Mkuu Kasheshe, wanachokisema wengi sio u-CCm wala u-Chadema. Watu wanasema JK amewaangusha, amewadanganya na wanachotaka ni kumuondoa yeye tu. Wabunge na madiwani wao, wanaweza kuendelea kuchagulika. Hasira za wengi ni kwa JK ambae anaonekana kutojali maslahi ya wengi na kuendekeza ushikaji.
Ukweli ni kuwa hayo unayoita mazingaumbwe, mwaka huu yatatokea. CCM inaweza kushinda sana Ubunge, ila u-Rais watu wanaelekea kuchoshwa na aliepo.
Kwa mara ya kwanza watu wanasema, CCM ni ya watanzania, Chadema, CUF na vingine vyote ni vya watanzania. Wagombea wote ni watanzania na hawaoni ubaya kumchagua wa upinzani mwaka huu.
Watu wengi walitoa angalizo wakati wa kumtafuta mgombea wa uRais wa CCM. Wakaomba washindanishwe wengi. Ukweli ni kuwa, kama wangekuwa makini wakati ule, JK angeshinda angeweza kupewa nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu kwa kishindo pia.