Wananchi wenzangu tunaojiuliza 'kulikoni raisi aanguke' naomba tujadili kwa dhati ya mioyo yetu kabisa na tutake majibu mazuri kabisa na kutoa ushauri na wanaopokea ushauri wautendee kazi. Ifike mahali taaluma za watu zifanye kazi na kazi hiyo ionekane. Watu waliopewa dhamana ya kuwa karibu na raisi waache mzaha na mambo ya kawaida tu. This is serious.
Mwaka 1997, Raisi Kikwete alipokuwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alizidiwa ghafla na kuanguka uwanja wa ndege wa Brussels, Ubeligiji akiwa safarini kuelekea nchini Cuba.
Mwaka 2005 katika kampeni, alizidiwa hapo hapo viwanja vya Jangwani Dar Es Salaam na kuanguka ghafla ikabidi kupatiwa huduma ya dharura.
Raisi aliwahi pia kuanguka mjini Mwanza.
Majuzi hivi amepatwa na dharura ya kuishiwa nguvu.
Leo kuanguka tena Jangwani ni tukio la ngapi, la tano, hadharani, hatuna uhakika na ambayo hatujayaona.
Wananchi tulipodai kupatiwa taarifa ya afya ya raisi wetu, baadhi ya watu na watendaji walidhani ni kebehi au kutaka udadisi usiokuwa na sababu, wakasahau kuwa Wananchi ni waajiri wa Raisi na wanapokuwa na wasiwasi juu ya usalama wa afya ya Raisi wao, pia hukumbwa na kiwewe na maneno mengi yakasemwe 'ndivyo sivyo', hatimaye kilio chetu kilisikika, na daktari wa Raisi akazungumza. Kama tulivyo wengi, na mapokeo yalikuwa mengi, wapo waliohoji undani wa ripoti ile kuwekwa hadharani na wapo waliohoji ni kwa nini ifichwe.
Wanaotunyima kujua hali ya afya ya raisi wanashindwa kuelewa kuwa wanajidanganya wenyewe, wanatudanganya sisi na wanamdanganya raisi, mwishowe tumebabaishwa tu.
Mimi si daktari wala mshauri wa Raisi, ila kwa mtizamo wangu na kwa vigezo vya fani yangu, nitasema Raisi anahitaji Mtaalamu wa Saikolojia. That's what he needs right now. Nifafanue. Mtu yeyote anapokumbwa na tatizo ambalo ni vigumu kulikabili (out of control) mara nyingi tatizo hilo huwa kama jinamizi kwake, na aghalabu jinamizi ni hali ya kuteseka kisaikolojia kwa woga na hofu ilyiopindukia (exaggerated fear), hii hutokea punde tu unapokuwa katika mazingira yale au yanayofanana na yaliyosababisha ukapatwa na tatizo uliloshindwa kulikabili. Hivyo ni dhahiri kuwa utakapokwenda kwenye eno lile lile, utakumbwa na mfadhaiko na woga na hofu yako itakutawala na utajikuta umeangukia tatizo lile llile (succumb to the same problem). Hali hii ndiyo inayowapata hata watu wenye kifafa, akiwa katika mazingira fulani ndipo anaanguka au kuweweseka. Linawapata pia watu wenye phobia. Na tTatizo la saikolojia kuliondoa linahitaji mtaalamu wa Saikolojia.
Nimemaliza!