Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kuna watu wanajifanya wamebobea kwenye mambo ya ICT. Lakini kwenye hili inaonyesha jinsi gani elimu yao ni bure. Lowassa ni kweli alihudhuria kikao bahari beach.

Na nashukuru mtoa mada kwa kutuwekea link ya YouTube kwa kumbukumbu wakati evidence zikiendelea Kuletwa.
 
Akili ya mchaga biashara, akale wapi, ni kuchezea hesabu tu za pesa utawapata hata maprofessor
 
sikupata pia. lakini waliowasafisha wale wa escrow sio waliowachafua. ungesema kafulila, zitto au filikunjombe ndo waliowasafisha ningekuelewa.

Mawili, eidha ujui uliloliandika AU umeamua kujiridhisha... Kuna wakati ubishi uwekwe kando facts zisemwe.... HADI AKINA OLESENDEKA WALILALAMIKA...

Ukiona unachafuliwa halafu na wewe unachafuka ujuwe linakuhusu kwa namna moja au nyingine
 
Ukweli UKAWA mmetuaibisha, naombea kusema tumeaibishwa; kitendo cha kumtaka LOWASA agombee URAIS kupitia UKAWA imetuonyesha walivyo waroho wa madaraka. mlituaminisha kuwa LOWASA no fisadi, mlipiga kelele mpaka akafukuzwa uwaziri mkuu sasa nchi inapata hasara kwa kuwalipa mawaziri wakuu wawili ndani ya miaka 10. LOWASA NA PINDA ni mzigo ulisababishwa na kelele za UKAWA hasa CDM. Kila kona tuliambiwa LOWASA ni fisadi mwizi na nk. leo mnatuambia kuwa ni mtu safi wakati mkijua siyo mtu safi, hivi nyie viongozi wa UKAWA mnafikiri watanzania ni mbumbumbu? tumewaunga mkono na kuwatetea vijiweni, kwenye mitandao leo hii mnakaribisha zimwi lililoshindikana CCM, UKAWA mtaliweza?

Nimgundua kuwa UKAWA siyo wapigania haki au ukombozi wa nchi hii bali ni wajasiliamali wanaotafuta pesa au kutaka madaraka badala ya kupigania wanyonge, kwa ilivyo UKAWA wapo tayari hata kutafuta mifupa ya binadamu ilimradi kwenda ikulu.

Nimeamini Dr Slaa siyo mwadirifu kama nilivyokuwa nikiamini kwa kuwa yeye ni padre, niliamini hakuna Padre anayeweza kuwa MWONGO. leo hii Padre Slaa atasimama jukwaani bila woga kumtetea LOWASA eti siyo mwizi? wakati anajua katika amri kuu za MUNGU kuna moja inayosema " USIMSEMEE UONGO" lkn leo Padre Slaa anasema uongo siyo dhambi. Ukweli tumeumia sana, sasa hatuna jinsi zaidi ya kuwaomba msamaha CCM.
 
Acha kutunenea wananchi wenzako uongo. Wewe ndio unaeona Mbowe kakufanya zuzu ila si watu wote. Acha siasa za uchonganishi. Najua unaumia kwa uamuzi wake ila huna namna zaidi ya kutapatapa.
Tujuavyo kundi fulani lenye maslahi binafsi ndilo lililotumia kila njia kufanikisha uongozi uliopo sasa kushika hatamu za uongozi wa nchi hii, na ndio kundi hilo hilo lililo nyuma ya mpango mzima kuwezesha mweshimiwa huyu kuingia madalakani kupitia Ukawa. Tunalijua hilo tunajiandaa kukabiliana nalo. Hakika wanasiasa wameonesha udhaifu mkubwa kuliko
 
Vivaaaa UKAWAAAA....Vivaa Lowassaa...


Bravooo...brilliant..., what a game...!!! fantastic, fabolous...magic...wooooww...!!!
 
Jinsi Edward Lowassa alivyo, inaonekana kuna kitu alichokidhamiria katika nchi hii.Labda kulipa kisasi.Lakini yote namwona kama ni changudoa wa kisiasa
 
Back
Top Bottom