2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 2,982
- 4,458
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama wamebaini nyumba iliyopo mtaa wa Ugindoni iliyotandazwa mashine zinazotumika kuchimba visima vya maji lakini badala ya kuchimba chini kuelekea maji yalipo, wanachimba kuelekea usawa yalipo mabomba ya mafuta yanayotoka baharini kuelekea bandarini.
Mafuta hayo yanachukuliwa baada ya 'flow meter' kusoma na kutambulika yamepokelewa nchini lakini kabla ya kufika kituo cha mwisho ndipo mabomba hayo yanapoelekea.
Ndani ya nyumba hiyo kuna mashine na mipira ambayo inavuta mafuta na kujazwa. Nyumba hiyo ina ulinzi mkubwa na taarifa za awali zinasema muhusika amepangisha eneo hilo lenye kodi ya milioni 60 kwa mwaka huku akiwa amelipa miaka miwili na hakuna shughuli inayoendelea zaidi ya kisima ambacho mabomba yake yanaelekea baharini.
=========
Nchi ilitafunwa na watafunaji wakafichwa ila sio na serikali. Wafichuaji walizibwa midomo. Inasikitisha sana