Kikatiba, Waziri Mkuu ndiye Msimamizi wa Mawaziri wote. Sasa Lukuvi na Kabudi watasimamia Mawaziri vipi?

hapa
Rais Samia leo amesema amewaondoa kwenye baraza la mawaziri Lukuvi na Kabudi ili wabakie ikulu kuwasimamia (kuwachapa viboko!) mawaziri wengine wote. Pia Rais Samia amesema nafasi za Kabudi na Lukuvi haziko popote kwenye muundo wa serikali (yaani haziko kikatiba).

Sasa hoja iko hapa.
Katika mazingira ambayo baraza la mawaziri ni chombo huru cha kikatiba katika kuendesha serikali, wajumbe wake wakitajwa kikatiba (Rais, makamu wa rais, Rais wa Zanzibar, waziri mkuu na mawaziri (sio manaibu waziri)), ni vipi mtu asiye mjumbe wa baraza la mawaziri (kama Lukuvi na Kabudi) akawa na mamlaka ya kusimamia utendaji kila siku wa baraza la mawaziri?
Ni vipi siri za baraza la mawaziri zitalindwa ikiwa wasimamizi wake (Lukuvi na Kabudi) sio wajumbe na hawakuapa popote kuzilinda?

Kikatiba waziri mkuu ndio kiongozi, msimamizi na kiranja wa mawaziri wote. Kwa kauli hii ya leo ya Samia (ambayo yeye mwenyewe amekiri haiko kikatiba) inapora mamlaka ya waziri mkuu katika kuwasimamia mawaziri wote ili kuwapa mamlaka Lukuvi na Kabudi.
Je, Lukuvi na Kabudi wanafanya kazi hizo kwa sheria ipi?
Watatumia mamlaka ipi ya kikatiba kufanya kazi hizo?
Watalipwa na nani kufanya kazi hizo ikiwa sheria na muundo wa serikali hauwatambui?

Je watawajibika kumsimamia (kumchapa viboko!) na waziri mkuu katika utendaji wake?

Nini kitatokea ikiwa utendaji(usimamizi) wa Lukuvi na Kabudi utakinzana na utendaji (usimamizi) wa waziri mkuu katika kuwasimamia mawaziri.
hapa mwalimu angejiuzuru boss kamkataa kiaina
 
Back
Top Bottom