mr cool
Member
- Apr 6, 2015
- 43
- 22
Lowassa kuna kitu anatafuta.siyo uongozi.hapana siyo bure.
Kweli xana kaka hyu atakuwa anatumiwa ndio maana anatafuta oungoz kwa udi na uvumba ili atomize matakwa ya wanaomtumia.
Lowassa kuna kitu anatafuta.siyo uongozi.hapana siyo bure.
Utaitwa msaliti sasa hivi....njoo kwa wazalendo
Sawa mkuu. Siasa sio ugomvi ni mawazo tofauti ya kufikia malengo ya maendeleo. Hakuna haja ya matusi. Iwe lowasa au pombe yeyote sawa tu.Mtatukana matusi yote, lakini haitasaidia, kila mtanzania yuko Huru kwenda chama chochote cha siasa anachokipenda!
Lowassa ni Chaguo la Mungu!
Slaa anagombea ubunge Karatu,,we unafanya mchezo na urais?
Ni zaidi ya pwagu na pwaguzi. Lakini nafikiri inakuwa maagizo hasa inapoingiliwa na wigizaji. Focus kubwa ya mbowe ni kupata viti vingi vya ubunge na hatimaye ruzuku kubwa, ni biashara. Lakini ni kujitia upofu kufikiria kwamba watashinda.
Mbowe amesema sivyo!Mimi sikuwa nimeamini lakini niliziona pia kwenye Chadema Blog
Hakika mi nimebaki dilema..niliachana na ccm baada ya kuona huyu mtu anatafta madaraka kwa udi na uvumba huku watu wanaomzunguka wote wakiwa na uchu wa rasimali za nchi hii rostam..chenge..karamagi..na wengine wenye uchu wa madaraka leo tena kapokelewa huku ambako ndiko kulikuwa kimbilio langu..mi kura yangu ni kwa magufuli lakini wabunge watoke ukawa..nimebaki dilema kwa kweli..Sahihisha,siyo kila mwenye mawazo tofauti na wewe ni CCM,kuna wanaCDM wenzako pia tunamawazo tofauti na viongozi wetu.
Simkatalii Lowassa kuwa Mwanachama wa CDM ila nakataa Lowassa kupeperusha Bendera ya CDM kwenye ngazi ya URAIS.
Ninasababu kubwa moja ua mbili,kwanza huyu Mtu amepoteza pesa nyingi sana wakati anataka kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM,leo tujiulize mimi na wewe atazirudishaje?Je hii haitakuwa mwanzo wa kuingia unajisi CDM ?Unadhani aliyezoea kula nyama ya mtu ukimbadilisha dini ataacha?
Pili huyu njia aliyotumia kusaka URAIS ndiyo njia aliyotumia kumasaidia RAFIKIYE mpendwa kuingia magogoni,tumeona jinsi maliasili zetu zilivyokuwa zinachotwa bila hata kukemewa na kiumbe yeyote.Rais alishika UTAMU wote hakuna mbunge wala nani kumkemea,jamani mnataka turudi miaka mingine kumi ya aina ile ile?
Tatu na mwisho inamaana miaka yote hii ishirini CDM imeshindwa kumrecruit KIONGOZI BORA wa kupeperusha Bendera ya CDM?
Je,viongozi wanawatendea HAKI watanzania waliojiaminisha kwao?
Hakika sina shida na Mbunge wangu JJMnyika Kura yake ipo wazi hana haja ya kuifuata kama alivyosema Mpoto nitampelekea mwenyewe lakini URAIS kama ni LOWASSA HAPANA na wala MAGUFULI pia hapati kura yangu wote hawa ni walewale tu.
Hizo ndizo sababu zangu mimi siyo CCM pole,ila ninamawazo tofauti na wewe.
Lowasa akijiunga na CDM narejesha kadi...
Sintokua na iman na chama kwa yale walionimezesha awali yalimuhusu mzee huyo..
Naikumbuka sauti ya mzee Slaa alipokua akimtaja lowasa kua fisadi ktk viwanja vya mwembe yanga..
Ikiwa CDM watamualika mzee huyo nidhahir kua walitudanganya kutokana na ufisad waliototajia kua unamuhusu huyo mzee...
MUNGU JAALIA KATIBA MPYA ILI NIWE NA NGUVU YAKUMPA KURA YANGU KIONGOZI ASIE NA CHAMA CHAKISIASA.
Nakipenda sana chama changu
Safari ya uhakika imeanza, aliye msafi ampige Lowassa jiwe
Freman mbowe ndiye mwkt wa chama cha siasa nchini mwenye elimu ndogo zaidi lakini amefanikiwa kuviuza vyama vitatu kwa mpigo chadema nccr-mageuzi na cuf kwa bei ya jumla kwa lowasa
ongera sana mbowe kwa kazi mzuri
Ndugu yangu hata CCM imebadilishwa. Hali ya kisiasa Tanzania haitakuwa ilivyokuwa na kama CCM haitabadilika itakufa na halikadhalika vyama vingine vyovyote vidipojibadili vitakufa. Nafikiri ulimsikia Kiongozi wa ACT juzi alivyosema kwa unyonge kuhusu mabadiliko haya. Hakuna hata siku moja Slaa alishasema anagombea bali watu walichukulia for granted kuwa ndiye mgombea, wahasimu wake wakielekeza nguvu kwake...na hii ndiyo UKAWA imewapa credit (to think outside the box)Lowassa kashaibadilisha Chadema.
1. Kabadilisha ratiba yao ya uchaguzi.
2. Kabadilisha mgombea wao. Dr. Slaa anakatwa kwa sababu ya Lowassa.
3. Kabadilisha bajeti yao ya uchaguzi.
4. Kabadilisha kauli zao kuhusu ufisadi.
5. Kabadilisha ilani yao ya uchaguzi.
Sasa tujiulize, nani anayebadili mwenzie? Chadema itambadili Lowassa au Lowassa anaibadili Chadema?
Lowassa yuko kwenye siasa muda mrefu kuliko umri wa Chadema. Kuamini kuwa Lowassa atabadilika ghafla ni kujidanganya kulikopitiliza.
Mpaka sasa Chadema haijabadili chochote kwa Lowassa, yeye ndio anawabadili.
Chadema badala ya kuleta mabadiliko, yenyewe ndio inabadilishwa...
Mtatukana matusi yote, lakini haitasaidia, kila mtanzania yuko Huru kwenda chama chochote cha siasa anachokipenda!
Lowassa ni Chaguo la Mungu!