GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Amerudi Jukwaani akahutubia kidogo tu kisha akaaga na kuondoka.

Mkutano wa CCM kufungua kampeni Jangwani umwekwisha kwenye saa TISA NA NUSU MCHANA!
 
Inawezekana ikawa ni saumu kutokana na mazingira yaliyopo.

Bila shaka tangu asubuhi alikuwa na kazi nzito za kichama katika kuhakikisha maandalizi yanaenda vizuri.

Pole yake.
 
Du! Naanza kuamini kwamba Jangwani kuna nguvu ya Upako wa Mungu. Atokaye kwa kina Sangoma S/wanga, B/moyo, Tanga na Pemba asitie mguu kamwe
 
hahahaha huyu jamaa si buree wadanganyika atatufia ikulu huyu hahahaha
 
Pamoja na chama kumpunguzia km 58 elf bado ana hofu na dhaifu hivyo?
 
amesononeka roho alipoona watu walio mbele yake wanavyoshangilia katikati ya umasikini unaotokana na ufisadi anaouchekea.

Ndio, amesononeka hadi kuanguka, e Bwana mrehemu kiumbe wako huyu. amen
 
..amerudi jukwaani akahutubia kidogo tu kisha akaaga na kuondoka. Mkutano wa ccm kufungua kampeni jangwani umwekwisha kwenye saa tisa na nusu mchana!
jamaa anumwa wanatuambia swaumu....hwa watu vp bana...asisngizie swaumu
 
Mambo ya bagamoyo hayaendani na swaum!

Aibu kwa kweli
 
hivi kwa nini waislam wengine hawadondoki dondoki wakati wa mfungo??? au wanafunga kinafiki? au wanakula kwa siri??
 
hahahaha huyu jamaa si buree wadanganyika atatufia ikulu huyu hahahaha

Na ikitokea hiyo, basi mkongwe mwingine ataula hapo Ikulu -- Dr Bilal -- kutokana na Katiba yetu. Huyu naye sijui iwapo atadumu muda mrefu.
 
Kama ni kweli basi hali yake ya kiafya si njema kabisa. Mtu huwezi ukawa unaanguka anguka hivyo kama uko na hali nzuri ya afya...
 
huyu kikwete atakuwa nusu mtu, na nusu. ama sivyo anawazuga watu, kwa kuwapima wajinga wake ni kwa kiasi gani wanampenda
 
atakuwa anaelekea milingotini kwa wale mapacha wawili waliorithi kazi ya marehemu baba yao (manake nguvu za giza zitakuwa zimeshamalizwa pale jangwani!!)

Washirikina utawajua tu haya milingotini na kuanguka wapi wapi? Huyu jamaa kazidiwa na kazi tu.
 
Nawashangaa sana CCM! Kwa nini wasitwambie ukweli ? Asiumwe yeye ni nani kwa sababu ni Rais, tukumbuke Rais hakujiumba mwenyewe.
 
hivi kwa nini waislam wengine hawadondoki dondoki wakati wa mfungo??? au wanafunga kinafiki? au wanakula kwa siri??

good question....

na bila shaka katika group ya waliokuwa jangwani kuna wengi tu wana saumu why yeye tu????

kuhusu ikiwa wanafunga kinafiki au wanakula kwa siri sidhani...bali nadhani kuna unafiki kwa kikwete kusingizia saumu kila anapoanguka..

saumu saumu......good scapegoat eehh!!!!!
 
Nawashangaa sana CCM! Kwa nini wasitwambie ukweli ? Asiumwe yeye ni nani kwa sababu ni Rais, tukumbuke Rais hakujiumba mwenyewe.

Tatizo Bi Kirembwe JK sasa hivi wanaCCM wamemsusia amebakia na wanafiki ambao wanamchekea usoni sasa ana majukumu mengi yeye ashughulikie mpasuko ndani kusuluhisha, yeye rais wa nchi na anavyopenda kusafiri basi nako anakutaka waswahili husema mtaka yote ..............
 
Back
Top Bottom