GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Kitu iko bomba...JAMAA alionekana kupoteza maneno mapema..kwanini hawakuona hilo wapambe wake???? Dhambi za kuwaendekeza mafisadi..kuwakana wanaCCM wengine..RIZZZ upo hapo!!
 
Nafikiri inabidi watu kuamua kama wanafikiri Bilal anaweza kuongoza taifa kama Goodluck wa Nigeria....Naona nyota ya Bilal inag'aa na inaweza kuwa blessing in disguise!
Yeye mwenyewe spana mkononi.
 
Hadharani ameanguka mara tatu, je, huko home kwake, yametukia matukio mamgapi???????:confused2:
 
Kikwete ni mgonjwa, kupunguza makali ya athari za ugonjwa ingebidi aache kufunga, wananchi tushajua anaumwa na haitampunguzia thawabu wala sifa kwa wananchi akiacha kufunga. Naamini hata dini zinaruhusu watu walio na matatizo ya kiafya kutofunga, hususan kama wana kazi stressful kama hii ya kampeni.

Kwani akisema ukweli kwamba ana ugonjwa na akaendelea bila kujiongezea kazi ya kufichaficha na kufunga hata pale asipostahili ndio atakosa huo urais ?

Asipofanya hivi atazidi kuthibitishia watu kwamba ni muongo-muongo na msirisiri bila sababu tu, mangapi mengine anaficha na kufanya kinyemela ?
 
Hivi kwa kujaribu kuficha habari ya tukio la Jangwani, maanake yake tatizo ni kubwa kuliko tunavyo liona, na huyo Msemaji wa Kampeni za CCM yupo kwa maslahi ya Tanzania au maslahi Binafsi, maana sioni mchango wake katika maendeleo ya tanzania zaidi ya kusikia kampuni yake imehusika na kusafirisha pembe za ndovu zilizoshkiwa asia.
na pia kwanini tukio limetokea alipo anazungumzia mafanikio katika kupigana na "Rushwa"

Inawezekana hapo kwenye rushwa kulikuwa na "psychological burden" kubwa sana, anaangalia umati wote ule wa watu halafu anaona kabisa anawadanganya waziwazi, kichwa kinapata overload mtu mzima chini.

Hamna cha bodyguard wala nini, misurupwete wote wanaduwaa tu. Bora bongo hatuna malicious incidents.
 
Nafikiri alikuwa anaongelea wale waliokuja kumdaka na kumbeba ambao kwa wao umuhimu ulikuwa kwa rais na si makaratasi ya hotuba ambayo watakuwa waliyakusanyakusanya tu bila kuangalia pages. Yeye anajua kabisa kuwa kuanguka kwake kunatokana na nini ambacho mimi na wewe pia tunatakiwa kujua kwani rais ni public figure. Tanzania tumepiga hatua hasa kifo cha JK Nyerere kilitufanya tukomae na kuona kuwa kuna maisha baada ya kiongozi mkuu kutoweka, hivyo sidhani tena kama afya ya rais kujulikana kunatishia usalama wa Taifa, kwani tuliisha pass hiyo test.

Mwaka huu mtasikia mengi
Anayedaiwa mganga wa kienyeji O(mwenye joho) aliyekuwa mkutanoni akiwa chini ya ulinzi wa polisi - Source Global Publishers
4.JPG
 
Kwenye misafara yote ya Kikwete lazima kuna waganga wa kienyeji! Mkulu anawahusudu sana hao ndo maana madaktari wake hawasikilizi
 
Mwaka huu mtasikia mengi
Anayedaiwa mganga wa kienyeji O(mwenye joho) aliyekuwa mkutanoni akiwa chini ya ulinzi wa polisi - Source Global Publishers
View attachment 12756

Ebwanaeee,

Kwa hiyo unataka kuniambia kuna vifantomu vililizidi lile "firewall" la kutoka Mlingotini lililopata kurudufiwa kule Mpanda kwa Mzee Pinda ?

Wabongo kwa ushirikina
 
Jamani hili suala linasikitishs. Baba wa watu anaumwa sana. Hata kama aking'ang'ania mithili ya inzi kufia kwenye kidonda, ukweli utabakia kuwa pale pale kwa Rais Kikwete anaumwa,tena sana. Ingekuwa vizuri akatoa kipaumbele kwa afya yake. Tanzania itabakia kuwa pale pala, Kikwete awepo ua la, awe rais au raia. CCM wakae chini waone huu ukweli kwamba mgombea wao anahitaji huduma ya matibabu na siyo mikikimikiki ya kampeini.
 
Mkuu MS huanzisha mada zake mwenye huwa haingii mada zisizokuwa za kishoga shoga. Sasa maadam mnapenda kusikia matusi ya kishoga na kutiana vidole vya macho, hakuna mtu anayewalaumu wala kuwaingilia. tatizo ni pale ushoga huo unapokuja hata kwenye vijiwe vya wanaume rijal.. na bila shaka sisi tunaweza tofauitisha kati ya mwana-mme/mke na shoga hivyo hatuna makengeza ya hoja. Mtu kesha fungiwa bado tu nyie mnaendelea kwa madai ya MS. jamani acheni Ujinga...
Sijui kama umenielewa kwa lugha yangu.

Ustaarabu kitu cha bure! Kwenye rap battles mtu akianza matusi tunahesabu kashindwa! Unathibitisha kuwa huwa unafatilia mijadala ya MS ila inakuuma pale madongo yanapoanza kurudi.
 
Kama ni kweli basi hali yake ya kiafya si njema kabisa. Mtu huwezi ukawa unaanguka anguka hivyo kama uko na hali nzuri ya afya...

Mkuu umesahau kauli mbiu yako. Ndivyo tulivyo. Rais wa Nigeria alikataa katakata kuachia madaraka wakati alijua fika kuwa atafia madarakani. Mobutu sese seko kukumbengdu wanzala bongo aling'ang'ania madarakani wakati akiwa na terminal Prostate, Rais Eyadema alifia kwenye ndege akiwa rais. Omar Bongo alifia madarakani wakati alijua kuwa amefika hatua ya mwisho kabisa ya Ukimwi. So sioni jipya mzee.
 
C' moon guys this can't be serious? Najaribu kuimagine ingekuwa Marekani raisi aonekane na soksi iliyotoboka kama hivyo, huyu si ndiye watu wanamsifu sana kwamba anapiga pamba za hatari? Halafu ina maana hao UWT hawana hata kitengo cha paramedic?

Soksi haijatoboka kinachoonekana ni vidole vya jamaa wa usalama aliyeko nyuma na yeye kakomaa kubeba angalau unyayo pamoja na kwamba kuna jamaa mbele kashamshika mguu!Anatetea unga wake!
 
Mkuu umesahau kauli mbiu yako. Ndivyo tulivyo. Rais wa Nigeria alikataa katakata kuachia madaraka wakati alijua fika kuwa atafia madarakani. Mobutu sese seko kukumbengdu wanzala bongo aling'ang'ania madarakani wakati akiwa na terminal Prostate, Rais Eyadema alifia kwenye ndege akiwa rais. Omar Bongo alifia madarakani wakati alijua kuwa amefika hatua ya mwisho kabisa ya Ukimwi. So sioni jipya mzee.

Kuna Mwanawasa wa Zambia pia....
 
Back
Top Bottom