Zao kubwa, bora zaidi na la mwisho kabisa la TAFAKARI ni MANTIKI...(Reasoning destination=LOGIC-the Climax of Reasoning). Na hakuna MANTIKI kuu ya maisha ya binadamu kama UTU! UTU ndio msingi mkuu wa maisha yetu, UTU ndio sheria asilia, kanuni, ustaarabu na taratibu asilia zipasazo kumfunga binadamu kulinda ubinadamu wake ili asiwe mnyama! UTU ndio MANTIKI iliyo kubwa kabisa!
Tukae chini, tuzame katika tafakari nzito, tufikie kilele cha juu kabisa cha tafakari, tutafikia MANTIKI ya maisha yetu, mimi napenda kuiita UTU!
Falsafa yetu ili iwe na tija kwetu, ni lazima ifungwe na MANTIKI HII = UTU! Falsafa zenye UTU, zitahitaji mfumo mahususi kuzisimamia, mfumo huo utazaa sera sahihi kuusimamia, sera hizo zitahitaji sheria mahususi kuzisimamia, sheria hizo zitahitaji imani, mila, desturi, itikadi, matendo, mitazamo, n.k. mahususi kuzifanya hai! Tunaweza kuanza mfumo hadi Falsafa, vilevile Falsafa hadi mfumo ni sahihi zaidi!
TUKAE CHINI! Nirudie tena, sishangazwi na chochote kitokeacho kwa sasa, kwani HULKA ZA BINADAMU ZINAPOFIKIA UKAMILIFU WAKE ZINAWEZA KUFANYA CHOCHOTE na matokeo yake siku zote huwa HASI, hali kadhalika MANTIKI INAPOFIKIA UKAMILIFU WAKE NAZO ZINAWEZA KUFANYA CHOCHOTE na matokeo yake huwa CHANYA!
Maisha ni Furaha kama haipo ni UPUMBAVU na UPUUZI MKUBWA, na hakuna furaha ya mtu ila watu!
Mungu wetu anaita sasa!
Falsafa ndiyo ingeamua nini kiwepo au kitokee nini kwa wakati gani!
Ni zaidi ya Dira ama msingi! Ni JINSI GANI TUNAPASWA KUISHI kwanini, kwa namna gani, ili iwe nini na kwa nani! Hapo ndipo Falsafa kuu inapohitaji kufanywa maisha yetu halisi, yaani kuanzia ngazi ya imani, mila, desturi, itikadi, mitazamo, mienendo, vitendo, n.k. vitakayosadifu na kufungwa na falsafa kuu. Kisha hayo yatazaa sera bora kusadifu na kufungwa na falsafa kuu, sera hizo zitazaa sheria zitakazosadifu na kufungwa na falsafa kuu, sheria hizo za kiuchumi, siasa na utamaduni zitazaa mfumo utakaosadifu na kufungwa na falsafa kuu! Hapo kila kitakachotokea, au tutakachotaka kufanya, kitapimwa kwa mizani ya falsafa yetu kuu!
TUJIULIZE LEO: Ni falsafa ipi ituongozayo, itufungayo na kututambulisha?
Sheria zinatungwa kwa jinsi watu wajisikiavyo tu, ameshawishiwa na mkewe ama rafiki yake mweupe, anasimama jukwaani "tunataka rais asishtakiwe 'katiba iseme' " wengine nao "tunataka utawala wa majimbo" hawa nao "tunataka serikali tatu/mbili/1" laiti kama tungekuwa na Falsafa yetu, kusingekuwa na malumbano yasiyokuwa na msingi kama yale yanayotokea Dodoma! Kila mtu angepima mawazo yake katika kupata mashiko kwenye falsafa yetu! Kama ameyaona anayawasilisha kwetu.
Ninaamini kabisa haya yatokeayo leo, yasingekuwepo kama tungekuwa na falsafa yetu, labda tu kama ingezaliwa kutokana na HULKA za binadamu na si MANTIKI ya mambo, naita UTU!
Taifa pasi na Falsafa bora, raia wake huongozwa na HULKA na MATAMANIO yao, na hapo UKINZANI ndipo uibukapo, ni chuki na visasi, hofu na umungu kila mtu atapigania kuwa juu ya mwenzake, mauaji kama pombe...matabaka, unyonge, n.k Haipo Falsafa ya kutufunga!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani, anaita sasa!
Zakumi,
Mkuu wangu shukran sana kwa kuliweka swali hili.. nadhani swala zima linatakiwa kutazwa toka nje ya sanduku la Uchadema au UCCM kwa sababu sio CCM ama Chadema wanaowawezesha Polisi kuwa brutal isipokuwa mfumo mzima wa kiutawala..
Nadhani unakosea unaposema hakuna umuhimu wa Falsafa ya uhai wetu kama WATANZANIA na sio fikra za uhuru wa bendera unaolenga sovereignty na mipaka ya nchi husika..Falsafa ni uhai wa WATU ktk mazingira (A system of values by which one lives) na hizi values ndio huwa Principal ya Utaifa wa watu hao.. Hivyo hata hao unaosema Fascism ni Falsafa kwa watu wale.. Hivyo kuwepo kwa Fascism ndiko kunako tulazimisha sisi kuwa na Principal zinazopingana na fikra kama hizi ili tuwe na zile zinazotulenga sisi kama Watanzania - Principles of reality. Na ndio maana muda mwingi nimesema sana kuhusu sisi kurudi nyuma na kujitazama, kujitambua who we are kwanza kama Taifa, laa sivyo leo hii tusingekuwa tunabishana humu isipokuwa kutazama ethics na values zetu kujua ni wapi tunakosea..Ukiona watu wanabishana juu ya jambo basi elewa ni kwa sababu wamepoteza DIRA hivyo ethics na values..
Binafsi yangu nimekuwa na matatizo na hili neno UTU linapochukuliwa kama faslafa kwa sababu UTU ni ile quality of being human ambapo maswala muhimu ya Uhuru, haki, na Usawa vinapotafsiri fikra, maamuzi na matendo yetu ktk mazingira tuliyopo. Hivyo faslafa kwa mapana yake tunatazama falsafa ya maisha..Haya yanayofanyika Tanzania leo ni kutokana na sisi wenyewe kutothamini UTU hivyo tumepoteza ethics na values hata kwa kutumia logical reasoning tunabishana kutwa nzima. Mtu atasimama kueteta Ufisadi, mwingine atasimama kutetea Polisi kwa sababu hatuna values ktk utu wetu isipokuwa ule anaouthamini yeye..
Kila mmoja wetu humu ana values zake aidha iwe za kiasili au imani ya dini au Upagan na hakuna control tena ndio maana tunazitetea. Jambazi sugu litasifika na kuitwa Pedejee - jizi hili!, Fisadi atasifiwa kwa kuiba mabillioni na kujengea wanawake nyumba na mashangingi na wanaolalamika ndio wenye wivu ujinga na hila. Pengine niongezee kusema (mtanisamehe) hata wakristu hapa janvini hawawezi kumtazama Muislaam kama mwenzao isipokuwa ni WALE, WAO against SISI kama kundi tofauti la kijamii ktk Utanzania wetu hivyo hata kuyasikiliza machungu yao inakuwa bughudha kwao. Amini maneno yangu huwa nashindwa kuelewa kwa nini jamaa zangu wakristu tunapowaambia serikali inawakandamiza waislaam wana question waislaam na sio serikali? halafu unaambiwa tuko pamoja!.. Chadema wanailalamikia serikali kuhusu Mafisadi nchini lakini wanaCCM wanawa question Chadema uhalali wa madai yaokuwa ni uzushi, wadini, wenye wivu na wakosa..
Ni katika hali hii ya utengano wa ambao uemtokana na kutokuwa na dira ya Kitaifa ndio maana kikila mmoja wetu anaiona haki upande wake na dhulma anapokosa..Hata ukimuuliza Chenge kuhusu Ufisadi atakuona mchawi tu kwa sababu kisha jitenga na kundi la maskini, wajinga na wenye maradhi. Vile vile ukimuuliza mwana CCM atakujibu kuwa Chadema wajinga wanalalamika tu kwa kila kitu wakati ni wao wenye kuleta vurugu.
Umoja wetu umesha kwisha vunjika na sii kazi rahisi kurudisha Umoja huu pasipo ku sacrifice UBINAFSI, UMIMI, USISI kwa kutambua sisi ni taifa moja lenye watu wenye tofauti zake za kijamii. Hata Nyerere alianzia hapo kabla ya kubuni Azimio la Arusha maana inakulazimu uanze na Watu (walikotoka na walipo) ktk Mazingira (maliasili na rasilimali zake) ndio unaweza kuipata picha halisi ya unakotaka kwenda. Tukiweza kundoa ubinafsi na kila mmoja kujenga Uzalendo mkubwa utakaolazimishwa na PATRIOT ACT ya kwetu kusisitiza UZALENDO wa kila Mtanzania kufuata falsafa yetu itayolingana na WATU na MAZINGIRA yetu -Principal of reality..
Mitazamo yote hii ya Ubinafsi inatokana na kwamba kila mtu kabeba msalaba wake hivyo badsi hata Chadema wakiingia Madarakani nina hakika watafanya kile wanacho kiamini japokuwa hakitakubaliwa na wengine. Mafisadi watalaani, pengine Polisi watatumiwa kuwanyanyasa wenye nacho na pengine mauaji kutokea..It all round up to what set of ideas or beliefs developed into policies relating to particu
AshaDii,Nakubaliana na Mario Puzo Pia, ila at the end of the day hata kama haoneshi anger ni mtu wa kuchukua 'action' mradi apata kile ambacho kapanga. Katika hili naweza tumika msemo ambao naukubali sana katika kupanbana na adui hasa katika vita (toka katika kitabu cha The Art of War), ni ya centuries ago but still applicable to any war which could ever occur.
If your enemy is secure at all points, be prepared for him. If he is in superior strength, evade him. If your opponent is temperamental, seek to irritate him. Pretend to be weak, that he may grow arrogant. If he is taking his ease, give him no rest. If his forces are united, separate them. If sovereign and subject are in accord, put division between them. Attack him where he is unprepared, appear where you are not expected. - sun wu (Chinese Military Strategist).
Nakubaliana na Mario Puzo Pia, ila at the end of the day hata kama haoneshi anger ni mtu wa kuchukua 'action' mradi apata kile ambacho kapanga. Katika hili naweza tumika msemo ambao naukubali sana katika kupanbana na adui hasa katika vita (toka katika kitabu cha The Art of War), ni ya centuries ago but still applicable to any war which could ever occur.
If your enemy is secure at all points, be prepared for him. If he is in superior strength, evade him. If your opponent is temperamental, seek to irritate him. Pretend to be weak, that he may grow arrogant. If he is taking his ease, give him no rest. If his forces are united, separate them. If sovereign and subject are in accord, put division between them. Attack him where he is unprepared, appear where you are not expected. - sun wu (Chinese Military Strategist).
..Is it a concidence you read the books that I read? Adui yetu wote ni mtu anayetaka kutuona tunasambaratishana kwa ajiri ya manufaa yake binafsi. Huyu tuombe Mungu amrudi na tumkate kwa nguvu zetu zote.
Unaona jinsi msemo huu unavyoweza kutubabaisha..Tunaposema Adui yetu? huyu adui ni nani maana CCM wanaweza kusema hivyo, Chadema wanaweza kusema hivyo, CUF, Waislaam, wakristu, Wahindi, waarabu, weusi au Wazanzibar wanaweza kusema hivyo...Na hii yote inatokana na sisi kutojitambua kama Taifa moja na watu gani. Hadi leo hii we have nothing in common isipokuwa politics zetu zinaelemea ktk KUTAWALA ama KUTAWALIWA ktk mipaka ya nchi huru.Adui yetu wote ni mtu anayetaka kutuona tunasambaratishana kwa ajiri ya manufaa yake binafsi
...Tulipokwama hatuwezi kutoka ikiwa sisi maskini wote hatutakuwa na agenda moja. Zama za Mwalimu maadui wetu wa nje walikuwa ukoloni mamboleo - Mabeberu Imperialists), Kupe wanyonyaji (wawekezaji) na kdhalika kisha maadui wetu wa ndani walikuwa Umaskini, Ujinga na Maradhi.. Leo hii nambie maadui wetu ni kina nani? kila mmoja wetu atamnyooshea kidole Mtanzania mwenzake kwa sababu ni CCM, Chadema, Muislaam, Mkristu, Mwarabu, Mhindi, Tajiri, Maskini, Mbara au Mzanzibar yaani tumerudi ktk hali mbaya sana kuliko wakati wote wa Utawala wa Nyerere...
..
Ndahani,
Nimwekea buluu sehemu hiyo! Adui yetu wote ni mtu anayetaka kutuona tunasambaratishana kwa ajili ya manufaa yake binafsi!
Mara ya kwanza nilifikiri nimeelewa vizuri na kuwa huu mtizamo utatufaa kama Taifa! Ghafla nikagundua kuwa CDM Watautumia kwa Mtizamo wao, CCM hivyo hivyo Polisi nao hivyo hivyo ....
Azimio Jipya,
Unaona jinsi msemo huu unavyoweza kutubabaisha..Tunaposema Adui yetu? huyu adui ni nani maana CCM wanaweza kusema hivyo, Chadema wanaweza kusema hivyo, CUF, Waislaam, wakristu, Wahindi, waarabu, weusi au Wazanzibar wanaweza kusema hivyo...Na hii yote inatokana na sisi kutojitambua kama Taifa moja na watu gani. Hadi leo hii we have nothing in common isipokuwa politics zetu zinaelemea ktk KUTAWALA ama KUTAWALIWA ktk mipaka ya nchi huru.
Unajua kwa nini Nchi za majirani zinatupiga bao leo hii?.. Ni kwa sababu wanajijua wao ni WATU gani na nini ethics na Values zao. Kenya hudai sehemu ya Tanzania kuwa yao kutokana na kuwajali makabila yao yaliyomo tanzania, Uganda, Malawi na hata Kongo hutanguliza kutazama WATU wake wamefika mipaka gani kufikia kudai ardhi hizo wakati sisi tunatazama ramani na kujaribu kuilinda mipaka hiyo.. In fact hatuna ushahidi pale mipaka inapoonyesha kula kwetu kama swala la Malawi..
Ujamaa ulikuja na mazuri yake mengi tu lakini pia Ujamaa ulitujenga kuwa kitu kisichokuwepo leo hii. Enzi za mwalimu hatukuwahi kuulizana kabila au dini lakini leo ni jambo la kawaida kabisa lakini tumefungwa akili zetu kutazama nje ya Ujamaa kwa kuendelea kuaminishwa kwamba sisi bado ni wajamaa wakati sio wajamaa bali wabinafsi. Hivyo CCM wanajitenga kama wao, Chadema wanajitenga kama wao, Polisi wanajitenga kama wao nasi walalahoi tunajitenga kama sisi na kila mmoja wetu akitazama maslahi yake.. UBINAFSI ndio sumu ya yote haya na ndio UTU unapotakiwa - Kushikamana, kupendana na kushirikiana kama Watanzania ni mada nzito zaidi ya utunzi wa falsafa yenyewe. Na ndio maana hata hiyo Katiba mpya tunayoitegemeahaitaweza kuondoa kero na karaha zetu kama haitawezi kutambua kwanza sisi ni WATU gani na tupo ktk mazingira gani. Nachoamini mimi sisi wote ni maskini.. Hivyo falsafa yetu lazima izingatie Umaskini wetu kwa kuwalinda watu maskini ambao ukombozi wao utatokana na umoja wao.
Tulipokwama hatuwezi kutoka ikiwa sisi maskini wote hatutakuwa na agenda moja. Zama za Mwalimu maadui wetu wa nje walikuwa ukoloni mamboleo - Mabeberu Imperialists), Kupe wanyonyaji (wawekezaji) na kdhalika kisha maadui wetu wa ndani walikuwa Umaskini, Ujinga na Maradhi.. Leo hii nambie maadui wetu ni kina nani? kila mmoja wetu atamnyooshea kidole Mtanzania mwenzake kwa sababu ni CCM, Chadema, Muislaam, Mkristu, Mwarabu, Mhindi, Tajiri, Maskini, Mbara au Mzanzibar yaani tumerudi ktk hali mbaya sana kuliko wakati wote wa Utawala wa Nyerere.
Mourinho,
Kuhusu swala la Nchi kukosa falsafa inayotuogoza.
Nadhani hii kuna wakati imejadiliwa hapa kama mada iliyeelta hoja na mitizamo mbalimbali!
Kuna ambao walidhani kuwa hili sio tatizo la msingi kwani kinachotakiwa ni uogozi unaotoa matokeo ya kazi iliyofanywa. Kuna wengi ambao waliunga mkono dhana hii Mimi nikiwa mmoja wao na kumbuka hara Mkandara aliona hii kama hoja.
Mkuu nadhani tusaidiane sasa! Falsafa ya Taifa iwe ni ipi? Tunaitoa wapi?
Mkandara. Zakumi na JingalaFalsafa, KUHUSU FALSAFA YA TAIFA!
Guys lets just be serious for some seconds!
1. Awali Mkandara ulituambia kuwa tuna various DIFFERENCES at individual level which form DIVERSITY at a community a Nation level.
2. THEN, Ukapendekeza kuwa tutafute kitu ambacho ni COMMON out of all differences which can form our community with its diversity respected and well taken care!
3. JangalaFalsafa anakubaliana na Mimi kuwa that COMMON UNITY which unity us all Should be UTU whatever that term stand for!
4. JangalaFalsafa ameonyesha jinsi ya kujenga sera, mifumo and policy from UTU which will meet the need of the TOTAL DIVERSITY! WHICH CAN BE TERMED AS FALSAFA YA TAIFA!
5. FALSAFA YA TAIFA, kama Zakumi ataniruhusu kuuita UTU WA TAIFA Haitapingwa na CCM, CHADEMA, WAKRISTO, WAISLAM, POLISI,WAPAGANI,MAKABILA, UKANDA,MASIKINI, TAJIRI ... NAME ALL THE DIVERSITIES !!!Haitapingwa maana jamii nzima itaelimika juu ya dhani hiyo na kuiona ya thamani kubwa kuliko hata tofauti zao.
6. Elimu ifanyike kuwaamsha Watanzania kuhusu umoja wao ambao hauwezi kupuuzwa wala kuchezewa na chochote kile ndani ya kuheshimiana na kuridhiana kwenye kila tofauti zetu na kutukuza umoja wetu kwa kila hali.
Je hii ndio namana ya kejenga falsafa ya Taifa itakayo liokoa taifa hili lisitumbukie kwenye giza kubwa lililoko mbele yake?
History will have to record that the greatest tragedy of this period of social transition was not the strident clamor of the bad people, but the appalling silence of the good people.
Zakumi,
Let me give you an answer. Do you remember the mutiny of 1964? Nyerere used that as an opportunity to retrain our army and it became the peoples army. When we take over we will retrain the police force to become the people's police and not the fisadi police.
Is it a concidence you read the books that I read? Adui yetu wote ni mtu anayetaka kutuona tunasambaratishana kwa ajiri ya manufaa yake binafsi. Huyu tuombe Mungu amrudi na tumkate kwa nguvu zetu zote.
AshaDii,
Nimesoma sana where I have blued! Inaonekana una insight fulani but honestly simalizii kujua kabisa kabisa kuwa nini hicho kimekusumuka kusema hivo? Najua hujali kufafanua ... !
zomba,
Nimeona picha uliotowa na ujumbe wake ambao naomba ninukuu "ILANI ILANI ILANI ILANI Watu wote mliokusanyika hapo maamriwa na Serkali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuondoka kwa haraka na kwa amani la sivyo tutatumia nguvu" Kwa kutumia picha hii ambayo ni msingi naomba kama hutajali nijuze haya:
- Kuwepo kwa kutumika hio Ilani iliyotolewa, je ina justify kipigo ama jinsi alivo uwawa marehemu Mwangosi?
- Naomba nijue msimamo wako wa tukio lote lililotokea Iringa na juu ya Kifo cha Marehemu Mwangosi.
- BTW katika vurugu zote ambazo hutokea kwenye mikutano ya CDM kwa mtazamo wako nani anatakiwa kulaumiwa kati ya police na CDM na hasa zaidi am more interested in understanding why wakulaumiwa alaumiwe kwa vigezo gani.
Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari
JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.
"Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa " alisisitiza kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa."Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.
Source: Political Issues
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya. Source: Political Issues
Do not approach police lines to attempt to cross to safety. Police are in place to confine the unrest and prevent its spread. Their orders are usually not to allow anyone to pass. The use of riot control measures, including rubber bullets, tear gas, and water cannons originate from the police line, and the likelihood of injury is greatest there.
Source: How to Survive a Riot: 2 Methods - wikiHow
Jasusi,
My take on when CDM takes over, the major change of all overall change in the system will be a brand new party in ruling for the first time since independence. The change in Tanzania and its citizens will be for the better (minimally) or for the worse (crucially) depending on how the major problematic issues in each sector will be tackled by CDM. While my belief is that it will be briefly for the worse... We should just brace ourselves for whatever is in store for us.
I genuinely don't believe that there will be so much change to the extent that everything will be alright overnight, It will take time with a combination of other lubricating factors. I believe there will be hard work and the times more complicated that they are right now. I also believe that MOST CCM leaders (some even considered as the so called 'Fisadi' will also be in the CDM action pic with the CDM's leaders blessings (whether visibly or under the carpet)
Nashindwa kuelewa kwa wale wenye kasumba ya kufikiria kuwa CDM ikija kila kitu kitakuwa sawa... Na kwamba Police watawasiliza wananchi kuliko viongozi wa serkali. Nakataliana na hilo, mambo mengi yatakuwa vile vile (na I say it confidently kabisa na God willing after years I am hoping to come back to the post and declare 'I said so').
I may be too cynical but that is what I believe. Hapa what matters ni kuwa wao CDM wakija maamuzi watayotoa will they be selfish to themselves or selfless?
zomba kuna wakati mwingine mkuu wangu sio lazima uchangie kitu hasa ktk maswala mazito kama haya kwa ushabiki wa chama. Uchadema na UCCM ni vitu vingine kabisa inapofikia kifo cha raia, mwananchi tena mwandishi wa habari ambaye hakuwa na silaha isipokuwa akiwa kazini. Zaidi ya hapo Polisi waliambiwa wazi kuwa huyo wanayempiga ni mwandishi wa habari na walimwona aki record pande zote mbili na mfarakano na hata huyo mkuu wa Polisi alimwona vile vile.1. Kumbuka haikuwepo ilani hiyo tu pekee, kwanza kabisa vyama vyote mkoani Iringa walishatangaziwa na Polisi wasifanye mikutano ya kisiasa wakati wa kampeni, wajizuie kwa wiki moja.
Ilani zilizotolewa zaidi ya hiyo ya kitambaa:
Halafu walitangaziwa siku ya tukio, licha ya hicho kitambaa cha ilani, walipewa ilani kwa njia ya vipaza sauti kuwa wasambaratike.
Kwa hiyo hili la Ilani utaona kuwa ni ukaidi ulifanywa makusudi kabisa na wanachadema wa Iringa, kwa nini? isitoshe:
Sasa wewe jiulize na ujibu, ikiwa mmepewa Ilani zote hizo na Polisi na mkakaidi na mkaingia kwenye vita na wao kwa dakika 30, halafu atokee mmoja hukohuko kwenye kundi linalipogana na Polisi aje amvae Mkuu wa kikosi, kwa nia yoyote ile, unafikiri kutakuwa na usalama kwake hapo?
2) Tukio lote lililotokea Iringa nalichukulia ni uvunjifu wa amani wa makusudi kabisa kwa "wapiganaji". Siasa sio kukaidi amri za Polisi kwa nguvu, hivi unategemea nini baada ya kuvunja amri za Polisi? Licha ya kuwawametangaziwa, hata ikitokea tu kuwa wamejikusanya kikundi cha watu ambapo polisi wanaona hapa kuna uwezekano wa amani kuvunjika basi wana haki ya kuwaambia watawanyike bila ilani yoyote ya kabla.
Sasa jiulize tena, hivi walikusudia nini hawa waliokaidi amri zote hizo na kupambana na mapolisi?
3. Ikiwa umeambiwa usifanye maandamano, ukayafanya kwa nguvu, ukatokea uvunjifu wa amani kwa polisi kuzuwia hayo maandamano, hapo unategemea nani alaumiwe?
Ikiwa unaambiwa usifanye mikutano siku fulani, wewe unaumuwa kufanya kwa nguvu wakaja polisi kuzuwia mkusanyiko huo ukakaidi na kupigana na Polisi ni nani wa kulaumiwa?
Conclusion:
Licha ya hoja zote hizo juu zinazoashiria uvunjifu wa amani wa makusudi kabisa, hata kwa bahati mbaya ukijikuta wewe ni mpita njia kwenye vurugu (riots) za namna hiyo na Polisi wameshatowa amri ya watu kutawanyika na wameshajipanga kuwafata na kuwatawanya wakitumia zana zao za kuzuwia fujo, usijaribu hata siku moja kuwafata wanapotokea na kuingia kwenye himaya yao kutokea walipo wanaotawanywa, kufanya hivyo ni:
1) amma kujitafutia kifo (suicide) kwa makusudi kabisa,
2) au kujitafutia kifo cha kujitowa mhanga (terrorism),
3) amma kujitafutia kifo kwa ujinga wa kwenda kuanzisha fujo na kutokujuwa namna ya kujihami yanapokushinda.
Chaguwa wewe ni yepi katika hayo yaliyomkuta Daudi?
Ukweli ubaki kuwa ukweli.