Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Kichunguu

Mimi bado naamini ni ajali tu na hakuna mazingira ya murder hapo.

Mkuu ni bora ubaki hivyo hivyo na imani hiyo lakini kwa nini serikali inafanya ujanja na uhuni katika swala la uchunguzi?
 
Ni nini mana ya UCHUNGUZI huru iwapo kuna MASHARTI kuhusiana na uchunguzi huo? Serikali si ilisema itakuwa SHAHIDI tu katika uchunguzi huo, kwa nini inapanga sasa ni nani anastahili kuufanya uchunguzi ambao umepangwa na familia? Kama kweli ipo sheria hiyo, haifai kwa sababu katika hili imeshajidhihirisha kuwa ni mbovu

Ingawa mimi siyo mtaalamu wa sheria, nakuhakikishia kuwa hakuna sheria ya namna hiyo, vinginevyo Rotary Club na Lions Club wasigekuwa wanaleta madakatri wao wa macho na kuruhusiwa kufanya kazi zao kwa muda bila kubugudhiwa na serikali. Daktari wa kufanya autopsy hana tofauti kabisa kiutendaji na dakari wa macho.
 
Invisible na wengine,

Mie naona ni vizuri TBC1? kuonesha Live,Hata CNN huwa wanakatisha habari na shughuli zote kama kukiwa na Breaking News.This is Breaking New and they are right to show the events.mambo mengine hatujui ila kuonesha ni haki na wamefanya Vyema.Wewe ungejuaje haya yote kama siyo TBC!?

Msilifanye suala hili kuwa la kisiasa,nilishasema toka jana..Ole wenu CHADEMA,kwa vyovyote vile bado mnalo...hata kama,kuna kosa lillishafanyika na lazima watu walinywe sasa nomatter who did but it will be like it is.Poleni coz mmeshikwa pabaya
 
Serikali imejaa wapumbavu.Wanayaogopa ya yule Daktari aliyemfanyia Sokoine autopsy alivyolikisha news mpaka wakampiga risasi babu wa watu na kuanza kumtrail from morning to evening ....

...Prof Shaba? kumbe ile risasi ya mguu alopigwa mguuni ni 'wao' sio walinzi? aiseeee!?
 
hii ni news kubwa, inahitaji coverage ya kutosha, kama TBC wameamua kuicover hii kwa dhati, basi tuwapongeze!, kiufupi hiyo ni breaking news
CNN wenyewe wakipata breaking news huwa wanaicover kwa kuirudia rudia mpaka inachosha, sembuse kifo cha Wangwe?, ambaye hivi recently amekuwa politically worth to watch?
 
Wewe mtanzania sasa unataka tu kuvuruga tu mambo, Kilichohitajika hapo ni daktari ambaye ange confirm procedure. Regardless anatokea wapi. Naona unajaribu kuvuruga tu mambo au ndo muhusuka wa mtandao wa mauaji!!!!! Tumechoka na uonevu wa kisiasa wa namna hii. Kwenye suala tata kama hili acha kuongeza utata usio na maana na hata unathubutu kusema "kama ipo sheria........." Nosence/hopeless.

Tutaendelea kuwekwa wajinga milele. Na sasa its a point of no return, then we are going to fight against this evil spirit of our leaders. Calling a vote through papers and turning us wild animals to be shooted. What kind of a country is it??

RIP Wangwe and take courage Wangwe's family as well as Big up!!!!!!!
 
Mkuu Gamba Heshima Mbele,

tusiwe na mawazo ya kimageuzi hata kwa vitu vya maana,Jana inajulikana wazi watu wa nyumbani walitaka kumdhuru Mwenyekiti na halisi akutudanganya kwamba walimsahngilia sana huku walitulizwa na kina Mrema.Dhambi ya ukabila ndiyo matokeo yake haya hapa..
 
Hivi postmortem ya kwanza iliofanyika dodoma imesema nini? na ile bastola ya malya mbona ina utata,mtu una basola unakubali kuibiwa kila kitu hupigi hata risasi moja hewani?
 
Kichuguu,

Kama hizo habari ni kweli hata mimi nitaishangaa sana serikali. Lakini mara nyingi kwenye cases kama hizi rumours zinakuwa na nguvu zaidi ya ukweli, Only time will tell.

Kwa daktari wa Kenya naweza kukubali, kama kuna sheria inayosema hivyo ni sawa, lakini nchi si ina wataalam wengi tu? Hasa wale wanaofanya kazi kwenye private hospitals ambao sio waajiriwa wa moja kwa moja serikalini.

Mimi bado naamini ni ajali tu na hakuna mazingira ya murder hapo.
Wewe mtanzania sasa unataka tu kuvuruga tu mambo, Kilichohitajika hapo ni daktari ambaye ange confirm procedure. Regardless anatokea wapi. Naona unajaribu kuvuruga tu mambo au ndo muhusuka wa mtandao wa mauaji!!!!! Tumechoka na uonevu wa kisiasa wa namna hii. Kwenye suala tata kama hili acha kuongeza utata usio na maana na hata unathubutu kusema "kama ipo sheria........." Nosence/hopeless.

Tutaendelea kuwekwa wajinga milele. Na sasa its a point of no return, then we are going to fight against this evil spirit of our leaders. Calling a vote through papers and turning us wild animals to be shooted. What kind of a country is it??

RIP Wangwe and take courage Wangwe's family as well as Big up!!!!!!!
 
Ni sheria gani ya nchi inayokataza mwili kufanyiwa uchunguzi na Daktari wa kigeni ?
 
... Daktari wa kufanya autopsy hana tofauti kabisa kiutendaji na dakari wa macho.

...ipo tofauti mkuu, pamoja na kwamba wote ni madaktari, lakini anayefanya autopsy ana link moja kwa moja kwenye Criminology kwenye mambo ya forensic. Huyu wa Autopsy, anakwena deep kuliko anaye sign post mortem ya kawaida. Ushahidi wake unaweza kuhatarisha hata 'usalama wa taifa'!
 
Familia iamue kwenda kumzika Kenya kusudi huyo dokta akamfanyie uchunguzi , tuone maajabu mengine kama kuna sheria ya inayozuia kumzika raia wa Tanzania nje.
 
Kichuguu,

Kama hizo habari ni kweli hata mimi nitaishangaa sana serikali. Lakini mara nyingi kwenye cases kama hizi rumours zinakuwa na nguvu zaidi ya ukweli, Only time will tell.

Kwa daktari wa Kenya naweza kukubali, kama kuna sheria inayosema hivyo ni sawa, lakini nchi si ina wataalam wengi tu? Hasa wale wanaofanya kazi kwenye private hospitals ambao sio waajiriwa wa moja kwa moja serikalini.

Mimi bado naamini ni ajali tu na hakuna mazingira ya murder hapo.

Mtanzania,

Familia imegundua kuwa mwili wa marehemu ulikuwa na matundu yanayoonyesha kuwa ya risasi. Kulingana na maelezo yale risasi zile zilikuwa mbili, zote zilianzia shingoni, moja ikatokea mdomoni na nyingine ikatokea tumboni. Wakasema wanaomba ifanyike autopsy nyingine tofauti na ile ya serikali, na wakati huo serikali kupitia waziri wake wa Kilimo ikakubali. Sasa kama serikali imebadilika msimamo wake ghafla na haitaki kutoa nafasi uchunguzi huo kufanyika ina maana kuwa kweli hiyo taarifa ya matundu ya risasi ni sahihi, na hivyo lazima kuna murderer ambaye serikali inataka kumficha. Mazingira haya yanatia uchungu sana ndugu yangu, kwani inaonyesha kuwa mbele ya serikali yetu raia ambao uhai si wa muhimu sana ukilinganisha na wengine.
 
Mie nataka kuulilza,

inaonekaana watu wanaju ammbo mengi zaidi kuhus msiba huu,
Je mnahisi au mnajua ni nani alihusika na kumpiga risaisi Wangwe kama mnavyosema?Kuna kitu nafikiri mie na ambao hatujui wapo wanojua.watuelezee
 
...Prof Shaba? kumbe ile risasi ya mguu alopigwa mguuni ni 'wao' sio walinzi? aiseeee!?

Ndio hivyo Mkuu.Nasikia alikuwa amelewa Moshi Club then akaanza kubwata ovyo yakamkuta.Kalazwa Hospitali wakampelekea a bottle of wine wakamwambia next time it will be your neck.
We have never heard of him since then.probably he was eliminated.
 
Mie nataka kuulilza,

inaonekaana watu wanaju ammbo mengi zaidi kuhus msiba huu,
Je mnahisi au mnajua ni nani alihusika na kumpiga risaisi Wangwe kama mnavyosema?Kuna kitu nafikiri mie na ambao hatujui wapo wanojua.watuelezee

Gembe ,

Watu wengi hawajui ni nani haswa aliyemuua Wangwe ndio maana wanataka private investigation . Ila suala la serikali kuchukua siku nzima na baadaye kukataa Dokta kutoka Kenya ni suspicious kiasi fulani . Pia lazima utambue ya kuwa watanzania wa leo sio wa miaka ya ile, siku hizi watu wana - insquisitive mind wamechoka na kukubali kukubali tuu.
 
Haya ni maajabu ya Musa.......iweje mtu anyimwe uhuru wakuchagua mtu wa kufanya uchunguzi eti kisa anatoka nje..my god!! indepenence iko wapi hapa... Mbona EPA tulileta kampuni kutoka nje ifanye uchunguzi???? singemsema basi BOT nisehemu nyeti na inahusisha usalama wa taifa bora tumchukue Assad Associate afanye uchunguzi sababu ni Mtanzania..mbona mkaenda kwa kampuni toka nje.....na kwanini hili la wangwe linakua treated tofauti????? .... Kita eleweka tu.... mungu saidia..!
 
...ipo tofauti mkuu, pamoja na kwamba wote ni madaktari, lakini anayefanya autopsy ana link moja kwa moja kwenye Criminology kwenye mambo ya forensic. Huyu wa Autopsy, anakwena deep kuliko anaye sign post mortem ya kawaida. Ushahidi wake unaweza kuhatarisha hata 'usalama wa taifa'!

Daktari wa autopsy ni daktari tu. Anachofanya ni kutafuta chanzo cha kifo na kuandika prescription yake ambayo ni ripoti inayoonyesha chanzo cha kifo. Ni jukumu la mtibiwaji kuitumia prescription hiyo kwa faida yake. Wanaofaidi prescription ya aina hii siyo pharmacy bali ni wanasheria na vyombo vye sheria. Daktari huyo anaweza kuitwa mahakamni kama kuna kesi ili kutoa ushahidi wake, lakini sioni tatizo kwa raia wa nje kutoa ushahidi kwenye mahakama zetu kwa vile huwa tunawashitaki na kuwafunga raia wa nje pia. Kipingamizi pekee ni kama sheria zetu za autopsy zinataka daktari wa autopsy kuwa amesajiriwa na serikali ya Tanzania tu, jambo ambalo sina uhakika kama kweli lipo.

Kuhatarisha usalama wa taifa ni jambo ambalo silioni hapa. Ni kama kusema kuwa kuna watu wakifa basi serikali ifiche sababu za vifo vyao kwa sababu za usalama wa taifa hata kama wameuwawa na wahalifu. Je sheria ya kumnyonga mtu anayekutwa na kosa la mauaji ina maana gani?
 
Naye Waziri wa Kilimo na Chakula Stephen Wasira, alisema serikali haina kipingamizi juu ya uchunguzi wa kifo cha Wangwe.

Lord have mercy !
 
Familia iamue kwenda kumzika Kenya kusudi huyo dokta akamfanyie uchunguzi , tuone maajabu mengine kama kuna sheria ya inayozuia kumzika raia wa Tanzania nje.
Rufiji,
Naona umeniwahi. Nilitaka kusema hilo hilo kuwa WAUPELEKE mwili Kenya na huko ukafanyiwe uchunguzi. Sasa kama MAFIA watataka na wao Dr wa KIMAFIA aende Kenya hilo litakuwa shauri lao na FAMILIA sasa inaweza ikakataa kumchukua huo DR. wa Dodoma. Kwanza ingebidi jina lake lipatikane. Sidhani kama SERIKALI itakataa mwili wa CW usipelekwe Kenya kwa uchunguzi. Sidhani kama kuna sheria kama hiyo. Mbowe alete ile HELCOPTER yake ya kukodisha na within few hours mwili utakuwa tayari umesharudishwa Tanzania kwa mazishi kuwa kesho. Hili nafikiri hakuna atakayelikataa. Pia watu wa Musoma naona inabidi wawatoe balu watangazaji wa TBC1 maana hawa jamaa kwa kweli wanachemsha. Kwa sasa hakuna anayesema waliomuua ni CCM au CHADEMA au Mafia wa madini. Watu wanataka kujua kafa na nini. Officially hadi sasa ni kuwa kafa kwa ajali ya gari. Ila wenzetu tayari wameshajua waliomuua ni CHADEMA.
Wenye mawasiliano na ndugu wajulisheni kuwa AU waupeleke mwili KENYA au wakubali kuwa WAMEMU-WANGWE ndugu yao na WAMZIKE, Yaishe-Ameni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom