Nimesikia kwenye news kwamba JK mkulu wa nchi atahutubia bunge 21 august 2008. Kama ndivyo Rais Jk atakidhi kiu ya wananchi kama ataeleza kwa ufasaha yafuatayo:
1. Hatua gani zimechukuliwa dhidi ya wezi wa EPA. Wananchi hawataki kusikia eti uliunda kamati ambayo haijakamilisha ripoti. Terms of reference ulielekeza wachukue hatua za kisheria na si kuandika taarifa nyingine kwani tayari Ernst+young walishaanika kila kitu. Kama hutaji hatua za kisheria zilizochukuliwa ni vema usiliongelee
2. Ufisadi wa Mkapa, yonah et al: tueleze hatua gani utachukua dhidi ya hawa kwa kuchukua kiwanda cha makaa ya mawe kifisadi. Usitueleze kiwanda kilikuwa katika hali mbaya. Kama kilikuwa katika hali mbaya kwa nini hawakutangaza tenda. Usijaribu kumtetea
3. Madini ya watanzania kuporwa: eleza kwa kina usipofanyia kazi mapendekezo ya kamati ya bomani. Pia utueleze kwa nini serikali yako imeanza m
azungumzo na wa-canada kuhusu kuwa exempted kwenye mapendekezo yanayotolewa na kamati ya bomani.
4. Ripoti ya richmond. Lieleze bunge kwa nini serikali yako inavuta miguu kutekeleza maamuzi ya bunge kuhusu ufisadi wa richmond. Mmegoma au?
5. Meremeta na mwananchi: tueleze jinsi makampuni haya yanavyohusika na usalama wa taifa. Je kupora madini ya watanzania ndo usalama wao? Nini kimejificha ndani yake? Waeleze wananchi hatua ulizokwisha chukua kwa wezi hawa?
6. Tanesco. Tueleze hatua utakazochukua kutuokoa watanzania dhidi ya mikataba ya kifisadi ya IPTL na mingine.Maneno matupu hayatusaidii kwani nasikia tanesco wanaandaa mapendekezo kwenda ewura kupandisha gharama. Huoni tunazidi kuumia sisi walala hoi
7. Zanzibar nchi si nchi? Toa msimamo wako ni upi? Unalishughulikiaje?
8. Mwafaka ccm na cuf: tueleze hatua binafsi unazochua kunusuru mazungumzo. Kwani tayari mamilioni ya tsh. Yameteketea tayari ktk vikao
9. Mgombea binafsi: tueleze msimamo wa serikali ni upi tueleze lini mnawasilisha mswada bungeni?
10. Maslahi ya wafanyakazi. Uliunda kamati kupitia maslahi ya wanafanyakazi. Mbona hatuoni mabadiliko?
11. Usalama wa chakula? Tueleze hatua gani unachukua tofauti na mkapa na waliokutangulia wengine. Si unajua chakula kitazidi kuwa haba duniani. Hivi hatuna uwezo wa kutoa trekta moja kila kata kwa kuanzia kama siyo kijiji chenye ardhi na hali ya hewa safi. Hatuoni kuwa kilimo kinaweza kutuokoa?
12. Bidhaa feki: vipi serikali imelala au?Mbona bidhaa feki zitatumaliza. Tueleze kwa nini zipo na hatua gani umechukua kama kiongozi wa nchi?
Hiyo ndo dazeni ya issues zangu ambazo ukizitolea maelezo kwa ufasaha wananchi tutakupa 5. Otherwise hotuba ikiwa kama ya mwisho wa mwezi uliopita utatuacha midomo wazi.
Nawasilisha ili wana Jf muongezee na hatimaye salva rweyemamu amfikishie ujumbe mh. Rais
isipokuwa hivyo nitapendekeza tuunde kamati kuchungua utayarishaji wa hotuba za rais
nawasilisha

Last edited by a moderator: