Duh! Wakuu nimeshitushwa sana na hii habari nzito sana, yaani mpaka sasa nimeishiwa nguvu kabisaa, ninaomba kuchukua fursa hii kumuombea Mkuu Marehemu Wangwe,
Kama kawaida ni lazima niseme ukweli wangu wa siasa, kwamba huyu marehemu nilikuwa simfahamu sana zaidi tu ya kumuona kwenye video za bunge, ambazo ninazo nyingi sana ambako yumo akitoa hoja ambako pia nimeshindwa kum-judge as far as vita vya ufisadi, exactly alikuwa upande gani. I was never impressed na hoja zake bungeni na hilo nimelisema mara nyingi sana hapa JF, na ukweli ni sijui sana aliyoyafanya ndani ya Chadema,
Ingawa pia nimeona some writtings zinazomhusu sana hapa JF, impression niliyoipata ni kuwa kuna matatizo sugu aliyoyakuta na kuyavalia njuga huko Chadema, against establishment na mimi kama Mwanamapinduzi wa kweli ni lazima ninaunga mkono anytime establishment yoyote inaposhambuliwa kwa manufaa ya wengi na kwa makosa ambayo ni proven kuwa yapo na ni sugu.
Ninaomba kumuombea kwa Mungu, amuweke mahali pema peponi na pia nawapa pole wana-Chadema wote, kwa huu msiba mzito sana!,
NB. wito wangu kwa wenzangu wengi hapa, nimeona vijembe vingi sana humu, ninasema kuwa hakuna sababu kama una ukweli weka tu hakuna sababu ya kuogopa, kama kuna mtu hapa au kiongozi yoyote amekukera na huu msiba sema ukweli, tusiziungukane hapa, naona tunaanza hii tabia mbaya sana ya kuzungukana naomba tuiache maana sio spirit ya JF hiyo, kama una machungu na mtu hapa au kiongozi weka wazi, maana sisi wengine kwenye hilo huwa hatuzunguki mbuyu na ndivyo inavyotakiwa, weka ukweli tena wazi!
Binafsi nimeamua kuufatilia kwa karibu sana huu msiba na ajali kwa ujumla, soon nitasema matokeo ya uchunguzi wangu hapa hapa JF, tena wazi!
Ahsante Wakuu!