Askofu Shoo aisifia ripoti ya Jaji Chande

Askofu Shoo aisifia ripoti ya Jaji Chande

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,079
Reaction score
3,406
Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Shoo amesema ameipokea kwa furaha Ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani, akisema imekuwa sehemu ya kuponya Taifa kutokana na majeraha yaliyotokana na matukio ya Oktoba 29, 2025 kwa kuweka wazi ukweli na kutoa mapendekezo muhimu.

Akizungumza kuhusu ripoti hiyo iliyotolewa Aprili 23, 2026 Jijini Dar es salaam, Askofu Shoo amesema endapo Serikali itayafanyia kazi mapendekezo yaliyomo, Tanzania itaendelea kuwa kisiwa cha amani, umoja na mshikamano, huku akisisitiza umuhimu wa kutumia ukweli kama msingi wa maridhiano ya Taifa.

Aidha, amesema ripoti hiyo ni hatua muhimu katika kujenga mustakabali bora wa Nchi, akieleza matumaini yake kuwa mapendekezo yaliyotolewa yataimarisha haki, utulivu na kuzuia kujirudia kwa matukio kama hayo siku zijazo.
 
Back
Top Bottom