Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
GAME THEORY,
kwa anayesema barabara ya Dar Dom ni mbovu aache uwongo ile bara bara ni nzuri sana tuu tatizo ni single carriage na haina taa bara barani kama M1 lakini ni lami tupu mpaka Dom..kinachotisha ile bara bara ni MAJAMBAZI wa silaha
Mkuu hapa ndipo naposhindwa na sisi Wabongo..Yaani mapungufu ulosema ni mazito sana kuliko hata hiyo lami hivyo sioni kabisa uzuri wa barabara hiyo. Sngle lane ktk Highway itokayo Dar hadi Dodoma ni miujiza ya Dunia. Sijaona nchi yeyote hata Afrika Ya Ethiopia yenye Highway inayotoka Mji mkuu kwenda Makao makuu ikiwa na barabara single lane, haina taa na zaidi ya yote makazi ya majambazi. Hiii ni hatari kubwa sana kiasi kwamba kuwepo kwa lami ni another problem badala ya kuwa solution. Lami inawafanya madereva kuendesha kwa mwendo wa kasi zaidi kuliko mashimo na kama barabara ndio kama ulivyosema basi hiyo barabara ni mbovu kishenzi..Kisheria single lane road hutakiwi kwenda zaidi ya Km 60 au 70 kwa saa, sasa mkuu nambie hilo linafanyika?
 
Hii ni ajabu sana, yaani mpaka leo hii hatuna angalau dual carriageway kweli?

Mimi siku zote Dodoma ndio hub ya uchumi wa nchi kuanzia biashara, mikutano na kila kitu.

Sasa watu wanasahau barabara.

Halafu mkuu Mkandara umezungumzia majambazi kushinda kandoni mwa barabara hizo.

Mimi nimewahi kusikia kwamba baadhi ya majeruhi wengi huuawa na majambazi au wananchi waishio kandoni mwa barabara hizo hasa zile zilizo porini kwa madhumuni ya kupora fwedha na vitu vingine vyenye thamani na mpaka leo sijapata uhakika na hili.
 
Samahani sikuji lakini what is your problem? Unataka nini? Kufariki kwa mtu hakufanyi msimamo wako wa awali kuwa sahihi. Kama wengine walikuwa wanapingana na mawazo ya marehemu na hata yako, kwa vile Amefariki hakufanyi wewe uwe sahihi. kwa hiyo sioni unaloshabikia hapa. Inasikitisha sana mtu anapojaribu kuonyesha alikuwa sahihi, sababu tu alikuwa anakubaliana na fikra za Marehemu na wengine walikuwa upande mwingine. Inasikitisha sana tena sana.



Na hili wataka lijibiwe na nani? Inasikitisha sana

msiba huwa nyumbani kwa marehemu, lakini kuuweka kwa Mbowe mtu ambaye alikuwa hasemi na Marehemu haina mantiki, bora uende kwa Slaa ambaye ni Katibu mkuu na Mbunge.
 
GAME THEORY,

Kisheria single lane road hutakiwi kwenda zaidi ya Km 60 au 70 kwa saa, sasa mkuu nambie hilo linafanyika?

Sheria ya Usalama barabarani ya TZ inaeleza mwendo kasi wa juu kabisa ni Km 80 kwa saa. Kutokana na sababu uliyotoa hapo juu mzee.

Miundombinu yetu hasa barabara bado tunakazi kubwa ya kufanya
 
Mnaweza kumsikiliza mpambanaji,mwanaume na kiboko yao wahafidhina kwenye mahojiano yake na KLH NEWS tizama kwenye Listen Show halafu Mahojiano na Wangwe ameweka vitu sana kwenye interview hiyo www.klhnews.com au tunaweza kumwita kidume GEORGE GALLOWAY A.K.A CHACHA ZAKAYO WANGWE.
 
Hapana Richard, kitaalauma mtu mwenye authority ya kuthibitisha tukio la ajali ndiye huyo ambaye waandishi wamemnukuu. Eye witnesses wanaweza kucomment, lakini bila kauli ya kamanda taarifa inachukuliwa kama uzushi! Haipendezi, lakini ndo hivyo. Ndo maana siku zote tunasoma habari za vifo Muhimbili kutoka kwa "Tibaigana" na madaktari, badala ya ndugu wa marehemu n.k. Ndugu wanaweza kusimulia kilichotokea lakini wao si source ya taarifa rasmi za kifo au ajali...na kwa kuwa hiii ndo taarifa ya kwanza ya kifo hicho, tunatarajia kwamba taarifa lazima itoke huko ilikotoka. Sasa baada ya hapo tutajua mengi kwa walioshuhudia tukio hilo.

Nimekuelewa ila nilitaka kujua kwamba leo hii mambo yamebadilika kumbe bado.

Unakumbuka siku ambayo marehemu Sokoine alifariki?

Tulianza kusikia nyimbo za maombolezo kwa saa kadhaa na baadae ndio mwalimu akazungumza na taifa.

Sasa anyway ile ilikuwa ni high profile lakini reporting inabaki palepale kwamba kuna ajali imetokea na ni mbunge wa Tarime. Nazungumza pia kuhusu wale marehemu wabunge wengine na mheshimiwa Mudhihir ambae kwa kudra za mwenyezi bado yu hai.

Kwa hio nnachoona ni kwamba inabidi kamanda wa polisi asubiri kila kitu kimefanyika kuhusu uchunguzi hasa wa ajali zinazohusisha "public figures" na ndio aje kwa waandishi badala ya kutoa habari nusunusu.
 
Mbunge wa Tarime Mhe. Chacha Wangwe (Chadema) amefariki dunia majira ya saa tatu za usiku (saa za Tanzania) katika ajali ya gari akitokea Dodoma kuelekea Jijini Dar-es-Salaam. Habari za kifo hicho zimethibitishwa na Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma Bw. Omar Mganga na uongozi wa Chadema.

Kwa mujibu wa habari zinazoendelea kuingia KLH News ajali hiyo imetokea saa tatu za usiku mahali panapoitwa Pandambili ingawa chanzo cha ajali yenyewe bado hadi hivi sasa hakijafahamika. Uongozi wa Chadema saa hii unakutana mjini Dodoma nyumbani kwa Mwenyekiti wake Bw. Freeman Mbowe na taarifa nyingine zozote zitapatikana baadaye.

Habari zaidi zinasema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa ajali hiyo haikutokana na kugongana na gari jingine isipokuwa kupasuka kwa mataria/tairi (kupata pancha) na gari imeharibika vibaya. Ajali hiyo imetokea wilayani Kongwa eneo la Pandambili. Muda mfupi uliopita mwili wa Marehemu umefikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambako ulipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. William Lukuvi pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi.

Mlolongo wa taarifsa za msiba zinaonesha kuwa zilianzia kwa Polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa Spika na hatimaye uongozi wa Chadema ambao ulituma ujumbe ulioongozwa na Dr. Slaa kuelekea eneo la tukio. Hata hivyo kabla ya kufika eneo la tukio walikutana na gari la kubebea wagonjwa la wilaya ya Kongwa lililokuwa likiuleta mwili Dodoma. Msafara wa Dr. Slaa ukaungana na gari hilo ili kulindikiza. Taarifa nyingine zinasema kuwa watangazaji wa TVT wameelekea eneo la tukio na bila ya shaka watatoa taarifa yao mapema asubuhi saa ya za Tanzania kuhusu eneo la tukio.

Majaribio yote ya kupata kujua ni nani aliyekuwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kumtambua Mhe. Wangwe bado hazijafanikiwa; tunatarajia Polisi kutoa taarifa yao kesho pia.

Vyanzo vya Bunge vinasema kuwa mapema kesho Spika wa Bunge ataongoza dua ya asubuhi na pia kuahirisha kikao cha Bunge ili kutoa nafasi kwa wabunge kuomboleza. Mapema asubuhi pia kikao cha kamati ya uongozi kitakaa na kujadiliana na familia ili kuandaa mipango ya mazishi na taratibu nyingine za maombolezo.

Mhe. Wangwe alizaliwa tarehe 15 Julai 1956 na kupata elimu yake ya msingi kwenye shule za Rosana na Magoto huko Tarime na baadaye kuendelea na elimu ya sekondari kwenye shula za Nyaroha na Kinondoni Muslim. Kabla ya kujiunga na Chadema Mhe. Wangwe aliwaku kuwa Katibu wa Mkoa wa chama cha NCCR Mageuzi na baadaye kujiunga na Chadema ambacho kilimsimamisha kugombea Ubunge wa Tarime.

Mwishoni mwa mwaka jana Bw. Wangwe alichaguliwa kukaimu nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa chama hicho kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa makamu Dr. Walid Kaborou. Hata hivyo Bw. Wangwe alisimamisha nafasi hiyo na Chama chake baada ya kudaiwa kuwa alikuwa akiuka maadili ya uongozi na kufanya mambo ambayo yalikuwa hayana maslahi ya chama.

Hata hivyo Bw. Wangwe aliendelea kusimamia msimamo wake wa kutaka mabadiliko ndani ya Chadema na alikusudia kuyaongoza mabadiliko hayo kwa kutangaza nia yake ya kugombea nafasi ya Uenyekiti katika uchaguzi mkuu wa chama hicho baadaye mwaka huu. Unaweza kusikiliza mahojiano ya KLHN na Mhe. Chacha Wangwe kwenye eneo la "listen shows".

MMJJ,
I was expecting in such a long, sort of eulogy, to see some highlights of the late Wangwe's successes, especially in CHADEMA where almost single handledly, he made CHADEMA a formidable party in Tarime and beyond. Let us be as fair as we can to this giant of multiparty democracy.
 
Namwomba Mwenyezi Mungu Ailaze Pahali Pema Peponi Roho Ya Marehemu Wangwe. Amina.

Nawapatia Pole Za Dhati Wanafamilia na Marafiki Wa Marehemu.

SteveD.
 
MMJJ,
I was expecting in such a long, sort of eulogy, to see some highlights of the late Wangwe's successes, especially in CHADEMA where almost single handledly, he made CHADEMA a formidable party in Tarime and beyond. Let us be as fair as we can to this giant of multiparty democracy.

duh.. I can never do anything right to the satisfaction of my critics. This is depressing.
 
Wakuu wala msinambie mimi mwenyewe nilisafiri kwa bus toka Dar hadi Mwanza nikachekwa sana na jamaa zangu kuwa mzee nimetoka majuu nachukua bus?.. Na kweli nilikwamba Singida, mkuu wangu Bongocelebrity akanianika mtandaoni nimechokaaa! Kwa hiyo najua ubaya wa barabara zetu.. Nakumbuka Uganda baada ya vita ya Kagera ile barabara ya toka kampala hadi Mbalala kuja Mpakani ilikuwa nyang'anyang'a ama kwechekweche (sijui lipi zito zaidi) kwa sababu ya vifaru, mabomu yaliyoitwa sabasaba waganda hawatasahau hilo!, lakini baada ya Vita tu kitu cha kwanza ilikuwa kuijenga Upya barabara hiyo. mazee ilijengwa within 5 years tena ikapanuliwa zaidi.. Sisi Wadanganyika ndio kwanza tunagawa viwanja kando ya barabara kuu sijui kesho wakitaka kupanua itabidi walipe fidia kwa wenye nyumba..
Cha ajabu basi kila Higway yetu ni lazima ipitie katikati ya mji ama kijiji yaani hata sielewi hawa wasomi wetu huwa wanafikiria kitu gani wanapochora ramani za mabarabara...
Aaaah inachosha jamani inachosha sana, sasa nambie huko Kigamboni nasikia viwanja vimetolewa kiholela kiasi kwamba kila mtu kapewa sehemu bila kwanza hizo sehemu kuwa designated kwa ajili ya majengo ya aina gani! mathlan Hotel za kitalii, maduka kama super market (shopping cetre) ama residential area yaani mtu ukiomba kiwanja unachagua sehemu tu.. fedha yako!.. Hii akili kweli jamani mmewahi kuona kitu hii sehemu yoyote ile?..

Kutokana na kifo cha Wangwe na Salome Mbatia vinatakiwa kufanyiwa uchunguzi kuhusiana na Mabarabara yetu. Najua wapo wataosema kwa nini leo hali wapo raia kibao wamekufa ktk ajali za barabarani lakini jamani ifike muda tuseme enough! Hiyo Barabara ya Dar Mwanza imeanza kujengwa toka mwaka 1982 na Wataliani wakaondolewa, sijii wakaja kina nani lakini hadi leo hii jamani hata hizo single lane bado nasikia ndio kwanza zimevuka Dodoma na Upande wa Mwanza zimefika karibu na Nzega... lini Zitapanuliwa hata kufikia hadhi ya Highway? Mungu ndio anajua..

Nooo jamani hivi sana nchi yetu inatisha tuache hizi siasa za kipuuzi tuzungumzie issue muhimu kuhusiana na vifo hivi..Bunge letu linatakiwa kutumia mifano kama hii kuamsha hoja mpya. Wananchi tumechokaaaa!
 
Duh! Wakuu nimeshitushwa sana na hii habari nzito sana, yaani mpaka sasa nimeishiwa nguvu kabisaa, ninaomba kuchukua fursa hii kumuombea Mkuu Marehemu Wangwe,

Kama kawaida ni lazima niseme ukweli wangu wa siasa, kwamba huyu marehemu nilikuwa simfahamu sana zaidi tu ya kumuona kwenye video za bunge, ambazo ninazo nyingi sana ambako yumo akitoa hoja ambako pia nimeshindwa kum-judge as far as vita vya ufisadi, exactly alikuwa upande gani. I was never impressed na hoja zake bungeni na hilo nimelisema mara nyingi sana hapa JF, na ukweli ni sijui sana aliyoyafanya ndani ya Chadema,

Ingawa pia nimeona some writtings zinazomhusu sana hapa JF, impression niliyoipata ni kuwa kuna matatizo sugu aliyoyakuta na kuyavalia njuga huko Chadema, against establishment na mimi kama Mwanamapinduzi wa kweli ni lazima ninaunga mkono anytime establishment yoyote inaposhambuliwa kwa manufaa ya wengi na kwa makosa ambayo ni proven kuwa yapo na ni sugu.

Ninaomba kumuombea kwa Mungu, amuweke mahali pema peponi na pia nawapa pole wana-Chadema wote, kwa huu msiba mzito sana!,

NB. wito wangu kwa wenzangu wengi hapa, nimeona vijembe vingi sana humu, ninasema kuwa hakuna sababu kama una ukweli weka tu hakuna sababu ya kuogopa, kama kuna mtu hapa au kiongozi yoyote amekukera na huu msiba sema ukweli, tusiziungukane hapa, naona tunaanza hii tabia mbaya sana ya kuzungukana naomba tuiache maana sio spirit ya JF hiyo, kama una machungu na mtu hapa au kiongozi weka wazi, maana sisi wengine kwenye hilo huwa hatuzunguki mbuyu na ndivyo inavyotakiwa, weka ukweli tena wazi!

Binafsi nimeamua kuufatilia kwa karibu sana huu msiba na ajali kwa ujumla, soon nitasema matokeo ya uchunguzi wangu hapa hapa JF, tena wazi!

Ahsante Wakuu!
 
Mkuu ES.
umesema wazi na clear kuna wanafiki wana beef na marehemu lakini hapa wanazuga wakati nafsi zako ziko kwenye celebration,wawe wakweli kama wewe kwa BHOKE MUNANKA.
 
Jina la Bwana lihimidiwe. Tuko pamoja na familia ya wafiwa na Watanzania kwa ujumla.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom