GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Huyu sindibadi sijui anatatizo gani manake kila kampeni anajipiga chini tu. Apumzoke kwa Amani!
 
Nadhani ana kifafa cha kampeni. Kashaanza kumgwaya Kiboko wa mafisadi Slaa!
 
From the security point of view they just need to appear normal just like everybody else. Kuvaa according to occasion ni sawa lakini hawa jamaa ni Kaunda suti kila mahali nimeshawaona na hizo kaunda suti airport, kwenye misiba anayohudhuria JK, kenye sherehe za ikulu almost everywhere. Kwa mfano katika hiyo picha kwenye post ya kwanza nawafahamu watu kama watatu hivi and tht is wht they have been wearing for years.

Inawezakana ikawa ndiyo dress code yao!
 
ukiangalia hiyo picha utaona makosa mengi mno ya hawa jamaa zetu wa UWT,
1) wote wamejitofautisha kabisa na Target (raisi), dress code yao inatoa mwanya mkubwa kwa snipers kujua nani ni nani, na hapo maana halisi ya bodyguard inapotea, ingekuwa busara kwa baadhi ya hao jamaa kuvaa nguo zinazofanana na Target,

2) ukiangalia hiyo picha, hicho kijiji chote cha UWT kimeconcentrate kwa Mgonjwa, na hakuna hata mmoja anaeangalia upende mwingine wowote, zaidi ya kuangaika kumbeba

3) Afya ya rais nadhani inajulikana zaidi na watu wa UWT, hivi kweli wanaweza kuja hapo au kutembea na raisi bila kuwa na kikosi cha Paramedics?, as far as i know hao jamaa wako trained kumguard huyo Rais, kwa hiyo palipaswa kuwa na kikosi kingine cha UWT ambacho kingefanya kazi hiyo ya kumzoa na kumshughulikia Mgonjwa wakati hao Bodguards wakiendelea na zoezi lao la ulinzi kama kawaida

4) nasema hao jamaa hawako trained kwa first aid, maana kwa ugonjwa wa kuanguka na hicho kiwingu kiasi hata huyo mgonjwa anakosa hata pa kupumulia

4) kunakuwaga na askari mwenye kitambi kikubwa nyuma ya raisi mara nyingi, vipi kwenye hii tukio hakwepo?, maana nadhani yeye ndio angekuwa wa kwanza kumdaka kabla hajafika chini, au yeye ni wa mapambo tu?

Askari mpambe(Aide de Camp) ndio alikuwa wa kwanza kumdaka kikwete kwa nyuma kabla jamaa kuja kumchota miguu sobesombe.Kwa mara ya kwanza nimeona kazi ya huyu askari kumbe nilifanya makosa kudharau uwepo wake maana bila yeye jamaa angejibwaga chini!angalia vizuri kwenye ile video anapoanguka.

Ila nimeshangaa wote wameconcetrate katika kumbeba huku wakimzingia hewa!Ila namsifu kikwete amejitahidi kuweka vijana kwenye timu ya ulinzi.
 
...Ila nimeshangaa wote wameconcetrate katika kumbeba huku wakimzingia hewa!Ila namsifu kikwete amejitahidi kuweka vijana kwenye timu ya ulinzi.

Nadhani lengo lao hasa ilikuwa ni kuficha aibu (kumbeba kuuondoa kwenye macho ya watu na camera).

Uongozi wa CCM wamejigamba ataunguruma Mwanza leo. Kaenda?
 
Pole sana JK. Kama Taifa kuna haja la kubadili katiba na kipindi cha uraisi kuwa kimoja tu cha MIAKA MITANO TU.
 
Naona mwana JF Mzee Wa Manyafu ktk page 26 ya hii topic, amefanya kazi kubwa kurudisha clip inayoonyesha Mh. Raisi Kikwete akianguka ghafla ktk video na pia masikitiko kwa vyombo vingi vya habari kuogopa habari hii.
 
Hawa madaktari wa JK ni wazembe, inakuwaje mkuu anajulikana kuwa ana kisukari na pressure, na amekuwa na tatizo la kuanguka mara kadhaa kwa nini hawampi ushauri mzuri (kama kutokufunga wakati akiwa na shughuli nzito kama hii na pia kumcheck muda mchache kabla ya kupanda jukwaani). Kipimo cha sukari huwa hakichukui hata dk 5.
 
Ulikuwepo. Maana ya kuanguka ni nini? Ana kifafa?

Leo unaweza kumkejeri binadamu mwenzio kwa ugongwa uliompata, kesho unaweza kukuta mungu anampa mtoto, wewe mwenyewe au ndugu yako ugonjwa huo huo (kifafa) ambao unadhani mungu kauleta duniani kwa baadhi ya watu tu na sio wewe, ndugu, jamaa au rafiki zako wa karibu. Tuwe na subira ya kudhihaki afya za binadamu wenzetu.
 
wewe ndio mzembe kweli, Hivi ukirudi jioni toka kazini kwako, alafu unafika home, na walioshinda nyumbani wanakuambia mtoto mmoja mchana alianguka, huwezi kuuliza aliangukaje? na wanasema alikuwa naongea alafu akaanza kurudia rudia maneno na mara kapoteza kauli, akaanza kufaint, huwezi kuwa na wazo la kusema inawezekana maralia, kifafa, nk? Ni jambo la kawaida kufikiri nini kitakuwa kinamsumbua mtu wako wa karibu, na kwa watz Rais ni mtu wetu wa karibu, tunamlipa. Alafu hilo la kusema sijui utazaa mtoto aje awe sijui na nini kwa sababu ulikejeli sijui aliyekuwa na nini, Hivi dunia hii ya dot.com bado mpo mnaoamini hivi????? Kazi kweli kweli
 
JAMANI UPDATE VIPI AMEFIKA MWANZA? huu muda karibu wa kumaliza mkutano hatusikii lolote toka Mwanza.
 
Jamaa huyo hana jipya, anaongea uongo hadharani, hayo ndomatokeo yake.
 
Hawa madaktari wa JK ni wazembe, inakuwaje mkuu anajulikana kuwa ana kisukari na pressure, na amekuwa na tatizo la kuanguka mara kadhaa kwa nini hawampi ushauri mzuri (kama kutokufunga wakati akiwa na shughuli nzito kama hii na pia kumcheck muda mchache kabla ya kupanda jukwaani). Kipimo cha sukari huwa hakichukui hata dk 5.

Mkuu Mkaidi mwenyewe..alipoanguka siku za nyumaalidai alipuuza maelekezo ya madaktari wake waliomwambia asisimani, asi "swaumu" nk.
 
Hili la JK kuanguka mara kwa mara ni hatari kwa mustakabali ya nchi yetu.

Naomba iwe ni mjadala muhimu sana hapa jamii forum maana urais unatuhusu watanzania siyo swala la kifamilia.

Saumu imeanza leo, waislamu wanakawaida ya kufunga lakini hatujasikia hili la kuanguka kama JK halafu mtu anakuja na hoja na dhaifu ya kufunga; ni swala la afya ya mgombea wa nafasi ya uraisi. Nafikiri watazania tuhoji swala hili kwa undani wake maana tusipojua ukweli wake tunaweza kudanganywa kuwa JK yuko fiti, anaweza kuongoza. Nafikiri kama mtu ni mgonjwa hafai kupewa nafasi kubwa ya urais maana anaweza kutupeleka kusikofaa.

Tujadili wagombea katika nyanja zao za maisha

msukosuko wa kiafya au Ugonjwa ungekuwa kigezo cha kumwachisha mfanyakazi sehemu ya kazi baadhi yetu tungekuwa hatuna ajira. Unajuaje labda mimi naumwa ugonjwa wa moyo, shinikizo au ukimwi niachishwe kazi hata kama natekeleza majukumu yangu kazini? Ni unyanyapaa huo? Kanuni ya afya na kazi iko wazi mtu anaombwa kuacha kazi kwa matatizo ya afya baada ya kushindwa kwenda kazini kwa miezi mitatu mfululizo na sio vinginevyo. Rais wa Nigeria aliendelea kuwa Rais hata baada ya kulazwa muda mrefu kule Saudi Arabia.
 
Kazi yako ya kubeba kokoto usilinganishe na kazi ya rais, na afya yako haituhusu ila ya rais inatuhusu, ukifa kwa ukimwi wakati mwingine hata jirani yako asijue. Kwa kutolea mfano wa rais wa Nigeria una maana gani unataka Kikwete afie madarakani au.
 
watanzania na unafiki ndiyo maana hatuna maendeleo sasa hii video ina kitu gani cha ajabu mpaka watu wengine wanaitoa kulinda heshima sijui nini upumbavu nothing graphic at all
 
Back
Top Bottom