GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Wananchi wenzangu tunaojiuliza 'kulikoni raisi aanguke' naomba tujadili kwa dhati ya mioyo yetu kabisa na tutake majibu mazuri kabisa na kutoa ushauri na wanaopokea ushauri wautendee kazi. Ifike mahali taaluma za watu zifanye kazi na kazi hiyo ionekane. Watu waliopewa dhamana ya kuwa karibu na raisi waache mzaha na mambo ya kawaida tu. This is serious.

Mwaka 1997, Raisi Kikwete alipokuwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alizidiwa ghafla na kuanguka uwanja wa ndege wa Brussels, Ubeligiji akiwa safarini kuelekea nchini Cuba.

Mwaka 2005 katika kampeni, alizidiwa hapo hapo viwanja vya Jangwani Dar Es Salaam na kuanguka ghafla ikabidi kupatiwa huduma ya dharura.

Raisi aliwahi pia kuanguka mjini Mwanza.

Majuzi hivi amepatwa na dharura ya kuishiwa nguvu.

Leo kuanguka tena Jangwani ni tukio la ngapi, la tano, hadharani, hatuna uhakika na ambayo hatujayaona.

Wananchi tulipodai kupatiwa taarifa ya afya ya raisi wetu, baadhi ya watu na watendaji walidhani ni kebehi au kutaka udadisi usiokuwa na sababu, wakasahau kuwa Wananchi ni waajiri wa Raisi na wanapokuwa na wasiwasi juu ya usalama wa afya ya Raisi wao, pia hukumbwa na kiwewe na maneno mengi yakasemwe 'ndivyo sivyo', hatimaye kilio chetu kilisikika, na daktari wa Raisi akazungumza. Kama tulivyo wengi, na mapokeo yalikuwa mengi, wapo waliohoji undani wa ripoti ile kuwekwa hadharani na wapo waliohoji ni kwa nini ifichwe.

Wanaotunyima kujua hali ya afya ya raisi wanashindwa kuelewa kuwa wanajidanganya wenyewe, wanatudanganya sisi na wanamdanganya raisi, mwishowe tumebabaishwa tu.

Mimi si daktari wala mshauri wa Raisi, ila kwa mtizamo wangu na kwa vigezo vya fani yangu, nitasema Raisi anahitaji Mtaalamu wa Saikolojia. That's what he needs right now. Nifafanue. Mtu yeyote anapokumbwa na tatizo ambalo ni vigumu kulikabili (out of control) mara nyingi tatizo hilo huwa kama jinamizi kwake, na aghalabu jinamizi ni hali ya kuteseka kisaikolojia kwa woga na hofu ilyiopindukia (exaggerated fear), hii hutokea punde tu unapokuwa katika mazingira yale au yanayofanana na yaliyosababisha ukapatwa na tatizo uliloshindwa kulikabili. Hivyo ni dhahiri kuwa utakapokwenda kwenye eno lile lile, utakumbwa na mfadhaiko na woga na hofu yako itakutawala na utajikuta umeangukia tatizo lile llile (succumb to the same problem). Hali hii ndiyo inayowapata hata watu wenye kifafa, akiwa katika mazingira fulani ndipo anaanguka au kuweweseka. Linawapata pia watu wenye phobia. Na tTatizo la saikolojia kuliondoa linahitaji mtaalamu wa Saikolojia.

Nimemaliza!

N kuanzia sekunde hii .... tumekuteua wewe uwe daktari wake wa saikolojia. Akianguka tena utakoma!
 
Fake, fake, fake....
Nchi inaongozwa kama mchezo wa mieleka.
Hatutakiwi kujadili tukio la kudondoka kwa bwana mkubwa.
Kwa sababu kudondoka mtu yeyote anaweza dondoka.

Hawa jamaa hawana la kutuambia coz hakuna la maana walilofanya.
So mimi nina imani kuwa ishu kama ile ya kudondoka inapangwa kwa makusudi ili tu watanzania wasahau ya maana na kukaa wakitafakari na kujadili yasio na umuhimu kama thread hii inavyofanya.

Tunachotakiwa ni kusahau kudondoka kwa Mkuu na kuendelea mbele na kuhoji nini madiwani, wabunge na Rais wamekifanya ili kujikwamua kutoka ktk baa la umasikini.
Na si kukaa kujadili sijui Jangwani kuna upako, au sijui ooh walitakiwa wamuache palepale chini wasimuinue, au sijui alvyoanguka aliangukia kisogo.

