Wizi wa mafuta uliogunduliwa na DC Sara Msafiri sijaiona Waziri au Waziri Mkuu au Rais akilisemea, ni mradi wa wakubwa?

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,037
1,154
Ukisikiliza na kuiona Habari ya wizi wa mafuta baada ya flow meter ulioibuliwa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni akishirikiana na kamati yake ya ulinzi na usalama unapata picha wa husika walifanya hujuma hiyo wakijua Kuna Kinga toka kwa vigogo wa Serikalini.

Ni mradi mkubwa ambao ulichukua muda wa miaka takiribani mitatu hadi minne kumalizika ukianza na ujenz wa nyumba na ukuta mkubwa, karakana ya kubadili mfumo wa gari za mchanga kuwa na uwezo wa kubebwa mafuta, ujenzi wa mabomba na connection ya kuibia mafuta baada ya flow meter, mfumo wa ulinzi katika nyumba ile n. k. Ukiona na ukasikia simulizi utafikiri ni movie kumbe kweli.

Kutokana na unyeti wa tukio lenyewe, niliitarajia Waziri wa nishati angetembelea, Waziri mkuu angetembelea kujionea hali ilivyo, hata kutoa tamko juu la hilo, hata mama mwenye nyumba kutoa neno.

Kunyamaza kwa wakubwa kunaweza kuhatarisha maisha ya Mh. Sara Msafiri na angepatiwa ulinzi wa ziada, maana kwa jinsi ilivyo ni hatari sana.

Nashangaa hata Waziri Mkuu yupo kimya, atakuwa anajua huo ni mradi yao maana hata wazir wa nishati, hataki kuliongelea. Ikumbukwe issue ya malori, faster Waziri Mkuu alisafiri maana haikuwa na maslahi kwao.

Wambura akaua majambazi wawili tu kapandishwa cheo, Sara Msafiri kaibua uhujumu uchumi uliodumu kwa muda mrefu lakini hakuna aliyelitolea tamko hata kama kuna uchunguzi wa kamati ya ulinzi na usalama Kigamboni. Usishangae DC akapigwa chini au kuhamishwa.

Mwenye nyumba hajulikani, Serikali wangeichukua hiyo nyumba na eneo hilo kama wanavyotaifisha Mali na magari yaliyobeba magendo, kutokufanya hivyo mimi naamin huo ni mradi wa vigogo wa serikalini.
 
Wewe ni mpumba.vu.

Unajua kazi ya rais? Au kwa kuwa Magufuli alikuwa mpenda kiki unataka wote wawe wapenda masifa.

Polisi walipeleleza kila kitu ndio wakamchukua mkuu wa wilaya na waandishi wa habari kwenda KUUZA SURA.
Ahsante! Wewe ndiye mmiliki nini! Rais Samia asimamisha uongoz soko la Kariakoo,kazi inayoweza ikafanywa na wazir wa tamisemi au Rc.
 
Nadhani kikawaida taarifa ya wizi hutolewa na msemaji wa Polisi au DG wa TPA kwa upande wa wizi wa bandarini. Huyu dada huwa namuona ana kakiherehere
 
Asije tu akahamishwa, ama pia mkuu wa (w) uzalendo umemshinda na huwenda vitu hivi vimekuwepo kipindi kirefu na pengine alikuwa anafahamu Ila tu Kwa Sababu pengine wanaohusika ni jopo tu la Mwendazake Kwa maana ya Yule Mwendazake alikuwa akizungukwa,

Na tukumbuke, serikali iliyopo si Ndo ileile, kama svyo, basi mkuu wa wilaya alipaswa tayari angekuwa ameshapata uungwaji mkono kutoka hapo juu, lkn kiiimya!!
 
Ahsante! Wewe ndiye mmiliki nini! Rais Samia asimamisha uongoz soko la Kariakoo,kazi inayoweza ikafanywa na wazir wa tamisemi au Rc.
Huna kazi ya kufanya hadi unatetea upuuzi wako huoo uliouandika
 
Unajua kazi ya rais? Au kwa kuwa Magufuli alikuwa mpenda kiki unataka wote wawe wapenda masifa.

Polisi walipeleleza kila kitu ndio wakamchukua mkuu wa wilaya na waandishi wa habari kwenda KUUZA SURA.
Huna akili wewe

Yaan Samia anaenda Sokon kariakoo kisimamisha watu

Suala zito km hili ,anachukulia poaa

Acha Ujinga.
 
Back
Top Bottom