GE2010 Kikwete apewa report ya kura za Slaa

GE2010 Kikwete apewa report ya kura za Slaa

Status
Not open for further replies.
Freeman Mbowe 2005 mikutano yake ilikuwa inajaza watu kama hii ya Wilberd Slaana matumizi ya HELKOPTA na la kushangaza Mbowe alikubali kushindwa kwa kishindo tena alihunduria kuapishwa kwa JK wakati CUF na TLP walikataa kukubali matokeo! jee DR. Slaa atakuwa tayari kufuata nyayo za Mwenyekiti wake Mbowe kukubali matokeo ya ushindi wa CCM wa TSUNAMI

CHADEMA munaota ndoto za mchana! hata mwaka 2005 mulikuwa na ndoto hizi hizi za kudai ushindi hewa! sasa ngojeeni 31 october mtakavyo garagazwa! ila tunamuomba Slaa akubali matokeo kama alivyofanya Mbowe 2005!

CHADEMA wacheni FITINA na UMBEA wa kuwasingizia viongozi wa CCM kuwa wananjama za kuwauwa viongozi wenu! huu ni uongo wa wazi kabisa na kama munaushahidi toka kwa USALAMA wenu wa TAIFA si mupeleke tuhuma zenu POLISI? munangoja nini? WACHENI KUWADANGANYA WANANCHI KUWA SLAA ATASHINDA! HUKO VIJIJINI NA MIKOA YA PWANI, KUSINI NA KUSINI MAGHARIBI, MIKOA YA KATI NA ZANZIBAR HAKUNA ANAEMJUWA SLAA ILA HUKO MBULU, UCHAGANI NA BAADHI YA MIKOA YA MAGHARIBI LABDA NDIPO ANAPOWEZA KUAMBULIA KURA CHACHE! TAKWIMU NILIZIWEKA HAPA LAKINI ZIMEFUTWA NA LA KUSHANGAZA NI KUWA FORUM HII INATAKA MAWAZO YA KUMSIFIA SLAA NA CHADEMA NA HUU NI UWOGA! KWANI WANAOAMUA NANI ATAKUWA RAIS SIO JAMII FORUM BALI NI WA TZ! NA WA TZ WENGI WANATEGEMEWA KUMPA KURA ZAO KIKWETE!

SASA KAMA NYINYI HAMTAKI KIKWETE AU LIPUMBA AWE RAIS HAKUNA ANAEWALAZIMISHA LAKINI SIO MULAZIMISHE WATU WOTE WAMPENDE DR.SLAA NA CHADEMA!

MUNASIKIAEEE!!

kufutwa kwa posts zinazomsifia kikwete ni jambo la kawaida hapa JF na hii itaharibu jukwaa kuwa huru, kama hamtaki kupata mawazo ya wengine ondoa kauli mbiu "where we dare to talk openly" iwe where we dont dare to talk about chadema openly".
 
Na wewe pia KADOGOO, unapenda forum inayomsifia KIKWETE tu, Kaka mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko, si kama 2005, SLAA anakubalika kote ndo maana jk ameshindwa hata kupumzika.

JK atapumzika vipi wakati Slaa hapumziki? hadanganyiki mtu hapa ni kwenda sambamba,mtu kwa mtu, nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda, uvungu kwa uvungu, mpaka kieleweke. mapumziko ni tarehe 31 Octoba, 2010.
 
kufutwa kwa posts zinazomsifia kikwete ni jambo la kawaida hapa JF na hii itaharibu jukwaa kuwa huru, kama hamtaki kupata mawazo ya wengine ondoa kauli mbiu "where we dare to talk openly" iwe where we dont dare to talk about chadema openly".
FIKRA MBADALA au FIKRA MGANDO?
 
Haya wamemwagika sasa, JF bana............. Love it!!!!!!!!!!
 
Mwenye kuamini hizo statistics kwa kweli hana tofauti na aliyeamini kwamba CCJ ni chama tishio... Hivi Watanzania tutaacha lini kuamini mazingaombwe?
.

majuha ndio waliwao. Hizo ni data za kupata kizingizio baada ya Slaa kushindwa na kikwete.
 
Hivi Redet ya Mukandala wapo? Au bado wanasubiri maagizo ya CCM ya namna ya kupika data ?


Hivi JF ya wanachadema iko wapi? Au bado wanasubiri maagizo ya Chadema ya namna ya kupika data ?
 
Hivi JF ya wanachadema iko wapi? Au bado wanasubiri maagizo ya Chadema ya namna ya kupika data ?
Usijibu posts za mwishoni just anza mwanzo na upitie kila uchambuzi then ndo utakuwa RAIA MWEMA
 
kufutwa kwa posts zinazomsifia kikwete ni jambo la kawaida hapa JF na hii itaharibu jukwaa kuwa huru, kama hamtaki kupata mawazo ya wengine ondoa kauli mbiu "where we dare to talk openly" iwe where we dont dare to talk about chadema openly".

Si kweli thread zinazomsifia JK zinafutwa bali Zinakosa MVUTO sababu hazipendwi na kujikuta zikienda rank za chini kabisa kwa umaarufu humu JF. Scroll down sana ndo utazikuta!!
 
Hawa waliompatia JK hii taarifa ni ya kweli au nia yao wanataka atoe/aongeze fungu pesa za kampeni ili wanufaike nazo
 
Mkuu, Dar imeamka sana sasa hivi. Watu wengi walikuwa hawaoni kuwa upinzani umekuwa kiasi cha kuaminika kuongoza nchi. Ila pia, wapinzani hawakuwahi kuonyesha seriousness ya kutoa mgombea/wagombea wanaoonekana kukubalika kwa miaka mingi. Lakini kubwa zaidi ambalo limebadilisha watu wengi wa Dar, ni utendaji wa serikali inayoomba ridhaa kwa mara ya pili.

JK alipata kura nyingi sana mwaka 2005 kwa kuwa watu wengi waliamini angeendeleza ufanisi wa serikali ya awamu ya tatu. Na kwakuwa alikuwa mmoja wa askari wa miamvuli, alionekana kufaa zaidi. Watu wamegundua kuwa walikosea. Dar haina wajinga Mkuu. Watu wanapiga kampeni ndani ya familia, kwenye vikao vya ndani ili Dr. Slaa achaguliwe. Sijawahi kuona kitu kama hiki katika siasa za Tanzania. Wengi wamekuwa hawajali sana nani anakuwa Rais, au Mbunge.

Mwaka huu, vijana wengi sana wamejiandikisha kupiga kura kwa mara ya kwanza. Na wengi wanasema imetosha sasa, lazima wabadilishe uongozi.

Very good, let us spread this message, vikao vya ndani na vya familia ndugu jamaa na marafiki ni namna nzuri ya kuleta mabadiliko mwaka huu 2010.
This is interesting news!
Embu tuamue kila kona ya nchi bila kumsubiri Dokta Slaa.

Thanks JF
 
Endelea kuota!
Ndoto ndiyo mwanzo wa uhalisia. Asiyeota kwa mambo makuu hafikirii na mtu asiyependa mabadiliko hata siku moja. It only who think the possibilities who are ready to embrace changes in their life, for those who live in their "reality" realm never dream for change, for them change is the threat. Nakutaarifu kuwa habari ndio hiyo, mabadiliko yanakuja. Nimepata taarifa kutoka katika kijiji cha ndani kabisa katika Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya, mpaka leo hii ukiitisha uchagu Rais Wao ni Dr.Slaa. Kumbuka hawana TV na Rediopekee huko ni Redio Tanzania na zingine kutoka Malawi. Dr.Mwakyembe anafanya kazi ya kuwatuliza wananchi wamchague Kikwete, huko hakuna Mzee wala kijana, Rais Wao Dr.Slaa na Mbunge wao ni Dr.Mwakyembe na wanasema hawachagui chama wanachagua mtu makini bila kujali yuko chama gani.
 
aa subutu mutaweza kuhimili mabomu ya machozi nyinyi? Wenzenu wa pemba ni madume kweli kweli! Miaka yote hiyo ya uchaguzi mabomu ya machozi mtindo mmoja na wengine walikimbilia mombasa na mogadishu na wale waliobakia pemba walikuwa ngangari mpaka kimeeleweka sasa ni serikali ya mseto!

Haya wenzangu chadema hayo munayaweza? Mwenzenu lyatonga mrema alishapitia hayo mabomu ya machozi kipindi cha omari mahita akiwa rpc kilimanjaro mpaka yamembabua ngozi yake masikini sasa utafikiri ana gonjwa la mbalanga! Na mwisho wake amerudia matapishi yake na sasa anataka angalau ubunge kwa huruma za ccm maana kila siku anamsifia jk na wala hana habari na mgombea wake wa urais kwa ticket ya tlp!

Hawa ndio aina ya viongozi wetu wa upinzani tulionao huku bara! Yaani slaa kwanza alitaka kugombea kiti chake cha ubunge ghafla kabadilika na sasa anataka urais!!! October 31 chadema mukileta vurugu halafu mukipigwa mabomu munadhani watu wa aina ya mbowe na slaa watawasaidia? Wao wanauwezo wa kupanda helkopta na kutoroka nchini! Lakini nyinyi masikini wenzangu musio na hata baiskeli mutaweza kweli kukimbilia shimoni mombasa au huko mogadisho kwenye vita? Kama walivyofanya wa pemba mwaka 2001? Aaa subutu! Mimi nawajuwa wachaga(watani) na wa mbulu hakuna watu waoga kama hao!
Mkuu, usiombee Tanzania ifikie hapo unapopasema. Maana moto kama huo ukiwaka, kuuzima ni kazi kubwa sana.

Usifikiri hata wa Pemba wanapenda kupigwa mabomu ya machozi. Ila ikibidi, kila mtu ana uwezo wa kuvumilia maumivu ili kufikia lengo la anachokiamini kama ukombozi wake na vizazi vijavyo.

Endapo itakuwa kwa interest ya chama chochote Tanzania kufikia machafuko ili kushika dola, damu itakayomwagika itakuwa katika mikono ya chama hicho husika.

Ushindi wa Dr. Slaa si wakwake mwenyewe, ni ushindi wa Tanzania mpya. Tanzania itakayojali maslahi ya rika, jinsia na kila mtanzania popote alipo ndani ya nchi yake. Dr. Slaa hana haja ya kuumia peke yake kwa manufaa ya nchi yake.

Usidhani hivyo ndivyo inavyokuwa wakati wananchi wanapochoshwa na watawala wasiowafaa. Wananchi ndio hujitoa muhanga kupambana na wakoloni, wanyonyaji na wote wanaotaka kuendelea kuwakandamiza au wanaokusudia kutaka kuwakandamiza.

Tusitishiane machafuko, sio ajenda kuu ya uchaguzi mwaka huu. Tusiombee machafuko, hayana tija kwa Taifa. Hasa Taifa kiwete kama letu.
 
.

mimi nimefanya ufuatiliaji wa hali ya kisiasa nchini inaonyesha kuwa baadhi ya wanaccm na wasio wanaccm wanasema kura ya urais watampa Kikwete ila ubunge itagemea hali ya hewa ya kisiasa nchini, kwa maana ya sifa na vigezo atakavyokuwa navyo mngombea wa udiwani au ubunge.
Mkuu, tunazungumzia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Nadhani wewe unazungumzia wa 2005. Ule si ulishapita na hicho unachosema ndicho kilichotokea.

Mwaka huu, yaani 2010, hata baadhi ya sisi wanachama wa CCM tumeapa kuwa, hatutampigia kura JK.
 
JK atapumzika vipi wakati Slaa hapumziki? hadanganyiki mtu hapa ni kwenda sambamba,mtu kwa mtu, nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda, uvungu kwa uvungu, mpaka kieleweke. mapumziko ni tarehe 31 Octoba, 2010.
Hivi kitandani kwangu mnataka kuja kufanya nini hasa?
 
taarifa hizi nilizisikia, sikujua zishaanza kusambaa... Inabidi kuanza kutafuta ukweli wake. Inasemekana slaa ameanza kukubalika vijijini sana, nini kinasababisha?

kukubalika vijijini kwa slaa kunatokana na matunda ya operesheni sangara. Pia ni baada ya wananchi wa huko kuanza kupima ukweli wa kile kinachoelezwa na wapinzani.
 
Habari zilizopatikana ndani ya kikao cha siri kati ya vigogo waandamizi wa usalama wa taifa,Kikwete na Kinana wiki iliyopita zimedokeza kwamba JK amepokea report inayoonyesha kura za Dk Slaa atakazopata october 31 2010.

Mpashaji wa habari amebainisha ya kwamba baada ya JK kupewa tathimini hiyo hakuamini alichoambiwa, zaidi aliongea kwa kiingereza maneno mawili '' Is it?''.

Hii ni taarifa fupi iliyotolewa wiki tatu zilizopita ikulu jijini dar es salaam ikiwa ni mpango wa usalama wa taifa kukamilisha awamu ya kwanza ya utafiti wao kwa baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa, kati, pwani na kaskazini. Machache yameibwa kwenye taarifa hiyo:

Mara: Dr Slaa 59.7%
Mwanza😀r Slaa 58.3%
Kigoma😀r Slaa 52.7%
Singida: Dr slaa 34.7%
Shinyanga: Dr Slaa 43.2%
Kilimanjaro: Dr Slaa 51.7%
Arusha: Dr Slaa 47.1%
Manyara: Dr Slaa 53.8%
Tanga😀r Slaa 46.2%
Dar es Salaam: Dr Slaa 66.4%
Geita: Dr Slaa: 62.7%
Kagera: Dr Slaa 48.2%
Dodoma: Dr slaa 42.4%
Tabora: Dr Slaa 57.6%

Hey wale jamaa wa TISS, Kitengo cha online info ongezeni na thanks za hapa. We ndugumi wa TISS mpelekee mzee hiyo laptop haraka muonyeshe hizo thanks, halafu imba habari ndio hiyo wa mwana FA, si alisema anapenda 'BONGO FLAVA' utasikia atajibu na 'nimefuliaaa...hi hi hi hi....

Presha inapanda....presha haishuki..
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom