Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Nyie kubalini tu vifo vya viongozi wenu, na siku zaidi ya mmoja watakufa kwa wakati mmoja na mtaambiwa ni mapenzi ya Mungu. Endeleeni tu kukubali maelezo ya watawala siku moja watatoa maelezo ambayo hayaingii kichwani na mtajikuta mnakubali kwa sababu hamtaki to rock the boat.

Sawa tusubiri wakati huo... kwa sasa hatujadanganywa...
 
Mungu saidia..tusifike kwenye chuki za ukabila..CCM hawajui outcome ya hili wanalotaka kulifanya.... mola epushia mbali hili na naomba uwaumbue hadharani.....Let us cross our fingers..!!

Wanajua sana....infact wapo ambao wameshajianzishia VIJIMILITIA vyao vya kujitengenezea na kulinda himaya na maslahi yao watanzania tukianza kukata vichwa....Usishangae soon FISADI akageuka kuwa MZEE WA VITA (Warload)...

Tunapelekana pabaya....

Tanzanianjema
 
Nimesoma kurasa chache sana kuhusu hili suala la Wangwe, na nina haya ya kusema.

Nilipopigiwa simu na kupewa taarifa,nilimwambia aliyenipasha habari kuwa reaction yangu ya kwanza ni kuamini kuwa amekufa kwa ajali ya gari bila kuwa na motive behind.

Nikaendelea kumwambia huyu ndugu, kwa kuwa mimi ni Mtanzania na nafahamu mambo ya Tanzania na jinsi tulivyo, reaction ya pili inaniambia hii haikuwa ajali kama ajali za kawaida kutokana na kukimbiza gari, ulevi au gari kuharibika, nikasema hii ni ajali ya kuchongwa.

Nikasema kuna watakaosema ni CCM, kuna watakaosema Chadema, lakini la mwisho ambalo ni kubwa na nitaliamini kama kawaida ya Utomaso wa Kitanzania na uzushi, ni mambo ya maslahi hasa ukizingatia alichofanya Wangwe kuhusu uchimbaji dhahabu Tarime.

Najinukuu kwenye ujumbe binafsi niliomwandikia huyu ndugu

28th July 2008, 03:49 PM
Rev. Kishoka
user_online.gif

Rev. Kishoka Edit
JF Senior & Premium Member
Join Date: Mon Mar 2006
Location: USA
Posts: 1,688
Rep Power: 66
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Thanks: 1,534
Thanked 1,633 Times in 721 Posts
Credits: 128,577

icon1.gif
Chacha wangwe
1. Killled in an accident. Case closed.
2. Killed in an appearance of car accident. Open for debate and motive!

Motive CCM, they need to paint Chadema bad and take over Tarime
Motive Chadema, Mbowe is in cahoots with someone to rid Chacha Wangwe
Motive Ufisadi, which aligns with motive CCM: The Buhemba or whatever Gold issues in his district he became a thorn and could have become a thorn again. Killers could be people behind Meremeta etc.

This is my take,

Nilichojiuliza cha kwanza ilikuwa je ajali ilitokeaje, aligongwa nja gari nyingine, lakini majibu ni kuwa Matairi yalipasuka wakati gari ikiwa kwenye mwendo mkali. Nikajiuliza kama ilikuwa ni usiku, Tanzania huu ni wakati wa kipupwe, ni nini ambacho kingesababisha matairi yote ya mbele yapasuke kama ardhi na lami imepoa?

Je alikuwa akiendesha gari yenye matairi kuukuu, alikanyaga msumari, chupa au ni vipi matairi yalipasuka?

Nikajiuliza je alikuwa pekee au alikuwa na abiria? ni nani alikuwa anaendesha gari, je aliyekuwa anaendesha gari alikuwa amekunywa pombe au kilevi chochote?

Kama nia ilikuwa ni kulala Morogoro, kutoka Dom mpaka Dar ni masaa 6 kwa mwendo wa kawaida, kwa nini ilimlazimu aondoke saa 2 usiku, alale Morogoro usiku wa manane ili kuwahi mazishi kesho yake ambayo yalikuwa yafanyike jioni?

Kwa nini walikuwa wanakimbiza gari (kama gari lilikuwa linakwenda kasi sana)? je kulikuwa na utelezi?

Sasa baada ya kuyasikia haya ya Malya, najiuliza tena, kwenye ajali na gari linapopinduka na hasa hili ambalo eti lilipinduka mara tano, mshituko wa ajali hauwezi kumpa mtu aliye ndani ya gari kupata fahamu za kuzima gari na kutoa funguo! Je Malya alitoa funguo kwenye gari lililopinduka kwa sababu gani? je mbona yeye hata mchubuko inasemekana hana?

Ikiwa yeye Malya ambaye alikuwa ni dereva fahamu zake ni kamili baada ya tukio, bila hata kutetereka, je alijua kuwa kutakuwa na ajali na hivyo aliji-condition kwa reaction?

Tumeambiwa Malya kapoteza simcard, Chacha kila alichokuwa nacho kimeibiwa, kulikuwa na mtu wa tatu kwenye gari, je utata huu mbona haueleweki?

Malya kapoteza Simcard lakini funguo za gari anachezesha mkononi?

LInakuja swali la mwisho, ni nani aliyetaka uhai wa Wangwe? kwa madhumuni gani? Je ni kweli alikuwa atoe hoja binafsi? je ni kweli alikuwa afungue kesi ya madai dhidi ya Chadema kesho yake?

Hakuna kinachoingilika akilini mwangu kusema kila kitu kilikuwa ni natural!

Kuna utata mwingi sana wa jinsi ajali yenyewe ilivyotokea, jinsi siku yenyewe ya mwisho wa uhai wa Wangwe hapa duniani ilivyoanza mpaka ikaisha!

Kama kawaida kama ni mkono wa mtu, basi mkono huu hauna utu wala woga, mana unajua wazi kuwa ulichokifanya utaleta utata ambao kamwe hautaweza kupatiwa ufumbuzi na kwisha Taifa kupangusa machozi na kuendelea na maisha huku simanzi likiwa mioyoni mwetu!
 
Mkama,

Nadhani sasa tunaweza kukubaliana kwamba aliyeandika habari ni mtu mmoja na ilitumika kwa magazeti yote yaliyoweka habari hiyo na wala hakuna swala la kudeseana. Swali la kujiliuliza ni kwamba je, kwanini walikubali kufanya hivyo?

Madai yako kwamba waandishi huwa wanadeseana kwa kuwa huwa wanabana posho, hilo sikubaliani na wewe hata kidogo. Kwanza hapo mwandishi ana risk kufukuzwa kazi kwa kuwa habari ile ikileta mushkeli kwa jamii, mhariri ndiyo huwa anakuwa responsible.

Kazi ya mhariri ni ku-proof read ile habari na ku-cross check kama habari aliyotumiwa ni ya kweli. Kuna sources nyingi za kufanya hivyo na kama mwandishi katuma habari bila ya kuwepo kwenye tukio basi wakati wa ku-cross check lazima atagundulika na hasa kwa news sensitive ambayo ilikuwa imevuta hisia za watu kama ilivyokuwa kwenye huo msiba. Kama wahariri wangefanya kazi hiyo sidhani kama kuna mtu angelalamika. Kinachotakiwa ni mtu kuwa fair kwenye analysis yake na pale mhariri anapo-detect chumvi basi lazima ajiulize na na kuifanyia kazi.

Siku nyingine habari huwa zinafanana lakini siyo neno kwa neno. Sometimes hata heading zinaweza kufanana lakini contents zikawa tofauti.

Kama ni swala la elimu, wahariri wote wana elimu na tena ya chuo kikuu lakini wametuambia Joseph Mbatia ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi. Hivi ili kujua kwamba Mwenyekiti wa NCCR ni nani lazima uwe na gazeti jingine la kulinganisha??

Mnafiki na yule ambaye anaandika habari kwa malengo tofauti. Mtu anaweza kuwa na PhD lakini bado akawa mnafiki, na kuna wengine ambao hawajasoma hata darasa moja na siyo wanafiki.

Kununuliwa kwa waandishi hakutokani na kuwa naa elimu duni. Unadhani kwanini watu wanasema kwamba RA kanunua wahariri? Mhariri ndiye anayeidhinisha habari itoke gazetini na anaweza kuibadilisha kwa jinsi yeye anavyoona inafaa na yeye ndiyo anakuwa responsible just in case habari ikiwa ina matatizo. Lini uliona mwandishi wa habari anaomba radhi? Wanao omba radhi huwa ni wahariri kwa kuruhusu kuchapa habari ambayo haikuwa na ukweli ama ili-ripotiwa kimakosa.

Tatizo letu ni kwamba tunawaangalia waandishi wa habari as if kile walichoandika ndicho ambacho huwa kinatoka gazetini kama kilivyo.

Waandishi waliotuhumiwa kununuliwa na mafisadi (RA) wote wamesoma na wana degree zao. Kila siku watu wanamtaja Balile na Muhingo Rweyemamu kwamba walinunuliwa na RA, na wote wana degree. Je, bado una hoja kwamba mwandishi kama hajasoma basi itakuwa rahisi kumnunua?

Mtu kama hana Elimu ya kutosha ktk maeneo yake hua hajui Madhara anayofanya ,ila hutambua baada ya madhara yamekwisha tokea.Kama vile Mangungo.
Kuapata digrii ktk karatasi sio Elimu hiyo digrii ni kitamburisho tu cha kuonyesha wapi amepita, Maana yawezekana kabisa kuipata hiyo karatasi kwa KUDESA kama walivyo DESA.

Unachoshindwa kuunganisha ni kua kitu chochote cha kipotofu ktk jamii ni matokeo ya upungufu wa ELIMU ya mtu husika.

Maana karibu vyombo vyote vya habari isipokua Tanzania Daima wameandika habari ya Mbowe ,kwa maana hiyo waandishi wetu hawana elimu wanahitaji Elimu.
Unafiki mkubwa na wa ajabu unakuja,Pale Serikali iliposema waandishi wetu hawana Elimu yawapasa kupata elimu MINGWIJI humu JF walikuja juu na kusema ni dharau wakapiga matarumbeta na kusema serikali imetoa kebehi kuu lakini hao hao waandishi leo wamewageuzia kibao na kuwaonyesha soka halisi haohao waliolalama na kupiga matarumbeta leo wanasema hawa waandishi hawana Elimu na wanasema imekua je wakashindwa kubadili hata maneno.Humu kuna unafiki mkubwa sana

Na unafiki wenyewe ukifurahia tu mwenzako anaponyoshewa vidole basi washangilia ,ukinyoshewa wewe ni kosa la jinai maana wewe ni msafi sana na usafi wenyewe unaji mark mwenyewe na kujipa maksi mwenyewe.
 
By the way, mlio kwenye fani ya IT na hasa imaging na visual programing, mnaweza kutengeneza simulation ya hii ajali ?
 
Hiyo Mkuu ndio suluhu tu nasi kupiga propaganda .

Mbowe Amezushiwa kua alitolewa bunduki ktk mazishi basi awapeleke ktk vyombo vya sheria huo ndio utaratibu halali na si vinginevyo.

Huko ikionekana alizushiwa yeye ndiye anaweza amau alipwe ama asilipwe huo ndio utaratibu wa msingi.
akiamua naye kulipwa mabilioni ili aje awapige cha juu hapa hiyo ni uamuzi wake.

mkamap,

Nianvyofahamu mimi humu ndani kuna makundi mawili makubwa yanayotofautiana kimawazo - jambo ambalo si baya kwa chombo huru kama JF.

Kuna wale wanaoona uchungu kwa yanayototendeka nchini chini ya uongozi uliopewa mamlaka na wananchi. Hawa hawako tayari kumtafuta mchawi nje ya hii serikali kwa sababu waliipigia kura CCM na serikali yale kwa ahadi zilizotolewa za kuleta matumaini ambazo sasa ni wazi hata kwa kipofu kuwa hazikuwa za kweli. Serikali isiyo na ubia na mtu, haiwezi kuwa held at ransom na kikundi cha watu na ikashindwa kufurukute hata kidogo.

Kuna wale ambao kwa sababu ambazo haziko wazi wanatetea hiyo hiyo system iliyokosa mwelekeo wa maendeleo katika karibu kila nyanja. Wao kila mara watatafuta mchawi nje ya hiyo serikali na kama kuna tukio lolote lile linaloweza kuipa ahueni serikali hawasiti kulishupalia. Vyama shindani kama CHADEMA ambayo imeonyesha kwa kiwango kikubwa kukabiliana na uovu katika jamii, kinakuwa target ya watu hawa kukizuulia kila aina ya vituko.

