over Kill. Ile Ijumaa na mwishoni mwa Jumaa kutakuwa na shamrashamra za watu kufurahia "Kikwete afanya Kweli".

Lakini kubwa zaidi atakalofanya ambalo naamini linaweza kuwa na alama kubwa zaidi ya Urais wake ni suala la Zanzibar kujitangaza kuwa ni nchi nje ya Jamhuri ya Muungano. Nimeandika kwa kirefu kwenye gazeti moja la Jumatano na nitaandika pia kwenye jingine kufafanua uzito wa hili. Katika kushughulikia hili, Watakuwa wamepitia hukumu ya Mahakama ya Rufaa na kujua tatizo lilipo na hivyo sitoshangaa kabisa kama Rais Kikwete atafanya kile ambacho kingefanywa miaka mingi iliyopita, nayo ni kuanzisha Mjadala wa Katiba ili mara moja na daima kuondoa kasoro za Muungano.

Nje ya hapa; I dare say itakuwa ni kuundwa kwa Kamati nyingine kushughulikia jambo jingine.

Mkuu Mwanakijiji,

1.Mmoja wa maafisa wa Muda Mrefu wa UWT hasa kitengo cha inteligensia,Dr. Hoseah atastaafu hivi karibuni na kama sikosei mwisho wa kufanya kazi utakuwa mwezi huu,ikiwa Mkuu atamstaafisha mapema itakuwa kichekesho,hivyo speculation zako bado hazinipi ukweli.

2.Katika watu waliobaki na makini katika sheria na wanasimamia sheri kwa dhati ni Mwanyika,JK hana Ubavu wa kumuondoa kwa sasa ila anweza kumbadilisha kama akitaka kwa matakwa yake na siyo kwasababu ya EPA.Unless if you are talking about the former State Attonery(Chenge).

3.Kuna jambo moja ambalo ni vigumu kulikubali hasa kwa hao,ila Mafisadi walishashinda vita hii dhidi yao na hata Mkuu kuna wakati flani alisema Nchi imetulia.Ugomvi wa CHADEMA na Marehemu wangwe uliwasaidia sana na dniyo mtaji wa kisiasa wa CCM kwa sasa.hapa ndipo wapinzani walipoanza kukosea.

4.Kwa uzoefu wangu katika hili,kitakachofanyiaka ni kubadili sheria ya maadili ya uongozi na kuongeza baadhi ya vipengele katika Sheria ya Fedha.imeshaonekana kuwawajabisha wezi wa pesa za EPA imekuwa ngumu sana sababu hakuna ushahidi wa kutosha kuwawajibisha moja kwa moja(Je serikali iko tayari kulipa kama wakishindwa kesi ikiwa?)
 
Nadhani sasa hivi hana ujanja isipokuwa kuchukua hatua kwa sababu gia ya kwanza ya "
Ripoti ya EPA" tumeichomoa mapema na tumeshamwambia Rais wetu kuwa hiyo haingii aje na nyingine. Anachoweza kufanya ni kusimama kuongoza.

a. Wakati Rais anazungumza na kuelezea hatua zilizochukuliwa kuhusu EPA vikosi vya Polisi vitakuwa kwenye nyumba na maofisa watakaotajwa na watu kutiwa mbaroni kufikishwa mahakamani. Miongoni mwao ni Mramba na Yona

b. Kiwira itatangazwa kurudishwa serikali baadaya kuwepo "irregularities" katika mchakato wa upatikanaji wote.

c. Rais atakubali kujiuzulu kwa Mwanyika kama Mwanasheria Mkuu na atatumia nafasi hiyo kutangaja jina la Mwanasheria Mkuu mpya ambaye ataapishwa pia kama Mbunge. Edward Hosea kuondolewa kutoka nafasi yake ya sasa na kuhamishiwa idara nyingine (kusubiri kupangiwa kazi nyingine).

Kimsingi, my instincts zinanilazimisha kuamini kuwa Kikwete atakachofanya ni kwenda to the other extreme ambayo itakuwa ni Over Kill. Ile Ijumaa na mwishoni mwa Jumaa kutakuwa na shamrashamra za watu kufurahia "Kikwete afanya Kweli".

Lakini kubwa zaidi atakalofanya ambalo naamini linaweza kuwa na alama kubwa zaidi ya Urais wake ni suala la Zanzibar kujitangaza kuwa ni nchi nje ya Jamhuri ya Muungano. Nimeandika kwa kirefu kwenye gazeti moja la Jumatano na nitaandika pia kwenye jingine kufafanua uzito wa hili. Katika kushughulikia hili, Watakuwa wamepitia hukumu ya Mahakama ya Rufaa na kujua tatizo lilipo na hivyo sitoshangaa kabisa kama Rais Kikwete atafanya kile ambacho kingefanywa miaka mingi iliyopita, nayo ni kuanzisha Mjadala wa Katiba ili mara moja na daima kuondoa kasoro za Muungano.

Nje ya hapa; I dare say itakuwa ni kuundwa kwa Kamati nyingine kushughulikia jambo jingine.

Muungwana hapa atakuwa amecheza karata ya ushindi kama itakuwa kweli mbona watu watashangilia lakini naombea yote hayo yaje na unafuu wa maisha(umeme bei ipungue zile hela za kulipia capacity charge,kodi ya mafuta na bei ya vyakula iwe nafuu) lakini kama ni maneno tuuuu itakuwa from hero to zero au unasemaje Mkjj
 
Nimeandika kwa kirefu kwenye gazeti moja la Jumatano na nitaandika pia kwenye jingine kufafanua uzito wa hili.

Nakumbuka mkuu ulisema utapumnzika kuandika magazetini ili upate muda wa kutafuta mkate wa kila siku.Vp tena mikate imesha patikana kwa wingi?Lakini baadhi yetu tulikusihi usikache tukaomba mchango wako....kama hivi jtano utatoa ujumbe.
 
Tayari Rais amekwisha kukabidhiwa taarifa.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo (Jumatatu, Agosti 18, 2008) amepokea rasmi ripoti ya uchunguzi wa upotevu wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (External Payments Accounts - EPA) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Kikwete amekabidhiwa ripoti hiyo na Mwenyekiti wa Timu iliyokuwa inafanya uchunguzi huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson P.M. Mwanyika.

Mwanasheria Mkuu huyo alifuatana na wajumbe wengine wa Timu hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Edward Hosea.

Rais amewashukuru na kuwapongeza wajumbe wa Timu hiyo kwa kazi kubwa na ngumu lakini nzuri.

Rais, baada ya kuwa ameisoma na kuitafakari ripoti hiyo, ataitolea maamuzi katika siku chache zijazo, na taarifa rasmi ya maamuzi hayo ya Rais itatolewa kwa wananchi.

Timu hiyo iliundwa na Rais Kikwete Januari 9, mwaka huu, 2008 katika tangazo rasmi lililotolewa kwa waandishi wa habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.

Wakati anaunda Timu hiyo, Rais aliipa muda wa miezi sita kukamilisha kazi yake, ambayo ilikuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.

Rais aliunda Timu hiyo baada ya kuwa amepitia Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Mwaka wa Fedha 2005/06 za EPA katika Benki Kuu Tanzania (BOT), uliofanywa na Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young, kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Kampuni hiyo ya Ernst and Young iliombwa na Serikali kuifanya kazi hiyo. Iliianza Septemba, 2007 na kumalizika Desemba, mwaka huo huo, 2007.

Rais Kikwete alikabidhiwa Taarifa hiyo Januari 7, mwaka huu, 2008 na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Siku ya tatu, baada ya kuwa ameisoma na kuifanyia kazi, Rais aliitolea maamuzi Taarifa hiyo, ikiwa ni pamoja na kuunda Timu ya Mwanyika.

Imetolewa na

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

18 Agosti, 2008
 
Watanzania vumulieni shida.....Mungu yupo
 
Miye kwa kweli mwenzenu sipendi kuzugwa: Angalia:

NB: Kiini cha ripoti hiyo ni wazi kiko kwenye kurudisha fedha badala ya hatua za kisheria kuchukuliwa. Sielewi kwanini Ikulu wamesisita hizo bila kutaja agizo la Rais la kuwachukulia hatua watu na makampuni yaliyohusika. Hivyo mtaambiwa fedha iliyorudishwa ambayo imekaribiana na kiasi kikubwa cha kilichoibwa na wote mtatakiwa kupiga makofi.
 
.....Rais amewashukuru na kuwapongeza wajumbe wa Timu hiyo kwa kazi kubwa na ngumu lakini nzuri.....

