Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Wakuu wa JF,
Nilikuwa sijachangia ktk mada hii na hakika muda umepita sijafuatilia humu ndani kwa sababu ambazo binafsi nilishindwa kuamini kila lililoandikwa humu. Niliacha kusoma ili nipate muda wa kufuatilia.

Lakini leo baada ya kuongea na mtu wangu Bongo, kuna habari hizi nimezipokea ambazo kwa kiasi kikubwa naanza kuziamini.

Inasemekana Wangwe amefanyiwa kile kilichomkuta Mwaikambo.. Yaani kauawa sehemu nyingine ya pale lilipokutwa gari ilikuwa staging tu...

Huyu kijana ambaye ni rafiki ya marehemu anafahamu mengi zaidi ya hayo kwa sababu kuna wakati mtoto wa marehemu alipiga simu akaipokea yeye na kudai kwamba wanarudi mjini Dodoma kwa sababu wameharibikiwa...Kijana amedai alikuwemo ndani ya gari wakati wote!..

Tatizo linakuja ni kwamba haiwezekani huyu kijana kupokea simu ya Marehemu kama angekuwa hai, hakuna sababu na hata hivyo angesema subiri na kumpa marehemu aongee na mwanaye - Bila shaka wakati huo Wangwe tayari alikwisha kufa (uawa)...

Habari ya msisitizo ni kwamba gari lile ktk hali iliytokuwepo haiwezekani mtu atoke hana jeraha unless mtu huyo alitupwa nje ya gari hilo kabla halijabondeka...

Haya ni baadhi ya maswali machache ambayo hadi sasa hivi hayana majibu!..

Baada ya kupitia posts karibu zote naamimi kuwa kama kweli kuna nia njema ya kutafuta ukweli basi, utapatikana. Mtiririko wote wa tukio mpaka sasa uko wazi na kama polisi wetu watakuwa makini, hawatashindwa hata kidogo kufikia ukweli. Na hili linatakiwa lifanyike haraka sana ili kutozipa nafasi umbeya na "spins" nyingi tu ambazo kwa hakika hazisaidii.

Binafsi nalaani kitendo cha TBC, chombo ambacho ningetumaini kutoa taarifa rasmi ama za upelelezi ama za serikali kutumiwa na kikundi kidogo kwa maslahi binafsi. Hii isipewe nafasi na ikemewe kwa nguvu na wote wapenda amani. Mungu ibariki Tanzania.
 
Now According to more dataz ni kwamba:-

ninaamini kwa 100%, kuwa kuna-assignment aliyopewa siku hizi za mwishoni na handlers wake, lakini akwa na kigugumizi kuipokea kwa mikono miwili kama ambavyo amekuwa akipokea zingine, yaani marehemu Wangwe, sababu huenda alishashituka kuwa sio nia njema, au hakupewa malipo ya assignment za mwanzoni, haiwezekani yeye binafsi aamue kufanya safari ile tena kwa saa alizo ondoka bila mtu yoyote muhimu zaidi ya Spika tu kujua,

FMES,
As a Jasusi I am interested in the handlers. Hatutaweza kufumbua kitendawili hichi mpaka huyo handlers afahamike. Na asipofahamika Tanzania itaendelea kuburuzwa na haya mazingaombwe, kwa sababu hii si mara ya kwanza kwa ajali ya gari kutokea katika mazingira ya utatanishi, na haitakuwa ya mwisho.
 
Prof. Kichuguu,

Wangwe kafa kwa ajali. Familia wameamua la maana kufanya uchunguzi wao binafsi. Haya mambo ya hearsay ni mabaya popote pale duniani. Wanasiasa wanapohusika inakuwa mbaya hata zaidi maana wanasiasa muda wote wana interests zao binafsi.

Njia pekee ya kuondoa rumours kama hizi ni ukweli na uwazi kwa asilimia 100. Bahati mbaya cultures zetu zimejaa kuficha ficha na matokeo majungu yanakuwa mengi mno.

Heri yetu wengine ambao hatuogopi kifo, "I am not afraid of death but in no hurry to die".

Nadhani hilo la kufanyika uchunguzi binafsi ndilo jambo la maana zaidi kufanyika kwa sasa hivi. Binafsi nilianza kwa kuamini kuwa Marehemu kafa kwa ajali ya gari kama zilizovyo ajali nyingine ambazo ni za kawaida sana nchini kwetu kutokana na hali za barabarab zetu, magari yetu na utumiaji wetu wa barabara: kuna post yangu moja huko nyuma inaongea hivyo. Lakini kadri muda unavyokwenda na ushahidi kujengeka kuhusu mazinigira ya ajali hiyo, nimefikia kuamini kuwa kifo kile hakikusababishwa na ajali ile. Endapouchunguzi utafanyika na tukaambiwa kuwa marejemu alifariki kwa ajali ile, basi nitaondoa wasiwasi wangu kuhusu assassination plot.

Hata hivyo kukamilika kwa uchunguzi wa aina hii kunahitaji pia wataalam ambo huenda hatunao. Utaalamu wa accident reconstruction na injury biomechanics kuonyesha kuwa maumivu aliyopata marehemu yalitokana na accident ile wala siyo accident nyingineyo unahitaji sana katika swala hili.
 
Mkuu Mtanzania, yaani kweli unaamini kwamba yule Deus Mallya angeweza kutoka kama alivyo, kama kweli alikuwemo ndani ya lile gari wakati "linapata ajali"??!!

Hebu angalia picha ya lile gari tena; please!
 
makabrasha ya malipo ya EPA DR SLAA aliyapata wapi? maana hayakuibiwa BOAT yale original yalibaki kulekule..

Mikataba mibovu ya madini ZITO aliipata wapi? maana original zenyewe hazikuibiwa.

Haya sio yakuanza nayo kabisa ,lazime shilingi uitazame pande zote.

What is your message in this???
 
Jamani, kuna advantage moja ya hii thread ni kuwa watu hawasubiri tena magazeti na radio kuhusu taarifa zao; Saa moja kuanzia sasa nitawawekea taarifa ya habari iliyotangazwa na TBC saa mbili za usiku za Tanzania na mtaona kuwa kama watu wanasikiliza taarifa ya habari tu basi wanaweza kupata habari ya ajabu sana kama walivyofanyiwa leo.

Hindsight is the best foresight.........that shall be proven after the post-mortem!!
The truth of the matter is, does JF, KLHnews or any other 'independent' news source have the same outreach as say TBC?

What people have in mind (on this board), shall not go away. People need some time to chill and let things sink in. At the moment there are so many theories....this thread has become an ideal place to plant propaganda.

Anyways, let me step back and watch some serious spinning goin on!
 
Mkuu Mtanzania, yaani kweli unaamini kwamba yule Deus Mallya angeweza kutoka kama alivyo, kama kweli alikuwemo ndani ya lile gari wakati "linapata ajali"??!!

Hebu angalia picha ya lile gari tena; please!

Mkuu,

Nimeona hiyo picha na ninaziona picha nyingi sana hata huku nje ambazo gari linaumia kuliko hata hilo la Wangwe na watu wanatoka salama kabisa huku wengine wanakufa.

Gari inategemea ulikaa wapi, ulifunga mkanda na mambo mengine.

Huyo kijana atakuwa mjinga sana kuhusika kumwua Wangwe na kisha yeye kubaki hapo.

Wacha tusubiri uchunguzi wa familia. Uzuri familia yao ina mtu kama prof. Wangwe ambaye naamini atawaongoza familia vizuri kwenye kutafuta ukweli.
 
Nadhani hilo la kufanyika uchunguzi binafsi ndilo jambo la maana zaidi kufanyika kwa sasa hivi. Binafsi nilianza kwa kuamini kuwa Marehemu kafa kwa ajali ya gari kama zilizovyo ajali nyingine ambazo ni za kawaida sana nchini kwetu kutokana na hali za barabarab zetu, magari yetu na utumiaji wetu wa barabara: kuna post yangu moja huko nyuma inaongea hivyo. Lakini kadri muda unavyokwenda na ushahidi kujengeka kuhusu mazinigira ya ajali hiyo, nimefikia kuamini kuwa kifo kile hakikusababishwa na ajali ile. Endapouchunguzi utafanyika na tukaambiwa kuwa marejemu alifariki kwa ajali ile, basi nitaondoa wasiwasi wangu kuhusu assassination plot.

Hata hivyo kukamilika kwa uchunguzi wa aina hii kunahitaji pia wataalam ambo huenda hatunao. Utaalamu wa accident reconstruction na injury biomechanics kuonyesha kuwa maumivu aliyopata marehemu yalitokana na accident ile wala siyo accident nyingineyo unahitaji sana katika swala hili.

Prof. Kichuguu,

Polisi wa kuchunguza tunao, japo sio kama hawa wenzetu huku nje. Ukisoma ile case ya polisi walioua raia wema Dar, utapata kujua kama tuna wataalamu wa kutosha wakiamua kufanya kazi.

Tatizo la TZ ni kwamba inategemea serikali inataka wafanye uchunguzi wa kweli au ule wa kibabaishaji.
 
Mtanzania,
Mkuu ni bora ukae kimyaaa kuliko kusema vitu kama vile sisi wengine hatupo majuu.
Katika hali hiyo ya gari mkuu huku watu huja na vifaa vya kumwokoa mtu toka ndani ya gari tena hulikatakata kupata kumwondoa mtu, lakini huyu kijana inasemekana kutokana na madai yake alifungua mlango akatoka nje..mlango upi hapo mkuu wa kufunguliwa na mtu aliyekuwa ndani ya gari hilo..
Kisha
 
Kuna watu wanasema ati kuna propaganda hapa , kama ni kweli wamekuja kutafuta nini? Asali?

Back to the issue, hivi taarifa ya uchunguzi mpya ikitofautiana na ya awali kuna atakayesalimika huko polisi? Maana yaliyotokea Bungeni yanaeleweka, What type of a nation tutakuwa ambao vyombo vyetu wenyewe vya kutulinda havifanyi kazi hiyo? Tanzania inaelekea wapi? Kwenye maisha bora ya kukolimbana?
 
Mtanzania,
Mkuu ni bora ukae kimyaaa kuliko kusema vitu kama vile sisi wengine hatupo majuu.
Katika hali hiyo ya gari mkuu huku watu huja na vifaa vya kumwokoa mtu toka ndani ya gari tena hulikatakata kupata kumwondoa mtu, lakini huyu kijana inasemekana kutokana na madai yake alifungua mlango akatoka nje..mlango upi hapo mkuu wa kufunguliwa na mtu aliyekuwa ndani ya gari hilo..
Kisha

Mkandara,

kama wewe hujaona haina maana na wengine hawajaona. Nimeandika mimi nimeona unless uniambie ni mwongo huna sababu nyingine yoyote ya ku question nilichoandika.

Pili gari lililopata ajali kukatwa huku ni kwasababu nyingi, hawawezi kumwondoa mgonjwa kwenye gari kama tunavyofanya sisi nyumbani. I hope umepitia mafunzo ya first aid, inatakiwa mgonjwa usimwondoe wala kumsogeza toka alipo ndani ya gari ili usije ukamletea madhara zaidi mpaka baada ya daktari ku assess hali yake, hivyo hukata gari ili kuwe na nafasi ya kumhudumia mgonjwa na kisha kumtoa.
 
Huyu kijana alikuwa dereva wakati wa safari hiyo ya kwenda Dar, ila baada ya kupata ajari anajaribu kukutaa kwamba hakuwa dereva inawezekana hana leseni ya kuendeshea kama ilivyo kawaida ya Bongo bora liende. Kijana Mallya pia inaonekana ana ujuzi wa kutengeneza magari (fundi magari wa chini ya miti) kwani alitoka gereji na gari hilo hilo kabla ya safari. Hicho pia kilimfanya Chacha kumchukua kijana huyo ili gari likileta matatizo safarini basi Mallya alishughulikie.

Vyama vya siasa havija husika kabisa na kifo hiki.
 
Tarime wazuia maziko ya Wangwe (Majira)

*Mbowe aponea tundu la sindano kuuawa na wananchi
*Wamkabili kwa mapanga, mishale, mikuki na marungu
*Familia sasa yaita mtaalamu wake kuchunguza maiti

George John, Tarime na Reuben Kagaruki, Dar

MWENYEKITI wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, amenusurika kauawa kwa mapanga na mishale, baada ya kuwasili katika kijiji cha Kemakorere, kuhudhuria maziko ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wake na Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe.

Sakata hilo lilianza kujitokeza jana saa nane mchana baada ya Bw. Mbowe kuwasili kijijini hapo akifuatana na viongozi wengine wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Bw. Augustino Mrema (TLP), Bw. Joseph Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Bw. Bob Makani Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA.

Baada ya kuwasili kwa viongozi hao, kundi kubwa la watu hasa vijana walianza kumzonga Bw. Mbowe kwa kumwonesha mabango mbalimbali kuhusu kifo cha Bw. Wangwe wakisema hakitokani na mapenzi ya Mungu bali ameuawa.

Baadhi ya mabango hayo yalisomeka ifuatavyo: 'Tarime bila Wangwe hakuna amani'; 'Hii ni ajali au risasi?'; 'Viongozi bora hufa kwa ajali na risasi, viongozi wasio waadilifu hufa kwa BP'na 'Hadi kieleweke CCM hawana chao, tutakufa tukiilalamikia Nyamongo'.

Mengine yalisema: 'CCM chunguza Richmond na vijisenti, hatutampata kama Wangwe';'Tutakumbuka msimamo, utetezi, ujasiri na hoja zako' na 'Nyota ya Tarime imezimika meseji sent.'

Kutokana na hali hiyo, watu wa usalama wakiongozwa na askari Polisi wa kawaida na wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliwazuia wananchi hao kumzonga kiongozi huyo, lakini hawakufanikiwa kirahisi na hivyo kumlazimisha kuingia uani ambako shughuli za maandalizi ya maziko hayo zilikuwa zikifanyika.

Hatua hiyo ilibadilisha kabisa mazingira ya msiba huo, ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wabunge na wanasiasa, vingozi wawakilishi kutoka Kenya na maelfu ya wananchi.

Hali hiyo ya kutisha ya baadhi ya wananchi kubeba mapanga, mikuki, sime na fimbo huku baadhi yao wakiwa wameziweka hadharani na wengine katika makoti na kujificha migombani, ilimfanya kiongozi wa ukoo huo, Profesa Samwel Wangwe, kuwaeleza baadhi ya viongozi msimamo wa ukoo kabla ya kutangazwa hadharani.

Baada ya maelezo hayo ambayo yalimhusisha pia Mkuu wa Mkoa, Luteni Kanali mstaafu Issa Machibya, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Bw. Liberatus Barlow, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Zitto Kabwe na viongozi wengine wa ukoo, iliwabidi kuingia ndani kwa dakika 10 kufanya mjadala wa kuzika au la.

Baada ya muda huo, viongozi hao walitoka nje na Profesa Wangwe kupanda jukwaani na kutoa matangazo ambayo muda wote yalikuwa hayasikiki kutokana na kelele za waombolezaji, wakidai hawamtaki Mbowe bali wanataka Mbunge wao.

Hata hivyo, Bw. Kabwe alionekana kuwavuta wananchi hao kwa kusema maneno ya kumpamba marehemu, kuwa alikuwa kiongozi aliyependa kutetea wanyonge, hasa wapiga kura wake, hivyo kulazimika kunyamaza na kusikiliza kilichokuwa kikielezwa na msemaji huyo wa familia.

Katika kauli hiyo ya ukoo, Profesa Wangwe alisema:
"Sisi kama ukoo baada ya kupokea mwili wa marehemu na kuufikisha hapa, maneno mengi yamesemwa na ili kuondoa maneno hayo, tumeona ni vizuri tukachunguza mwili wa marehemu kwa kutumia mtaalamu wetu ambaye atawasili wakati wowote kuanzia sasa ... naomba sasa tuwe watulivu wakati tukisubiri hatua hiyo na mwili leo hauzikwi,” alisema Profesa Wangwe na kushangiliwa.

Kauli hiyo pamoja ya kuonesha imani kwa wananchi, lakini bado wangine walianza kutoa maneno yaliyolenga kwa Mbowe kuwa "tunataka Mbunge wetu si Mbowe," hali hiyo ilimfanya Mkuu wa Mkoa kusimama na kuomba amani.

Hata hivyo, kauli hizo hazikueleweka kwa wananchi hao hasa vijana, hivyo kumlazimu Mkuu wa Mkoa kuita polisi na kumsindikiza Bw. Mbowe katika gari lake, ambapo pamoja na ulinzi huo mkali, bado wananchi hao walimfuata hadi alipoingia ndani ya gari na kusindikizwa kwa ulinzi mkali kuelekea Tarime na hatimaye Musoma.

Pamoja na Bw. Mbowe, viongozi wengine waliohudhuria msiba huo wakiwamo wa Kenya, kila mmoja aliondoka kivyake wakihaha kutafuta magari ya kuwavusha ili kuepuka kipigo hicho kilichokuwa kikitangazwa na wananchi.

Kiongozi wa wabunge 20 waliotumwa kuwakilisha Bunge, Bw. William Shelukindo, akielezea hali hiyo alisema katika historia hajawahi kuona kitendo kama hicho lakini ilionesha jinsi wananchi hao walivyompenda Mbunge wao.

“Imesikitisha kweli imenifanya kutosoma salamu za Spika wa Bunge hata kutoa ubani wa Bunge tumekimbia kuepuka kufa pale...sasa vitu hivi vitaandaliwa utaratibu wake, lakini nawaomba wananchi watulie wamzike mbunge wao,” alisema Bw. Shelukindo.

Kwa upande wake, Waziri aliyewakilisha Serikali Bw. Steven Wassira, alisema kitendo hicho kimewasikitisha, lakini alisema hakuna njia ya kupata ukweli wa kifo cha Mbunge huyo hivyo ni vema familia kama ilivyoamua, kufanya uchunguzi huo upya katika kujiridhisha.

Bw. Wassira aliwataka wananchi wa jamii ya Tarime kuamini kuwa Bw. Wangwe amekufa na hakuna siasa kwenye jambo hilo.

"Sisi hatukuja hapa kufanya siasa , Rais (Jakaya Kikwete) alipoenda kutoa heshima hakuwa anafanya siasa, tumekuja kushirikiana na familia kufanikisha mazishi," alisisitiza Bw. Bw. Wassira na kuongeza;

"Sisi hatuna mgogoro, kama serikali tunakubaliana nao (wanafamilia) na tunaafiki uamuzi huo kwa heshima ya marehemu na familia." Bw. Wassira alisema tukio hilo ni kubwa na ni la majonzi na yanakuwa makubwa zaidi kutokana na kifo chake kuwa cha ghafla.

Alisema kabla ya kifo chake alizungumza na Bw. Wangwe Bungeni jioni akiwa mzima lakini walivyopata taarifa za kifo chake ilishangaza sana. Alisema baada ya kupata taarifa za kifo chake alikuwa wa kwanza kumjulisha kaka yake Profesa Wangwe.

Aliwataka wananchi wa Tarime kuwa wavumilivu kwani tukio hilo sio la kwanza kuwatokea na kutolea mfano kifo cha Baba wa Taifa, Marehemu Julius Nyerere.

Awali, baada ya Profesa Wangwe kutoa kauli hiyo, Bw. Kabwe alisema watahakikisha uchunguzi unafanyika na kutangaza hadharani matokeo yake na kusema tayari Polisi wamemkamata mmoja wa abiria waliokuwa wakisafiri na Mbunge huyo siku ya ajali.

"Kama kila kitu kitakwenda sawa tunatarajia kesho (leo) uchunguzi utakuwa umekamilika," alisisitiza. Alipoulizwa kama vurugu zilizojitokeza jana hazitaweza kujirudia leo Profesa Wangwe alijibu: "Mimi na wewe hatukujua kama haya (vurugu) yatatokea siwezi kusema kesho itakuwaje."

Shughuli za ujenzi wa kaburi hadi hatua hiyo inafikiwa, zilikuwa zimekamilika.
 
KUTOKA MAGAZETI YETU:

Alikufa akienda Dar kuwashitaki Mbowe na Slaa

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, aliyekufa njiani akienda Dar es Salaam Jumatatu iliyopita, pamoja na mambo mengine alikuwa amepanga kufungua kesi dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, imefahamika.

Uchunguzi wa gazeti hili, umegundua kuwa mbali na kuhudhuria maziko ya Mbunge wa Kwanza wa Tarime, marehemu Bhoke Munanka, alipanga pia kufungua kesi ya kupinga kusimamishwa umakamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Baada ya kufungua kesi hiyo, ambayo pia ingemhusisha Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa na Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA, alikuwa amepanga pia kuzungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

Kesi hiyo ingefunguliwa kwa niaba yake na kampuni ya uwakili ya Kakamba & Partners Advocates ya Dar es Salaam, kuitaka Mahakama Kuu ya Tanzania, ibatilishe uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu ya CHADEMA katika kikao chake cha Juni 28 mwaka huu.

Katika malalamiko yake, Bw. Wangwe angelalamikia uhalali wa kikao hicho, njama zilizotumiwa na wajumbe kumsimamisha na uvunjifu wa sheria uliofanywa na wajumbe wa Kamati hiyo.

Hatimaye marehemu Wangwe angeitaka Mahakama imrejeshe katika nafasi yake ya umakamu Mwenyekiti na kuizuia kamati hiyo kumsimamisha au kumfukuza uanachama wa CHADEMA na kulipa gharama za kesi na chochote ambacho Mahakama ingeona kinafaa.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, marehemu Wangwe alikuwa amepanga kuzungumzia matumizi ya ruzuku ya sh. milioni 66 za kila mwezi, madeni ya uchaguzi ambayo Bw. Mbowe anakidai chama zaidi ya sh. milioni 200.

Ajenda nyingine ni uteuzi wa wabunge wa viti maalumu na alichodai kuwa ni utendaji wa kibabe katika chama.
 
As a Jasusi I am interested in the handlers. Hatutaweza kufumbua kitendawili hichi mpaka huyo handlers afahamike. Na asipofahamika Tanzania itaendelea kuburuzwa na haya mazingaombwe, kwa sababu hii si mara ya kwanza kwa ajali ya gari kutokea katika mazingira ya utatanishi, na haitakuwa ya mwisho.

Hakuna haraka mkuu, tumesema kuwa hakuna jiwe litaachwa un-turned, yote yatawekwa hapa wazii, exactly nani aliyehusika na sababu, kwa sababu haiwezekani damu za Wangwe zikutwe kwenye kiti cha nyuma ya gari, wakati yeye alikuwa amekaa mbele,

Na haiwezekani damu zitoke kwa nyuma ya mwili wake, na mbele kusiwe na hata tone, something is not right, lakini yote tutayaweka wazi hapa hapa, tunayakaribia.
 
KUTOKA MAGAZETI YETU:

Mnyika: Sina la kusema kuhusu kifo cha Wangwe

Na Said Mwishehe

KAIMU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. John Mnyika, amesema kwa sasa hawezi kuzungumza lolote kuhusiana na kifo cha Bw. Wangwe.

Bw. Mnyika alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam, wakati waandishi wa habari walipofika ofisi za CHADEMA wakimtaka kutoa ufafanuzi kuhusiana na maswali mengi yanayoulizwa na wananchi kuhusu utata wa kifo cha marehemu Wangwe.

Alisema uongozi wa CHADEMA tayari umekabidhi barua kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema wakimtaka kuchunguzwa kwa ajali hiyo ya gari iliyosababisha kifo cha mbunge wao haraka ili ukweli uweze kujulikana.

"Kwa utaratibu wa kiafrika na hasa Tanzania, huwezi kuwa na mijadala wakati leo (jana) tupo katika harakati za kumzika mwenzetu, sitaki kusema lolote na nitakuwa tayari kuzungumzia mambo ya mazishi tu ambapo tayari viongozi wangu wameondoka Dar es Salaam kwenda kuzika Tarime kwa ndege ya kukodi," alisema Bw. Mnyika.

Alisisitiza kuwa kila kitu ambacho CHADEMA inaweza kuzungumza kuhusiana na tukio hilo kipo kwenye maandishi ya barua waliyomwandikia IGP Mwema na yeye yupo ofisini kwa ajili ya kutoa taarifa zinazohusiana na mazishi tu.

Akiwataja baadhi ya viongozi waliokwenda katika mazishi hayo jana ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia na Mwenyekiti wa TLP Bw. Augustino Mrema.
 
*Mbowe aponea tundu la sindano kuuawa na wananchi
*Wamkabili kwa mapanga, mishale, mikuki na marungu

*Familia sasa yaita mtaalamu wake kuchunguza maiti

George John, Tarime na Reuben Kagaruki, Dar

MWENYEKITI wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, amenusurika kauawa kwa mapanga na mishale, baada ya kuwasili katika kijiji cha Kemakorere, kuhudhuria maziko ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wake na Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe.

Sakata hilo lilianza kujitokeza jana saa nane mchana baada ya Bw. Mbowe kuwasili kijijini hapo akifuatana na viongozi wengine wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Bw. Augustino Mrema (TLP), Bw. Joseph Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Bw. Bob Makani Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA.

Baada ya kuwasili kwa viongozi hao, kundi kubwa la watu hasa vijana walianza kumzonga Bw. Mbowe kwa kumwonesha mabango mbalimbali kuhusu kifo cha Bw. Wangwe wakisema hakitokani na mapenzi ya Mungu bali ameuawa.

..................

Baada ya muda huo, viongozi hao walitoka nje na Profesa Wangwe kupanda jukwaani na kutoa matangazo ambayo muda wote yalikuwa hayasikiki kutokana na kelele za waombolezaji, wakidai hawamtaki Mbowe bali wanataka Mbunge wao.

...................

Kauli hiyo pamoja ya kuonesha imani kwa wananchi, lakini bado wangine walianza kutoa maneno yaliyolenga kwa Mbowe kuwa "tunataka Mbunge wetu si Mbowe," hali hiyo ilimfanya Mkuu wa Mkoa kusimama na kuomba amani.

Hata hivyo, kauli hizo hazikueleweka kwa wananchi hao hasa vijana, hivyo kumlazimu Mkuu wa Mkoa kuita polisi na kumsindikiza Bw. Mbowe katika gari lake, ambapo pamoja na ulinzi huo mkali, bado wananchi hao walimfuata hadi alipoingia ndani ya gari na kusindikizwa kwa ulinzi mkali kuelekea Tarime na hatimaye Musoma.

Mbowe umelikoroga linywe sasa....
 
Naona uchunguzi wa pili utafanywa na Wakenya kama inavyoonyesha hapa chini:

Uchunguzi mpya unataraijiwa kufanywa na timu ya madaktari kutoka hopitali ya Dk. Wilfred Kisuka Machage wa jimbo la Kurya, Kenya.
 
Quote:- Zion Train Zion Train has no status.

niombeeni kazi ya mimi kuwalinda hawa watu,sidhani kama kuna mtu atathubutu kuwagusa.(msifikiri utani huwa kwenye ukweli siweki mzaa)
M.Kijiji wewe na ES ndiye mliyenifanya nijiunge hapa JF,uchungu mlio nao kwa nchi yetu ,umenifanya nami niwe pamoja nanyi tupigane.

Mkuu Zion,

Heshima mbele, tupo ukurasa mmoja hapa, wote tunasaidiana kulijenga taifa kwa utunishi wa bure online, siku moja tutahamishia mapinduzi na uchungu huu wa taifa letu kwenye ground zero,

Salute!
 
I hope umepitia mafunzo ya first aid, inatakiwa mgonjwa usimwondoe wala kumsogeza toka alipo ndani ya gari ili usije ukamletea madhara zaidi mpaka baada ya daktari ku assess hali yake...

I'm puzzled, really puzzled! Hata mimi pia niko ng'ambo, nimefanya first aid, najua kanuni muhimu za first aid, so acha kuzuga watu hapa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom