Kikatiba, Waziri Mkuu ndiye Msimamizi wa Mawaziri wote. Sasa Lukuvi na Kabudi watasimamia Mawaziri vipi?

Rais Samia leo amesema amewaondoa kwenye baraza la mawaziri Lukuvi na Kabudi ili wabakie ikulu kuwasimamia (kuwachapa viboko!) mawaziri wengine wote. Pia Rais Samia amesema nafasi za Kabudi na Lukuvi haziko popote kwenye muundo wa serikali (yaani haziko kikatiba).

Sasa hoja iko hapa.
Katika mazingira ambayo baraza la mawaziri ni chombo huru cha kikatiba katika kuendesha serikali, wajumbe wake wakitajwa kikatiba (Rais, makamu wa rais, Rais wa Zanzibar, waziri mkuu na mawaziri (sio manaibu waziri)), ni vipi mtu asiye mjumbe wa baraza la mawaziri (kama Lukuvi na Kabudi) akawa na mamlaka ya kusimamia utendaji kila siku wa baraza la mawaziri?
Ni vipi siri za baraza la mawaziri zitalindwa ikiwa wasimamizi wake (Lukuvi na Kabudi) sio wajumbe na hawakuapa popote kuzilinda?

Kikatiba waziri mkuu ndio kiongozi, msimamizi na kiranja wa mawaziri wote. Kwa kauli hii ya leo ya Samia (ambayo yeye mwenyewe amekiri haiko kikatiba) inapora mamlaka ya waziri mkuu katika kuwasimamia mawaziri wote ili kuwapa mamlaka Lukuvi na Kabudi.
Je, Lukuvi na Kabudi wanafanya kazi hizo kwa sheria ipi?
Watatumia mamlaka ipi ya kikatiba kufanya kazi hizo?
Watalipwa na nani kufanya kazi hizo ikiwa sheria na muundo wa serikali hauwatambui?

Je watawajibika kumsimamia (kumchapa viboko!) na waziri mkuu katika utendaji wake?

Nini kitatokea ikiwa utendaji(usimamizi) wa Lukuvi na Kabudi utakinzana na utendaji (usimamizi) wa waziri mkuu katika kuwasimamia mawaziri.
Yawezekana Lukuvi akaja kuwa Waziri Mkuu. Nawaza tu kwa sauti
 
Lukuvi atakuwa kama Mshauri Mkuu wa Mh. Rais kuhusu mambo yote ya uongozi kwa ujumla navyoona mimi, kitu ambacho ni kizuri sana sanaaa..
...Vipi kuhusu ubunge wake?...baraza la mawaziri halitoshi kumshauri?....hivyo vyeo havipo kikatiba, Sasa wakistaafu na hivyo vyeo vipya watapewa pension?
 
Nani asiye jua lukuvi,na kabudi ni watu potential !?, ameona kuwaacha hawa watu italeta mijadala mirefu ,so ameamua kutuliza hali ya hewa! Binafsi nimekuelewa kuwa ,hao wameachwa Kama washauri wakuu wa rais !! yaani kwa lugha ya mtaani watakuwa ni wakuda ,yaani wanaangalia wazr gani,au katibu yupi hawajibiki kikamilifu ,wanamshauri rais afanye Jambo !!! ila sijajua mishahara yao itakuwa na reflection ya idara gani.yote juu ya yote ,ametumia busara ku settle Mambo!!
Hawana potential wowote. Ile statement ya "hagombei uspika"ni alarm tosha kuwa ni kifungo cha kisiasa flani hivi. Jiulize, je Rais kaambiwa na Lukuvi kuwa hagombei?
 
Tanzania mzima inajua kuwa mama amebugi kuwaondoa akina lukuvi, ushauri WA wazee ndiyo umefanya warudishwe
Hakuna mtu muhimu mbele ya anayechezea taasisi ya Urais. Ataondolewa tu. Alichofanya bi Tozo ni kuwapiga pini. Anawatoa kwenye siasa anawaingiza kwenye utaalam huku wakiwa washazeeka
 
... hatoki kirahisi Mkuu! Ni process fulani ndefu tofauti na mawaziri wa kawaida ambao taarifa za kuondolewa kwao wanaweza kuzipatia bar. Pengine ndio maana mama hakutaka maprocess marefu kaamua atumie shortcut fulani hivi.
Hivi kazi ya wabunge ni nini?!?

Kabudi na lukuvi wanaenda ikulu kumshauri mini tens rais..
Ssh kachemka. Na lugha rahisi ni kuwa ikulu kuna marais watatu kwass.
 
Vipi kama niwashauri wa raisi, pengine hata wa shauri binafsi kama Sheria zetu zina zungumzia Hilo, au hats kama sheria haitamki ni maswala ya kanuni TU, je kwanini tusiwe wakuangazia sasa kwenye uelekeo wa Sheria na kanuni Kwa lengo la kuboresha kama tumeona mapungufu, badala ya kulalamika na kilaumu kila jambo hata Yale tusiyoyajua, Nii Imani yangu humu jukwaani tunao wataalamu wa nyanja zote. Ni wakati was kurejesha kwa jamii. Cc@Mayala
Hoja yangu imejikita kwenye kile ambacho Rais Samia amekisema kuwa, hao kina Kabudi na Lukuvi atawapa jukumu la kumsaidia kuwasimama (akasema kuwachapa viboko!) mawaziri wake. Kwa lugha ya malkia hao jamaa wanakwenda kuwa overseers wa baraza lake la mawaziri.