Kumbe zile hadidu za rejea zilikuwa ndo zilivyokuwa! Kumbe alitaka ripoti ya uchunguzi siyo hatua dhidi ya wezi.
 
Kama huyu Rais amekubali kupokea 'Ripoti' ambayo hakuagiza basi hutuna Rais. Kwa kumfanya yeye kuwa ni bwege kiasi hicho basi wanaondesha nchi ni watu wengine kabisa.
 
Miye kwa kweli mwenzenu sipendi kuzugwa: Angalia:

NB: Kiini cha ripoti hiyo ni wazi kiko kwenye kurudisha fedha badala ya hatua za kisheria kuchukuliwa. Sielewi kwanini Ikulu wamesisita hizo bila kutaja agizo la Rais la kuwachukulia hatua watu na makampuni yaliyohusika. Hivyo mtaambiwa fedha iliyorudishwa ambayo imekaribiana na kiasi kikubwa cha kilichoibwa na wote mtatakiwa kupiga makofi.

Post dated cheque with no money in the account
 
Mkjj, Hebu tujikumbushe. Mbona wameruka kipengele cha kuchukua hatua? wamekipa umuhimu cha kurudisha fedha? suala la kurudisha fedha lilikuwa ni suala la mwisho na si la kwanza.

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI WA HESABU KATIKA AKAUNTI YA MALIPO YA MADENI YA NJE (EXTERNAL PAYMENT ARREARS ACCOUNT – EPA) ILIYOKO BENKI KUU YA TANZANIA

Nafurahi kuwaarifu kuwa, kazi ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka wa fedha 2005/06 za Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje yaani External Payment Arrears (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania imekamilika. Kazi hiyo ilifanywa na Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Ilianza Septemba, 2007 na kukamilika Desemba, 2007. Juzi tarehe 07 Januari, 2008 Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikabidhiwa Taarifa hiyo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Rais ameisoma, ameifanyia kazi na kuitolea maamuzi.

Historia ya EPA

Katika miaka ya 1970 mpaka 1990 nchi yetu ilikuwa inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa fedha za kigeni. Benki Kuu ya Tanzania ilipewa jukumu la kusimamia matumizi ya fedha za kigeni kwa niaba ya Serikali. Benki Kuu ndiyo iliyokuwa na mamlaka ya kupanga na kuamua nani agawiwe fedha za kigeni na kiasi gani!

Kwa ajili ya kuwahudumia wafanyabiashara, mashirika na makampuni yanayoagiza bidhaa na huduma kutoka nje, Akaunti maalum ilifunguliwa katika Benki ya Taifa ya Biashara kwa wakati huo. Akaunti hiyo ilijulikana kwa jina la External Payment Arrears (EPA) au Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje, kwa tafsiri ya Kiswahili.

Waagizaji wa bidhaa au huduma kutoka nje waliwajibika kulipa kwenye Akaunti hiyo, fedha ya Tanzania yenye thamani inayolingana na fedha za kigeni zinazotakiwa kulipia bidhaa au huduma hiyo huko nje. Baada ya waagizaji wa ndani kufanya hivyo, kutegemeana na upatikanaji wa fedha za kigeni, wauzaji au watoaji huduma wa nje walilipwa. Benki Kuu iliamua nani alipwe na Benki ya Biashara ilifanya malipo.

Juni, 1985 iliamuliwa kuwa shughuli za akaunti hiyo zihamishiwe Benki Kuu kutoka Benki ya Taifa ya Biashara na zimeendelea kuwepo hapo mpaka sasa. Katika Benki Kuu kikaundwa kitengo maalum cha kusimamia na kuendesha shughuli za akaunti hiyo kilichojulikana kama Debt Management Unit chini ya Kurugenzi ya Sera (Directorate of Economic Policy).

Kwa sababu ya tatizo la upungufu wa fedha za kigeni kuendelea, malimbikizo ya madeni hayo yalizidi kukua mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, mwaka 1999 deni hilo lilifikia dola za Kimarekani 623 milioni. Kati ya fedha hizo, dola 325 milioni ndilo deni la msingi na dola 298 milioni ni riba yake. Baadae likaongezeka kufikia dola 677 milioni.