Mimi siijui CHADEMA na wala simjui Mbowe apart from the fact kwamba ni chama shindani na mwenyekiti wake ni Mbowe. Naweza kudiriki kusema kuwa watu wanaoniimpress CHADEMA, Mbowe si mmoja wao. Lakini matendo ya serikali chini ya CCM has driven me to a point ya kutokuiamini tena na niko tayari kuungana na mtu ama kundi lolote lile litakaloonyesha upinzani wa kweli dhidi yao.

Mkamap, nakushangaa kwa jitihada zako za kuwakatisha tamaa hawa watu ambao kwa akili yangu kidogo nawaita mashujaa. Kupambana na zimwi la CCM na taasisi zake kunahitaji ushupavu ambao watu wengi yawezekana ama hawana au wanalinda maslahi ya kibinafsi na si ya Taifa. Hawa watu ambao wamejitolea mhanga - kumbuka msururu wa waliojaribu na hatima zao - ndio tegemeo tu hai lililobaki kwa nchi yetu ya Tanzania.

Hebu fikiria kwamba sasa Mkapa anaweja kuzomewa na vijana mtaani bila kujali aliwahi kuwa Raisi, watoto wa shule wanaweza kuwataja hadharani mafisadi bila kujali huyu ni mwenyekiti wa maadili wa CCM, wananchi wanaweza kulala barabarani kumzuia Kikwete asipite bila kuwasikiliza bila kujali ni Raisi wa nchi, JF wanaweza kumkoma nyani giledi bila kujai ni CEO wa multinational conglomerate - jamani hii ni achievement dhidi ya UFISADI.

Mkamap, wewe pamoja na wote unaokubaliana nao ukianza kupima haya kwa mtizamo wa CCM na CHADEMA, huitendei mema nchi yako ya Tanzania. Sisi wengine hata kuwa mwanachama tu wa chama chochote hatujafikiria na mimi nimejiunga na JF mwaka huu baada ya kufuatilia mada mbalimbali kwa miaka karibu miwili. Niliridhika na maoni ya wachangiaji na hata pale wanapotofautiana, lengo kubwa ni kuisaidia nchi yetu.

Mwisho naomba katika hili msitukatishe tamaa na kama mnayo imani ya kweli kweli kuwa JF si huru, MKAE PEMBENI. Nimeshuhudia kejeli, majigambo, uwongo na mengine mengi tu, lakini hili la JF kuwa CHADEMA imetia fora na kama ikithibitika hivyo na mimi nitakaa pembeni.
 
Halima Mlacha
Daily News; Saturday,August 02, 2008 @00:01

Aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, aliyekufa ajalini Jumatatu wiki hii, siku inayofuata ilikuwa awasilishe ombi la dharura mahakamani akitaka iamuru arejeshwe katika wadhifa wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, HabariLeo imebaini.

Wakili wa mwanasiasa huyo ameliambia gazeti hili kwamba walipanga waiwasilishe hati hiyo ya dharura Mahakama Kuu Dar es Salaam Jumanne asubuhi. Wakili huyo, Mathew Kakamba wa Kakamba and Partners Advocates, alisema katika hati hiyo Wangwe alikuwa aiombe Mahakama isimamishe kwanza uamuzi wa kusimamishwa kwake wadhifa wa umakamu hadi kesi ya msingi aliyokuwa ameifungua juu ya suala hilo itakapokamilika.

Alisema kabla mbunge huyo hajaondoka Dodoma, alizungumza naye kwenye simu saa tisa alasiri ambako aliahidi kuhudhuria mahakamani kesho yake kama ilivyopangwa. "Kusema ukweli majira ya saa tisa siku aliyoondoka nilizungumza naye na akaahidi kuwahi kesi, nilipomuuliza kwa nini anaondoka usiku, alisema ni kwa sababu anataka pia awahi maziko ya mwanasiasa Bhoke Munanka," alisema Kakamba.

Alisema kesi ya msingi ya Wangwe dhidi ya wadhamini wa chama hicho, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho Dk Wilbrod Slaa, tayari ilishafunguliwa tangu Julai 21, mwaka huu katika Mahakama Kuu. Alisema katika kesi hiyo ya msingi ya madai pamoja na mambo mengine, Wangwe alisema mkutano uliofanyika Dodoma na kumsimamisha umakamu, haukuwa halali na kwamba uamuzi waliotoa haukuwa wa haki.

Kwa mujibu wa hati ya kesi hiyo, Wangwe alitaka Mahakama itoe agizo kuwa mkutano uliofanyika Juni 28, mwaka huu, pamoja na uamuzi wote uliotolewa ni batili. Alitaka mahakama itoe amri ya kumruhusu kuendelea na wadhifa wake wa umakamu mwenyekiti wa Chadema Bara na itoe amri ya kisheria ya kudumu dhidi ya Mbowe, Dk Slaa na wakala wao na kuwazuia kuchukua hatua yoyote ya kumsimamisha wadhifa wake au uanachama.

Gazeti hili pia lina taarifa za kuaminika kuwa baadaye Jumanne, Wangwe alikuwa azungumze na waandishi wa habari Dar es Salaam juu ya alichoamini kuwa ni jaribio la kuvuliwa wadhifa wake na uanachama wa chama hicho. Baadhi ya masuala ambayo dondoo zake alizisambaza kwa watu wake wa karibu (gazeti hili linazo), Wangwe alikuwa azungumze kuwa sababu zote zilizotolewa na Mbowe dhidi yake, hasa suala la kuvujisha siri za chama hicho kwa CCM ni za uzushi.

Dondoo zinaonyesha angezungumzia kukerwa na mtiririko wa mgogoro ndani ya Chadema, kiasi cha kuonekana inaendeshwa "kiujanja ujanja." Wakati huo huo, Mwandishi Wetu anaripoti kutoka Tarime kuwa utata uliogubika kifo cha Wangwe, jana ulitatuliwa baada ya uchunguzi wa mwili wake kubaini kuwa kifo chake kilitokana na ajali na hakupigwa risasi.

Uchunguzi huo uliochukua zaidi ya saa tano, uliwashirikisha madaktari watatu ambao waliombwa na familia kuufanyia uchunguzi mwili huo. Wanafamilia waliongozwa na Profesa Samwel Wangwe na madaktari hao ambao hata hivyo, walikataa kutaja majina yao. Uchunguzi huo ulianza saa tano na kumalizika saa 10.00 jioni.

Madaktari hao, mmoja alitoka Dar es Salaam, daktari mwingine alitokea Musoma na mwingine alikuwa mwakilishi wa hospitali ya wilaya ya Tarime. Uchunguzi huo ulifanyika chini ya usimamizi wa Polisi kwa lengo la kujiridhisha. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiliongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe. Wangwe alisema sasa familia imejiridhisha na uchunguzi wa marehemu na walilazimika kufanya hivyo kutokana na utata ulioigubika, hivyo kulazimika kuwaita madaktari wao.

"Sasa hatuna shaka na mtu yeyote wala chama chochote," alisema Wangwe na kuongeza kuwa wanaenda kuzika na hawana hofu. Juzi ndugu wa Wangwe waligoma kuzika mwili wa marehemu, kwa maelezo hawakuwa wanaamini kuwa ndugu yao amekufa kwa ajali ya gari. Hivyo walilazimika kuahirisha maziko hayo ili kujiridhisha zaidi, kwani Wangwe alikuwa kiongozi wa watu. Maziko yalifanyika kijijini hapo jana jioni na kuhudhuria na umati wa watu ambao haukulingana na waliokuwapo juzi.

Baadhi ya viongozi wa upinzani waliokuwapo katika maziko hayo yaliyofanyika kwa amani walikuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia. Habari zinasema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alishauriwa asihudhurie maziko hayo jana kutokana na vurugu zilizotokea juzi baada ya yeye kufika msibani hapo.
 
mkamap,

Nianvyofahamu mimi humu ndani kuna makundi mawili makubwa yanayotofautiana kimawazo - jambo ambalo si baya kwa chombo huru kama JF.

Kuna wale wanaoona uchungu kwa yanayototendeka nchini chini ya uongozi uliopewa mamlaka na wananchi. Hawa hawako tayari kumtafuta mchawi nje ya hii serikali kwa sababu waliipigia kura CCM na serikali yale kwa ahadi zilizotolewa za kuleta matumaini ambazo sasa ni wazi hata kwa kipofu kuwa hazikuwa za kweli. Serikali isiyo na ubia na mtu, haiwezi kuwa held at ransom na kikundi cha watu na ikashindwa kufurukute hata kidogo.

Kuna wale ambao kwa sababu ambazo haziko wazi wanatetea hiyo hiyo system iliyokosa mwelekeo wa maendeleo katika karibu kila nyanja. Wao kila mara watatafuta mchawi nje ya hiyo serikali na kama kuna tukio lolote lile linaloweza kuipa ahueni serikali hawasiti kulishupalia. Vyama shindani kama CHADEMA ambayo imeonyesha kwa kiwango kikubwa kukabiliana na uovu katika jamii, kinakuwa target ya watu hawa kukizuulia kila aina ya vituko.

Mimi siijui CHADEMA na wala simjui Mbowe apart from the fact kwamba ni chama shindani na mwenyekiti wake ni Mbowe. Naweza kudiriki kusema kuwa watu wanaoniimpress CHADEMA, Mbowe si mmoja wao. Lakini matendo ya serikali chini ya CCM has driven me to a point ya kutokuiamini tena na niko tayari kuungana na mtu ama kundi lolote lile litakaloonyesha upinzani wa kweli dhidi yao.

Mkamap, nakushangaa kwa jitihada zako za kuwakatisha tamaa hawa watu ambao kwa akili yangu kidogo nawaita mashujaa. Kupambana na zimwi la CCM na taasisi zake kunahitaji ushupavu ambao watu wengi yawezekana ama hawana au wanalinda maslahi ya kibinafsi na si ya Taifa. Hawa watu ambao wamejitolea mhanga - kumbuka msururu wa waliojaribu na hatima zao - ndio tegemeo tu hai lililobaki kwa nchi yetu ya Tanzania.

Hebu fikiria kwamba sasa Mkapa anaweja kuzomewa na vijana mtaani bila kujali aliwahi kuwa Raisi, watoto wa shule wanaweza kuwataja hadharani mafisadi bila kujali huyu ni mwenyekiti wa maadili wa CCM, wananchi wanaweza kulala barabarani kumzuia Kikwete asipite bila kuwasikiliza bila kujali ni Raisi wa nchi, JF wanaweza kumkoma nyani giledi bila kujai ni CEO wa multinational conglomerate - jamani hii ni achievement dhidi ya UFISADI.

Mkamap, wewe pamoja na wote unaokubaliana nao ukianza kupima haya kwa mtizamo wa CCM na CHADEMA, huitendei mema nchi yako ya Tanzania. Sisi wengine hata kuwa mwanachama tu wa chama chochote hatujafikiria na mimi nimejiunga na JF mwaka huu baada ya kufuatilia mada mbalimbali kwa miaka karibu miwili. Niliridhika na maoni ya wachangiaji na hata pale wanapotofautiana, lengo kubwa ni kuisaidia nchi yetu.

Mwisho naomba katika hili msitukatishe tamaa na kama mnayo imani ya kweli kweli kuwa JF si huru, MKAE PEMBENI. Nimeshuhudia kejeli, majigambo, uwongo na mengine mengi tu, lakini hili la JF kuwa CHADEMA imetia fora na kama ikithibitika hivyo na mimi nitakaa pembeni.

Mkuu Habari yako .
Wengi hua hawakubali wakati muafaka lakini wanakuja kukili baada ya mambo kutokea.

kama sijakosea Hakuna jambo ambalo CCM imeshawatuhumu chadema ama kuwazushia Tofauti na HAYATI Makamu mwenyekiti wa CHADEMA kukituhumu chama chake nitakubaliana na wewe ukinihakikishia kua RIP Chacha alikua ni CCM.

Wapinganaji wakweli hamuwaoni na hamtawaona maana mmeshakwisha fumbwa macho .

KTK MAISHA muogope sana mtu yeyote anaye TAKE advantage ama kupanda mgongongo wa jamaa baki tu kwa makosa ya jamaa huyo ili apate kuvuka aendako ,maana kuna siku ataupandilia mgongo wako na suluba lake utajuta na kulia na kusaga meno.

Wakati TINGATINGA na Dr Salim inapandiliwa mgongo watu wengi waliona sawa na kufurahia neno tingatinga lilimwa kitabu na MWL sasa migongo yetu yapandiliwa twabeka too late.Ukumbuka mpanda mgongo hapandi mara moja.

Watu wanampa SIFA za bure RA wakati RA hana ujanja wowote na Akili ya fasta namna hiyo.

Hawa unaowaita wapiganaji wanashindwa kupigana na kutafuta moto uliko hii ni kwa sababu lengo lao si hilo,ila lengo lao ni kutumia hizo migongo kufika waendako.TUWENI WENYE AKILI KAMA NYOKA.

Kwa haraka haraka ukiangalia na ninavyoona mimi MAFISADI wale original walioko serikalini walimufuata RA awawekee pesa walizoiba maana RA anavijikampuni ,Hata hiyo RICHMOND ni viongozi hao hao walimtumia RA kupitisha mambo yao.

Huyu RA sema ana ngekekewa imemwangukia akatumiwa ktk dili la EPA na RICHMOND LAKINI si kama sifa mnazompa kila kitu RA, sifa za bure hizo,RA ni moshi tu hakuna kitu ,watu kama kukolimbana wameanza siku nyingi

Hao wapiganaji unaowaita waambie waende hatua nyingi zaidi watafute MOTO uliko Na wawapeleke mahakamani maana kesi anaweza fungua mtu yeyote na ukawakirisha ushahidi wako,wanasubiri nini?? wao ni mikutano ya hadhara tu ili 2010 wapate majimbo zaidi na fedha ziishie makao makuu.
 
Mag3
Unaonekena una hoja, lakini Mkamap naye ana point, tukumbuke kuwa si rahisi kujua mlengo au kundi la mtu anayejadili humu JF isipokuwa kwa hoja yake. Unaweza ukawagawa watu makundi kama ulivyo gawa halafu usijijue uko kundi gani kutokana na mtazamo na itikadi yako ya kisiasa. Mbaya zaidi ni pale unapoweza kuchanganya ukereketwa wa chama ukaonekana kama uzalendo. Haki haina sura, itikadi wala rangi, haki ni haki. Anachosema Mkamap ni namna na utaratibu wa kila raia kupata haki, ambao usipofuatwa na mtu yoyote lazima ukemewe na ndicho tunachopigania siku zote.

Tunapoona chombo kilichokuwa kinatupa matumaini ya kuleta haki nacho kinayumba lazima tukemee kwa nguvu zote. Anachokemea Mkamap ni unafiki wa watu humu JF ambao sasa unaweza kuwa mbaya kuliko hata ule wa system iliyotufikisha hapa. Lets come back to our senses, ndiyo! kuna habari zimekuwa exagerated kuhusu Mbowe kule Tarime, lakini ni nani hakutegemea hayo?,Hizi ni siasa! Ni wiki chache tu zimepita Marehemu alijadiliwa humu, marehemu alikuwa na marafiki zake, waliomuunga mkono, leo wale marafiki zake wanaonekana maadui zake na wale waliomsema vibaya wanajifanya leo wao ndo marafiki na wazalendo! Acheni unafiki! CHADEMA acheni kukimbia kivuli chenu. Moto huu mliuwasha wenyewe, na akina RA na washirika wao ndo wanachukua advantage. Ambayo ni kawaida katika political game. Sifurahii kuyumba kwa CHADEMA kwani ndio waliokuwa wamebakia, lakini tumaini lilianza kupotea baada ya kufukuzwa marehemu u makamu mwenyekiti (hasa utaratibu uliotumika). Leo hii mnajichanganya zaidi pale mnapotaka vyombo vya habari viandike habari mnavyotaka ninyi. You are asolutely Wrong! sasa hivi siyo kipindi cha nyie kutegemea kuandikwa vizuri. Mlitegemea nini, Mbowe ahudhurie msiba wa mtu ambaye kila mtu anajua ni adui yake na kila mtu ali pay attention kuona kinachotokea, na kesho yake wauze magazeti. Matokea yake hayatakiwi kushangaza. Nashauri CHADEMA wakae chini watulie kivuli kipite wajipange upya, tuendeleze libeneke.
Tutafakari sequence ya matukio haya ndani ya CHADEMA (kwa kutokuzingatia tukio la kifo cha Wangwe pekee yake) tutafute chanzo chake Objectively kuanzia uchanguzi wa Desemba 2007, tuzipime hoja za marehemu Wangwe (Ukabila, ruzuku kwa wananchi), tuzingatie kwa nini watanzania wanamlilia Wangwe na nini kinaandikwa zaidi (alichotuachia Wangwe ili tumkumbuke) halafu ndo tutafute mchawi.
 
Mkuu Habari yako .
Wengi hua hawakubali wakati muafaka lakini wanakuja kukili baada ya mambo kutokea.

kama sijakosea Hakuna jambo ambalo CCM imeshawatuhumu chadema ama kuwazushia Tofauti na HAYATI Makamu mwenyekiti wa CHADEMA kukituhumu chama chake nitakubaliana na wewe ukinihakikishia kua RIP Chacha alikua ni CCM.

Wapinganaji wakweli hamuwaoni na hamtawaona maana mmeshakwisha fumbwa macho .

KTK MAISHA muogope sana mtu yeyote anaye TAKE advantage ama kupanda mgongongo wa jamaa baki tu kwa makosa ya jamaa huyo ili apate kuvuka aendako ,maana kuna siku ataupandilia mgongo wako na suluba lake utajuta na kulia na kusaga meno.

Wakati TINGATINGA na D

Watu wanampa SIFA za bure RA wakati RA hana ujanja wowote na Akili ya fasta namna hiyo.

Hawa unaowaita wapiganaji wanashindwa kupigana na kutafuta moto uliko hii ni kwa sababu lengo lao si hilo,ila lengo lao ni kutumia hizo migongo kufika waendako.TUWENI WENYE AKILI KAMA NYOKA.

Kwa haraka haraka ukiangalia na ninavyoona mimi MAFISADI wale original walioko serikalini walimufuata RA awawekee pesa walizoiba maana RA anavijikampuni ,Hata hiyo RICHMOND ni viongozi hao hao walimtumia RA kupitisha mambo yao.

Huyu RA sema ana ngekekewa imemwangukia akatumiwa ktk dili la EPA na RICHMOND LAKINI si kama sifa mnazompa kila kitu RA, sifa za bure hizo,RA ni moshi tu hakuna kitu ,watu kama kukolimbana wameanza siku nyingi

Hao wapiganaji unaowaita waambie waende hatua nyingi zaidi watafute MOTO uliko Na wawapeleke mahakamani maana kesi anaweza fungua mtu yeyote na ukawakirisha ushahidi wako,wanasubiri nini?? wao ni mikutano ya hadhara tu ili 2010 wapate majimbo zaidi na fedha ziishie makao makuu.

Mkamap,

Hivi unaijua vizuri Tanzania ilivyo - ngoja nikupe mfano kidogo. Mwaka 1977 iliyojulikana kama EAC ilikufa. Pesa za pensheni za wastaafu ilikabidhiwa serikali na mpaka leo miaka karibu arobaini bado wanaidai serikali. Hiyo hiyo serikali mpaka juzi tu imeweka pingamizi mahakamani kuhakikisha hii kesi haifunguliwi ikijua kabisa haiwezi ikashinda kesi kama hiyo. Serikali inayoweza kutumia mahakama kunyima wananchi wake haki yao.... This can only happen in Tanzania.

Hiyo katiba inayompa haki mwananchi kwa mkono wa kushoto, inaichukua kwa mkono wa kulia na jeuri yote ya serikali na viongozi inaanzia hapo. Njia moja tu iliyobaki ya kudai action, ni kuappeal kwa wananchi. Nguvu ya wananchi hivi sasa inaanza kupamba moto na mageuzi makubwa duniani yamechochewa hivyo. Ni lazima tupige kelele na kupaza sauti maanake sauti ya wengi ni kama tsunami huwezi kuinyamazisha - mwulize marehemu Ceausescu wa Romania.

Masikitiko yangu ni kuwa tuna watu kama wewe mnaojaribu kuziba masikio kwa kuweka pamba. Kuna siku itabidi mtoe account ya matendo yenu na hapa usifikiri utampata godfather wa kumwegemea. RA kwangu ni just another dude in a big filthy pond iliyojaa mafisadi wakubwa kwa wadogo, wake kwa waume na kila moja anayeogelea kwenye hilo tope. Itakuwa kazi rahisi kuwatambua kwa uchafu wao. Muda wa kujisafisha ni sasa na unazidi kuyoyoma.
 
...kuna mambo unapaswa kuyaelewa kwanza hapa, ni kuwa kilichomsukuma Rostam kukutana na wahariri wa magazeti na kuandika habari za kupikwa kilikuwa kitu gani?

Kwa nini alifikia hatua ile?alikuwa anataka kuficha kitu gani?

Ajali ilipotokea alikuwa Nje ya Nchi ila akarudi usiku uleule tena kwa kutafuta ndege kwa nguvu kubwa sana hapo alipokuwa , nini kilimsukuma kufanya vile?

Ukiweza kupata majibu unaweza ukaelewa kinachoongelewa hapa .

Inaonekana una majibu. Hebu yatoe basi ili kuunganisha nadharia yako ikae sawa.
 
Mkamap,

Hivi unaijua vizuri Tanzania ilivyo - ngoja nikupe mfano kidogo. Mwaka 1977 iliyojulikana kama EAC ilikufa. Pesa za pensheni za wastaafu ilikabidhiwa serikali na mpaka leo miaka karibu arobaini bado wanaidai serikali. Hiyo hiyo serikali mpaka juzi tu imeweka pingamizi mahakamani kuhakikisha hii kesi haifunguliwi ikijua kabisa haiwezi ikashinda kesi kama hiyo. Serikali inayoweza kutumia mahakama kunyima wananchi wake haki yao.... This can only happen in Tanzania.

Hiyo katiba inayompa haki mwananchi kwa mkono wa kushoto, inaichukua kwa mkono wa kulia na jeuri yote ya serikali na viongozi inaanzia hapo. Njia moja tu iliyobaki ya kudai action, ni kuappeal kwa wananchi. Nguvu ya wananchi hivi sasa inaanza kupamba moto na mageuzi makubwa duniani yamechochewa hivyo. Ni lazima tupige kelele na kupaza sauti maanake sauti ya wengi ni kama tsunami huwezi kuinyamazisha - mwulize marehemu Ceausescu wa Romania.

Masikitiko yangu ni kuwa tuna watu kama wewe mnaojaribu kuziba masikio kwa kuweka pamba. Kuna siku itabidi mtoe account ya matendo yenu na hapa usifikiri utampata godfather wa kumwegemea. RA kwangu ni just one in a big filthy pond iliyojaa mafisadi wakubwa kwa wadogo, wake kwa waume na kila moja anayeogelea kwenye hilo tope. Itakuwa kazi rahisi kuwatambua kwa uchafu wao. Muda wa kujisafisha ni sasa na unazidi kuyoyoma.

Kaka
wewe kama unaona nimeweka pamba ni heri yako wewe uliyezibua hizo pamba, Lakini wote wanaojitokeza na kunjionyesha mbele ya kadamnasi yakua ni wapiganaji wema HERI yao Lakini siku litakapopigwa paragumu watalia na kusaga meno.

Ngoja nitoke kidogo na samahani kwa nukuu hii.
Si kila mmoja aniitaye Bwana Bwana (Yesu) ni wa upande wetu siku ya mwisho Nitawakana watu hawa maana si kondoo wa zizi hili.

Kuongea ya RA kama wewe waona ni upande wake heri yako wewe,Ila mimi ninachoongelea huu uzushi wa kumzushia kila jambo si mwema maana ana haki zake pia kama binadamu wengine.
 
Zipo mkuu, mfano buccal NTG for angina pectoris ina kick within 2 minutes..........

Inategemea mtu ana aina gani ya cardiac issues na dawa gani anayotumia mfano Calcium blockers (cardizem), beta blockers (atenolol) n.k OPD yake ni tofauti...lakini hapa ninapoishi protocol ya "code blue" ya li impending or actual infarct ni "MONA" from MONALISA na hiyo N inasimama kwa Nitroglycerin ambayo kama nilivyosema huko juu depending na application inaweza kukick within 2 min na kuokoa maisha........LOL

hiyo ni kwenye "nutshell" ki-layman...

kwahiyo mkulu FMES hakuwa kachekesha.... na yapo madawa mengine kedekede ya kimarekani yanafanya kazi chapchap hasa kwa ER!! kama unashida sana ni PM (lakini kuna fees ina apply) bwahahahahahahaha.

tuwe tunajaribu ku-research kidogo kabla ya kudhalilisha au kujidhalilisha....na hiyo ndio kisa cha Wangwe (RIP), anasema kweli watu wanamgeuza kichekesho na kumpandikizia uadui usio na maana...kwani ni uongo kwamba mapesa mengi yanaishia HQ ya chadema? kwani ni uongo kwamba wabunge wengi wa kuteuliwa wa chadema aidha ni wachagga au wananasaba za kichagga..........tuwe makini sana na kuacha maushabiki yasio ya lazima.

wkend njema!!.

