Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
kwanza R.I.P Wangwe!
pili kumbukumbu zangu zinanikumbusha kwamba mbowe alishawahi kusema, "anajua njia wanazotumia (hao watu) kuua viongozi, na nikaandika thread ili mbowe ahojiwe na njama zifahamike ili viongozi wanusurike, watu wakaniona mie ovyo, sasa sishangai lolote linalotokea maadamu baadhi ya watu kama mbowe washasema wanajua jinsi gani viongozi wanauliwa na "tunakataa" kufuatilia, then let the blood spilling continue. Na tusipige kelele.

Pia nafikiri wengi humu wanaojifanya wanataka kushuhurikia na kutaka kujua ukweli kuhusu wangwe ni wanafiki ! Mlichukua hatua gani baada ya mbowe kusema anajua njia wanazotumia kuulia viongozi ? Sasa leo hii watu wanasema mara wangwe kapigwa risasi na ajali ya kufa imekuwa kama kifuniko, na wengi tumekubali, je ile hoja ya mbowe kusema tuipuuzie. Mwisho kuhitimisha, Mbowe pia alisema kwamba "watauawa" sana mwaka huu hadi wote wamalizane. Tunataka "clues" ngapi tena zaidi ya hii ?

Kuna soo many dots za kuunganisha btwn Mbowe na tofauti za Wangwe. Sisemi kwamba Mbowe kamfanyizia Wangwe, but there is a possibility. Tafuteni ile thread niliyoanzisha ya mbowe kuhojiwa maana najua itaraise many issues!!

Humu naona watu wengi wanakuwa fed na wrong info ambazo zinaegemea upande mmoja. Na usipokuwa makini, utaendelea tu kukubali kila kinachoandikwa.
 
Swali la kujiuliza ni vipi kama ripoti ya uchunguzi wa Daktari huko Tarime itatofautiana na ile ya Dodoma ?

sio kila kitu kitegee ripoti toka kwa daktari, kuna clues nyingi sana ambazo tunaweza kuzitumia na baadae kuunganisha na hiyo ripoti toka kwa daktari. Kwenye crime scene yoyote ile naamini "wazee" watataka kujua who your friends and who your enemies are, well, je tumeshajiuliza hayo kwenye hili suala la wangwe ?
 
Mgagagigikoko,
Mkuu hii imekaaje lakini?.. Ebu nipe fikra zako.
Habari za Utata sijui kama ni ngonjela ama kweli lakini kutoka Tarime hadi jana Alhamisi Bendera za Chadema na CUF zilikuwa nusu mlingoti sio CCM... Wamekuja shtuliwa baadaye.
Pili, Wajumbe wa CCM hasa viongozi wa juu wameuchuna, waliokwenda kuzika unawahesabu hali vyama vingine vyote wametuma viongozi wao wa juu kuhudhuria mazishi.. Nasikia ati viongozi wa chama tawala waliaga maiti Dodoma imetosha, haya maneno kweli ama ya watunzi..Na kama kweli kuna sababu gani hasa maanake binafsi mkuu nimeshindwa kabisa kuelewa.
Wenye taarifa za karibu jamani ebu naomba list ya viongozi wa serikali toka CCM waliokwenda Tarime!
 
Kwa kweli the big point na hiki kifo ni kwamba hili taifa tunakwenda wapi? Inakuwaje anapotokea mwanasiasa kutaka mabadiliko tu anapatwa na kifo? Tunajua kuwa rais wa Jamhuri hahusiki, lakini as the president wa taifa anajionaje na hizi never ending dramas?

Kila yanapotokea matatizo kama haya yanayowaacha wananchi katika wasi wasi maswali mengi, imani na serikali inashuka sana, inaonekana ndani ya serikali yetu kuna baadhi ya viongozi au watu wenye serikali yao pia tofauti na hii tunayoijua, je ni kina nani hawa? Facts zote za hii ajali ziko wazi kuwa hii ajali haikuwa Amri ya Mungu na imefanyika kwa ufundi mkubwa sana, kwa sababu hata maelezo ya kila aina yatolewe kuhusiana na hii ajali, haiwezekani kuwa huyu kijana Mallya, ndiye aliyekuwa dereva wa ile gari, lile gari haliwezi kuwa limebiringita tu kwenye ardhi, tena yenye mchanga na kushia kuonekana kama limepondwa na jiwe kubwa sana,

Huko majuu magari yanayofanana na hili la ajali, huwa unayaona mahali maalum, kwa mfano kwa mji kama New York, ukienda mahali panapoitwa Hunts Point, ambako magari hupongwa pondwa na mitrekta mikubwa kama milima, ili yaende kuyeyushwa tena na kuwa chuma na hupondwa mengi kwa mpigo na kupakiwa kwenye magari maalum, sasa haiwezekani gari likapinduka njiani tu na kuwa kama limesgwa na ile mitrekta ya NY,

Kuanzia uchawi bungeni, mpaka this kind of accident, tunaenda wapi? Marekani kuna wakati kulikuwa na mafia mmoja mkubwa sana kwa jina la John Gotti, huyu alikuwa ni mafia lakini kila akipelekwa kweye mikono ya sheria alikuwa akiishinda serikali, karibu mara kumi, ikafikia mahali wananchi wakaanza kumuamini kuwa na yeye ni serikali, kwani matatizo yao ambayo yanatakiwa kwenda kwenye sheria, wakaanza kwenda kulalamika kwa huyu Gotti, badala ya kituo cha polisi, rais Clinton alipoingia, akaletewa hii taarifa ya huyu mafia kuwa ana undermine serikali, ndipo siku moja alipowaita wakubwa wote wa law enforcement na kuwapa mwezi mmoja kumuondoa huyu mafia by any means necessary, haikuchukua muda mkuu akafikishwa mahakamani, sheria na haki zote zilivunjwa kwa makusudi ili kumpeleka jela maisha, ambako alishia kufa akiwa huko, end of the story! baadaye na mtoto wake pia wakamfilisi kila kitu na kumtia jela pia!

