Kwanini Tanzania Waziri Mkuu akijiuzulu na Baraza la Mawaziri linavunjika?

Mkuu Wakili wa shetani, hili ni suala la kikatiba. Kwa mujibu wa Ibara ya 55, ibara ndogo za 1 na 2 ya Katiba yetu ya Tanzania, Mawaziri na Manaibu Mawaziri huteuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.

Hadi hapo, ni rahisi kuelewa kuwa Mawaziri na Manaibu wao hupatikana pale tu anapokuwepo Waziri Mkuu. Yaani, anapokuwepo Waziri Mkuu nao huwepo na asipokuwepo Waziri Mkuu nao hawatakuwepo.

Hivyobasi, lolote linalomtokea Waziri Mkuu na kumfanya asiendelee kushika nafasi hiyo huwaathiri moja kwa moja Mawaziri na Manaibu wao(Ibara ya 57 (2) (e)). Na uteuzi wa Mawaziri na Manaibu wao wengine utafanyika pale tu Waziri Mkuu mpya atakapopatikana.

Kikatiba, ni lazima Rais ashauriane na Waziri Mkuu katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu wao. Asipokuwepo huyo wa kushauriana na Rais, uteuzi haufanyiki na Mawaziri na Manaibu wao wanapoteza nafasi zao hapohapo.
 
Kwa mujibu wa katiba ipo hivyo lakini kwenye uhalisia sidhani kama hili linatekelezwa. Hili linatoa picha kuwa Rais yupo juu ya katiba. Mfano 2020, Magufuli aliwateuwa mawaziri wawili kisha ndio akapeleka jina la Majaliwa bungeni.

Nchi hii katiba huwa inakanyagwa na waliowekewa kinga na hiyo hiyo katiba. Hizi loop holes ndio zinafanya watawala kuwa juu ya sheria na kufanya lolote na hakuna la kuwafanya. This is madness.
 
Back
Top Bottom