Kipi kilichomvutia Rais Samia kumpa Biteko Unaibu Waziri Mkuu?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Kihistoria watu wote waliowahi kupata Unaibu Waziri Mkuu cheo ambacho si cha kikatiba bali huja tu kwa utashi wa raisi aliyepo madalakani, ukiwaona na kuwatathimini unagundua kwamba walikuwa na kitu cha ziada, ambacho kinaleta kishindo kikubwa Kwa kiwango cha kutikisa baraza zima la mawaziri.

Kwa maneno mengine waliopata kuwa na utendaji uliotukuka Kwa kiwango cha kuwa tishio hata kwa serikali nzima.

Tukija kwa Doto sikatai kwamba ni waziri mzuri lakini ni waziri mzuri kama walivyo mawaziri wengine. Ingekuwa kama ilivyokuwa zamani jpm akiwa waziri akapewa huo unaibu waziri mkuu, angalau ingeleta maana.
Hata ingekuwa siku za makonda akiwa wa moto ingebuniwa nafasi kama ile isingeleta shida.

Sasa huyu ndugu kapewa licheo kapewa liwizara pasua kichwa namna hiyo najiuliza huyu mbaba wa watu si wanamuonea tu!?
 
Mawe na utajiri wa madini, tumia akili kula vizuri na boss wako tumia akili mtanganyika
 
Mama anazitaka kura za kanda ya ziwa Biteko atawafanya wana kanda ya ziwa wamkubali mama.

Hii nafasi Makonda ingemfaa kweli
 
  1. Kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa watu wa kanda ya huko
  2. Kuna pigo tunaandaliwa huko kwenye madini rejea kupelekwa mkwe utalii na maliasili
  3. Zawadi kwa waprotestant kwakuwa hawakuandika waraka
  4. Kuwianisha mambo maana yule wa Kigoma yuko peke yake
 
Anatokea kwenye big voting block, ni usukuma/unyamwezi wake tu, Chadema na Lisu,walivuruga kabisa kanda ya ziwa, kwa kuelezea madudu ya samia na ccm, tiketi pekee anayotegemea samia kuitumia kwenye uchaguzi ni uhusiano wake na Maghufuri(msukuma), inabidi aonyeshe bado analinda regacy ya maghu, sasa kwa vile kanda ya, ziwa pamechafuliwa, ikabidi atafutwe msukuma/nyamwezi ambae wasukuma wataona samia hajawatupa, ni hicho tu,
 
Anataka kuwin influence ya kanda ya ziwa, na kuwaonyesha Sukuma gang kuwa yupo pamoja nao!!
Una jicho kali sana. Tangu day 1 baada ya uteuzi ule, nilisema hivyo.. ukizingatia kuwa Chadema walikuwa wameweka kambi kule Kanda ya ziwa na walikuwa wanaubadilisha upepo wa kisiasa.

Kikubwa ni kuwin influence ya watu wa Kanda ya Ziwa ambao kwao Jiwe alikuwa ni zaidi ya CCM na walikuwa wanahisi kama wametengwa na utawala wa mama.

Narudia tena mbussi una jicho kali sana.
 
Kihistoria watu wote waliowahi kupata unaibu waziri mkuu cheo ambacho sii cha kikatiba bali huja tu kwa utashi wa raisi aliyepo madalakani, ukiwaona na kuwatathimini unagundua kwamba walikuwa na kitu cha ziada, ambacho kinaleta kishindo kikubwa Kwa kiwango cha kutikisa baraza zima la mawaziri.

Kwa maneno mengine waliopata kuwa na utendaji uliotukuka Kwa kiwango cha kuwa tishio hata Kwa serikali nzima.

Tukija kwa doto sikatai kwamba ni waziri mzuri lakini ni waziri mzuri kama walivyo mawaziri wengine. Ingekuwa kama ilivyokuwa zamani jpm akiwa waziri akapewa huo unaibu waziri mkuu, angalau ingeleta maana.
Hata ingekuwa siku za makonda akiwa wa moto ingebuniwa nafasi kama ile isingeleta shida.

Sasa huyu ndugu kapewa licheo kapewa liwizara pasua kichwa namna hiyo najiuliza huyu mbaba wa watu si wanamuonea tu!?
Hofu ya 2025
Kanda ya ziwa hadi sasa haitabiriki
 
Hon. Dotto Mashaka Biteko
biteeko%20ed.jpg

Picha:IPPMedia.
Asipo angalia, yaliyomkuta yule aliyepiga saini wa Bandari atakuwa ni yeye. Vyeo hivi, pamoja na kuwa na Nguvu, ya uhalisia na za Hisia. Zina utata unao ambatana nao.
Sina la ziada zaidi ya mimi nijiunge na wengine na kukaa kuleee.
Hongera zake Mchapa kazi.
 
Nawaza kimya kimya kwanini asiteuwe mtu kutoka Msoga gang.

Kama kweli kateuliwa kwasababu za ukanda kama comment nyingi zinavyojibu,basi nguvu ya Sukuma gang ni kubwa na ndio yenye uwezo wa kuikoa CCM hasa lake zone.
 
Kihistoria watu wote waliowahi kupata Unaibu Waziri Mkuu cheo ambacho si cha kikatiba bali huja tu kwa utashi wa raisi aliyepo madalakani, ukiwaona na kuwatathimini unagundua kwamba walikuwa na kitu cha ziada, ambacho kinaleta kishindo kikubwa Kwa kiwango cha kutikisa baraza zima la mawaziri.

Kwa maneno mengine waliopata kuwa na utendaji uliotukuka Kwa kiwango cha kuwa tishio hata kwa serikali nzima.

Tukija kwa Doto sikatai kwamba ni waziri mzuri lakini ni waziri mzuri kama walivyo mawaziri wengine. Ingekuwa kama ilivyokuwa zamani jpm akiwa waziri akapewa huo unaibu waziri mkuu, angalau ingeleta maana.
Hata ingekuwa siku za makonda akiwa wa moto ingebuniwa nafasi kama ile isingeleta shida.

Sasa huyu ndugu kapewa licheo kapewa liwizara pasua kichwa namna hiyo najiuliza huyu mbaba wa watu si wanamuonea tu!?
BITEKO ana kitu cha ziada ambacho mawaziri wengi hawana, huwezi kukijua ni siri ya mkuu wa nchi!
 
Back
Top Bottom