.Umewaza niliyowaza. Kuna taarifa mbili za kifo cha yule dogo. Kafa ghafla na kajiua! Baada ya hapo hakuna taarifa nyingine iliyotoka hata ya mazishi. Poor boy was only 32 years. RIP kamanda!
.Mhhh, hapo kweli kuna madudu mengi ya kufanya libichwa bovu lianze kuzunguka.
Taarifa ya kwanza inasema alikutwa amekufa nyumbani kwake baada ya majirani kuvunja mlango sasa 8.45 (sina hakika kama ana maana ya 8.45 AM au 2.45 PM). Hata hivyo hao majirani zake ni akina nani kama huyo juu alikuwa anaishi kweye Barracks za TISS? Na walikuwa wanatafuta nini au wanamtaka wa nini mtu ambaye ni bachelor?
Taarifa ya pili ndiyo inalikoroga kabisa. Hivi mtu akijipiga risasi (hata kama ni mdomo) mlio wa bunduki hautoki nje? Na hao wenzake walio mkuta amekufa ni akina nani na walikuwa wanatafuta nini?
Ukiwaza zaidi kuhusu hizi repoti 2 unazidi kupata kizunguzungu.....you end up smelling evil!
Hata kura za maoni nyingi zinazoendeshwa sasa zinaonesha Slaa anampita JK kwa mbali sana. Kama Slaa ataweza kuwateka watu wa vijijini basi mambo yatakuwa magumu kwa CCM. Chama cha Mafisadi kijiandae kwa anguko la kihistoria. Soon kitaanza kuwa chama cha upinzani. Watanzania wengi sasa wameshaishtukia CCM.
sehemu zote walizofanya tafiti zinaendana na hali ilivyo, ila ya dar nimeshangaa aisee!!!
Umewasiliana na mtu mwenye access na simu + TV. Embu watafute wale wasio na simu wala TV wanaoshinda kwenye maboda ya mpunga upate maoni yao
Wazee tusipuuze, tujaribu kucheck viashiria!!!!.....Kwanza jiulizeni kwanini majuzi kati CCM waliamua kuwatuma makada wake(wazee kwa vijana) kwenda kila jimbo ili Kuongeza kasi ya kampeni???? Na wale makada walioshinda kura za maoni lakini CC ikawaengua (akiwamo Bashe na Mwakalebela) CCM ishaanza kuwaangukia... Hali ni mbaya saaaana kwa CCM wazee!!! Kwahiyo tusimpuuze huyu jamaa, tutafiti.
Issue ya REDET na Synovate waulize wenyewe... lakini ukitumia medula oblangata uliojaliwa na Mungu, ulizia uchaguzi wa serikali za mitaa CCM iliibuka na kura kiasi gani? Alafu jiulize ni kitu gani cha ajabu kimetongea tangu wakati huo mpaka sasa? Jiulize kipi CHADEMA imekuja nacho cha ajabu ambacho kitaweza kubadili matokeo kiasi hicho? Jiulize CCM inaowabunge wangapi? Niulize CCM inatarajia kupata wabunge wangapi? Jiulize wabunge na madiwani wa CCM ambao wametapakaa nchi nzima hawana mchango kwa kura za Rais wao.
Sisi waTanzania watu wa ajabu sana tunaamini mazingaombwe mno....
usalama wa taifa hauna ushahidi
.Si kweli thread zinazomsifia JK zinafutwa bali Zinakosa MVUTO sababu hazipendwi na kujikuta zikienda rank za chini kabisa kwa umaarufu humu JF. Scroll down sana ndo utazikuta!!
Hivi kitandani kwangu mnataka kuja kufanya nini hasa?
kukubalika vijijini kwa slaa kunatokana na matunda ya operesheni sangara. Pia ni baada ya wananchi wa huko kuanza kupima ukweli wa kile kinachoelezwa na wapinzani.
Mkuu, Kikwete hasimamiii sera za chama hata kidogo bali sera za ujangili wa Rostam Azizi na rafiki yake Richmonduli Edward Lowasa na maisha bora kwa wanamtandao na familia zao. Na usipuuzie taarifa hizi. Nakwambia ukweli sasa hivi nimetoka kupiga simu kijijini kwetu nimeongea na dada yangu aliyeko huko anasema mwaka huu watu wanachagua CHADEMA wamechoka na ahadi hewa na bla bla za CCM na kaniambia mambo mengine ya ndani sana (siwezi kuyaandika hapa). Kama watu wa vijijini wamepata mwamko huo basi ndo mwisho wa CCM.
Muhimu: CHADEMA wekeni mikakati ya kulinda wizi wa kura na kuingizwa kwa masunduku yaliyojaa kura za CCM kutoka usalama wa taifa. Hatika ukombozi wa Watanzania umewadia.
Mdee and Slaa Kawe 90% :becky:Jimbo la Ubungo, Slaa & Mnyika - 89%
.
Mstaafu mmoja wa UWT anasema kwamba, vifo vya hawa jamaa,UWT havitangazwa duniani kote kwa sababu ya asili ya kazi yao kwamba moja ya kiapo chao ni kuwa tayari kufa wakati wowote ukiwa kazini. Kiapo hiki ukikikataa siku ya kwanza tu ndio inakuwa ukomo wa kutafuta ajira huko. anasema kujiua pia ni kosa la kiamaadili kwa sababu wana vitengo vya kudhibiti saikolojia kwa kuwa muda mwingi wanahodhi silaha na kujua mambo nyeti. Wanaoweza kutangazwa ni wale viongozi wa juu ambao kanuni imewaweka wazi kwa umma.
Inaaminika kwao kwamba kufikiria kujiua ni jambo la hatari si kwa anayechukua uamuzi huo tu bali hata kwa watumishi wengine na raia wa kawaida wasio na hadhi ya kujitetea.Wakati wote wa kazi za utumishi mfanyakazi anatakiwa kuwa na akili timamu isiyotiliwa mashaka.Fikra za kujiua zinadhibitiwa wakati wote wa somo la saikolojia kwa kuwa kwao kutamani kujiua kunaweza kwenda sambamba na kuua na wengine kabla ya kufikia uamuzi huo.
Anasema taarifa alizonazo ni kwamba kifo cha mlinzi wa Chief Justice ni cha kawaida na ndio taarifa sahihi lakini watu hawawezi kuamini kwa sababu vifo vyao haviwekwi wazi kama ilivyo kwa raia wa kawaida.