ni mfumo wa ccm ndo hatari. mfumo wa ccm ndo unaowalea wezi na mafisadi. dawa ni kuuondoa huo mfumo na si kudeal na mtu mmojammoja.Hebu naomba nisaidieni, wanaoharibu mustakabali wa nchi ni watu waliopo CCM au jina tu CCM?
pale ccm hata ukipeleka malaika hawezi kubaki safi sababu mfumo wote wa ccm ni mchafu kuanzia juu hadi chini.
embu nipe sababu za kwanini lowassa alipokuwa ccm ulitaka asiibe ili iweje? kwa nini asiibe wakati wenzake wote wanaiba? ambao hawaibi ccm imewapa heshima gani zaidi ya kuwatenga na kuwadhalilisha? kina warioba ambao si wezi wamefanyiwa nini na ccm?
wastaafu waliokuwa wanaitumikia ccm kiuadilifu, na hata watumishi waadilifu ndani ya serikali ya ccm leo hii, wamefanyiwa nini na ccm? ukiwa ccm kuwa mwizi si optional ni lazima.
Ukiwa ccm na ukataka kuacha wizi na uzembe hatua ya kwanza ni kutoka nje ya ccm kama alivyofanya lowassa.