GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

That could very well be their dress code...now I don't know how you would call it...is it business casual, business professional, or casual? For sure it is not casual....

Hahaha ahahah ahaha !!!!!!!!!!!!!!!!!! Sasa hapo dhana ya secret service si inapotea kabisa, a sniper will be excecuting their job kirahisi kabisa..........................
 
Hahaha ahahah ahaha !!!!!!!!!!!!!!!!!! Sasa hapo dhana ya secret service si inapotea kabisa, a sniper will be excecuting their job kirshisi kabisa..........................

Inapotea kivipi?

Maana nadhani wanatakiwa wavae according to the occasion au sivyo?
 
Down in the memory lane kuna watu waliliona hili, suprisingly bado kuna watu wanajiuliza akianguka tena daktari atasemaje?
Rais Kikwete akianguka tena daktari atasema nini?


Ansbert Ngurumo​

Source: Tanzania daima - Oct. 11, 2010 - Bofya hapa

NAANDIKA kwa uangalifu mkubwa kwa sababu mada yenyewe ni nyeti, kuhusu mjadala uliotawala wiki hii juu ya afya ya Rais Jakaya Kikwete, hata baada ya ofisi yake kujitetea na daktari wake kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari. Wananchi wamekataa kunyamaza. Kwa nini?

Ni vigumu kuwanyamazisha watu, na si vema kuwanyamazisha, wanapojadili suala gumu na zito kama hili. Na hapa si tu kwamba wanajadili, bali wanamjali rais wao; na wanaipenda nchi yao.

Na katika hili hatugombani na rais hata kidogo. Tunamfariji. Rais ni mgonjwa kwa daktari wake; ni kiongozi kwa wananchi wake. Ingawa ugonjwa wa rais ndiyo ajira ya daktari wake, naamini kwamba sote, na daktari akiwamo, tunaguswa sana na msukosuko wa kiafya unaomgusa rais kwa namna yoyote ile.

Na inapofika mahali ofisi ya kiongozi mkuu wa nchi ikatoa idhini kwamba daktari wake azungumze hadharani kuhusu afya ya mgonjwa wake, ujue kuna tatizo kubwa. Lakini kubwa ninaloliona hapa ni kwamba kisaikolojia rais amefedheheshwa na matukio ya kuzidiwa na kudondoka hadharani pamoja na lile la kuishiwa nguvu hivi karibuni jijini Mwanza, na njia mojawapo ya kuyakabili na kupunguza porojo juu ya afya yake ni kufanya hiki walichofanya wiki hii.

Binadamu yeyote mwenye akili timamu na moyo wa utu, atamuonea huruma rais wetu, atamtakia mema na hata kumwombea apone (hata kama wanatuambia hana tatizo). Ndivyo tunavyofanya sasa. Lakini kuna jambo la ziada.

Tuna ugomvi na wasaidizi wa rais. Hatuwezi kuwaa cha wamdhalilishe na kumfedhehesha kiongozi mkuu wa nchi, halafu wakatoa taarifa za kujisafisha. Wakitaka kutoa maelezo rasmi wajiandae vizuri zaidi.

Katika blogu yangu ya Kiingereza (Let's Face It) nimelijadili suala hili kwa kifupi, nikisisitiza kwamba kiongozi wa nchi hapaswi kuzidiwa na kuanguka hadharani; na nikatoa mifano ya wachache waliovunja kanuni hii, Rais Kikwete akiwamo.

Nimedokeza pia kwamba kuzidiwa kwa Rais Kikwete Jumapili iliyopita akiwa anahutubia umati wa waamini wa Kanisa la African Inland (AIC), Mwanza, lilikuwa tukio la tatu ninalokumbuka kumpata hadharani ndani ya miaka 12.

Alipokuwa waziri wa mambo ya nje ya ushirikiano wa kimataifa, aliwahi kuzidiwa ghafla mwaka 1997 katika uwanja wa ndege wa Brussels, Ubelgiji, akiwa njiani kuelekea Cuba. Ilibidi alazwe kwa saa nane kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari.

Tunakumbuka pia kilichomtokea mwaka 2005, siku moja kabla ya uchaguzi mkuu; alipozidiwa ghafla na kudondoka kutoka jukwaani, akakatiza hotuba yake katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam. Viongozi waandamizi waliokuwapo, wanausalama, wanahabari na wananchi waliokuwa uwanjani na hata waliokuwa wanafuatilia katika redio na runinga, walipatwa na mshtuko mkubwa.

Baada ya ‘mgonjwa' kupewa huduma hospitalini, aliweza kuzungumza na vyombo vya habari akiwa nyumbani kwake, akasema alianguka kwa sababu ya uchovu wa kampeni, na kwa kuwa siku hiyo alikuwa amefunga. Naamini tukio hilo lilimpatia pia ‘kura za huruma.'
Sijui tukio jingine la kuanguka kwake hadharani au faragha, lakini hili la Mwanza la juzi, lilikuwa la tatu. Kwa serikali iliyo makini, na kwa wahudumu wanaotaka tuwaamini kwamba wanatimiza wajibu wao katika kumhudumia kiongozi mkuu wa nchi, tukio la Mwanza lilipaswa kuepukwa.

Wanaofanya kazi kwa karibu na rais wamekuwa wakisimulia jinsi ambavyo katika miezi yake ya awali ya utawala wake, alikuwa akipatwa na hisia mbaya kila alipokumbuka anguko la jangwani.

Fedheha ya kuanguka hadharani ilimnyima imani ya kujiamini mbele ya umma, kiasi kwamba alikuwa akizungumzia mara kwa mara kwa utani ili kuliondoa kwenye hisia chafu.
Miaka minne baadaye, linapomtokea tukio jingine linalofanana na hili katika mazingira ya jukwaani mbele ya umma, linamtonesha vidonda na kumdhuru kisaikolojia. Kujiamini kunatoweka tena.

Hawezi kusema hadharani, lakini sasa hivi rais anapaswa asaidiwe kuondokana na hofu ya kusimama hadharani.
Baada ya yote yaliyotokea, haitoshi kauli ya dakatri wa rais kwamba "tumejifunza, na tunaahidi kuwa waangalifu zaidi" inaeleza kwamba anatambua kosa lake na wenzake, lakini haitoshi.

Wanapaswa wafanye jambo la ziada la kumuimarisha rais mwenyewe kimwili na kisaikolojia. Bila hivyo, ataanguka tena, na tutaambiwa "hana tatizo la kiafya."
Haitoshi kabisa kusema kwamba rais hana tatizo lolote la kiafya, bali uchovu pekee ndio umesababisha matukio yote hayo.

Tunavyojua, kwa kawaida, watawala na wanajeshi hawaanguki hovyo hovyo - tena hadharani. Si kawaida, ni aibu, na haitarajiwi kwa watawala na wanajeshi kuzidiwa na kuanguka hadharani.

Inakuwaje Amiri Jeshi Mkuu, mtawala na mwanajeshi kitaaluma azidiwe na kudondoka mara kadhaa, halafu wasaidizi wake wanacheka cheka na kusema hakuna tatizo? Wanamdanganya yeye au wanatudanganya sisi?

Si tu rais ni mwanajeshi, bali anatunzwa kama mtoto - anakula vizuri, anapimwa afya kila mara, analala pazuri, anasafiri kwa raha katika daraja la juu kwenye ndege, anafunguliwa hata mlango wa gari, anapangiwa ratiba ya kazi, anapangiwa hata muda wa kulala.
Ndiyo, anafanya kazi zinazoweza kumchosha akili lakini hayuko peke yake.