Wakati umefika kwa serikali yetu kufanya usafi, kuna uchafu somewhere, na kaserikali flani hivi ndani ya serikali yetu kuu, walianza kama mchezo lakini sasa inaanza kuwa out of the control, matokeo ni sisi wananchi kukosa imani na serikali ya sasa, haya mambo niliyoyapata kwenye uchunguzi kwamba sasa kiongozi hawezi kusafiri bila some very stupid measures it is scary!

Nimeziona facts zote za hii ajali, ninasema kuwa haikuwa ajali ya Mungu, ni ajali iliyotengenezwa tena kwa kiufundi sana, na waliokuwa wanajua wanachokifanya, ni nani hawa? Ajali kama hii iliwahi kumkuta Mwaikambo, ukweli ni kwamba walinzi wa ubalozi wa Rwanda, ambako hiii the so called ajali mbaya ya gari ilipaswa kuwa imetokea, walisema hawakuiona hiyo ajali, lakini walisema wazi walichokiona, na mkulu mmoja aliyehusika sana na mazishi ya ule msiba, anasema kuwa alionywa na wakulu flani kuwa azibe mdomo wake, na kupewa zawadi ya ubalozi, sasa kusingekuwepo na hizi kumbu kumbu tusingekwua na wasi wasi na hii ajali, sasa ni ajali ngapi zaidi zitokee ndipo serikali yetu iamke na kuwachukulia hatua hiii serikali ndogo ndani ya serikali kubwa?

Kwa kweli hiki kifo ni huzuni kubwa sana, ingawa nilikuwa simfahamu sana marehemu, sisi tutaendelea tu na uchunguzi na tutasema wazi matokeo, lakiin something serious need to done na serikali yetu kuhusu hiii tabia, tutapoteza viongozi wote na kuwakosa viongozi wazuri wapya kwa sababu ya kuogopa, sasa tutapata wapi maendeleo?

Mungu Ambariki Marehemu Wangwe na wananchi wote wa Tarime, tuko nyuma yenu na huu msiba mzito wa taifa!
 
Now According to more dataz ni kwamba:-

2. Je CCM wanaweza kuwa na interest na kifo chake? Hapana, not CCM collectivelly as chama, kwa sababu sio siri ndani ya CCM nzima kuwa jimbo la Tarime ni la wapinzani, ni so bad kwamba CCM as chama inajua kuwa hata vyama vyote vya upinzani vikipigwa marufuku kugombea uchaguzi wa bunge kule, ikaachwa CCM peke yao kwenye ballot, bado wananchi wa Tarime, hawataipigia kura CCM, cha maana sana hawataenda kwenye kupiga kura,

CCM haijawahi kupoteza hata one minute kufikiria jimbo la Tarime, jimbo la Zitto, jimbo la Dr. Slaa na hata jimbo la Ndesamburo, haya ni kwa maneno ya baadhi ya viongozi wa CCM nilioongea nao leo, binafsi ninaiunga mkono hii theory 100%, kwamba CCM as a chama, haiwezi kuwa na interst na kifo cha Wangwe.

3. Chadema as chama, hapana, some individulas ndani ya Chadema may be, lakini kazi iliyofanyika kwenye ajali ni too professional kuwa imefanywa na individiduals wa ndani ya Chadema, hata kama wangekuwa na interest lakini wasingeweza kufanya ile kazi kwa ufundi kama ilivyofanyika,



Heshima yako mkuu....duuh hii habari inabadilika sura kila dakika.....nakubaliana na wewe kuwa CCM kama taasisi hawahusiki na kifo....lakini is it possible that some few individuals from CCM or people associated with CCM wamefanya hili ili kukisambaratisha CHADEMA wakitumia mwanya wa tofauti ya marehemu na uongozi wa CHADEMA?....lengo likiwa kuassociate CHADEMA na kifo cha Wangwe....in that way....kikose credibility na kukiweka katika wakati huu mgumu hasa ukichukulia kuwa CHADEMA (through wabunge wake) wamekuwa mstari wa mbele kushikia bango ufisadi.......because trust me if CHADEMA is implicated in any ways, shape or form.....they will be on the defence....ili kukinusuru chama chao....and not on the offense in ufisadi! That might even spell they downfall hence making their future very gloomy......

Kabla ya marehemu hajachukua ubunge alisota ndani kwa kesi za kubambikiwa zilizokosa kichwa wa miguu, literally marehemu alitoka jela na kuingia moja kwa moja kwenye kampeni....baada ya kushinda kesi yake iliyojaa mizengwe! Huenda bado alikuwa na wabaya wake walioshindwa kwenye kesi na sasa wakaamua kukatisha maisha yake.....

Also as a point of clarification....CCM wenyewe ndiyo walioboronga kwenye jimbo la Tarime baada ya kuaswa na wananchi kuwa wasimsimamishe Chambiri.....ambaye alikuwa hatakiwi kabisa....lakini kwasababu wanazozijua wenyewe CCM hawakusikiliza hili....marehemu akapeta kiurahisi.....wananchi wa Tarime wana hulka moja.....huwezi kuwalazimisha wafanye kitu....obviously I am not trying to marginalize marehemu's victory...NO in no way....but kulingekuwa na mgombea mwingine kungekuwa na ushindani zaidi.....wananchi walishasema heri wampe kura zao mbwa kuliko Chambiri.........
 
"I'm greatly relieved that the universe is finally explainable. I was beginning to think it was me." by The Great Jewish Comedian, Producer, Director, Movie star and Writer..Woody Allen.

RIP CHACHA WANGWE..hakika ulikuwa kipenzi changu ktk wanasiasa wa wabongo! Pumzika kwa amani bingwa. Ni dhahiri kuna watu walishindwa kukuelewa, lakini wakina sisi tunao amini ktk no nonsense tulikuwa pamoja nawe ktk kipindi hiki chote..Muchos Graciasi, it was great to have you, hommy. We will miss you miserably.

Kuna tabia mbaya sana ktk jamii ya TZ ya kujenga uadui na watu tusiokubaliana nao kimawazo. Kulikuwa hakuna haja ya "ku-cross psychological boundaries" za huyu marehemu "chamaa" kwasababu tu hakuwa akikubaliana na baadhi ya watu ktk Chadema au bungeni! The dude was pushed to the breaking point psychologically kiasi kwamba akawa 'desperate' kupata mtu wa "karibu"/ rafiki, hii ikapelekea naivette ya kudili na watu "shady" kama chalii Mallya. Tabia hii ya uadui wa bila sababu ipo hata hapa JF, na kwa bahati mbaya "mijitu" mingi hasa ile 'mi-prominent members' wanadhani ni sahihi..ni u-selfish ambao hauelezeki! Kulikuwa na sababu gani ya kum-label marehemu mijina mibaya lukuki, ati kwasababu tu hakubaliani na makao makuu ya chama? kwahiyo alitakiwa awe bwana ndio kama ushoga wa "wa-rangi rangi " hapa JF? humanity na individuality kama binaadamu upo wapi kama kila mtu atakuwa na fikra sawa na wenzake kwa wakati wote?! C'mon pple hii ni civility 101 na lazima tujifunze kwamba utofauti si uadui!

Sasa Chadema lazima wanajuta..maana nina amini hii wamesukumiwa "cross bomba," zigo la mavi kwenye mlango mkuu..je nani atalizoa? kulikuwa kuna kila jinsi ya kukubaliana kutokukubaliana na Wange, isitoshe shutuma zake zilikuwa na merits..now why akawa public enemy number one chamani? Hii kitu ni PR disaster kwa Chadema na Upinzani kwa ujumla! Inasikitisha sana.

Dogo Mushi,
Kuna siku nilikwambia hapa kuwa, mdomo uliponza kichwa kikakatwa! sasa unaona matunda ya uropokaji wako? nadhani utakuwa umejifunza..

Rip Wangwe.

Goodluck ya'll
 
Kiungani.
Hata BBC inamilikiwa na Roastam Aziz au CCM? nimekuwekea link ya BBC WORLD SERVICE juu ya Mbowe kutimuliwa nayo huiamini? basi tusubiri KLH NEWS ina balanced story. lakini hiyo hiyo KLH NEWS siku mbili zilizopita imeleta habari za uongo za DR.Masau na MWANAKIJIJI akakiri kuwa sources zake zina utata.

Duh yaani una-spin mpaka habari za BBC? Kaazi kweli kweli!
 
Kwa mujibu wa maelezo ya watu kuhusu habari hii ni vema ikasubiriwa ripoti ya wachunguzi huru kabla ya kuendelea.

Kwa nature ya hiki kifo kuna number of assumption can be made.Ni busara kusubiri ili kupata wigo mdogo wa kujadili ukweli kuhusu hili.Ktk wakati mugumu ndio unapima competence ya watu hasa ya kufikiri.
 
Haya Sasa mambo yamezidi kuwa makubwa. Sijui kama kuna aliyekiwsha post hii kutoka gazeti la Mwananchi

Wangwe ahofiwa kupigwa risasi familia yagoma kumzika
*Wahisi ana alama za kupigwa risasi shingoni
*Mbowe, Zitto wafanyiwa fujo msibani, wakimbilia Musoma

*Mrema, Mbatia, Lipumba wasema wataendelea kubaki


Waandishi Wetu, Tarime


NDUGU wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime kwa tiketi Chadema wamegoma mwili wa ndugu yao kuzikwa ili kuruhu uchunguzi wa kifo chake ufanyike kutokana na hisia za wanafamilia kwamba alipigwa risasi hakufa kwa ajali ya gari kama ilivyotangazwa na vyombo vya usalama na ofisi ya Bunge.

Msemaji wa familia hiyo, Prof. Samuel Wangwe alisema kuwa kutokana na kifo hicho kuwa na mashaka mengi familia imeamua kufanya uchunguzi wa kina ili ijiridhisha na sababu za kifo cha mbunge huyo.

Akizungumza katika hadhira iliyokusanyika nyumbani kijijini Kemakorere, alisema familia imepata mashaka makubwa kutokana na mambo mengi na hasa sababu za kifo ambazo zimedaiwa kuwa ni ajali.

"Mambo mengi yamesemwa sasa kama familia tumeamua kufanya uchunguzi huru na wa kina ili kubaini sababu ya kifo cha marehemu, katika uchunguzi huu familia itatoa daktari wake na serikali," alieleza.

Alisema kuwa familia imeamua kusitisha maziko hayo kutokana na mwili wa marehemu kubainika kuwa na jeraha ambalo wanadhani limetokana na kitu kingine na wala si ajali ya gari kama ilivyoelezwa.

Alipoulizwa na gazeti hili iwapo familia imefanya uchunguzi wa awali na kubainika kuwa kifo cha marehemu kimetokana na kushambuliwa kwa risasi, Prof Wange alisema kuwa ni kutokana na utata huo familia imeamua kufanya uchunguzi wa kina kwa kuzingatia taratibu na sheria.

"Ni kweli mwili wa maerehemu umekutwa na jeraha, lakini mimi sijaliona, na wala sijui kama ni la risasi, lakini kikubwa tunafanya uchunguzi kesho (leo) ili kuondoa utata wote huo, hii ni haki ya familia tumetaka hivyo na serikali imeridhia," alieleza.


Kwa upande wa serikali, msemaji wa serikali Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, alisema kuwa serikali imeridhia kufanyika kwa uchunguzi huo ambapo familia itatoa wataalamu wa kufanya uchunguzi na serikali kutoa mwakilishi wake.

"Serikali imeruhusu uchunguzi huru ufanyike ambapo utahusisha daktari wao wa familia na sisi kwa upande wetu serikali tutatoa daktari pia," alisema Wasira.

Ndugu mwingine wa marehemu, Kefa Wangwe, aliutangazia umati wa waombolezaji waliojitokeza kwa ajili ya maziko ambayo yalipangwa kufanyika jana kijijini kwao kwamba yameahirishwa ili kuruhu uchunguzi wa sababu za kifo cha marehemu.

Kefa alisema familia yao imeamua kuwa Marehemu Chacha hatazikwa hadi hapo madaktari watakapo uchunguza mwili wake na kubaini kifo cha mwanasiasa huyo kimesababishwa na nini.

Keba alisema familia ya marehemu akiwamo kaka yake Prof. Wangwe, waliamua kuufunua jeneza na kudai kuwa kulikuwa na alama za kupigwa risasi shingoni iliyotokea mdomoni nyingine tumboni na kusababisha kifo chake.


Kefa ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa vipindi viwili hadi 2005 na kaka yao Prof. Wangwe, walisema mdogo wao hatazikwa kwanza hadi tume iundwe ikishirikisha familia ya marehemu, Serikali na madaktari bingwa ili kubaini kifo cha ndugu yao kwani kina utata. Mwili wa marehemu ulitarajiwa kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Mkoa Musoma ukisubiri kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Habari ambazo timu ya waandishi wetu walioko Tarime na Kijijini kwa Wangwe walizopata kutoka ndani ya familia zilisema kuwa uchunguzi wa mwili huo ulifanywa na Dk Turwa Mrimi ambaye alibainisha kuwa mwili wa marehemu ulikuwa ukionyesha kuwa alipigwa risasi mdomoni na kutokea nyuma ya shingo, pamoja na kuwa na jeraha liloonyesha kuchomwa na kitu chenye ncha kali pajani kulia.

Kutokana na hali hiyo, ndugu walilazimika kukaa kikao na kujadiliana hatma ya hali hiyo, huku wakifanya mawasiliano kuagiza daktari mwingine zaidi.

Diwani wa Kata ya Kemambo, Agustino Neto Sasi, alithibitisha kufanyika kwa kikao hicho na kusema "Siwezi kueleza kuhusu taarifa ya utafiti, ninachojua ni kweli daktari ameletwa na familia na mwili umefanyiwa uchunguzi sasa tungoje familia itatoa jibu."

Uchunguzi mpya unataraijiwa kufanywa na timu ya madaktari kutoka hopitali ya Dk. Wilfred Kisuka Machage wa jimbo la Kurya, Kenya.

Prof. Wangwe alisema kuwa Dk. Mrimi ambaye anadaiwa kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu jana hakuwa daktari bingwa anayehusikana na uchunguzi, lakini kutokana na kuibuka utata familia imeamua kumpata daktari mbigwa ambaye ni mtaalamu.

Kutokana na hali hiyo, ibada ya maziko ambayo ilikuwa ianze saa 5 asubuhi ilikwama hali ikizidi kuwa tete na kusababisha wananchi kukaa vikundi wakisubiria hadi pale walipotangaziwa kwamba imeamuliwa kuzuia maziko.

'Baadhi' ya viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, Manaibu Waziri Gaudensia Kabaka, Dk James Wanyancha na Naibu Waziri wa Miundombinu wa Kenya na ambaye pia ni mbunge wa Kurya, Willfred Machage, na wakuu wawili wa wilaya za Kurya Magharibi na Mashariki Getonga na Ama Shamba.


Wengine waliohudhulia ni wabunge Nimrodi Mkono, Zito Kabwe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia. Pia wabunge 20 ambao wamewakilisha Bunge.

Katika eneo la nyumbani ambako mwili ulikuwa umehifadhiwa, vurugu zilianza kuzuka huku vijana wakiwa na mabango ambao yanaonyesha kwamba hawaamini kwamba Wangwe amekufa kwa ajali. Mengi ya mabango hayo yalikuwa yakisema kwamba wanataka uchunguzi wa kina kuhusu kifo hicho.

Katika eneo hilo, baada ya kuwa na hisia za kifo hicho kimetokana kuuwawa kwa risasi, iliwalazimu baadhi ya viongozi wa Chadema, akiwamo Kabwe kupewa ulinzi mkali ambapo alikuwa analindwa na mabaunsa watatu.

Katika msiba huo kijijini Kemakorere ambako alizaliwa Wange, Zitto alikuwa na walinzi hao kila mara na kila alipokwenda ambao walikuwa wakimlinda na kumfuata.

Habari zilizopatikana zimeeleza kuwa kutokana na wasiwasi huo mara baada ya kufika Tarime, Zitto aliwasiliana na viongozi wa chama wilaya na Jeshi la Polisi ambapo walikaa kikao cha siri na maofisa wa polisi kuhusu suala la usalama wa viongozi.

Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Wilaya, Anderson Deogratias Chacha, alithibitisha kufika polisi, lakini alisema siyo kwa ajili ya maswala ya usalama wa Zitto wala Mbowe, bali ilikuwa ni kuwapelekea taarifa za hali ya ulinzi na jinsi walivyojipanga kama Chadema.

Alisema Chadema walipanga mkakati wa ulinzi kutokana na kubainika kuwa kuna kundi la watu wamepewa fedha kwa ajili ya kufanya vurugu. Hata hivyo, baada ya Mbowe kufika umati ulianza kusikika ukipiga kelele na kusema wanataka pia kumuua kwa vile Wangwe ameuawa na kudai Mbowe ni muhisika

Kutokana na kelele hizo, kuendelea vijana walizidi kurusha mawe na kuzuka vurugu kubwa hatua ambayo ililazimu polisi kuingia eneo hilo na kuwatawanya watu kwa lengo la kuimarisha ulinzi kwa viongozi wa chama na serikali waliokuwa huko.

Kundi kubwa la wananchi lilikuwa likipita sehemu mbalimbali huku likiimba kuwa Wangwe ni Mandela wao, wengine wakiimba, Barrack Obama
.

Bado nasubiri kwa hamu matokeo ya autopsy itayofanyika halafu nione polisi na serikali watayachukuliaje. Ni bahati kuwa merehemu alikuwa na kaka wenye akili ya kujua la kufanya wakati wa utata. Uzuri ni kuwa jeraha la risasi huwa linajulikana waziwazi kwa vile tissues za mweili zinaharibiiwa uniformly. Nadhani mtu kama Professor Wange ni hawezi kufikia conclusion ya namna hiyo bila kuwa ameridhika kuwa yale ni majeraha ya risasi kweli.

Ninachoona hapa ni kuwa hii independent autopsy itaonyesha chanzo cha kifo kama ni ajali au ni risasi. Ikionekana kuwa chanzo cha kifo siyo ajali, basi utatakiwa uchunguzi mzito wa kipolisi kubaini motive ya wauwajii, na kuwafikishe mbele ya sheria wale wote walioshiriki kwenye kupanga na/au kutekeleza mauaji yenyewe.
 
WANGWE AITISA MUSOMA NZIMA WALIOSEMA KUWA NI MZIGO NDANI YA CHAMA CHAO,MBONA WANGWE ANAPENDWA KULIKO MTU YEYOTE MUSOMA HATA WATU WALIOPOKEA MAITI YA MWALLIMU NYERERE HAWAKUFURIKA KAMA WANGWE.
TIZAMENI WENYE.
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/31/habari1.php

Hilo silishangai kwa WaTanzania kwani kila ukiwaibia na kuwafisidi halafu ukakutwa na maswaibu ndipo utawaona kama wanakupenda ,ila ukiwa ndani ya kashfa na matatizo basi hata kijijini kwako wanakulaani na kukuombea umauti tena wanakuswaga ile mbaya ,lakini siku serikali ikisema inakuondoa na kukuweka kando basi wale wale waliokuwa wanakuponda na kukuwekea ngumu ndio watakuwa wa kwanza kukuita shujaa,watakutandikia zulia jekundu watakupokea kwa vifijo na vigelegele huku matalumbeta yakitoa sauti mfano wa tembo aliekasilika ,kiasi hata Kikwete anashindwa kuwafahamu wananchi wa Tanzania ,chukulia Lowasa na Chenge baada ya kujiuzulu Kikwete na CCM walikuwa wawatimue kutoka kwenye Chama lakini walipotazama kijijini waliona hali nyengine watu wanapokewa kushinda Raisi , akaona bora ajinyamazie na kukaa kimya , wananchi wanashindwa kueleweka ,sasa umefika wakati mambo yatizamwe tu kwani hakijulikani nini cha kufanywa kila linalofanywa linaleta mgogoro.

Ukimuondoa fisadi kijijini wanampokea kwa shangwe inaonyesha vijijini kuna matatizo ya kuelewa kinachoendelea.
 
ndugu zangu; twendeni taratibu. Kuna nguvu zinazoipigania nchi yetu; zenye kutaka sehemu ya nchi yetu, zenye kutaka ubia wa aina fulani hivi. Nguvu hizi hasi zimebanwa mahali pabaya sana na ni imani yangu kuwa lolote wanalofany katika kujibu kubanwa kwao watahakikisha ni political.

Ndio maana tangu mwanzo binafsi siamini kama suala hili ni la vyama ila limefanywa ili liwe la vyama na matokeo yake the real culprits wapo wanatanua mahali fulani. Na hata hapa mjadala bado unazunguka kati ya Chadema na CCM na kwa kufanya hivyo tunapoteza muda kweli kufikiri nje ya box. Kuna majaribio ya kulazimisha watu kubakia ndani ya box hili la vyama lakini when everything is said and done, itakuwa ni ajali ya kawaida yenye mambo yasiyo ya kawaida; au ni ajali ya kupangwa na ambao wahusika wake wanaweza kuwa ni kama mhimili wa uovu na ndani yake wanaweza kuwemo wanasiasa, wafanyabiashara, n.k (the axis of evil).

Hebu leo kama tunaweza tufiikiri nje ya sanduku la vyama na tuone kama tunaweza kureason nani mwingine nje ya vyama hivi anaweza kunufaika zaidi na kifo cha Wangwe. Vinginevyo, tunawapa break ya kutosha tu kundi la watu fulani. Of course hii haina maana zile political angles zisiwe explored bali ziwekwe kwenye context yake.
 
Nje ya vyama, ndani ya vyama, katikati vya vyama, ni nani angetaka Wangwe afe?

Wale wanaotuongoza kwenye hisia za utata (sizikatai outright) ila wale wanaoona writtings on the wall ndio watujibu hilo. Nani angetaka kumuua Chacha ?
 
Nimechoshwa na hii tabia ya baadhi ya watu humu ndani kutaka kutumia CCM play book kwa kusema ya kuwa kifo cha Wangwe kinahusiana na mgogoro wa Chadema . Jamani migogoro hipo sehemu yoyote hata kwenye familia , lakini hii haitoshi kusema ya kuwa watu ndani ya Chadema wanahusika na hili !

Swali ninalojiuliza kama kweli mtu anata kumuua mtu mwingine , utasubiri mpaka ugombane naye ndiyo ufanye hivyo au ? Kama alivyosema Mheshimiwa ES , hili zoezi zima linaonekana limefanywa kwa utaalamu wa hali ya juu na kiasi fulani wameacha foot prints kidogo sana ambazo zinahitaji Forensic Expert kuzinga'mua .

Ni lazima tutambue ya kuwa TBC sio credible source kwani ni propaganda mashine ya CCM , kwa hiyo wanachojaribu sasa kufanyani kuset tone ya hii debate . Wazalendo kama tutakuwa sio waangalifu tutauingia huu mtego kichwa kichwa ...na huu ndio utakuwa mwisho wa kuzungumzia EPA , Richmond, Mikataba ya Madini , Kiwira...

Watu wa Morogoro wana msemo mzuri unaosema ....KALAGA BAO.
 
Now According to more dataz ni kwamba:-

2. Je CCM wanaweza kuwa na interest na kifo chake? Hapana, not CCM collectivelly as chama, kwa sababu sio siri ndani ya CCM nzima kuwa jimbo la Tarime ni la wapinzani, ni so bad kwamba CCM as chama inajua kuwa hata vyama vyote vya upinzani vikipigwa marufuku kugombea uchaguzi wa bunge kule, ikaachwa CCM peke yao kwenye ballot, bado wananchi wa Tarime, hawataipigia kura CCM, cha maana sana hawataenda kwenye kupiga kura,

CCM haijawahi kupoteza hata one minute kufikiria jimbo la Tarime, jimbo la Zitto, jimbo la Dr. Slaa na hata jimbo la Ndesamburo, haya ni kwa maneno ya baadhi ya viongozi wa CCM nilioongea nao leo, binafsi ninaiunga mkono hii theory 100%, kwamba CCM as a chama, haiwezi kuwa na interst na kifo cha Wangwe.

3. Chadema as chama, hapana, some individulas ndani ya Chadema may be, lakini kazi iliyofanyika kwenye ajali ni too professional kuwa imefanywa na individiduals wa ndani ya Chadema, hata kama wangekuwa na interest lakini wasingeweza kufanya ile kazi kwa ufundi kama ilivyofanyika,

Now who did it, jawabu so far ndio ninalikaribia kwa sababu japo sijawajua lakini my instinct inaniambia kuwa ni wale wale waliowahi kuhusika na ishu kama hii in the past, sio siri sasa kuwa Wangwe, alikuwa akitumiwa na mikono mizito kutoka ndani ya CCM, lakini sio chama kuleta mtafaruku ndani ya Chadema, hili nimelithibitisha leo,

Unasema CCM haiwezi ,huoni kama tatizo la Marehemu ndani ya Chama chake linaweza kutumiwa ili kuleta mtafaruku ndani ya Chama kwa Tanzania nzima, ikiwa marehemu aliondolewa au aliuliwa kiprofeshonal hii ni kusema kama wauaji hawakujulikana lawama itakuwemo ndani ya Chama Cha Chadema na kwa vile kulikuwa na msuguano viongozi wa juu watahusishwa moja kwa moja,kwamba ndio waliomuua ila hakuna ushahidi hivyo zitabaki chuki na Chama kitasambaratika kwa kupoteza imani.

CCM na serikali yake inaiona Chadema ni Mwiba kwani mambo yote yanayofichuliwa huanzia huko ndani mwa Chadema ,nini kifanywe ili kuivuruga Chadema..Chadema wana mgogoro,Chadema wanaelekea kuumaliza mgogoro wao ,ikiwa tutamkatisha Wangwe maisha yake na kupoteza ushahidi ,na kulisukumia jambo hili ndani ya Chadema kwa kutumia nyenzo zetu bila ya shaka viongozi wa juu wa Chadema watakuwa matatani na wanaweza na wao wakauliwa au kuondolewa kwenye shughuli za Chama au kufukuzwa,kutakuwa na mgogoro.

Sasa angalia habari za mwanzo za kwenye magazeti na redio za Serikali zilikuwa kila zinapotaja kifo cha Wangwe zilihusisha mgogoro na wakuu wa Chama,tazama harakat za kuukarabati mwili wa maremu na kupelekwa kwao kwa ajili ya tayari maziko ,sina uhakika lakini wengine mambo ya maziko hufanywa kijijini kwao haya nasikia yalishughulikiwa na bunge haraka haraka ,mwili ulikwenda huko kuzikwa tu kama alivyofanyiwa Dr.Omar Ali Juma
Ila wandugu wa huko naona machale yaliwacheza na kutaka kuupekuwa mwili.

Walichokiona walikuwa na wasiwasi nacho kuwa moja ni risasi na jenginne kitu chenye ncha kali hawakuridhika wakamwita daktari wa familia bila ya kusita akasema ni majeraha ya risasi ,wakamweka kando na kutafuta mtaalamu wa mambo hayo ambe wamemuagizia kutoka mkoa jirani Kurya wa Kenya unaoonyesha kuna mahusiani ya kikabila ,ndipo tulipofikia tunasubiri na yeye atoe mpya au kusema aliosema daktari wa familia hayana kosa.

Sasa nikirudi kuishupalia CCM na Serikali yake ambao walikwisha fanya uchunguzi na kumfunga maiti tayari kwa maziko ,wakubwa kama itabainika jamaa alikumtwa risasi basi moja kwa moja CCM na serikali zinahusika na ni kamtindo ambako kipo ndani ya utawala wa Tanzania lakini naona kanaribia kuumbuliwa.

Serikali itahusika kwa sababu wachunguzi wake walificha kusema kuwa marehemu alikutwa na jeraha la risasi sio moja inavyosemekana ni mbili ,ole wao ikiwa risasi hizo bado zimo mwilini,wachunguzi wa serikali itabidi wajitahidi wawezavyo la si hivyo inabidi waishie jela ni kuisababishia Serikali aibu na matatizo kama haya tunayoyafikiria kuwa imehusika.

Kuhusika kwa CCM ni kuzusha mgogoro ndani ya Chadema kwa kumuondoa Chaha wangwe na natumai poit hiyo inaweza kuplay kutokana na msimamo wa Chadema kuisakama Serikali na watendanji wake.CCM hawahitaji kushinda Tarime na hilo siwezi kulipa kipau mbele ila CCM inaweza kabisa kufanya kwa kuhatarisha umoja wa Chadema , Huwezi kujua ni mtazamo wangu tu.
 
Mimi nadhani, MWkjj ametoa changamoto nzuri. We have to break it down simply.
Ndani ya chama:
Nje ya Chama:
Sasa tukianza kulist kwanza connections instead of names pia tutafika mbali zaidi.

Kwa mfano:
Ndani ya chama: - leadership strife - possible culprits: uongozi wa Chadema, motive: threat ya Wangwe kuchukua uongozi etc
Kama tutaweza kuweka vitu hapa logically tutafika mbali.

Mimi binafsi naamini kuwa hii link ya chama is very weak. Ile theory ya Mwkjj ya Axis of Evil makes more sense as this is a rogue ragtag group of people with similar interest who engineered, that is why it was kept so tight and controlled.
I think that we have to look beyond Wangwe as MP and look more closely :
- his business and life outside politics (when not in Bunge what was he doing to earn a living?)
- his role within the party including the alleged information collector role. From what I understand he was collecting information for Chadema about the dirty deals of CCM including EPA, Kiwira etc. Was there a personal fallout with other Chadema information collectors, was he negotiating with people he had spied on?
- personal life - is there a jealous husband, jilted wife, angry lover?

This the stretch of my brain that I could come up with spontaneously, I welcome others to think and put aside poltiical affiliation, loyalty etc.
 
Nje ya vyama, ndani ya vyama, katikati vya vyama, ni nani angetaka Wangwe afe?

Wale wanaotuongoza kwenye hisia za utata (sizikatai outright) ila wale wanaoona writtings on the wall ndio watujibu hilo. Nani angetaka kumuua Chacha ?
Historia inaonyesha kuna hisia za kuuliwa viongozi hapa Tanzania ni si jambo geni hivi hujasikia msamiati kumkolimba ? Mtu akisikia tu mbunge fulani amekufa ghafla utasikia jirani akijibu wameshamkolimba ! Nini maana yake ?
Kuondoshwa kwa Wangwe ni kutaka kuisambaratisha Chadema ,lakini picha inaonyesha matatizo ndio yameanza kutimuliwa na kurushiwa mawe akina Zitto na wenziwe wa Chadema huenda ikawa ni mafanikio ya kumuondoa Chacha kama ni mpango ila kuna ushahidi ambao unasemekana ulikuwa na ushirika wa upande wa Chadema na CCM au serikali jamaa alisafiri Libya ,alisafiri Masri,alisafiri Swiss huwezi kujua kama ni profesion wa kupindua magari na yeye kutoka salama ,wapo watu aina hiyo.Tungojee dakitari kutoka wilayani Kurya nchini Kenya atupe picha kamili.
 
Unasema CCM haiwezi ,huoni kama tatizo la Marehemu ndani ya Chama chake linaweza kutumiwa ili kuleta mtafaruku ndani ya Chama kwa Tanzania nzima, ikiwa marehemu aliondolewa au aliuliwa kiprofeshonal hii ni kusema kama wauaji hawakujulikana lawama itakuwemo ndani ya Chama Cha Chadema na kwa vile kulikuwa na msuguano viongozi wa juu watahusishwa moja kwa moja,kwamba ndio waliomuua ila hakuna ushahidi hivyo zitabaki chuki na Chama kitasambaratika kwa kupoteza imani.

CCM na serikali yake inaiona Chadema ni Mwiba kwani mambo yote yanayofichuliwa huanzia huko ndani mwa Chadema ,nini kifanywe ili kuivuruga Chadema..Chadema wana mgogoro,Chadema wanaelekea kuumaliza mgogoro wao ,ikiwa tutamkatisha Wangwe maisha yake na kupoteza ushahidi ,na kulisukumia jambo hili ndani ya Chadema kwa kutumia nyenzo zetu bila ya shaka viongozi wa juu wa Chadema watakuwa matatani na wanaweza na wao wakauliwa au kuondolewa kwenye shughuli za Chama au kufukuzwa,kutakuwa na mgogoro.

Sasa angalia habari za mwanzo za kwenye magazeti na redio za Serikali zilikuwa kila zinapotaja kifo cha Wangwe zilihusisha mgogoro na wakuu wa Chama,tazama harakat za kuukarabati mwili wa maremu na kupelekwa kwao kwa ajili ya tayari maziko ,sina uhakika lakini wengine mambo ya maziko hufanywa kijijini kwao haya nasikia yalishughulikiwa na bunge haraka haraka ,mwili ulikwenda huko kuzikwa tu kama alivyofanyiwa Dr.Omar Ali Juma
Ila wandugu wa huko naona machale yaliwacheza na kutaka kuupekuwa mwili.

Walichokiona walikuwa na wasiwasi nacho kuwa moja ni risasi na jenginne kitu chenye ncha kali hawakuridhika wakamwita daktari wa familia bila ya kusita akasema ni majeraha ya risasi ,wakamweka kando na kutafuta mtaalamu wa mambo hayo ambe wamemuagizia kutoka mkoa jirani Kurya wa Kenya unaoonyesha kuna mahusiani ya kikabila ,ndipo tulipofikia tunasubiri na yeye atoe mpya au kusema aliosema daktari wa familia hayana kosa.

Sasa nikirudi kuishupalia CCM na Serikali yake ambao walikwisha fanya uchunguzi na kumfunga maiti tayari kwa maziko ,wakubwa kama itabainika jamaa alikumtwa risasi basi moja kwa moja CCM na serikali zinahusika na ni kamtindo ambako kipo ndani ya utawala wa Tanzania lakini naona kanaribia kuumbuliwa.

Serikali itahusika kwa sababu wachunguzi wake walificha kusema kuwa marehemu alikutwa na jeraha la risasi sio moja inavyosemekana ni mbili ,ole wao ikiwa risasi hizo bado zimo mwilini,wachunguzi wa serikali itabidi wajitahidi wawezavyo la si hivyo inabidi waishie jela ni kuisababishia Serikali aibu na matatizo kama haya tunayoyafikiria kuwa imehusika.

Kuhusika kwa CCM ni kuzusha mgogoro ndani ya Chadema kwa kumuondoa Chaha wangwe na natumai poit hiyo inaweza kuplay kutokana na msimamo wa Chadema kuisakama Serikali na watendanji wake.CCM hawahitaji kushinda Tarime na hilo siwezi kulipa kipau mbele ila CCM inaweza kabisa kufanya kwa kuhatarisha umoja wa Chadema , Huwezi kujua ni mtazamo wangu tu.
I couldn't agree with you more ...yaani kama ulikuwa unausoma ubongo wangu . Swali ninalouliza ni vipi kama uchunguzi wa Daktari utabaini ya kuwa akikuwa kifo cha kawaida ?
 
Kama kuna risasi polisi wetu itabidi watupe majibu ,na wao watakuwa wanajua dili kamili ni nani na nani walihusika na hivyo walitumiliwa kuficha ukweli wa matundu ya risasi ,tusubiri tume watakayoundiwa.Ndivyo tulivyozoea lakini hawa itabidi wahukumiwe azabu kali sana .
 
I couldn't agree with you more ...yaani kama ulikuwa unausoma ubongo wangu . Swali ninalouliza ni vipi kama uchunguzi wa Daktari utabaini ya kuwa akikuwa kifo cha kawaida ?

Dakitari wa mwanzo ameshasema risasi usitegemee wa pili kusema ni kifo cha kawaida ,huyo wa pili labda ameitwa kuja kuchokoa na kuitafuta risasi yenyewe ,halafu hisia za kumwita daktari wa mwanzo kwa wanafamilia ni baada ya kuona kuna alama ya tundu la risasi ,wakuria wengi wanauzoefu wa kujua tundu la risasi,mambu ya madaktari ni kuanda ushahidi ndio ukaona hata serikali imepewa nafasi ya kuweka daktari wake ili ushahidi uzidi kunoga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom