Ni kweli kabisa nakubaliana na wewe. Lakini naomba nikuulize swali dogo, REDET na Synovate kwanini hawajatoa matokeo ya tafiti zao? Hivi kweli unaweza kuamini kwamba Synovate walifanya utafiti unaogusa coverage ya kampeni za wagombea kwenye vyombo vya habari tu? I think hako kakipengele kalitakiwa kuwa sehemu ya major report kuhusu perception ya watu kuhusu wagombea na pia iwapo uchaguzi ungefanyika wangempa nani kura na kwanini. Kitendo cha Synovate kutuletea utumbo wa utafiti ule unaashiria something is wrong some where na ndio maana hujasikia REDET wala Synovate.
Mwaka 2005, mpaka mwezi mmoja kabla ya uchaguzi walishatoa set mbili za polls na zote CCM ilikuwa inaongoza. Utafiti wao ulianza hata kabla ya nominations, na kama unakumbuka Prof. Mwandosya ali-discredit hizo polls za REDET. Mzee Kingunge baada ya Kikwete kuwa nominated na Mkutano Mkuu wa CCM, akasema kwamba wasomi wa REDET walishatoa matokeo hata kabla ya nominations na ndio uzuri wa kuwa na tafiti ambazo ni credible.
Sasa mwaka huu kigugumizi kinatoka wapi? Hao Synovate wanakuja na report ya kitoto mpaka unaanza kujiuliza hivi hawa walichokuwa wanafanya ina maana watanzania hatujui? Au hatusomi magazeti, au hatuangalii TV au hatusikilizi radio? Maana huo utafiti hauhitaji hata kupoteza resources au kuita waandishi wa habari eti unaenda kuwapa report kuhusu utafiti ambao uko wazi mbele ya kila mtu. Tuambie kilicho jificha ndani ya wapiga kura ili tuone ni kitu gani ambacho wapiga kura wanaangalia, wangapi wameishafanya maamuzi ya kura zao na wangapi ambao hawajafanya maamuzi.