kwani what is mita 5? Watu watasimama umbali wa mita 5 kutoka kituo cha kura na kuizingira kituo, na hakuna masunduku kuingia wala kutoka! Unafikiri huko pemba walifanyaje? Mpaka wanapotangaza matokeo ya kura hata usiku wa manane watu hawaondoki.
Na usitake kuwatisha watu na eti matukio ya 2001.. Unafikiri tunaogopa? Tumeshafunguka macho na hatuogopi vitisho :mad2: Mnataka kuwatisha watanzania million 40? Hatuwezi kutwaliwa na genge la wahuni wachache! Maneno kama ya kwako ni hamasa tosha kwa wananchi kujitokeza na kulinda kura zao!
aa subutu mutaweza kuhimili mabomu ya machozi nyinyi? Wenzenu wa pemba ni madume kweli kweli! Miaka yote hiyo ya uchaguzi mabomu ya machozi mtindo mmoja na wengine walikimbilia mombasa na mogadishu na wale waliobakia pemba walikuwa ngangari mpaka kimeeleweka sasa ni serikali ya mseto!
Haya wenzangu chadema hayo munayaweza? Mwenzenu lyatonga mrema alishapitia hayo mabomu ya machozi kipindi cha omari mahita akiwa rpc kilimanjaro mpaka yamembabua ngozi yake masikini sasa utafikiri ana gonjwa la mbalanga! Na mwisho wake amerudia matapishi yake na sasa anataka angalau ubunge kwa huruma za ccm maana kila siku anamsifia jk na wala hana habari na mgombea wake wa urais kwa ticket ya tlp!
Hawa ndio aina ya viongozi wetu wa upinzani tulionao huku bara! Yaani slaa kwanza alitaka kugombea kiti chake cha ubunge ghafla kabadilika na sasa anataka urais!!! October 31 chadema mukileta vurugu halafu mukipigwa mabomu munadhani watu wa aina ya mbowe na slaa watawasaidia? Wao wanauwezo wa kupanda helkopta na kutoroka nchini! Lakini nyinyi masikini wenzangu musio na hata baiskeli mutaweza kweli kukimbilia shimoni mombasa au huko mogadisho kwenye vita? Kama walivyofanya wa pemba mwaka 2001? Aaa subutu! Mimi nawajuwa wachaga(watani) na wa mbulu hakuna watu waoga kama hao!