Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,809
- 24,451
Duh!!Ni kweli amedondoka madodyguard wa bongo ni wa hovyo wamemwacha hadi mzee mzima analamba mchanga badala ya kumwahi asidondoke jumla!
Ingawa mimi siyo shabiki sana wa K. Kwete tangu avunje ahadi aliyoniahidi mwaka 2005 ya ari mpya, nguvu mpya na maisha bora kwa kila mtanzania, lakini bado namheshimu sana kama kiongozi wa taifa langu. Hao walinzi wake inabidi waadabishwe kama kweli walimwacha mzee mpaka akala dafrao kwanza ndipo wakamuokota ingawa pia inawezekana hawakujua kuwa mzee atarudia tena mchezo huo.
BTW: Mbona K. Kwete amekuwa rais wa kukolapsikolapsi mara kwa mara wakati wa kampeini? Je huku kukolapsi kwake kunaonyesha upungufu wanguvu mwilini na ubongoni mwake kukabiliana na majukumu mazito ya kuongoza taifa maskini kama hili?? Je hii inaweza kuwa inaonyesha kwa nini tangu akamate madaraka hajaweka vizheni imara ya taifa hili bali tunakwenda na upepo tu kama vile hatuna dereva? Je inawezekana kuna sababu ya msingi kutafuta dereva mwingine mwaka huu wa elfu mbili na kumi?
Mimi siyo mtaalamu wa historia ila ni mpenzi mkubwa sana wa historia. Kwa marekani, historia ya karibu inatuambia kuwa Rais Kennedy alikuwa na matatizo sana ya kiafya lakini alikuwa imara sana mbele ya umma na vile vile alikuwa na akili sana kiasi kuwa maumivu yake ya mwilini hayakuingiliana na uwezo wake wa kufanya maamuzi magumu kama yale ya mvutano kuhusu merikebu za Urusi kwenda Kyuba; kwa hiyo raia wa kawaida hawakujua lolote kuhusu matatizo ya kiafya ya Kennedy hadi baada ya kuwa ameuwawa ndipo watu wake wa karibu wakayatoa nje. Kwa huyu mzee wetu kuanguka anguka hadharani mara kwa mara bila hata kuwa ameweka mataputapu kunaonyesha kuwa huenda ana matatizo makubwa sana kuliko tunavytaka kuamini, na matatizo hayo yanaweza kuwa yanaingiliana na uwezo wake wa kufanya maamuzi magumu ya kitaifa.
History will tell..............