Rais hajasema anawateua kuwa washauri wake bali anawateua kuwa wasimamizi na watendaji rasmi wa kiserikali nje ya katiba!
 
Zanzibar-ASP mtuambie nyie wazenji labda mnamuelewa mzenji mwenzenu.
Hata sisi wazenji bado hatumuelewi huyu mama, kwa kuwa hata yeye hajielewi.

Juzi alisema anafanya mabadiliko ya baraza la mawaziri ili kuwaondoa wote wataka urais wa 2025 ili wakapiganie vyema huo urais huko nje ya serikali yake na kumuacha yeye akifanya kazi za kiserikali, leo anasema wale wataka urais aliowafukuza anawaleta ikulu ili kumsaidia kuendesha serikali yake!

Nani anaweza kukuelewa?
 
Rais Samia leo amesema amewaondoa kwenye baraza la mawaziri Lukuvi na Kabudi ili wabakie ikulu kuwasimamia (kuwachapa viboko!) mawaziri wengine wote. Pia Rais Samia amesema nafasi za Kabudi na Lukuvi haziko popote kwenye muundo wa serikali (yaani haziko kikatiba).

Sasa hoja iko hapa.
Katika mazingira ambayo baraza la mawaziri ni chombo huru cha kikatiba katika kuendesha serikali, wajumbe wake wakitajwa kikatiba (Rais, makamu wa rais, Rais wa Zanzibar, waziri mkuu na mawaziri (sio manaibu waziri)), ni vipi mtu asiye mjumbe wa baraza la mawaziri (kama Lukuvi na Kabudi) akawa na mamlaka ya kusimamia utendaji kila siku wa baraza la mawaziri?
Ni vipi siri za baraza la mawaziri zitalindwa ikiwa wasimamizi wake (Lukuvi na Kabudi) sio wajumbe na hawakuapa popote kuzilinda?

Kikatiba waziri mkuu ndio kiongozi, msimamizi na kiranja wa mawaziri wote. Kwa kauli hii ya leo ya Samia (ambayo yeye mwenyewe amekiri haiko kikatiba) inapora mamlaka ya waziri mkuu katika kuwasimamia mawaziri wote ili kuwapa mamlaka Lukuvi na Kabudi.
Je, Lukuvi na Kabudi wanafanya kazi hizo kwa sheria ipi?
Watatumia mamlaka ipi ya kikatiba kufanya kazi hizo?
Watalipwa na nani kufanya kazi hizo ikiwa sheria na muundo wa serikali hauwatambui?

Je watawajibika kumsimamia (kumchapa viboko!) na waziri mkuu katika utendaji wake?

Nini kitatokea ikiwa utendaji(usimamizi) wa Lukuvi na Kabudi utakinzana na utendaji (usimamizi) wa waziri mkuu katika kuwasimamia mawaziri.
Mimi siwez kujadili kwanini wamepewa kazi maalum,
mpaka nijue kwanini alitamka atawatoa waliokuwa kwenye
kinyang'anyoro cha 2025 wakajipange vizuri.
Danganya toto.
 
Hata sisi wazenji bado hatumuelewi huyu mama, kwa kuwa hata yeye hajielewi.

Juzi alisema anafanya mabadiliko ya baraza la mawaziri ili kuwaondoa wote wataka urais wa 2025 ili wakapiganie vyema huo urais huko nje ya serikali yake na kumuacha yeye akifanya kazi za kiserikali, leo anasema wale wataka urais aliowafukuza anawaleta ikulu ili kumsaidia kuendesha serikali yake!

Nani anaweza kukuelewa?

Changamoto.
 
Nimejifunza kuwa kuna mtu anawekwa Kando kinamna. Amesema "kuwasimamia vizuri hawa Mawaziri waweze kutenda. Yaani hawa vijana nilioapisha Leo wanahitaji usimamizi mzuri". That was a very strong indirect message to someone who was playing behind the back of her Excellency. Open the code!!!!
Haswaa, wewe ndio umeelewa mada hapa. Na ndio msingi wa hii hoja.
 
Rais anawapeleka wabunge kuwafungia Ikulu inaruhusiwa?

Anasema atawapa kazi huko za kusaidia saidia kusimamia mawaziri wakati hawa ni wabunge wanaotakiwa wakawatetee wananchi wao majimboni.

Hapa mimi sijaelewa mama ana mpango gani na maamuzi hayo.

Wakikubali wataenda kuwa waosha vyombo ikulu.

Wakatae ulaghai huu haraka kulinda heshima zao.

Wakawatetee wananchi waliowachagua. Waachane na hizi laghai za wajanja wa mjini wanaomshauri mama mambo ya janja janja.
 
Lukuvi atakuwa kama Mshauri Mkuu wa Mh. Rais kuhusu mambo yote ya uongozi kwa ujumla navyoona mimi, kitu ambacho ni kizuri sana sanaaa..

Waziri Mkuu haihusiani na hili, Mh. Rais anaweza kumteua mtu yeyote/watu kadhaa kuwa wasaidizi wake kwa mambo mbalimbali, kwa jinsi yeye Mh. Rais atakavyoona inafaa, na haulizwi kwa hili, ana mamlaka hayo.

Ila hii ni red light kwa Majaliwa, 2025 akirudi kuwa PM, basi amshukuru Mola kwa sana.

Atakuaje mshauri wakati yeye Lukuvi na Kabudi ndio aliwataja kuwa threat wake 2025
 
Back
Top Bottom