Hayo yoote hayana umuhimu.
Watanzania msipumbazwe tena, kumekucha sasa kueni macho na watu wanaochezea akili zenu.

Tumeshashuhudia hawa jamaa wakituongoza kwa style ya skendo kila kukicha.

Mfano:
Wiki hii tunafuatilia swala la Richmond.
Basi watanzania woote akili zetu na mijadala yote inakuwa juu ya Richmond.

Kisha kabla Richmond haijapatiwa ufumbuzi wanafumua la Kagoda.

La kagoda halijaisha wanafumua ufisadi ktk stendi ya mkoa iliyopo hapa Dar.

La stendi ya mkoa halijaisha wanafumua EPA.

La EPA halijaisha wanakurupusha la vijisenti,

Vijisenti halijaisha linakuja la mahakama ya Kadhi.

La Kadhi halijaisha linakuja la Yona na Mramba kupandishwa kizimbani.

Hilo nalo halijaisha linakuja la serikali ya mseto ya wazanzibari.

Kama hiyo haitoshi linapandishiwa jingine la Liyumba wa BOT.

Mara linakuja lingine, mara lingine, mara lingine.......

Na mpaka leo hii watanzania hawajui hata waanzie wapi.

Watanzania hizi danganya toto mpaka lini?
Amkeni jamani hawa jamaa wanawachezea akili jamani...chonde chonde

Ni aibu kwa chama kama CCM kuzindua kampeni kisha kushindwa kutoa mikakati yake ijayo.
 
Haya hapo kwenye mguu judge fo yo self....
 
Attachments

  • kikwete.jpg
    kikwete.jpg
    51.6 KB · Views: 80

hoja FAKE
 
Alinifurahisha alivyorudi ulingoni kwa mara ya pili.Nilimuona kama mcheza mpira fulani mashuhuri. hata kupepesuka au kuyumba au hata kuanguka.Unasimama na kuendelea na mapambao.Ipo hiyo wa JF. JK anatisha. fagilia waaa waaaa..Na bado hawamuwezi tena.ni kwa kishindo tu hiyo ndiyo dawa.
any way.mlitaka aseme sera zake ni kipi atafanya awamu ijayo ili muige.si umesikia akisema,wengine kazi yao kutoa copy.kwa maana nyingine wanajikongoja.muacheni hadanganyiki.waanze na wao hao wanaompinga tuone kama wana nyimbo. pengine wana ngonjera tu mmmmm.:clap2:
 
Sidhani kama kwa sasa tunahitaji kuuliza maswali mengi juu ya afya ya Rais Kikwete - ina maana kwamba, "Jakaya Kikwete ni Mgongwa". Huu ndio ukweli unaoweza kupatikana kutokana na ushahidi wa wazi; na historia itahukumu hivyo!

Tukiachana na propaganda za siasa, za eti Rais Kikwete yupo "physically fit = timamu kiafya" tutakuwa tunajidanganya ilhali yu-mgonjwa na anahitaji utabibu makini na wa kina. Mwanzo ilikuwa 1997 (Brussels - Ubeleji), ikawa Jangwani (Desemba, 2005), ikatokea Mwanza (alipoishiwa nguvu) na sasa Agosti, 21, 2010 (Jangwani)....lazima tukubali kwamba, "KIKWETE NI MGONJWA". Inafahamika kwamba viongozi wengi wa Afrika na hata dunia afya zao hufichwa sana...ili kutokutoa nafasi kwa wapinzani wao kisiasa kutumia ugonjwa wao kama "fimbo ya kisiasa" [yametokea Nigeria kwa Oumaru Yar'adua hadi alipokufa ndipo hali yake ilipojulikana].

Juu ya afya ya JK, kwa nini suala lake lisiwekwe hadharani na kama kuna mabingwa wa tiba (hata tiba mbadala) waweze kumsaidia? Wapo wanaosema eti ni msongo (stress)...sidhani kama ni msongo! Wapo wanaodai kwamba anafanyakazi sana...! Eti! Kama kufanya kazi sana, wapo wanaofanyakazi sana na tena ngumu na kulala hoi bin taabani na kukicha wapo juani wakitafuta "shilingi"...na wapo wanaodai eti Rais Kikwete alizidiwa kwa sababu ya kufunga (swaumu) Ramadhan! Nashangaa, tena nashangaa sana.....kwa mujibu ya mafundisho ya Uislam - Mtume Muhammad [saw] amesema, "FUNGENI MPATE AFYA"; na hakika mtu anayefunga kwa kawaida anapata afya ya akili na kiwiliwili na si kuanguka!

Kwa maana hiyo, anguko la JK haliwezi kunasibishwa na aidha kufunga au kufanyakazi kwa muda mrefu...na hata mazingira (yawe ya joto na au baridi) kwa ujumla lazima tukubali kwamba Rais wa Nchi (na mgombea wa CCM kwa tiketi hiyo) anaumwa na anahitaji utabibu makini na wenye tija kwake na si utashi wa kisiasa.

Nadhani si vema kwa wasaidizi wa rais (wataalamu wa afya ya mwili na akili) kuficha matatizo yanayomsumbua Rais Kikwete kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka haki ya kiongozi huyo ya kupata nafuu juu ya hali yake. Haitakuwa vibaya kwao (wataalamu wa afya ya mwili na mwili) kama wakitoa ushauri weledi kwa wanasiasa wanaomzunguka JK ili kuondoa fedheha inayoweza kuwakuta pale ukweli utakapojionesha wenyewe...! Japokuwa ni nadra sana kwa wataalamu (hususan wa dunia ya tatu) kutoa ushauri "mgumu" juu ya hali ya afya ya kiongozi wa juu kama JK, bado ipo nafasi ya kufanya hivyo ili kutoa nafasi kwa wapambe wa kisiasa wanaomtumia JK kama mtaji wa kisiasa kufanya kazi ya ziada na "kumpumzisha" mgombea huyo!
 
Fake, fake, fake....
Nchi inaongozwa kama mchezo wa mieleka.
Hatutakiwi kujadili tukio la kudondoka kwa bwana mkubwa.
Kwa sababu kudondoka mtu yeyote anaweza dondoka.

Hawa jamaa hawana la kutuambia coz hakuna la maana walilofanya.
So mimi nina imani kuwa ishu kama ile ya kudondoka inapangwa kwa makusudi ili tu watanzania wasahau ya maana na kukaa wakitafakari na kujadili yasio na umuhimu kama thread hii inavyofanya.

Tunachotakiwa ni kusahau kudondoka kwa Mkuu na kuendelea mbele na kuhoji nini madiwani, wabunge na Rais wamekifanya ili kujikwamua kutoka ktk baa la umasikini.
Na si kukaa kujadili sijui Jangwani kuna upako, au sijui ooh walitakiwa wamuache palepale chini wasimuinue, au sijui alvyoanguka aliangukia kisogo.

Hayo yoote hayana umuhimu.
Watanzania msipumbazwe tena, kumekucha sasa kueni macho na watu wanaochezea akili zenu.

Tumeshashuhudia hawa jamaa wakituongoza kwa style ya skendo kila kukicha.

Mfano:
Wiki hii tunafuatilia swala la Richmond.
Basi watanzania woote akili zetu na mijadala yote inakuwa juu ya Richmond.

Kisha kabla Richmond haijapatiwa ufumbuzi wanafumua la Kagoda.

La kagoda halijaisha wanafumua ufisadi ktk stendi ya mkoa iliyopo hapa Dar.

La stendi ya mkoa halijaisha wanafumua EPA.

La EPA halijaisha wanakurupusha la vijisenti,

Vijisenti halijaisha linakuja la mahakama ya Kadhi.

La Kadhi halijaisha linakuja la Yona na Mramba kupandishwa kizimbani.

Hilo nalo halijaisha linakuja la serikali ya mseto ya wazanzibari.

Kama hiyo haitoshi linapandishiwa jingine la Liyumba wa BOT.

Mara linakuja lingine, mara lingine, mara lingine.......

Na mpaka leo hii watanzania hawajui hata waanzie wapi.

Watanzania hizi danganya toto mpaka lini?
Amkeni jamani hawa jamaa wanawachezea akili jamani...chonde chonde

Ni aibu kwa chama kama CCM kuzindua kampeni kisha kushindwa kutoa mikakati yake ijayo.
naona na wewe umeleta ya kwako ili tuache kuhofia afya ya mkuu wanchi

sawa bana
 
Alinifurahisha alivyorudi ulingoni kwa mara ya pili.Nilimuona kama mcheza mpira fulani mashuhuri. hata kupepesuka au kuyumba au hata kuanguka.Unasimama na kuendelea na mapambao.Ipo hiyo wa JF. JK anatisha. fagilia waaa waaaa..Na bado hawamuwezi tena.ni kwa kishindo tu hiyo ndiyo dawa.
any way.mlitaka aseme sera zake ni kipi atafanya awamu ijayo ili muige.si umesikia akisema,wengine kazi yao kutoa copy.kwa maana nyingine wanajikongoja.muacheni hadanganyiki.waanze na wao hao wanaompinga tuone kama wana nyimbo. pengine wana ngonjera tu mmmmm.:clap2:

Karibu tena mkuu
 
......ishu sio kwamba wasanii wanakikubali CHAMA ..... JK ameshaongea na don wa wasanii ..CLOUDS ...hakuna msaniii ambaye CCM itamtaka akatumbuize imkose....wanawalipa vizuri...na wanawapa deal nyingine ie malaria no more!!!

...siku wakipanda chadema au CUF ....kama kuna msanii atakayedhubutu kupanda basi ni wale ambao ....wameshajitoa muhanga......kama kina mkoloni,john walker,etc ambao hawapo kwenye ufalme wa ruge na kusaga!!

Ni sehemu ya zile 50bn za kampeni
 
Kwa hoja zako ushauri na mtazamo unaonekana una mapenzi mema na Rais wetu. Nadhani akisoma hili atalifanyia kazi.
Wananchi wenzangu tunaojiuliza 'kulikoni raisi aanguke' naomba tujadili kwa dhati ya mioyo yetu kabisa na tutake majibu mazuri kabisa na kutoa ushauri na wanaopokea ushauri wautendee kazi. Ifike mahali taaluma za watu zifanye kazi na ionekanemk. Watu waliopewa dhamana ya kuwa karibu na raisi waache mzaha na mambo ya kawaida tu. This is serious.

Mwaka 1997, Raisi Kikwete alipokuwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alizidiwa ghafla na kuanguka uwanja wa ndege wa Brussels, Ubeligiji akiwa safarini kuelekea nchini Cuba.

Mwaka 2005 katika kampeni, alizidiwa hapo hapo viwanja vya Jangwani Dar Es Salaam na kuanguka ghafla ikabidi kupatiwa huduma ya dharura.

Raisi aliwahi pia kuanguka mjini Mwanza.

Majuzi hivi amepatwa na dharura ya kuishiwa nguvu.

Leo kuanguka tena Jangwani ni tukio la ngapi, la tano, hadharani, hatuna uhakika na ambayo hatujayaona.

Wananchi tulipodai kupatiwa taarifa ya afya ya raisi wetu, baadhi ya watu na watendaji walidhani ni kebehi au kutaka udadisi usiokuwa na sababu, wakasahau kuwa Wananchi ni waajiri wa Raisi na wanapokuwa na wasiwasi juu ya usalama wa afya ya Raisi wao, pia hukumbwa na kiwewe na maneno mengi yakasemwe 'ndivyo sivyo', hatimaye kilio chetu kilisikika, na daktari wa Raisi akazungumza. Kama tulivyo wengi, na mapokeo yalikuwa mengi, wapo waliohoji undani wa ripoti ile kuwekwa hadharani na wapo waliohoji ni kwa nini ifichwe.

Wanaotunyima kujua hali ya afya ya raisi wanashindwa kuelewa kuwa wanajidanganya wenyewe, wanatudanganya sisi na wanamdanganya raisi, mwishowe tumebabaishwa tu.

Mimi si daktari wala mshauri wa Raisi, ila kwa mtizamo wangu na kwa vigezo vya fani yangu, nitasema Raisi anahitaji Mtaalamu wa Saikolojia. That's what he needs right now. Nifafanue. Mtu yeyote anapokumbwa na tatizo ambalo ni vigumu kulikabili (out of control) mara nyingi tatizo hilo huwa kama jinamizi kwake, na aghalabu jinamizi ni hali ya kuteseka kisaikolojia kwa woga na hofu ilyiopindukia (exaggerated fear), hii hutokea punde tu unapokuwa katika mazingira yale au yanayofanana na yaliyosababisha ukapatwa na tatizo uliloshindwa kulikabili. Hivyo ni dhahiri kuwa utakapokwenda kwenye eno lile lile, utakumbwa na mfadhaiko na woga na hofu yako itakutawala na utajikuta umeangukia tatizo lile llile (succumb to the same problem). Hali hii ndiyo inayowapata hata watu wenye kifafa, akiwa katika mazingira fulani ndipo anaanguka au kuweweseka. Linawapata pia watu wenye phobia. Na tTatizo la saikolojia kuliondoa linahitaji mtaalamu wa Saikolojia.

Nimemaliza!
 
2yz9yxh.jpg

Ha ha ha
Mkuu Nyambala, the guys wa PSU are so distinct utawaona bila kuuliza
1 Kaunda suit nyeusi au kijivu
2 wanamapanki
3 wote viuno vimetuna(silaha)
4 kutokana na mazoezi nafikiri wote ni weusi tii
Bahati mbaya kuna wenye vitambi uchwara, wangeshauriwa wabadili muonekano, you can smell them a mile away.

Yaani wala hazijifichi Mkuu. Ukiangalia hiyo picha kwenye viuno ziko nje nje. Hivi bado wana mtindo wa kuzichomeka kwenye chupi/boxer?
 
Nimepima. Kama unaniuliza kama nimepima hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI, ndio.

Ila hapa Mganyizi hajazungumzia kupata ushauri wa kupima virusi vya UKIMWI Angaza. Anazungumzia ushauri wa afya ya kisaikolojia. Hiyo bado sijapima kwa sababu sijapatwa na hali inayohitaji huduma hiyo.

Itakapotokea nitapima pia

Asante kwa ushauri
 
Nakubaliana na wewe kuwa CCM watazipata kura, wote waliohudhuria Jangwani leo wawe chadema au cuf au independent watajikuta wanaipigia CCM kura, manake muungwana kwa kuanguka kwake kamaliza kila kitu.
ICHONDI

Sidhani kama JK kajiangusha, wewe hufikirii mfedheheko alioupa, kama kuanguka ni staili ya kupata kura basi na Mwanza nako aanguke apate kura za wasukuma au simple awe anaanguka kila mkutano ili apate nyingi.
 
Kuna kitu kimejificha katika hali halisi ya afya ya rais wetu na hii si haki kwa wapiga kura, inatakiwa tuelezwe kinaga ubaga kwamba ana matatizo gani kuhusu afya yake? Alidondoka jangwani wakati wa kufunga kampeni hapohapo, alianguka Mwanza alipoalikwa na maaskofu. Ingekuwa vyema wasemaji wa chama hiki watuambie ukweli ikizingatiwa kwamba rais wa nchi ni mtaji wa nchi tunatumia gharama nyingi sana katika chaguzi hizi sasa inapotokea tunawekeza kwenye afya yenye utata kwa kweli sio haki kwa uchumi wetu na maendeleo ya nchi.
 
VIJANA JAZZ BAND...NAO WALITUMBUIZA....ukiacha kina BITCHUKA.....NA WENGINE KIBAO....KWA KWELI WASANII WENGI WANAKIKUBALI HIKI CHAMA.........aaaaaahh nilitaka kusahau.. CHEGE NA MHESHIMIWA TEMBA NAO WALIKUWEPO HASA NYIMBO YAO YA MKONO MMOJA WEKA JUU...WEKA JUU....... it was colourful day for CCM SUPPORTERS.......!
Wengine tunajadili afya ya rais wetu wewe huna hata habari unaongelea Jazz band tuuuuu kwani walikwenda kushindana ugobogobo jangwani. Nyie ndio huwa hammtakii mema rais huku mkijidai mnampenda.

Eti it was colourful day, colourful day wakati mtu analamba mchanga tena mhusika mkuu wa mkutano, angekuwa mwingine basi, you must be joking.
 
Mwaka 1990 Papa John Paul II aliendesha Ibada takatifu katika eneo hilo hilo la Jangwani na kulifanya eneo hilo kuwa sehemu takatifu. Hivyo inaonekana muuza sura amezoea kubeba madudu mfukoni anapokwenda pale ambayo kimsingi hayakubaliki kutokana na Imani ya pale.
 
Suala la afya huwa ni la mtu binafsi si la kisiasa.unaga ubaga ni katika sera zake tu.Hilo ndilo linamuhusu mpiga kura.
Kuna kitu kimejificha katika hali halisi ya afya ya rais wetu na hii si haki kwa wapiga kura, in kutoaatakiwa tuelebazwe kinaga ubaga kwamba ana matatizo gani kuhusu afya yake? Alidondoka jangwani wakati wa kufunga kampeni hapohapo, alianguka Mwanza alipoalikwa na maaskofu. Ingekuwa vyema wasemaji wa chama hiki watuambie ukweli ikizingatiwa kwamba rais wa nchi ni mtaji wa nchi tunatumia gharama nyingi sana katika chaguzi hizi sasa inapotokea tunawekeza kwenye afya yenye utata kwa kweli sio haki kwa uchumi wetu na maendeleo ya nchi.
 
Back
Top Bottom