Juhudi za Kulipa Madeni

Juhudi za kulipa malimbikizo ya madeni hayo ziliendelea kadri fedha za kigeni zilipopatikana. Kwa nia ya kutaka kutafutia ufumbuzi wa haraka tatizo hilo na kupunguza mzigo wa madeni, Serikali ilianza kutafuta njia nyingine mbalimbali. Mwaka 1994, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ilianzisha Mpango wa Kununua Madeni (Debt Buy Back Scheme). Yaani waliokuwa wanaidai BoT waliombwa wakubali kulipwa sehemu tu ya madeni wanayodai. Wapo wadai kadhaa walikubali na madeni yao yakauzwa chini ya mpango huo. Taarifa za mwaka 2004 zinaonyesha kuwa madeni ya thamani ya dola 228 milioni yalilipwa chini ya mpango huu.
Pili, Serikali ilifanya juhudi ya kupata msamaha wa madeni hayo kutoka nchi wanachama wa Paris Club. Serikali iliomba kuwa pamoja na kutusamehe madeni ya kiserikali toka nchi zao wasaidie tusamehe na madeni ya makampuni yao kwetu. Yapo pia madeni ambayo yamelipwa na makampuni ya Bima baada ya makampuni yaliyouza bidhaa na huduma Tanzania kushindwa kulipwa. Madeni ya dola 216 milioni yalihusika chini ya michakato hii. Hivyo basi, deni la dola 444 milioni lilipungua katika ile jumla ya dola 677 milioni. Kwa hiyo mwaka 2004 deni katika Akaunti ya Malipo ya Nje lilikuwa dola 233 milioni. Yalikuwepo mawazo ya baadhi ya watu kuwa pengine deni hilo lisilipwe au tulikatae. Walikuwepo waliokubali madeni yao yafutwe na wengine waliagiza fedha zao zipewe NGO. Lakini, baadhi ya wadai waliendelea kudai na wengine hata kushitaki mahakamani. Hivyo BoT ililazimika kuendelea kulipa kadri wadai walipojitokeza.

Ulipaji kwa Idhini

Katika utaratibu wa malipo ya madeni ya EPA kanuni zinaruhusu mdai kuamua deni lake kulipwa kwa mtu au kampuni nyingine. Kanuni zinamtaka mdai kutoa hati iliyothibitika kisheria ya yeye kuidhinisha malipo hayo yafanywe (Notarised Deeds of Assignments) hivyo. Pia yapo masharti ya kutimizwa na kampuni au mtu aliyeidhinishwa kulipwa hilo deni. Utaratibu umetumika kufanya malipo kadhaa ya madeni katika Akaunti ya EPA.

Matatizo ya Mwaka 2005/6

Katika ukaguzi wa Hesabu za BoT za mwaka wa fedha 2005/6, Agosti, 2005 kuligundulika matatizo katika ulipaji wa madeni kwa utaratibu wa idhini ya kulipwa wakala wa mdai katika akaunti ya EPA. Kukajitokeza kutokuelewana kati ya Benki Kuu na Mkaguzi Deloitte and Touche’ aliyegundua tatizo hilo. Baadaye mkaguzi huyo alisitishwa kuendelea na kazi. Serikali ikaingilia kati na tarehe o4 Desemba, 2006 ilimuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhakikisha kuwa ukaguzi wa akaunti hiyo unafanyika kwa kina. Aidha, ilimuagiza atafute kampuni ya kimataifa ya ukaguzi ifanye kazi hiyo kwa niaba yake. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali, ndiye kwa mujibu wa Sheria ya BoT mkaguzi wa Hesabu za Benki Kuu. Hata hivyo kwa mazingira hayo maalum Serikali ilimtaka CAG atafute mkaguzi mwingine wa nje.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alifanya hivyo na matokeo ya mchakato wa kutafuta kampuni hiyo uliochukua miezi mitano (Januari hadi Mei, 2007) ndipo ikapatikana kampuni ya Ernst and Young.
UKAGUZI

Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young wakaanza kazi hiyo Septemba, 2007 na kuikamilisha Desemba, 2007. Wakaguzi hao wamefanya kazi nzuri iliyothibitisha kiwango cha juu cha weledi (Professionalism) cha wakaguzi hao. Tunawapongeza, tunawashukuru. Tunatambua kuwa walipata matatizo mengi hasa ya kupata taarifa zilizo sahihi kwa sababu ya matatizo ya utunzaji wa kumbukumbu. Madeni haya ni ya miaka 27 na zaidi iliyopita. Kumbukumbu zimehamishwa kutoka NBC kwenda BoT. Hata huko NBC shughuli zilikuwa zinafanywa katika matawi mbalimbali nchini tena miaka hiyo hapakuwa na kompyuta hivyo kumbukumbu zote ziliwekwa kwenye majalada. Pamoja na matatizo hayo ukaguzi wa hesabu za mwaka 2005/6 ulikamilika kwa kiwango cha kuridhisha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ukaguzi katika mwaka wa fedha wa 2005/2006 uliochunguzwa, katika mwaka 2005 yalifanywa malipo ya jumla ya Shilingi 133,015,186,220.74 kwa Makampuni 22 ya hapa nchini. Makampuni hayo ni: Bencon International Ltd. of Tanzania, VB & Associates Company Ltd. of Tanzania, Bina Resorts Ltd. of Tanzania, Venus Hotel Ltd. of Tanzania, Njake Hotel & Tours Ltd., Maltan Mining Company Ltd. of Tanzania, Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment Ltd., B. V. Holdings Ltd., Ndovu Soaps Ltd., Navy Cut Tobacco (T) Ltd. of Tanzania, Changanyikeni Residential Complex Ltd., Kagoda Agriculture Ltd., G&T International Ltd., Excellent Services Ltd., Mibale Farm, Liquidity Service Ltd., Clayton Marketing Ltd., M/S Rashtas (T) Ltd., Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloloma and Brothers na KARNEL Ltd.

Aidha, ukaguzi umebaini kwamba kati ya fedha hizo, kiasi cha Shilingi 90,359,078,804.00 zililipwa kwa makampuni kumi na tatu (13) ambayo yalitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizo batili na za kugushi. Hivyo, Makampuni hayo hayakustahili kulipwa chochote. Makampuni hayo ni: Bencon International Ltd. of Tanzania, VB & Associates Company Ltd. of Tanzania, Bina Resorts Ltd. of Tanzania, Venus Hotel Ltd. of Tanzania, Njake Hotel & Tours Ltd., Maltan Mining Company Ltd. of Tanzania, Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment Ltd., B. V. Holdings Ltd., Ndovu Soaps Ltd., Navy Cut Tobacco (T) Ltd. of Tanzania, Changanyikeni Residential Complex Ltd., Kagoda Agriculture Ltd.

Aidha, ukaguzi umeendelea kubaini kuwa Makampuni tisa (9) ambayo yalilipwa jumla ya Shilingi 42,656,107,417.00 hayakuwa na nyaraka za kuonyesha stahili ya malipo na hivyo kuwafanya wakaguzi washindwe kuhakiki uhalali wa malipo hayo. Makampuni hayo ni: G&T International Ltd., Excellent Services Ltd., Mibale Farm, Liquidity Service Ltd., Clayton Marketing Ltd., M/S Rashtas (T) Ltd., Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloloma and Brothers na KERNEL Ltd.

Wakati huo huo Makampuni mawili, yaani, Rashtas (T) Ltd na G&T International Ltd., kumbukumbu zake za usajili katika daftari la Msajili wa Makampuni nchini hazikuweza kupatikana.

Uamuzi wa Rais

Baada ya kuipitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na ya Mkaguzi wa Nje, yaani, Kampuni ya Ernst and Young, Mhe. Rais amesikitishwa na kukasirishwa na taarifa ya kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa makusudi wa sheria, kanuni na taratibu za uuzaji wa madeni ya nje vilivyofanywa katika taasisi muhimu na nyeti kama vile Benki Kuu. Kwa hiyo, ameamua kuwa hatua za kisheria na kiutawala zichukuliwe dhidi ya makampuni na watu waliohusika na vitendo hivyo viovu.

Kwa ajili hiyo Rais ameamua yafuatayo:-

1. Ametengua uteuzi wa Dkt. Daudi A. Balali kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

2. Ameagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ikutane mara moja kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya Maofisa wote wa benki, walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha hasara hii kwa taifa.

3. Shughuli za ulipaji wa madeni katika Akaunti ya EPA zisimamishwe mara moja mpaka hapo taratibu za uhakiki na utaratibu mpya utakapotengenezwa.

4. Rais amewaagiza; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Inspekta Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kuchunguza na kuchukua hatua zipasazo za kisheria kwa makampuni na watu waliohusika na uhalifu huu. Rais amewataka watumie ipasavyo mamlaka na madaraka waliyo nayo kwa mujibu wa sheria. Aidha, amewataka wakamilishe kazi hiyo katika kipindi cha miezi sita. Amemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe kiongozi wa kazi hii. Amewataka wahakikishe kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.

5. Rais pia amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kushirikiana na kuwasaidia watendaji wakuu hao wa vyombo vya dola katika kufanikisha jukumu lao hilo. “Watu wengine wenye taarifa za ziada pia wazitoe kwa Timu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wenzake”.

6. Kutokana na hatua ya kutengua uteuzi wa Bwana BALALI, Mhe. Rais amemteua Prof. BENNO T. NDULU (Naibu Gavana) kuwa Gavana Mpya wa Benki Kuu. Halikadhalika, amemteua Dkt. ENOS S. BUKUKU (Katibu Mkuu – Miundombinu) kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu (Fedha na Uchumi). Pia amemteua Ndugu Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu. Uteuzi huu unaanza mara moja.

(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU MKUU KIONGOZI

IKULU,
DAR ES SALAAM
09 Januari 2008
 
Wakati mwingine napata shida kumuelewa Rais wangu

Rais amewashukuru na kuwapongeza wajumbe wa Timu hiyo kwa kazi kubwa na ngumu lakini nzuri.

Rais, baada ya kuwa ameisoma na kuitafakari ripoti hiyo, ataitolea maamuzi katika siku chache zijazo, na taarifa rasmi ya maamuzi hayo ya Rais itatolewa kwa wananchi.

Rais bado hajaisoma ripoti hiyo, lakini ameshaanza kuishukuru Kamati kwa kazi nzuri! amejuaje wamefanya kazi nzuri?

Je majukumu ya Kamati hiyo yametimizwa?
- Je watuhumiwa wamechukuliwa hatua zozote za sheria? HAPANA
- Je fedha zilizotolewa isivyo halali zimerudishwa? HAPANA
- Mtuhumiwa namba moja Marehemu Daudi Balali alihojiwa? HAPANA

lakini bado Mh Rais anatuambia kazi iliyofanywa na Kamati ni nzuri! Tumekubali sasa tunasubiri taarifa hiyo rasmi.
 
Lakini ni kipi kinachopmfanya rais wetu aonekane ameshindwa? Ukisikiliza maneno yake na kusoma mikakati yake, inaonekana kuwa ni mizuri sana. Kwa nini utekelezaji unakwama? Ni tatizo la rais mwenyewe au wasaidizi wake? Nauliza hivi kwa sababu imefika wakati watu wengi wenye shida wanaamua kukimbilia wka rais mwenyewe kuomba msaada. kwangu mimi hii inamaanisha kuwa waliotakiwa kuyatatua matatizo hayo (wasaidizi wa rais) hawafanyi kazi yao sawasawa. Tuendelee kumlaumu kwa makosa ya wasaidizi wake pia? labda hapa kosa lake ni kutowabadilisha haraka iwezekanavyo na kuchagua timu itakayom,pa ushirikiano wa kutosha.
Lakini pia kuna uwezekano kuwa kuna kitu kinamfanya ashindwe kuyafanya hayo mabadiliko ambayo tunayatamani. Ukisikiliza maneno yake, anaonekana kuwa ni mtu anayependa kuifanyia kitu fulani nchi lakini inaonekana kuna kitu kinamkwamisha

Tatizo linalomtafuna JK ni "UMWENZETU", Kila kitu wanaangalia je huyu ni CCM?, Nchi inavipaji chungu nzima hawavitumii kisa sio wana CCM. Ile dhana ya kwamba uongozi ni "ULAJI" Inampoza Rais, anadhani kumpa mtu ambaye si mwana CCM Post ya Kufanya kazi ni kumpa Ulaji. Wakati umefika sasa watu wajue kuwa nchi haitapata maendeleo kupitia kwa wana CCM Bali ni watanzania wote wenye nia njema na nchi.
 
TUnataka pesa zetu sio makaratasi hayo yenye vingereza vigumu
 
Back
Top Bottom