Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,362
- 1,130
Binafsi yangu nalitazama swala hili kama ni la kimfumo zaidi ya kuwalalamikia Polisi nchini maana tumesha poteza DIRA yetu. Kwa mtazamo wa haraka unaweza kabisa kuwalaumu zaidi Polisi na kutoa tafisri zote za kazi na majukumu yao lakini pia tunatakiwa kutazama amri waliyopewa ktk shughuli na kazi zao za siku hiyo.
Nimefuatiulia sana mijadala mbali mbali ktk ukumbi huu wa JF kusema kweli nimeshindwa hata kuchangia kwa sababu watu wote mnakwepa ukweli kuwa mfumo wa Utawala nchini bado ni wa chama kimoja chenye mamlaka juu ya ya kuwepo vyama vingi. Tunajidanganya sana kuwepo kwa UHURU wa vitabuni, HAKI za vitabuni na USAWA unaotazama ujenzi wa siasa za Ujamaaa na Kujitegemea..Kifupi Wadanganyika wamezidi kuchanganyikiwa zaidi..
Wadanganyika kwa fikra za Kijamaa tumeunda makundi ya chuki badala ya kukubali tofauti zetu kuwa msingi wa maendeleo yetu. Tofauti ya CCM na Chadema kuwa ni za kiitikadi na sio Kijamii, tofauti baina ya waislaam na Wakristu ni za kiimani na sii za kijamii lakini imefikia tunalazimishana hata ya kiimani na Kiitikadi kama yale ya Kikomunist tuwe jamii moja isiyotambua tofauti (diversity) hizi. Huwezi kupambana na tofauti hizi za jamii pasipo kuweka sheria inayopingana na kuwepo tofauti hizi kama alivyofanya Nyerere, ama Warusi ama Wachina. Hutaki tofauti ziwepo unazikwaza tofauti hizo kwa sheria (left) au kama unazikubali tofauti kuwa sehemu ya jamii basi unaziwezesha tofauti hizi kushiriki sawa ktk ujenzi wa jamii hiyo (right) - Hakuna kitu nusu nusu ingekuwa hivyo wanafalsafa wangeisha andika aina hii ya mfumo wa kiutawala ktk jamii.
Kina Nyerere hawakuwa wajinga kuzima kabisa Ukabila, Udini na makundi baina yetu kwa serikali kuchukua jukumu lote la uongozi na kufuta kuwepo kwa tofauti za kiimani na makundi ya kisiasa (vyama vingi) ili kujenga Taifa moja lenye fikra moja na mwelekeo mmoja tofauti na nchi za Ulaya ambao walitambua tofauti zao (diversty) wakaziwezesha tofauti hizo kwa haki na usawa ili wapate kuishi pamoja kwa kutambua na kuthamini UTU wao. Diversity ni pamoja na ku accept one another for who we are, hivyo kuwepo kwa vyama vingi hakuna maana ya Uadui isipokuwa kukubali kutokubaliana ktk misingi ya kiitikadi..
Maadam leo tumekubali kuwepo kwa vyama vingi inatulazimu tukubaliane na kuwepo kwa falsafa zinazokinzana na ndizo hua nguzo ya usajili wa vyama. Lakini bahati mbaya tanzania usajili wa vyama umetokana na chuki baina ya watu na watu ndani ya vyama. Kama simpendi dr.Slaa siwezi kuwa Chadema na kama zimpendi JK basi lazima nijiunge na Chadema sio CCM. Siwapendi waislaam siwezi kuwa CUF na sasa imefikia Uchadema nao kupewa tafirisi ya zile zile za chuki baina ya makundi ya watu. Yote haya yanatokana na mfumo mbovu wa kiutawala unalenga kujenga Taifa moja lenye watu waitwao WATANZANIA lakini tofauti zao za kijamii (diversity) haikubaliki. Leo hii Chadema ni adui wa CCM hata kama mtajaribu vipi kupamba hoja zenu za Utaifa.
Ndugu zangu, tunaelekea kubaya sana, tumechukua mfumo ambao sii wa Kikokumunist wala Kibepari isipokuwa kati kati na kwa kuiga ambapo tunataka Utaifa kwa kujenga Taifa la watu wasiokuwepo. Tunazo tofauti zetu wenyewe sio sawa na zile za Urusi, ama Ulaya na lazima tuzikubali na kuziwezesha kisheria ili tupate kuishi pamoja laa sivyo CCM na Chadema watakuwa maadui wa kudumu na mwenye kushika Mpini (nguvu ya dola) ndiye mwenye haki zote (winner takes all). Tunaendeleza mfumo wa kikoloni kwa sababu mfumo mzima haukutokana na watu wake bali tumeiga na kuchambua chambua manyambuyambu ya ukoloni.
Hivyo basi, kutofautiana kimawazo ni jambo moja tofauti na kutokubali kuwepo kwa fikra ama kundi pinzani. Kinachotokea Tanzania ni kwamba tofauti zetu hazikubaliki na wala hazitakiwi kuzungumziwa ktk UTANZANIA maana sisi wote tunaamini kuwa ni Watanzania hatuna makundi kumbe makundi hayo yapo na yanakubalika kijamii. Na ndio maana hata maandamano haya yanasemekana ni ya Chadema, wanaofanya fujo ni Chadema sio wanaCCM, wanaCUF na wala hawataitwa watanzania ktk dhana ile ya Utanzania japokuwa msingi wa maandamano haya ni kwa Watanzania.
Nitaendelea kuomba tusiwalaumu sana Polisi kwa sababu wao wamepewa order ya kuchukua hatua yoyote necessary kuzuia maandamano ya Chadema (sio Watanzania) na wanaifanya kazi hiyo kwa kufuata maagizo toka juu kwa wenye kushika mpini. Tutaendelea kuwa katika hali hii hadi siku tutakapo kubali kwamba sisi ni watanzania na tuna tofauti zetu za kifira ambazo zimepewa haki ya kikatiba kushiriki kikamilifu ktk ujenzi wa taifa hili. Kama hatutakubali kuwepo kwa fikra tofauti kama za wanaChadema dhidi ya Utawala wa CCM ama hata fikra za mwalimu, basi itakuwa kazi bure hata kuwa hukumu wote watakao endeleza chuki maana mfumo wenyewe umejengwa kututenganisha..
Mkandara,
Tunahitaji elimu maalum kwani inaweza kutuepusha kufikia ufumbuzi kwa njia ya Maumivu na taabu kama tunayoipitia sasa.
Unyama ni utambulisho kwa Wanyama wote wanaoishi mbugani pamoja. Unyama ni commonness na unity inayofanya diversity ya hao wanyama wengi. Kwa kuwa wanyama WANATII unyama wao na diversity yao kama jamii wanakuwa HAWANATATIZO linaloipata jamii ya WATU na UTU wao.
Wanyama wanakubaliana ndani ya Unyama wao kuishi pamoja huku wakizingatia utofauti wao kama wanyama lakini usio pinga unyama wao. Yaani, tumbili, simba, chui, viboko, tembo nk pamoja na kuwa wanaonekana tofauti napamoja na kuwa wanazingatia tofauti zao na kuziheshimu lakini bado ni Wanyama na kwa kuzingatia tofauti zao wanajenga ecosystem ambayo nayo inawatedea haki kwenye uso wa dunia kwa kuwapa maisha bora na yeneye mafanikio.
Kwa jamii hii ya wanyama hakuna tatizo la elimu kwani Divesity imetumika ku reinforce the unity which is the essence.
Kwenye familia Baba kama kiongozi anajikuta na watoto kumi. Anajitahidi kuwajenga pamoja na tofauti zao za ujana kuwa LAZIMA kutotofautiana na lazima kuwa familia moja yenye umoja na mshikamano. Inafika hata wakati mwingine anapitiliza na kuwalazimishia, Imani, lafudhi ya lugha ya kabila lao, aina ya mavazi, sanaa, itikadi za siasa, mke au mume wa kuoa au kuolewa nk. Wanapokuwa kwenye umri mdogo hilo linaonekana kama kuwezekana na kuonekana kama familia iliyoshinda tofauti zote na kusimamia UTU na maadili ya familia na/au kwa mtizamo mpana unaweza kuliona TAIFA LETU!
Sasa lina miaka 50 kila mtoto kakomaa! Sio motto tena!!Anajitambuana anataka kujielelza kila mmoja kwa uhalisia wake.
Mkuu wangu umeniambaia sasa tujitahidi tuwaelimishane kuwa "KIMSINGI TOFAUTI ZETU HAZINA TATIZO .." wote kama familia au TAIFA tuzikubali kwa hekima na busara na kuzielekeza kujenga "Umoja wetu" wa UTU kwa kuwa wote sisi ni WATU kama familia na kama Taifa. Kwani Mbona WANYAMA na UNYAMA wao huko mbugani wamefuzu na kulitekeleza jambo hili kwa VITENDO. Mbona WATU wa ulaya na UTU wao wa ulaya wameweza?
Itashindiakana vipi kwa UTU wa WATU wa Tanzania wenye umriwa miaka 50? Tuuite UTU wa Watanzania kuwa ni UTANZANIA kwani ni kweli Utu ni mmoja lakini wenye kubeba Tofauti (Diversity) kadhaa zinazoendena na kila Mtu!
VEMA! Tukubaliane kuwa sasa Tutoe elimu ya Utanzania unaobeba na kuheshimu tofauti za kila mtu na imani yake, itikadi yake, jinsia, tamaduni, mavazi, taaluma nk. Nasisitiza elimu kwani bila elimu tutafikiaje lengo hilo? Mtaniambai?
Kwa kuwa Almasi itabakia kuwa almasi, Unyama kuwa unyama na Utu kuwa Utu, basi tunaamini hatuwezi kama Watu kushindana na ukweli huo.
Kwa kushindwa kuelimishana na kutii elimu hiyo basi Uasili ambao ndio Utu na Ubinadamu wetu utatuadhibu vikali kama njia ya UASILI HUO Kutafuta Utambulisho wake usiopingika kwa mamlaka yeyote ya kibinadamu. Tuki elimika, kuerevuka na kukubali kukokota tofauti zetu katika kujenga na kurutubisha Utu amabao ndio Utanzania wetu tutaokoka waandishi wa habari kulipuliwa kinyama, vijana kukibizwa mtaani na polisi kama panya na paka, VITA, MAJANGA, MATESO, MAUMIVU ambayo honestly "IS JUST A WAKE UP CALL" ya kuturudisha kwenye Uzalendo na Utanzania wetu unaobeba tofautizote kwa HESHIMA NA UELEWA unaoatikana ndani kabisa kwenye UTU wa MTU.
1. Ni nani atoe elimu hiyo? 2. Kama Sio CHADEMA ni CCM? 3. Kama sio kwa njia ya ELIMU juu ya swala hili ni njia IPI Itumike?
4. Kama njia zote zikikataliwa si kweli kwamba kinachotokea sasa hivi Tanzania tukiache kienedelee kwa amani na utulivu kwani MWALIMU atakaye tufaa atabaki kuwa ni MAUMIVU NA MISUGUANO MIKALI! Kwani huko Ulaya na Marekani walifika vipi hapowalipo? Kwa Chaki na Mwalimu wa darasani au Maumivu ya Minyukano kama inayoendelea hapa kwetu sasahivi? Ninaami kuna tumaini jema na kuwa Tutakubali kujieleimisha na kubadilika kwa hekima na busara.