Msishabikie vyama vya siasa kama klabu za mpira wa miguu hata kufikia kutunga uongo ili kupata ushindi wa hira hata kufikia kuhusisha usalama wa taifa, hiyo ni hatari na sumu. Watanzania wanashabikia chama cha siasa na mgombea wake hata kama hafai bila kutambua athari zake baadaye, ni vyema kuhamishia ushabiki huo katika vilabu vya michezo kwa sababu vikifungwa familia zao zitaendelea kula na kulala salama. shibikieni vilabu vya michezo kama simba, yanga, manchester, chesea kwa kuwa wakifungwa familia zetu zitaendelea kula lakini ushabiki wa chama utawatokea puani kutokana na ushabiki wa kujuana na hatimaye kumchagua kiongozi mbovu na baadaye familia zetu zinaanza kutaabika.
Kila mtu ampatie mgombea kura ya ndio baada ya kutafakari kwa makini na sio kushinikizwa na wakereketwa na mashabiki wa vyama. msukumo wa makundi kuelekea kumpata rais, mbunge na diwani bora hauwezi kuipeleka nchi kule tunakotaka. Ni dosari kubwa kukishambulia chama cha CCM baada ya kuonekana chama cha CHADEMA ni mbadala katika siasa za Tanzania. Ni kosa ambalo wachache wanapaswa kujihadhari na mamluki wa siasa za mageuzi ambao wamejiingiza katika vyama vya upinzani kwa ajili ya kuwachanganya watanzania. Chama bora ni kile kinachozungumzia sera badala ya watu.
CCM sio mtu ni chama chenye sera ni vema kuchambua sera zake na kuonisha na sera za vyama vingine na hatimaye kutathmini sera hizo kwa namna bora ambayo kila mmoja wetu atanufaika nazo. Kuzungumzia watu, Kikwete dhidi ya Slaa bila kuchambua yale ambayo wanataka kuwafanyia watanzania haina manufaa kwetu. Tupiganie sera sio, tupiganie watu. Tukumbukuke kwamba, wagombea wote wanakwenda kusimamia sera za vyama vyama na si vinginevyo baada ya kupata ushindi.