Wenyeji wa Karamay, Xinjiang wanufaika na utajiri wa ‘Mlima wa Mafuta Meusi’

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
微信图片_20230724081604.jpg


微信图片_20230724081608.jpg


Mji wa Karamay uliopo mkoani Xinjiang, China, ni mojawapo ya maeneo yenye maajabu makubwa ya kiikolojia duniani. Tangu enzi na dahari mji huu ulihifadhi hazina iliyokuwa tuli kwa mamilioni ya miaka na baadaye kugeuka kuwa ardhi inayotema mafuta. ‘Mlima wa Mafuta Meusi’, unajulikana sana kama “Mlima tajiri zaidi nchini China”.

Katika kipindi cha miaka 60 iliyopita, Karamay imepitia mabadiliko ambayo hayajawahi kushuhudiwa, kutoka umaskini na kurudi nyuma hadi ustawi, kutoka jangwa kubwa la gobi hadi bustani ya kijani na kutoka ardhi isiyo na watu hadi yenye watu wengi. Nilichokihisi hapa kikubwa ni uvumilivu uliooneshwa na vizazi vya wafanyakazi wa mafuta na wakazi wa Karamay, waliokuja kutoka kote nchini ili kufikia lengo la kuchimba mafuta kwenye ardhi yao. Watu hawa wenye ndoto iliwachukua miaka mitatu tu kujenga jiji la mafuta kwenye jangwa lenye ukiwa.

Kwa lugha ya kabila la Wauyghur, Karamay inamaanisha “mafuta meusi” na hata jina la mji huu limepatikana baada ya kugundulika mafuta haya. Hivyo katika mwendelezo wa safari yangu ya kutembelea mjini Karamay mkoani Xinjiang, nimefika hadi kwenye mlima huu tajiri sana nchini China na kushuhudia kwa macho yangu jinsi mafuta yanavyotokota kwenye visima mbalimbali vya mafuta ambavyo vimehifadhiwa.

Baada ya kufunga safari ya takriban saa moja, na kutembea umbali wa kilomita mbili hivi kuelekea kaskazini-mshariki mwa mji wa Karamay, hatimaye tulifika kwenye mlima huu wenye mandhari yenye mazingira ya asili ya kuvutia. Kama kawaida tulipofika tu wenyeji wetu walitupokea na mara moja bila kupoteza muda walianza kazi yao ya kututembeza huku wakitupa maelezo ya kina kuhusu mlima huo. Kutokana na mafuta ghafi kufurika kwa miaka mingi, eneo hili likaunda mabwawa mengi ya lami. Bwawa kubwa zaidi lina urefu wa mita 13 na eneo la kilomita za mraba 0.2. Mafuta ghafi ya hapa yana ubora wa hali ya juu na hayawi mepesi kwa urahisi.

Tukirudi nyuma kabisa, wakati Jamhuri ya Watu wa China ilipoanzishwa, ilikuwa inahitaji sana mafuta. Ukosefu wa mafuta ulifanya maendeleo ya uchumi yawe ya polepole sana. Hivyo baada ya kugundulika dalili za uwepo wa mafuta kwenye Mlima wa Mafuta Meusi, Mei 29 mji wa Karamay ukazaliwa. Baada ya hapo ilipofika Juni 16 mwaka 1955 wahandisi wapatao 36 kutoka makabila madogo walikwenda kwenye ‘Mlima wa Mafuta Meusi’ kuchimba mafuta wakistahamili upepo, joto kali, na ukosefu wa maji.

Hatimaye, Oktoba 29 mwaka huohuo, Kisima Namba 1 cha mafuta cha Karamay, kikaashiria kuzaliwa kwa eneo la mafuta la Karamay, ambalo ni kubwa na la kwanza katika China Mpya. Hadi kufikia mwaka 1959, eneo la mafuta la Karamay likawa ndio kubwa zaidi nchini China kwa upande wa uzalishaji wa mafuta ghafi. Baada ya miaka hamsini, Karamay pia ukawa mji wenye nguvu, mvuto, na mzuri ambapo watu wanaishi maisha yenye mafanikio.

Kwa kuwa ‘Mlima wa Mafuta Meusi’ ndio eneo la kwanza kabisa kugunduliwa mafuta huko Karamay, hivi sasa limehifadhiwa na linatumika kama kivutio cha watalii. Ukiangalia pande zote, utaona maelfu ya mashine za kuchimbia mafuta zikisukuma mafuta mchana na usiku, na kutengeneza mandhari ya kipekee ambayo huvutia watalii kutoka nchini na nje ya nchi kwenda kujionea.

Kwa maana hiyo na sisi tulipofika juu ya kilima cha eneo hilo lililohifadhiwa, tuliona visima vingi vya mafuta. Sifa moja ya visima hivi ambayo ilinishangaza sana ni kwamba ukiruka ama ukitoa sauti kubwa basi mapovu ya mafuta yanaonekana kuwa mengi, ama kwa maneno mengine ni kwamba mafuta yanaonekana kutokota zaidi kama yaliyokuwa yanapikwa jikoni.

Moja ya kitu kilichonivutia zaidi kwenye kilima hiki, ni kuwepo kwa kisima cha mafuta chenye umbo la namba nane. Namba nane kwa Wachina ni namba yenye bahati. Pia kuna mnara wenye urefu wa mita 2.5 ulioandikwa maneno matatu ya kuchongwa mbele yake yasemayo Mlima wa Mafuta Meusi. Karamay imejenga eneo hili la kitalii likiwa na kauli mbiu ya “Maonesho ya Mafuta na Kupata Uzoefu wa Utamaduni”.

Katika kilima hicho pia kuna sanamu la mtu akipiga gitaa ambalo inaaminika kwamba ukiligusa, basi utaondoa mikosi yote iliyokuwa inakuandama, utapata baraka na mambo yako yatakwenda vizuri. Hakuna mtu asiyependa kupata baraka, hivyo mimi na wenzagu tukajikuta tukifuata mkumbo na kuligusa sanamu hili mmoja baada ya mwingine ili nasi tupate baraka.

Mafuta yanayochimbwa Karamay, mbali na kutumika kwenye ndege na magari pia yanatumika kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo za urembo, vitu vya zawadi n.k. Kwa sasa kampuni kadhaa maarufu za ndani na nje kama vile Halliburton (DBS Drill), Shirika la Viwanda la Kujenga Meli la China, Kiwanda cha Mabomba ya Chuma cha Baoji, na Kampuni ya Mashine ya Jiangsu Jinshi zipo Karamay. Maonesho ya Kimataifa ya China (Karamay) ya Teknolojia ya Mafuta, Gesi na Petrokemikali na Vifaa pia yamekuwa jukwaa lenye ushawishi mkubwa zaidi la maonesho ya vifaa vya petroli na biashara katika China Magharibi na hata Asia ya Kati.
 
Mafuta yanatumika kwa kazi gani haswa??Kwasababu hata oil chafu ni nyeusi na kitaalamu yanaitwaje
 
Back
Top Bottom