Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa ndani

Ndugu zangu,
Imeniumiza Sana kugundua nchi hii haina Chama cha upinzani ila wachumia matumbo tu.

Lowasa akiwa CCM atakuwa mwizi, fisadi na mgonjwa.
Ila akiwa CHADEMA ni mtu Safi ni mwenye afya na mwaminifu.

Mimi ninamkubali Sana Lowasa ila chadema ni matapeli wanamchafua mtu kwa hila na unafiki Mungu awalaani kwa kuwarubuni watanzania.

Lowasa ukishika uongozi jua Hao siyo watu kaa nao kwa akili, wamependa pesa zako!.

Ukishika tu madaraka sambaratisha kwanza ngome ya huyu mmachame.

Ndugu zanguni kama siasa haikuingizii pesa achana nayo wenzenu wanatafuta pesa nyie mnajiita Makamanda.

ndugu tuliaaaaa, lowassa kuja (UKAWA) ni mpango wa MUNGU kabisa njia za MUNGU siku zote si zabinadamu,

LOWASSA ndiye Rais wa awamu ya tano

ccm mtapoteana mwaka uhu mlikejeli sana kuungana kwa vyama vya upinzani,(UKAWA)

kama mngekua na akili mngejiuliza kulikoni maana haija wai tokea tangu mfumo wa vyama vingi kutokea nchini,

mngejua kwamba MUNGU Alikuwa anawapa ishara ya kuwa mwisho wenu umewadia,

mbaya zaidi Huyu LOWASSA kwenye kutafuta wadhamini mlipoona umati wa watu mkaanza majungu na kumkataa MASIHI maskini ya MUNGU,

Hata hamkujua kwamba MUNGU alikua anawapa nafasi ya mwisho

jiandaeni kisaikolojia maana kimbunga kinakuja,
 
Alisema asipopitia mlangoni atapitia dirishani.naona chadema ndio dirishani.wananchi tuepuke sana vyama ambavyo viko tayari kuungana na mafisadi kwa sababu ya fedha. Chadema mmekuwa mfano mbaya sana kwa vyama vya upinzani hapa.nchini.
je unaweza kuweka ushahidi wa wazi hapa na kama ukishindwa mod tafadhali mtendeeni haki yake ya kumfungia kwenye jukwaa hili.
 
jamani leo huyuhuyu kawa msafi!alialika viongozi wa dini matapeli kote nchini wazee uchwara kibao lkn ccm wakasema hutufai piga chini tunataka watu safi . we unataka madaraka kwa namna yoyote ale. nanyie chadema kwa uroho wenu mmeingia mtegoni .
 
Inanishangaza mno na kunisikitisha kwa CDM hata kujihusisha tu na Fisadi Lowasa.
Dhambi mnayotenda haisameheki.Na kumbukeni hamtashinda Uchaguzi kwa sababu ya kumruhusu Lowasa akae na nyinyi we a.Mmejinajisi.Hata kama hamtamteua agombee urais,lakini mkimpatia hata uanachama tu mmekwisha.

Kama kweli wewe ni mwanamageuzi unatakiwa uachane na siasa za ukonsevativu, uwe unabadilika kulingana na mazingira na fursa ikija itumie, lowasa hata kama ni fisadi kwa mchakato uliotumika kumpata mgombea ccm kafanyiwa rafu za hatari, so kwa kitendo hicho jamaa kachukia na ukiufunua moyo wake hakika utakutana na utitiri wa hasira na visasi. Sisi wanamageuzi tatizo letu ni ccm hatuna budi kumtumia bwana mamvi kuwavuruga hawa jamaa kwetu ni mtaji make haitaji kumpiga xray kuona sumu ya visasi na hasira iliyomjaa ktk chemba zote nne za moyo bwana mamvi hata kwa kuangalia kwa macho tu unaziona. Cdm hatutajali huko nyuma tulisema nini tunachojali ni kutumia hasira za huyu robot kuwamalza ccm, make hata tukimkataa baada ya kujiuzulu yeye ccm waliendelea kupiga dili za escrow na katiba yetu pendekezwa wameibaka. Watanzania mnatakiwa kuelewa kudumaa kwa tz tatizo ni ccm so hata shetani akija kutupa sapoti ya kuangamiza hili zimwi heko watz tupokeeni hiyo sapoti.
 
Mpaka aibu yaani

Dr. Slaa hana sababu ya kuhama CDM kisa Lowassa, kwa nini musiulize huyo Lowassa alikuwa anakaa vipi CCM? Mbona muda wote mulikuwa naye hadi mumuengue si kwa sababu ya ufisadi bali kwa sababu ya kumuogopa asiwachenjie.

Kama ni ufisadi kaufanya siku nyingi inakuwaje leo anapotaka kuhama ndo munajifanya mmeuona ufisadi huo. Hata hivyo Lowassa ni hadhina nzuri sana kama atahamia upinzani maana anazijua mbinu zote za wizi atazianika ili watanzania waelezezwe vizuri namna wanavyoibiwa. Huyu ni Lowassa mmoja lakini mafisadi wengine wote papa bado wapo CCM.
Njoo Lowassa karibu ujitakasa ukiwa upinzani achana na wadhambi hao wausubiri moto wao. Japo nisingependa wakuteue kugombea Urais maana utamaduni wetu na mila zetu bado hujazijua itakubidi kujifunza kwanza na kuheshimu taratibu na matakwa ya wananchi tofauti na huko ulikotoka. Zidumu nia njema za watanzania wenye nia njema na chi yetu.
 
Yaani hii mechi ikianza UKAWA 1000, CCM 0, dak ya 89... washambuliaji hatari

UKAWA....

1: Edward Lowassa..Capt..striker hatari

2: Dr. Slaa, striker hatariii

3: Prof. Lipumba..striker..hatariii

4: Mbowe...striker...hatariii

5: Mbatia...striker hatariiiiii...

6: Maalim Seif .. Striker hatariiii...

7: Jussa..striker ..hatariiii....

8: Lembeli...maweee, striker hatariii sana

9: Wenje...right winger

10: Lissu, analijua Tundu...haaaatariiiii

11: Prof. Safari...ni shiiidaaaaa

12: Mnyika...striker, Moto mkubwa

13: Salum Mwalimu...striker..

14: Kafulila, Suarez..weweeee

15: Mkosamali.. striker...

16:Joshua Nassary...Dogo Janja, Neymar

17: Nchimbi....Middle

18: Msigwa...middle..

19: Bulaya...kipa..

20: Mdee, striker...hatariii

21: Lema, Ibrahimovic...haaaa

...

CCM...

1: Magufuli...Capt..

2: Amina... mshangiliaji..

3: Makinda...Forward..

4: Mary Nagu...Forward..

5: Migiro, beki...

6: Asumpta Mshana, middle

7: Kibajaji...mshangiliaji...

8: Nape Kipa....magoli mengi tu


Yaani....CCM hakuna wachezaji kabisa..
 
bado ni mafununu tu

* Bado huamini? Kuna huyu jamaa huwa anafuatilia sana habari za CHADEMA....kapost Twitter

11796268_1609680635982263_569234009707087670_n.jpg
 
Mbona hizi picha ziko tofauti tofauti, picha ya kwanza naawaona mbowe na slaa wapo na magwanda meupe, ya pili ya kikaoni wapo na magwanda ya khaki!au walienda nyumbani kubadilisha nguo
 
kumya kingi kina mshindo mkuu .....kazi imeanza ..tutaheshimiana tu...hizi tabia za kukatakata watu na kupiga virungu kama sisi kuku ....haikubaliki. ...CDM mwedo mdundo mpaka ikulu

Ngonyai itabidi aje na slogan kali zaidi ya ile ya matumaini '.....hamshahamsha walio lala lango la ikulu lipo wazi...'
 
CDM wasije wakasema hatukuwaonya.Hii ni hatari.Huwezi ukawa chama kinachodai kinasimamia uadilifu na uzalendo ukamchukua fisadi kama huyu Lowasa.Mimi sitakuwa sehemu ya uchafu huu.

Kwa ujumla mimi sielewi kabisa, lakini kwa vyovyote vile na katika mazingira yoyote yale ambayo kwa njia moja ama nyingine yatapelekea hiki kitu kuwa kweli, basi pasipo na chembe yoyote ya shaka nitakuwa nimeamini kuanzia sasa kuwa ni kweli Tanzania hatuna vyama vya upinzani bali tuna vyama vinavyoongozwa na watu ambao sio viongozi bali ni wale wenye uroho tu wa madaraka. Haiingii akili, mtu yule yule unarudi nyuma na kisha kula matapishi yako! And frankly speaking, shame on you, CHADEMA!

Umesema ukweli japo unauma sana.Na hata wale wenye NIA ya kusaidia hawana nguvu.I wish kungekuwepo na mgombea binafsi.

Namuangalia Dr.Slaa akitoka nje atakuja kutuambia nini watanzania?Je,tutamuamini?Ninajiuliza kwa sauti hivi ni kweli CDM imekuwa chama cha kifamilia kama wanavyokinanga?Kwamba Mtei akiongea basi wote mnakubali?Nimeshangazwa na hilo.

Ila kama kuna hata mwenye AIBU japo kidogo basi aikubali huo ujinga.

Na kwangu ni NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO kwa Lowassa.

Duh nimeamini cdm ni uchaga damu. Yani wao hela mbele tu. Alafu slaa na mbowe ni wanafiki Wa kutupwa

Kama kuna kiongozi atakayekusikiliza, sidhani,maana wote yaelekea wamelambishwa ASALI tayari,hakuna cha LISSU wala SLAA wote ni wamoja tu

Mtaongea yote leo, ila ukweli utabaki kuwa ukweli.

Si ninyi ndio mliosema Lowasa Mwizi?

Sasa kama mlishindwa kumpeleka mahakamani, safari hii na yeye atawapeleka mahabusu kabisa.

Hivi umewai kuona wapi adui yako akakusaidia kufichua wezi wanaokuibia?

Hii ndio siasa bwana, unapigiwa mziki ukicheza unalipishwa kiingilio.
 
Nini Kamanda Edward Lowassa; hata aje Shetani Mkuu, Lucifer, as long as the strategy ni kuiondoa CCM, Chadema au chama kingine chochote kimpe support. Say no to CCM by all means.

Hebu naomba nisaidieni, wanaoharibu mustakabali wa nchi ni watu waliopo CCM au jina tu CCM?
 
kama hii habari ni kweli,nitaanza rasmi kupigia kura ccm japo roho inauma maana hakuna namna nyingine tena,siwezi kupiga kura ccm wakiwa ndani ya upinzani bora nipigie kura ccm wakiwa ndani ya ccm,
 

Mtaongea yote leo, ila ukweli utabaki kuwa ukweli.

Si ninyi ndio mliosema Lowasa Mwizi?

Sasa kama mlishindwa kumpeleka mahakamani, safari hii na yeye atawapeleka mahabusu kabisa.

Hivi umewai kuona wapi adui yako akakusaidia kufichua wezi wanaokuibia?

Hii ndio siasa bwana, unapigiwa mziki ukicheza unalipishwa kiingilio.

Saccoss ya wakaskazini inazidi kuongeza mtaji. Billion 10 zimewafanya mmeuza saccoss.
 
Back
Top Bottom