GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Kwa mujibu wa Tanzania Daima;
Alipopanda jukwaani na kuanza kuhutubia tena, Kikwete alianza kwa kusema: ¡°Nimefungulia jamani¡*niliishia hapa kwenye¡*naona wamevuruga hotuba yangu¡±
Shida yangu ni hapo mwisho anaposema naona WAMEVURUGA hotuba yangu.Je mh. Rais anahisi kuwa kuna watu walio nyuma ya tukio la yeye kuanguka?Jus thinkin aloud.

Mkuu nilivyotafsiri mimi ni kuwa Jk alikuwa kama amezinduka, kwa hiyo mdomo ulikuwa unaongea tu bila kujua yuko wapi. Alikuwa hajapata fahamu vizuri. Lasivyo asingeweza kusema vile mbele ya mic na kadamnasi ile. Hata hivyo inaonekana alikuwa hakumbuki ameishia wapi kwenye hotuba mpaka alipoambiwa
 
Mwaka ule kule mza alitaka kukabwa na mganga labda safari hatuombei watu wake wa karibu wasije wakataka kufanya ya mganga
 
Yeees
Ndio maana Zanzibar wamesitisha kampeni wakati wa mfungo wa Ramadhani.Hata hivyo mpiganaji anayeanguka na kuinuka kuendelea na vita ni mpiganaji shujaa aliyedhamiria kuendelea na vita na anayejiamini kwa analopigania./
 
Nakubaliana nawewe mkuu,
Hivi JK kwa sasa yuko wapi?
Anafanya nini?
Na hali yake vipi?
Nasikia anaelekea Mwanza kuendelea na kampeni, CCM wanamtumia vibaya rais wangu kina Makamba nafikiri wanasema bora punda ....... lakini mzigo wa tajiri ufike.
 
Inaonekana alianza jisikia vibaya kitambo, anasikika akisema "aisee..." kama anajisikia ovyo, halafu ana pause muda, hajakaa kidogo huyo! Sikiliza kuanzia sekunde ya 25
 
Ndio maana Zanzibar wamesitisha kampeni wakati wa mfungo wa Ramadhani.Hata hivyo mpiganaji anayeanguka na kuinuka kuendelea na vita ni mpiganaji shujaa aliyedhamiria kuendelea na vita na anayejiamini kwa analopigania./
Type yenu ndiyo mnamponza rais kwa vijisifa vya kinafiki nafiki ili uonekane unampenda kumbe unataka kitumbua chako kiendelee kunona kwa mgongo wa mgonjwa.
 
du, ahsante sana wote waliotuletea video katika Youtube..
pole JK. inabidi root cause ya tatizo hili la kuishiwa na nguvu na kudodoka litatuliwe na siasa iondolewe katika afya!!. Dr. Mfisi hebu toa ufafanuzi!!
Ilishaelezwa hapa hapa JF tatizo la JK...
 
Nimeona, asante. I wish ningekuwa naweza kui copy niweke kwenye kabrasha langu
Yaani jana nimeshangaa sana. Nilipiga simu nyumbani kuongea na ndugu zangu. Wakati Rais anapatwa na shida hii hawakufahamu kwani walikuwa safarini, kufika nyumbani jioni wameangalia taarifa ya habari, mimi nikapiga simu nikauliza kama wameona Mh Rais yaliyomsibu wakabaki kunishangaa. Yaani mimi niliye mbali na Tanzania ndio nimewataarifu walioko ndani ya Tanzania!!

Kweli mkono wa CCM mrefu. Ila namshukuru huyu mdau aliyerudisha clip hapa

unaweza copy kama un RealPlayer SP
 
Mkuu nilivyotafsiri mimi ni kuwa Jk alikuwa kama amezinduka, kwa hiyo mdomo ulikuwa unaongea tu bila kujua yuko wapi. Alikuwa hajapata fahamu vizuri. Lasivyo asingeweza kusema vile mbele ya mic na kadamnasi ile. Hata hivyo inaonekana alikuwa hakumbuki ameishia wapi kwenye hotuba mpaka alipoambiwa
Yote hiyo nikutaka kuwaonyesha watanzania kwamba yuko fit vinginevyo hakupaswa kuendelea kuhutubia..
 
Mkuu nilivyotafsiri mimi ni kuwa Jk alikuwa kama amezinduka, kwa hiyo mdomo ulikuwa unaongea tu bila kujua yuko wapi. Alikuwa hajapata fahamu vizuri. Lasivyo asingeweza kusema vile mbele ya mic na kadamnasi ile. Hata hivyo inaonekana alikuwa hakumbuki ameishia wapi kwenye hotuba mpaka alipoambiwa

No - walikuwa wamechanganya changanya kurasa za hotuba, very simply!
 
Kitu kinachowasumbua daima CCM ni kutosema ukweli daima. Kusema ukweli sasa imekuwa kwao mwiko. Wakitaka kujaribu kusema ukweli, basi lazima wanapitia njia za vichochoroni ili wananchi wenyewe waone 'ukweli' wanaotaka uelweke.

Hebu tazama: Baada ya tukio. Mwenyekiti wa kampeni ya CCM Abdulrahman Kinana aliwaambia waandishi wa habari:

"Kwa mujibu wa madaktari wake sababu iliyosababisha tukio la leo ni upungufu wa sukari mwilini na kushuka kwa pressure kwa sababu alikuwa amefunga, baada ya kupatiwa sukari (glucose) aliweza kupata nguvu na kumaliza hotuba yake."

Maana ya maneno haya kwa yeyote anayefahamu masuala ya afya (siyo lazima awe daktari) ni kwamba JK ana kisukari – tena kile cha kushuka ambacho ni very serious. Halafu to complicate matters ana blood pressure – also a serious health condition.

Swali langi ni kwamba kwa nini inawawia vigumu kwa serikali kutamka rasmi, bila kigugumizi, kwamba JK ana kisukari na blood pressure, kitu ambacho kinamsumbua kwa miaka mingi na ndiyo asili ya kudondoka dondoka?

Kufunga swaumu hapa inaingiaje? Mwaka 2005 tuliambiwa pia alikuwa amefunga ingawa haikuwa Ramadhani. Inawezekana ilikuwa ni funga ya Sunna ambayo JK huwa anaitimiza.

Lakini pia kuna kuanguka kule Mwanza katika hafla moja ya Kanisa. Hatukuambiwa kuwa pia alikuwa amefunga (au hata funga ya Sunna) ila tu tuliambiwa kwamba alizidiwa na uchovu wa kazi nyingi na safari ndefu ndefu.

Nafahamu fika kwamba CCM wanashindwa kusema ukweli (kwamba JK ana kisukar/pressure) hasa katika kipindi hiki cha kampeni kwa sababu zilizo wazi – kwamba wananchi watakuwa wanaombwa kumchagua rais ambaye afya yake siyo nzuri.

Lakini ukweli unabakia pale pale -- JK hayuko fiti kiafya – na kwamba CCM hawataki kulikubali hilo. Ukweli na uwazi wa utawala wa CCM uko wapi? Ni kinyume kabisa na kile kile alichotamka JK mwenyewe hapo hapo Jangwani kuhusu mafanikio ya utawala wake katika miaka 5 iliyopita.

Ingekuwa enzi za zamani wakati wa vyombo vya habari vya serikali tu (na chama) ndivyo vinatawala, habari hii isingejulikana na Watz wengi. Wengi labda wangehadithiwa tu na waliokuwapo Jangwani.

Lakini enzi hizi za free press ni vigumu kufunika – pamoja na kwamba serikali imefanya kazi kubwa ya kuvishawishi/kuviamuru baadhi ya vyombo vya habari visiandike habari hizo.
 
Sasa kama Swaumu inamdondosha mtu vipi kama angekuwa mchezaji ligu kuu na acheze mechi ya Simba na Yanga kama ile ilyopita? Atakuwa marehemu siku hiyo! Hapa issue siyo kufunga. Kama wengi wanavyosema...ana tatizo na tatizo lenyewe hatarishi kwa maisha yake.

Nafikiri inabidi watu kuamua kama wanafikiri Bilal anaweza kuongoza taifa kama Goodluck wa Nigeria....Naona nyota ya Bilal inag'aa na inaweza kuwa blessing in disguise!
 
Acha hizo wewe, mtu anaumwa halafu unasifia ujinga badala ya kulaani wao kumrudisha kuongea wakati he was not fit... we hukuona alivyokua anashindwa kupanga hata karatasi??? When he came back, he was disoriented and that was not good

Ushujaa upi unaoutaka wakati mtu anateseke, kama ni ushujaa, basi angekuja na kusema wazi kwamba alizidiwa na aseme ukweli kuhusu hali yake

nimesoma sehemu wanasema huwa anakaidi baadhi ya ushauri wa madaktari... inabidi apate good washauri nasaha

Hili ndiyo tatizo la kuwa na katiba inayompa rais madaraka makubwa, wakati mwingine anajiona yeye ni everything. Kawaida PSU wanakuwa na amri juu ya nini rais afanye kama wanaona akifanya otherwise usalama wake unakuwa matatani. Yaani katika masuala yote yanayo muhusu yeye kiusalama wa mwili wake hapaswi kushauriwa bali kuamriwa.
 
I believe here in JF is where we dare to talk openly. Nimeambatanisha video iliyokuwa imeondolewa ya JK kuanguka jangwani 2010.


IKo wapi Mbona haionekani mkuu?? au Monster kashaipitia?
 
Last edited by a moderator:
Hivi kwa kujaribu kuficha habari ya tukio la Jangwani, maanake yake tatizo ni kubwa kuliko tunavyo liona, na huyo Msemaji wa Kampeni za CCM yupo kwa maslahi ya Tanzania au maslahi Binafsi, maana sioni mchango wake katika maendeleo ya tanzania zaidi ya kusikia kampuni yake imehusika na kusafirisha pembe za ndovu zilizoshkiwa asia.
na pia kwanini tukio limetokea alipo anazungumzia mafanikio katika kupigana na "Rushwa"
 
Kwa mujibu wa Tanzania Daima;
Alipopanda jukwaani na kuanza kuhutubia tena, Kikwete alianza kwa kusema: ¡°Nimefungulia jamani¡*niliishia hapa kwenye¡*naona wamevuruga hotuba yangu¡±
Shida yangu ni hapo mwisho anaposema naona WAMEVURUGA hotuba yangu.Je mh. Rais anahisi kuwa kuna watu walio nyuma ya tukio la yeye kuanguka?Jus thinkin aloud.

Nafikiri alikuwa anaongelea wale waliokuja kumdaka na kumbeba ambao kwa wao umuhimu ulikuwa kwa rais na si makaratasi ya hotuba ambayo watakuwa waliyakusanyakusanya tu bila kuangalia pages. Yeye anajua kabisa kuwa kuanguka kwake kunatokana na nini ambacho mimi na wewe pia tunatakiwa kujua kwani rais ni public figure. Tanzania tumepiga hatua hasa kifo cha JK Nyerere kilitufanya tukomae na kuona kuwa kuna maisha baada ya kiongozi mkuu kutoweka, hivyo sidhani tena kama afya ya rais kujulikana kunatishia usalama wa Taifa, kwani tuliisha pass hiyo test.
 
Back
Top Bottom