Rais wetu si dhaifu kama wananchi wake ambao wengi wanalalala au kushinda njaa; wanapata mlo mara moja moja (na wenyewe haujakamilika virutubisho); wanafanya kazi nzito na ngumu zinazokula nguvu ya mwili na akili; wana pato duni sana (chini ya shilingi 1000 kwa siku); wanakabiliwa na magonjwa hatari na hawana huduma ya matibabu inayoeleweka na inayoaminika; wanaishi katika mazingira hatari; wanakabiliwa na magonjwa sugu kwa miaka mingi; wanatembea kwa miguu au baiskeli, bajaji au wanasafiri kwa malori na mabasi mabovu; hata kwa wanaosafiri kwa ndege, wanatumia madaraja ya chini yanayochosha; wanalala kwa saa 2 au tatu kila siku; wanasumbuliwa na umaskini wa kutisha kiasi kwamba kila wanapolala hawana tumaini kama wataiona kesho.

Watanzania hawa hawazimii, hawaishiwi nguvu wala hawaanguki, aanguke rais mwenye afya isiyotetereka (kama tulivyoelezwa) na mwenye matunzo ya viwango vya juu? Hapa ndipo kuna swali kuu ambalo daktari wa rais, Dk. Peter Mfisi, hajalijibu.

Na ingawa tunajua kuwa afya ya mgonjwa ni siri yake na daktari wake, kwa kuwa Dk. Mfisi amepewa ruhusa na mteja wake (rais) kutangaza taarifa hiyo, alipaswa kujua kwamba ripoti yake ingeibua maswali mengine yaliyofichika.

Kwanza, wapo wanaosema amekwenda mbali kuliko alikopaswa; kwamba ingetosha tu yeye kutoa tamko kwamba rais anaumwa nini, au kwamba haumwi bali amezidiwa kutokana na uchovu tu.

Kauli hiyo pekee kutoka kwa daktari wa rais ingekuwa na uzito wa kutosha, na labda ingeibua maswali machache zaidi.

Pili, uungwana wa kawaida unatulazimisha kukubaliana na daktari, maana sisi hatuna taarifa za ziada. Lakini kwa kuwa daktari na mteja wake wamewasiliana na sisi kwa kutumia taarifa ya kisiasa kupitia vyombo vya habari; wala hakuna mwanahabari au mwana taaluma mwingine aliyeonyeshwa faili la afya ya rais, wananchi wana haki ya kuendelea kujadili suala hili na kuhoji maswali zaidi, hata yanayoudhi. Tusiwachukie. Tuwavumilie.

Hili la kuchoka na kuzidiwa si kosa binafsi la rais, bali ni la wasaidizi wake, ingawa naye ana uamuzi wa kufanya au kuacha jambo lolote analopangiwa. Washauri wa rais katika fani mbalimbali lazima walinde heshima yao kwa kuzingatia kwamba wao ni wataalamu wa maeneo husika.

Rais anapaswa awasikilize wao wanapomshauri kwa kuwa ndio wataalamu aliowateua au aliokabidhiwa. Ni makosa makubwa rais kudhani kwamba wataalamu waliomzunguka ni matarishi wa kumbebea mafaili na kuimba vibwagizo vyake kwa madhumuni ya kisiasa.
Yeye mwenyewe amekiri kwamba walimshauri akawagomea. Tungetarajia mambo mawili: kwanza, wataalamu hao wangelinda heshima ya taaluma zao kwa kujiuzulu kazi, kwa sababu hawana sababu ya kufanya kazi ya kumshauri kiongozi asiyeshaurika. Hawana kazi ya kufanya Ikulu.

Pili, baada ya tukio la Mwanza, rais alipaswa awawajibishe, kwamba wameshindwa kummudu na kumlindia afya na heshima mbele ya umma. Bahati mbaya, kama ilivyo kawaida yake, badala ya kuwawajibisha kwa kumfedhehesha, amewatetea! Wamepata bahati ile ile wanayofaidi mafisadi wanaocheka vizuri na wakubwa - kulindwa.

Matarajio yetu ni kwamba wasaidizi wamejifunza, lakini wajue bado wananchi wanahoji: Kama rais ni mzima kiasi tulichoelezwa, mbona anazidiwa na kuanguka? Kama ni uchovu tu, na kama wanasema wamejifunza, watatuambia nini iwapo rais atazidiwa tena hadharani kwa mara ya nne?
 
Inapotea kivipi?

Maana nadhani wanatakiwa wavae according to the occasion au sivyo?

From the security point of view they just need to appear normal just like everybody else. Kuvaa according to occasion ni sawa lakini hawa jamaa ni Kaunda suti kila mahali nimeshawaona na hizo kaunda suti airport, kwenye misiba anayohudhuria JK, kenye sherehe za ikulu almost everywhere. Kwa mfano katika hiyo picha kwenye post ya kwanza nawafahamu watu kama watatu hivi and tht is wht they have been wearing for years.
 
From the security point of view they just need to appear normal just like everybody else. Kuvaa according to occasion ni sawa lakini hawa jamaa ni Kaunda suti kila mahali nimeshawaona na hizo kaunda suti airport, kwenye misiba anayohudhuria JK, kenye sherehe za ikulu almost everywhere. Kwa mfano katika hiyo picha kwenye post ya kwanza nawafahamu watu kama watatu hivi and tht is wht they have been wearing for years.

What makes you think some of them were not among the crowd wearing regular clothes?
 
2yz9yxh.jpg


Huo mguu wa Kikwete soksi imetoboka kisigino...ni kwamba ana mikasoro chungu mzima, ajiuzulu!
 
What makes you think some of them were not among the crowd wearing regular clothes?

Maybe on this one but I have been on events sometimes in the past ambapo nakuwa nawafahamu watu karibu wote except the ones in Kaunda suit!
 
Unajua huo mguu sikuuona aisee

Halafu yaani hakukuwa hata na stretcher ya kumbebea? Shameful..

C' moon guys this can't be serious? Najaribu kuimagine ingekuwa Marekani raisi aonekane na soksi iliyotoboka kama hivyo, huyu si ndiye watu wanamsifu sana kwamba anapiga pamba za hatari? Halafu ina maana hao UWT hawana hata kitengo cha paramedic?
 
C' moon guys this can't be serious? Najaribu kuimagine ingekuwa Marekani raisi aonekane na soksi iliyotoboka kama hivyo, huyu si ndiye watu wanamsifu sana kwamba anapiga pamba za hatari? Halafu ina maana hao UWT hawana hata kitengo cha paramedic?

Namna hii kweli watu wataona umuhimu wa kuwa na paramedics vijijini, lakini anywayz stretcher kwani ni sh ngapi? Sema usikute kwa mitizamo ya kibongo waliona kumuweka kwenye stretcher itakuwa na madhara politically. Maana ingeonyesha how serious the situation was.
 
C' moon guys this can't be serious? Najaribu kuimagine ingekuwa Marekani raisi aonekane na soksi iliyotoboka kama hivyo, huyu si ndiye watu wanamsifu sana kwamba anapiga pamba za hatari? Halafu ina maana hao UWT hawana hata kitengo cha paramedic?

Nyambala...nguo za ndani za watu huwaga ni siri yao kwa kweli maana unaweza ukamwona dada mrembo, maridadi, na mwenye madaha huku ndani kavaa chupi kuukuu iliyotoboka....
 
Nyambala...nguo za ndani za watu huwaga ni siri yao kwa kweli maana unaweza ukamwona dada mrembo, maridadi, na mwenye madaha huku ndani kavaa chupi kuukuu iliyotoboka....

Yea nimewahi kuona hiyo enzi za UMMISETA
 
Nyambala...nguo za ndani za watu huwaga ni siri yao kwa kweli maana unaweza ukamwona dada mrembo, maridadi, na mwenye madaha huku ndani kavaa chupi kuukuu iliyotoboka....
Mkuu wangu, yawezekana huyo dada kafanya makusudi ili usipate taabu wee hukujua tu!
 
2yz9yxh.jpg


Huo mguu wa Kikwete soksi imetoboka kisigino...ni kwamba ana mikasoro chungu mzima, ajiuzulu!

...mmm, taratibu mkuu! mimi nimeona kama ni kidole kilichojitokeza cha kiganya cha yule sekurity mwenye kisogo mbele ya yule aliyevaa mawani, au??:confused2:
 
.

Watanzania kama niwajuavyo hawawezi kumpa Dr Slaa kura kwa kampeni za namna hii. kukiondoa chama kikongwe kwenye madaraka kunahitaji sera madhubutu. kusuburi Kikwete aanguke ndipo mshangilie sio utamaduni wa mtanzania na hakika chadema mtazikosa kura hivi hivi amini nawaambieni. Uzeni sera mbadala ili tuwaondoe CCM bila hivyo mnapoteza muda

Nakubaliana na wewe kuwa CCM watazipata kura, wote waliohudhuria Jangwani leo wawe chadema au cuf au independent watajikuta wanaipigia CCM kura, manake muungwana kwa kuanguka kwake kamaliza kila kitu . Ile kuanguka ndio njia ya kurelease nguvu za giza, na wote mliokuwa Jangwani nguvu hizo zimewaingia na mtashangaa siku ya kupiga kura usione mgombea mwingien ukajikuta unatia alama ya vyema kwa muungwana. I know watu watacheka sana na kuniona kama mlevi, mshirikina but wale wanaosoma bible watakumbuka hata yesu alivyokuwa anawaoa mapepo watu wenye shida walikuwa wanaanguka, na mapepo yale yalikuwa yanakwenda somewhere, sometimes yaliwaingia nguruwe. Hapo Jangwani kwenye mikutano ya injili watu wenye mapepo wakiombewa wanaanguka wakati pepo lile likitoka linakuwa na nguvu ya ajabu sana. Muungwana alikwa anaachia pepo la kuwaingia maelfu waliokuwa pale, ni energy kubwa sana inatakiwa na ndio maana alidondoka na baada ya dakika kadhaa akarudi jukwani.

Woote mliokuwa Jangwani leo, yamewapata, mtaimba JK hadi October 31. Oyaa chekeni sana wana JF, but believe me JK ni msanii, anajua Dar huenda wakamgeuka, leo kaamua kunyunyiza sumu, na i am sorry to say, imewaingia nyoote lol

Ushauri wangu kwa vyama vya upinzani, wa-avoid wanachama wao na wapenzi kwenda kwenye mikutano ya kampeni ya ccm, mtabadilishwa mawazo si kwa sababu ya sera bali kwa sababu ya sumu ya nguvu za giza!!!
 
CCM yazindua kampeni kwa mshindo mkuu jangwani
Marlaw na kundi lake wakifanya vitu vyao ambapo ule wimbo wa pipi umepigwa remix na kuw ccm ccm ccm..
JK akimalizia hotuba yake baada ya kurejea kupata
huduma ya kwanza kwa kuanguka
Mgombea mwenza Dk Mohamed Ghalib Bilal akihutubia
Rais wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akitia ubani uzinduzi huo
JK akiondoka baada ya kuzindua kampeni
Msafara wa JK ukiondoka jangwani
Sehemu ya umati wa watu uliofika jangwani leo
Rais wa Zanzibar Dk Karume na Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowassa wakiondoka
Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mh. Benjamin Mkapa (nyuma mwenye kapelo ya kijani) wakiondoka
Mgombea mwenza Dk Mohamed Ghalib Bilal akiondoka
 
...mmm, taratibu mkuu! mimi nimeona kama ni kidole kilichojitokeza cha kiganya cha yule sekurity mwenye kisogo mbele ya yule aliyevaa mawani, au??:confused2:

You are right BabaDesi
 
Back
Top Bottom