YournameisMINE,

Mimi sio daktari lakini pia nina idea na madawa yote uliyoongelea. Hayahitaji uwe na mtu pembeni wa kukubebea dawa na kukupatia ukizidiwa.

Hata Angina inaanza kwa maumivu makali hasa chest na mara nyingi mgonjwa ana muda
wa kuchukua dawa zake na kumeza. Sidhani anahitaji kuwa na mtu wa kumbebea dawa in case anazidiwa.

Hiyo ni tofauti na magonjwa kama kisukari au hata athma ambayo mtu anaweza akaanguka, asijitambue na mtu mwingine anaweza kumsaidia kwa kumpa hizo dawa.

Suala hapa sio dawa inafanya kazi baada ya muda gani bali namna ya kuchukua hizo dawa.

Pia kwa Tanzania dawa zinazotumika kwa sehemu kubwa ni hizo calcium blockers au beta blockers.

Hii story ya kuwa na mtoto wa kubeba dawa ni yale yale ya Kawawa funika kikombe. Watanzania tunaongoza kwa story za mitaani na kuzihalalisha kama ukweli.

Kolimba alipata stroke shauri ya pressure kubwa ambayo alikuwa nayo kwenye hicho kikao. mambo mengine yote ni hearsay tu.
 
Nafikiri ni inhaler hiyo!

Zipo dawa nyingi ambazo zinahitaji kuzila mara kwa mara, ukiacha kula umekwenda na maji, na sitashangaa kama hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Kolimba. Hata hivyo huyu mtoto wake na yeye mwenyewe walikuwa wazembe kidogo kukubali kuingia kwenye kikao bila hizo dawa na kukubali huyu kijana asiingie kama kweli ndiye alikuwa anashikilia uhai wake!

Kitila,

Ni kweli kuna dawa nyingi zinahitaji kula/kunywa mara nyingi lakini huhitaji mtu wa kukusaidia.

Ni magonjwa machache sana kama Athma, Kisukari nk. ambayo unaweza kuzidiwa ghafla bila kujitambua na usipate muda wa kunywa dawa.

Magonjwa ya moyo ni tofauti, hata hiyo Angina unaanza kusikia maumivu na kwa kuwa unakuwa unalielewa tatizo lako basi mtu anakunywa dawa. Huhitaji kuwa na mtu karibu wa kukubebea dawa just in case mambo yanakuzidia.

Ukipata stroke ghafla sidhani kama hata huyo kijana anaweza kukusaidia kukunywesha hizo dawa.

Hili ndilo lilikuwa tatizo langu kwenye story ya FMES, bado naamini ni hearsay kama ya Nyerere kumwambia Kawawa funika kikombe.
 
YournameisMINE,

Mimi sio daktari lakini pia nina idea na madawa yote uliyoongelea. Hayahitaji uwe na mtu pembeni wa kukubebea dawa na kukupatia ukizidiwa.

Hata Angina inaanza kwa maumivu makali hasa chest na mara nyingi mgonjwa ana muda
wa kuchukua dawa zake na kumeza. Sidhani anahitaji kuwa na mtu wa kumbebea dawa in case anazidiwa.

Hiyo ni tofauti na magonjwa kama kisukari au hata athma ambayo mtu anaweza akaanguka, asijitambue na mtu mwingine anaweza kumsaidia kwa kumpa hizo dawa.

Suala hapa sio dawa inafanya kazi baada ya muda gani bali namna ya kuchukua hizo dawa.

Pia kwa Tanzania dawa zinazotumika kwa sehemu kubwa ni hizo calcium blockers au beta blockers.

Hii story ya kuwa na mtoto wa kubeba dawa ni yale yale ya Kawawa funika kikombe. Watanzania tunaongoza kwa story za mitaani na kuzihalalisha kama ukweli.

Kolimba alipata stroke shauri ya pressure kubwa ambayo alikuwa nayo kwenye hicho kikao. mambo mengine yote ni hearsay tu.

sawa msee,

nadhani nimekuelewa vizuri! tungekuwa live ninge shake hands nawe kwa kuonyesha class hapa!

Ila kubebewa dawa bado ni possible , si unajua tena MABOSI wa kibongo!? kila kitu lazima kuwe na mtu pembeni wa kumfanyia...kwahiyo sishangai kama vijidonge alikuwa navyo mtoto..

thank you bro, have a good night.
 
•Zitto: Mbowe hakumzika Wangwe kwa sababu za kiusalama

*Aahidi kutumia nafasi yake bungeni kuishughulikia TBC

Na Reuben Kagaruki

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Mwenyekiti wake, Bw. Freeman Mbowe, alishindwa kuhudhuria maziko ya mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, baada ya vyombo vya usalama kusema havina uhakika wa kumhakikishia ulinzi.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Kabwe Zitto, baada ya kuwasilisha malalamiko ya chama chake kwa Jukwaa la Wahariri, akidai habari zilizokuwa zikiandikwa na vyombo vya habari kuhusu kifo na mazishi ya marehemu Wangwe 'ziliiumiza' CHADEMA na Mwenyekiti wake kwa ujumla.

Bw. Zitto alitoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya wahariri waliotaka kujua sababu za Bw. Mbowe kutohudhuria maziko ya Bw. Wangwe yaliyofanyika juzi kama si kwa kuhofia usalama wake kutokana na vurugu.

Alikiri Bw. Mbowe kutohudhuria maziko hayo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali mstaafu Issa Machibya na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Bw. Liberatus Barlow, kuwaeleza viongozi wa CHADEMA kuwa hawana uhakika wa kumhakikishia ulinzi.

"Hatukuona sababu za kumpeleka kuhudhuria maziko wakati vyombo vya usalama viliishatuhakikishia kuwa havina uhakika wa kumpa ulinzi," alisema Bw. Zitto.

Hata hivyo, wenyeviti wenzake, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Bw. Augustine Mrema (TLP) na Bw. James Mbatia (NCCR-Mageuzi) walihudhuria.

Bw. Zitto alidai kuwa wasiwasi huo ulitokana na taarifa zilizokuwa zikiandikwa na vyombo vya habari kuhusu kifo cha Bw. Wangwe huku baadhi ya vyombo vya habari vikijaribu kukihusisha na mgogoro ndani ya chama chao.

Alidai kuwa habari zilizoandika kuwapo kwa vurugu siku ambayo maziko ya marehemu Wangwe yaliahirishwa, ili kutoa mwanya mwili wake ufanyiwe uchunguzi tena na familia yake zilikuwa za upotoshaji.

Alidai kuwa siku hiyo, Bw. Mbowe hakuondolewa nyumbani kwa marehemu Wangwe chini ya ulinzi wa Polisi, wala wananchi hawakuwa na mapanga na mishale kama ilivyoripotiwa.

"Viongozi wote waliokuwa pale kwa umoja wao waliondolewa eneo hilo kwa taratibu za kiusalama, kumlenga Mbowe kuwa aliondolewa kwa sababu za kiusalama peke yake si kweli," alisema Bw. Zitto.

Aliongeza kuwa kilichojitokeza siku hiyo ni wananchi kuwa na munkari wa kuondokewa na kiongozi wao.

"Siku hiyo hakuna panga lolote lililoinuliwa dhidi ya kiongozi wetu, Mbowe alipowasili alipokewa na walinzi wa chama na wananchi walikuwa wakimwambia tumeondokewa na kiongozi wetu tumebaki na wewe (Mbowe) peke yako," alisema Bw. Zitto.

Alikiri kuwa wananchi walikuwa wamebeba mabango tena kwa wingi lakini hakuna hata moja lililokuwa na ujumbe wa kukilenga chama hicho wala Mwenyekiti wake.

Bw. Zitto alihoji kuwa kama kweli habari hizo hazikulenga kukichafua chama chake, ilikuwaje waandishi wa habari hawakuandika taarifa za kufukuzwa kwa wana-CCM waliofika kwenye msiba huo wakiwa wamevalia sare za chama chao.

Alipinga taarifa kuwa maziko ya marehemu Wangwe yaliahirishwa kwa sababu ya vurugu, kwa sababu yeye alishiriki vikao vya familia na hata kwenye uchunguzi.

"Familia ilikuwa na shaka na kifo cha marehemu hivyo walikubaliana wafanye uchunguzi mwingine," alisema na kuongeza kuwa kilichozusha wasiwasi ni kuchelewa kutangaza uamuzi huo, kwani walifanya hivyo kusubiri viongozi.

Alisema taarifa ambazo chama hicho kinazo kutoka vyanzo vya CHADEMA na vingine vya kiserikali kwa maana ya Polisi na Usalama wa Taifa, ni kwamba kulikuwa na wasiwasi ambao walikuwa nyuma ya kile alichokiita upotoshaji wa vyombo vya habari.

Katika hatua nyingine, Bw. Zitto alisema chama chake kimesikitishwa na kile alichokiita vyombo vya umma kutumika vibaya na hakutarajia kama televisheni ya Taifa TBC1 ingekuwa inarudia mara kwa mara habari za kuhusisha kifo cha marehemu Wangwe na mgogoro ndani ya chama chake.

"Walikuwa wakifanya marejeo ya mgogoro wa chama na kifo cha Bw. Wangwe, kama chama hili hatutaliacha hivi hivi na mimi nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma sitaliacha, kwa sababu ni matumizi mbaya ya fedha za umma," alisema.
 
Suala hapa sio dawa inafanya kazi baada ya muda gani bali namna ya kuchukua hizo dawa.

...Hii story ya kuwa na mtoto wa kubeba dawa ni yale yale ya Kawawa funika kikombe. Watanzania tunaongoza kwa story za mitaani na kuzihalalisha kama ukweli.

Kolimba alipata stroke shauri ya pressure kubwa ambayo alikuwa nayo kwenye hicho kikao. mambo mengine yote ni hearsay tu.

Hata kama ingekuwa ni plausible mtoto kutembea na kifurushi cha dawa za baba hii bado ni "Kawawa funika Kikombe" kwa sababu Kolimba asingekubali mtu aliyebeba dawa zake za kufa na kupona asiruhusiwe kuingia nae ndani.

Na hata kama tukikubali kwamba mtoto hakuruhusiwa kuingia na baba, bado ni "Kawawa funika kikombe" kwa sababu Kolimba, Katibu Mkuu wa CCM, angewaambia waliomkatalia mtoto kuingia kwamba basi nipasieni kifurushi changu cha dawa za kufa na kupona kutoka kwa mtoto kikakae kwenye meza pembeni yangu!

Kwa hiyo, either way you cut it, the narration is still about as good as "Kawawa funika kikombe." You couldn't be more correct, Mtanzania.
 
true, jamaa huenda alikuwa na angina/ischemic attacks..huenda ilikuwa unstable na hivyo unpredictable!! angina ikiachiwa bila udhibiti inaweza ku-develop kuwa Myocardial Infarction (MI)...good news ni kwamba dawa zake hasa NTG unaweza kuchukua prophylactically, sasa sijui Kolimba alikuwa na HD ya aina gani na dawa gani alikuwa anatumia kiasi kwamba akupata dose prophylactically kama alijua anaenda kwenye gauntlet!!?? au pengine hakujua, walimstukiza!?....vyovyote vile, hawa jamaaz itakuwa waliua bila kukusudia!! siku tukichukua nchi watajibu na hili.

Hahahaha...sawa bana...I see you are very much in your element when it comes to these medical issues.....
 
hivi hawa CHADEMA kwanini wasiwe na mtu mmoja tu kama msemaji rasmi juu ya sakata hili? haya mambo ya mara Mnyika, mara Slaa, mara Zitto nadhani yatawaletea shida...yaani wanakuwa kama genge la wahuni ambalo kila mtu anaweza kusema vile anavyofikiria binafsi na sio kama chama. INAKATISHA tamaa...
 
Mkuu wangu Nyani, kumbe na wewe umemshitukia jamaa, si unamuona nilifikiri niko peke yangu tu kumbe na wewe umemshitukia saafi sana,

JF Experts wote wako sawa mkuu, hakuna anayezusha hapa kwa sababu hupewi hicho cheo bila ya kuwa na uwezo nacho, halafu kama unatuona hapa JF ni wazushi Mkulu Wangu MMJ ameshasema mara nyingi sana, kwa nini usende mbele kusikouwa na wazushi?

FMES
Nimesoma hoja zako ni nzuri lakini ondoa hilo neno 'wote' linapoteza sifa ya maelezo yote kwani ni hasty generalization, otherwise uko sawa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom