AshaDii
Platinum Member
- Apr 16, 2011
- 16,190
- 18,078
Habari wana JF,
Hali ya nchini kwetu Tanzania hadi hapa tulipofika kwa sasa haijalishi kuwa tunaenda wapi mana tayari tumefika pabaya… Kwa kundi ama hali yoyote ile ifikapo pabaya dawa pekee ni suluhu ya hio hali mbaya iliyopo iondolewe mara moja kwa njia mbadala. Ikumbukwe kuwa unapokuwa na hali mbaya mara nyingi kama sio zote HAIJALISHI hio njia mbadala ni ipi maadamu tu ipatikane nafuu ya hio hali mbaya kutoweka.
Ifikapo hali imedorola hadi kuwa mbaya kwa wahusika, maneno matamu na kutia moyo hayana maana tena! Ahadi za kuwekewa uahueni kwa maneno yaliyowahi tayari kutamkwa na kujirudia kama nyimbo za chorus hazina maana tena! Kupozana na kupeana pole kwa maneno ya faraja na kusihi hakuna mana tena! Hii yote kwa sababu hali inapokuwa mbaya kamwe haipati unafuu bila suluhu ya kupunguza ama kuitoa kabisa hio hali ambayo kwa wakati huo tayari ni sugu.
Mara nyingi hata magonjwa kama vile kansa inapokuwa imepatwa katika kiungo na ikaonekana ni sugu ipo njia mbili tu za kutibu; unaua kabisa kiungo kwa kukata kabisa kitoke ili kisisambaze maeneo mengine, ama unaacha na hatima yake ni kifo cha kutaraji ukibaki unahesabu siku za kufa. Swali linabaki kama unaweza kupona kwanini ukubali kuhesabu siku za kifo chako?
Kwa muda mfupi sana kumetokea vifo (ambavyo tuna habari navyo) kwa mkono wa Jeshi la Polisi viwili. Ndani ya mda mfupi vijana wawili wenye nguvu ya kutosha kabisa kujenga taifa letu hili lililo sugu ya kutojengeka wamefariki.
Tarehe 27/08/2012 Ally Zona kafariki Morogoro baada ya polisi kuingilia kati maandamano yaliyokuwa sio rasmi ya CHADEMA kusababishia vurugu zilizopelekea kurushwa kwa risasi na hatimae kumpata yeye kichwani moja wapo ya risasi hizo, iliyopelekea kifo cha papo hapo.
Siku 5 baadae Jana tarehe 02/09/2012 kimetokea kifo kingine tena, safari hii mmoja wa wanahabari mashuhuri anaejulikana kwa jina la David Mwangosi. Vifo hivi vinasikitisha sana… Natoa pole toka moyoni kwangu kwa wafiwa wa hao marehemu. Sie tunalia kama taifa, wao wanalia kuwa mtoto/baba/kaka/mjomba na pengine tegemezi la familia limeyeyuka ghafla kwa njia ambayo ingeweza kabisa kuepushwa! Inasikitisha… Na inauma pia.
Maswala/swali ya msingi ya kujiuliza tokana na matukio hayo (Na mtazamo wangu juu ya hayo):-
Ni kweli kuwa kila vifo vya polisi ambavo vimekuwa vikitokea vinahusiana moja kwa moja na CHADEMA?
Kumekuwa na misemo kwa baadhi ya wananchi na hata pia wanajamvi kuwa chanzo cha vifo hivi ni vurugu za wana CDM; labda kwa sababu tu hizo vurugu chanzo chake huwa uwepo wa CDM hapo. Nabaki najiuliza na kushangaa, jamani watu wanapoteza maisha lakini bado tu hamfunguki na kutakasika hayo macho kuona picha halisia jinsi ilivo? Mie nakataliana na hii Imani kuwa CDM ndio wanasababisha kupelekea vifo hivo.
Wananchi wenzangu wanaomini katika hili, naombeni sababu za msingi za kuamini hivo na hapo hapo mnipe jibu kuwa wale vijana wanao uwawa kule migodi ya Barrick tena kwa kulinda maslahi ya wageni sio wazawa ni CDM husababisha? Mnasemaje kuhusu vifo vya vijana watatu walio uwawa hata wiki haijaisha kama tu wanyama Fulani, ha hapo hapo ni dhahiri kuwa case closed?
Ni kweli kila itokeapo kifo hicho kwa njia moja ama nyingine hao marehemu linakuwa ni kwa ajili ya makosa yao na uzembe wao hao marehemu?
Ingekuwa kuwa kila wanaofariki wapo katika kundi husika ambalo kwa kesi hizi za vurugu ni CDM, walau kunaweza kukajengwa chembe ya mbegu kichwani kuwa marehemu alikuwa akirusha mawe na kuletea fujo hao polisi wa kutuliza vurugu. Inakuwaje pale mtu ambae yupo kando kabisa anauwawa? Hapa ni dhahiri kabisa kuwa makosa na uzembe (tena wa makusudi) husukumwa na polisi wenyewe. Ni dhahiri pia kuwa Polisi wanakuwa hawana umakini na kazi yao, inakuwa kama vile wanabahatisha tu. Kwa kusahau wajibu wao kuwa wao ndio tegemeo na ulinzi wa mwananchi wa kawaida dhidi ya lolote lile ambalo laweza mtishia usalama!
Katika kutuliza hizo vurugu utumiaji wa silaha wa polisi hulenga nini hasa?
Ni ajabu sana, pamoja na kusema sio polisi na sina ujuzi huo - mimi nadhani na ninaamini kuwa katika taratibu za kazi kila kazi ina namna yake ya kufanya tokana na level ya hio dhana inayofanyiwa kazi. Inakuwa vipi kuwa kutuliza vurugu kunasababishia kutumika kwa vyombo vyo moto moja kwa moja kwa wananchi badala ya mbadala kama vile angani? Inakuwaje pale ambapo mwananchi wa kawaida hana silaha yoyote anauwawa bila kifikiria hata mara mbili? Hapa inanifanya nitoke na hitimisho kuwa polisi wanakuwa wamelenga kabisa kuwa lazima wajeruhi ama kuua mmoja kama kukomesha/fundisho ama kwa sababu zozote zile walizo nazo!
Madhara ya Vifo kwa mkono wa Polisi yanasukumwa zaidi na muitikio kuliko tukio lenyewe!
Maelezo na muitikio wa Wakubwa wa Polisi
Kutokea kifo tokana na uzembe wa kutumia silaha kwa polisi ni swala moja, Ila inapokuja swala la polisi kushindwa kuvaa kosa lao na kuwajibika ipasavo ni KERO ambayo kimsingi inaumiza na kushindwa kutoa picha kamili. Kuwa wao polisi ni wajinga ama wanatambua kuwa wananchi ndio wajinga? Mfano mdogo Kifo cha Marehemu Ally Zona Morogoro kimeelezwa na kamanda wa Polisi Morogoro kuwa kilisababishwa na kitu kizito kilichomgonga marehemu kichwani na sio risasi kama ilivodhaniwa…
Hii inaibua wazo na imani kwangu kuwa; yawezekana kabisa imesemekana hivo ili yeyote Yule asikamatwe kwa ajili ya kifo cha marehemu, kuwe na kielezo kuwa haieleweki hicho kipande kilitoka katika silaha ipi tofauti na kuripoti kuwa ni risasi.
Muitikio wa Viongozi wa juu wa Serikali
Katika hali ya kawaida ilitakiwa viongozi kuonesha ushirikiano hata kwa matamko ya swala zima lililotokea Morogoro kwa kusababisha kifo cha huyo kijana. Sio tu kwa msingi wa kifo cha marehemu, ila kwa msingi wa kusema chama kilicho kikubwa kwa upinzani kwa njia moja ama nyingine kinahusika na kufariki kwa Marehemu. Hasa baada ya kuingilia shughuli ambayo tayari ilishatolewa taarifa kuwa ipo na kutajajiwa. Kama lipo lililosemwa basi nimepitwa anatambua tafadhali anijuze.
Wanachi kuchukuliwa kuwa ni wajinga na wapumbavu!
Kwa mtitiriko na mwenendo mzima wa jeshi la polisi ni wazi wamechukulia kuwa mwananchi hana haki (kwa upande mwingine naweza kubaliana na hii mana jamii kwa upana haijuwi haki zake). Kwamba wanaweza kuvamia na kuamua lolote hata kuua. Na haijalishi kabisa wakiua wanaweza eleza lolote lile maadamu tu ionekane wameitikia hata kama ni kwa kusafisha jina lao ili kuonekana wana haki ya kufanya hivo maadamu wanafanya kazi yao.
Marehemu kuchukuliwa kana kwamba ni 'disposable'
Mwananchi wa kawaida na chini amechukuliwa kama vile mtu ambae hata haki, hana maana,hana tija wala umuhimu wa kulindwa. Anaendeshwa vyovyote vile na kupelekeshwa watakavo. Hata hivo Polisi inatakiwa watambue hizi ni nyakati nyingine… Na kubwa kuliko wananchi tumechoka! Hio inafanya hata kumshusha thamani huyo mwananchi anapofariki. Jinsi alivokufa na kuharibiwa Marehemu David Mwamgosi, maneno hayatoshelezi… Inasikitisha.
Kwa mtiririko unavoenda, kwa namna inavochukuliwa na sharia pamoja na jeshi la polisi ikiambatana na serkali ni kana kwamba vifo hivi vya kusikitisha ni kosa lao marehemu. Kana kwamba kufa kwao hakuna mana wala tija, kana kwamba ni sawa tu na kwa namna nyingine ikicheza kama ahadi kuwa inaweza kutokea na HAKUNA ambalo tunaweza kufanya.
Kwa kiasi Fulani inaweza kuwa wapo sawa na ni ukweli. Na hio yote itaonesha na kudhihirishwa na nguvu ya sisi wenyewe wananchi kwa kuwapa nguvu hio kwa ukimya, woga na tabia yetu ya kutotaka shari. Nadhani imefika wakati wa kila mmoja wetu kujihusisha kwa njia moja ama nyingine kuwa kila mmoja wetu, haijalishi upo ndani ya chama, haijalishi upo CDM ama CCM, haijalishi lolote lile zaidi ya Utambuzi, Ujuvi, Uzalendo wa kutaka kusongesha nchi yetu kuwa mahala salama kwa KILA mwananchi!
Kitu ambacho CHADEMA wanatakiwa kujifunza:
Wamepokelewa kwa mikono miwili na wananchi, inatakiwa wajipange hasa. Hizi vurugu ambazo zimekuwa mara nyingi zikihusishwa na wao kwa namna moja ama nyingine wanawajibika. Inawezekana Serkali inafanya makusudi kabisa ili kuwachafua kuwa wao wanaleta fujo hadi kusababisha vifo – Nasihi kama mkereketwa wasafishe hilo ili Watanzania wajue ukweli.
Wanafanya kazi nzuri ya kuhamasisha na kuwaamsha wananchi kwa silaha yao ya ‘Movement for Change'. Ila hio pekee haitoshi… Kazi, Malengo, Mipango na nguvu zaidi inahitajika. Wanaweza wakawa wamekubalika na kuzidi kuongeza wafuasi kila kuchapo; ila ukweli unabaki kuwa CCM wana mizizi mirefu hivo silaha kubwa ya kung'oa huo mzizi ni lazima iandaliwe kwa Uadilifu, Umakini, Uzalendo, Nguvu na Umoja!
Kitu ambacho CCM inatakiwa kujifunza:
Uhakika wa kudumu kwao katika uongozi daima wa Serkali unazidi kupungua kadri siku zinavoenda. Ni wazi kuwa matatizo ya ndani ya chama hasa yalioendeshwa tokana na mgawanyiko imekuwa kazi kurekebisha. Wanachi wamechoka na wanatambua kila ambalo linafanywa na serkali, kuwa hata kama wakitaka kutokujihusisha katika kashfa kama hizi wanahusika moja kwa moja. Kwa maana wakiwa kama wao ndio tuliowapa dhamana ya kuwa viongozi wetu, wametuangusha na wanatuumiza. CDM inaweza isiwe na nguvu kama CCM, ila kwa sasa ni dhahiri nguvu ya Umma ipo mgongoni kwao…
Kitu ambo Wanaharakati/Wananchi tunatakiwa kujifunza:
Kuongea ama kukemea mitaani/majumbani/kwenye vyombo vya habari pekee HAITOSHI! We have to take action, na action sio lazima uende ukapigane na mtu. Jamii yetu imezungukwa na wananchi ambao hawaelewi nini kinaendelea kwa mapana hapa nchini. Kuna ambae ukimuuliza habari zozote za siasa alizosikia hapa karibuni atakujibu kwa kujidai kabisa kuwa "Diamond kaalikwa Ikulu"; kwake hio ni siasa na anakuwa kamaliza.
Nadhani imefika wakati kama vile ambavo ilisisitizwa kuhusu ugonjwa wa UKIMWI kugusia katika mkusanyiko wowote wa watu zaidi ya watano bila kujali ni mkutano wa kijiwe/kazi/shughuli BASI hata elimu ya yajirio (na umuhimu wa kujua hayo) kwa wanachi wenzetu iwe hivo. Hasa wale ambao kabisaa haelewi pa kuanzia ama kuishia hasa kwa yale yanayojiri nchini kwetu kwenye hii Tanzania yetu.
Hii kelele ya mara moja haitatibu tatizo letu sugu… Tukitaka kutambua kuwa na sie tuna tatizo; tujiulize kelele zote kuhusu Dr. Ulimboka yakwapi? Nini kimefanyika cha maana? Kwa mtindo huu kweli tunadhani kunaweza kukakwa na mabadiliko chanya yoyote? Kwa njia moja ama nyingine turudishe uzalendo tulioupoteza na kuujenga upya…. Habari na namna alivofariki Marehemu David imenigusaa… Nawasilisha hayo yote juu yakisukumwa na hicho kifo kama moja ya sababu.
Pamoja Sana.
AshaDii.
"Usually when people are sad, they don't do anything. They just cry over their condition. But when they get angry, they bring about change" - Malcom X