Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,163
HABARI zilizonifikia hivi punde, zinaeleza kwamba sehemu ya hotuba ya RAIS inasema;
"Mheshimiwa Spika, nimepokea ripoti ya uchunguzi wa upotevu wa fedha za EPA na tayari nimekwisha vikabidhi vyombo husika kwa ajili ya utekelezaji." mwisho wa kunukuu, na baada ya hapo ataendelea na mambo mengine muhimu ya Kitaifa na suala hilo hapo ndio utakuwa mwisho wake kujadiliwa kwani, "liko mikononi mwa vyombo husika".
Hapa kuna maswali, vyombo husika ni vipi? Si ndio alivyovipa kazi, na badala ya kufanya kazi, vikaja na RIPOTI, kwa hiyo sasa tutegemee na kusubiri RIPOTI nyingine kutoka "VYOMBO HUSIKA"..... Hii inawezekana Tanzania pekee
Eti anataka kusema nini? kama anatarajia kuwa kauli hiyo itawashtua watanzania na kuwafanya wamashangilie, basi asubiri kushtuka yeye mwenyewe.
Waliomba muda tukawapa, kama wanadhani wataendelea kupewa muda wakati wote, they are in for surprise.
Hakuna atakayeacha kuyajadili haya hata kama yakipelekwa kwa nani, tunachotaka kuona ni hatua madhubuti zinachukuliwa dhidi ya watuhumiwa wote. Hiyo hadithi ya vyombo husika imeshapitwa na wakati