Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Sasa nyie watu wa mkoa wa Mara sijui wakurya au wajita mkimaliza kulumbana na kujionyesha mlivyo na misimamo mjibu ama mkubali hoja yangu kuwa watu wa mara wana fujo au la!!!!

Halafu wewe Magabe Kibiti usijifanye kuwa wewe ndo mkurya peke yako hapa mtandaoni na kuwaona wakurya wengine siyo wakurya.Kwani Tarime nzima unakaa wewe???Araaaaaaaa!!wewe mkurya wa wapi?? Ulitahiriwa wapi??Yani unajiona wewe ndo mkurya tuu,mkiambiwa mmezoea mifujo mnakuja juu.Wewe ukoo wa nani wewe magabe wewe???,na usijifanye una uchungu sana na tarime.Umesikia???

Muraa amang'ana kasarakire. Chacha amefariki na hatuna uwezo wa kumrudisha. Tumshukuru mungu kwa zuri na baya. Nina imani kubwa amefariki kwa ajali ya gari na wala si risasi.
 
Jana Halisi ulisema Mbowe alishangiliwa na watu pale nyumbani kemakorere Tarime kwa kuitwa Rais Rais,Mbona ulikuwa ukituhadaa..ukweli ni kwamba alisaidiwa na baadhi ya viongozi kuhifadhiwa ndani kuogopwa kupigwa na kukatwana mapanga.Ndiyo maanda jana nilisema ole wenu CHADEMA.hata kama alihusika Mtu mwingine ila bado dhambi ya kumsimamisha wangwe bado iko mikononi mwenu mpaka hapo uchunguzi Rasmi utakopokamilika
 
Huyo Dr. atakaye fanya uchunguzi atakuwa peke yake?bila mwakilishi kutoka serikalini au serikali ilisha fanya uchunguzi wake?na je report hizi mbili za familia na serikali zikitofautiana si inaweza ikazusha mambo mengine tena?
 
Serikali itawakilishwa na Daktari wake pia
 
chacha wangwe alipigwa risasi kichwani na abiria aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma baada ya hapo dereva akiogongesha gari kwenye mti. wala ile gari hai ja roll! insingweza ku roll wind screen ikabaki, iligongeshwa kwenye miti tena kwa upande wa chacha aliyekuwa kakaa kiti cha mbele cha abiria ili kumuongezea michubuko kadhaa! Ila still wakitafuta daktari huru wa kufanya postmorterm watakuta risasi kichwani!
Ndugu zangu wakurya naomba kwa hili msione aibu hata mkiitwa wakorofi bora kujitenga na hii serikali JK na tulianzishe balaa kwa kudai nchi yetu isiyo ya kifisadi, sababu huu ni unafiki tena wa kudharau raia kama vile wote ni wajinga, haya mambo yana mwisho, na hapa hili kundi linalojiita mafia limegonga pabaya saaana, wamekosea saaaana! na mnajua kabisa kuwa FBI yote TZ asilimia kubwa inatokea Mara, sasa kwa nini mnajaribu kucheza mchezo usiochezeka!!!
Hapa piga uwa lazima kieleweke haraka sana, JK kama unataka tittle yako ya kuitwa mkuu wa kaya weka haya mambo wazi kwa haraka sana, otherwise soon utakuwa raia tu na tutangaza raia wetu!

Jamaa wamegonga pabaya, walidhani tarime nao ni ndio mzee, i am glad that we are setting the standards, hakuna kuzika zika tu eti ni mapenzi ya Mungu, no. Kwa hili watu wajifunzwe kuwa wakurya ndo wanajeshi tangu enzi na enzi and you cant fool them, wanaijua risasi na jeraha la risasi
 
Huyo Dr. atakaye fanya uchunguzi atakuwa peke yake?bila mwakilishi kutoka serikalini au serikali ilisha fanya uchunguzi wake?na je report hizi mbili za familia na serikali zikitofautiana si inaweza ikazusha mambo mengine tena?

Kwani ripoti ya awali iliyo fanywa na serikali inasemaje? ama huwa haitolewi mpaka.... mi nilidhani inatolewa kabla ya kuzika ama...?
 
Kumuua Wangwe ili kuisambaratisha CHADEMA - kama ulivyodai - maana yake CHADEMA ni tishio au Wangwe ni tishio. Unakubali Wangwe hakuwa tishio. Kwa hiyo tunabaki na CHADEMA. Ukitaka kuuwa watu CHADEMA ili kuisambaratisha CHADEMA unatafuta wale vinara ambao ni tishio na sio Marehemu.
Nadharia yako bado ina matatizo.
Hapana chijana bado unayumba yumba katika ufahamu,Labda nijaribu tena kuweka sawa.
Ndani ya Chadema kuna mgogoro kati ya Wangwe na wengine au uongozi.
Sasa kwa picha ilivyo ikiwa Wangwe atauliwa moja kwa moja vidole na mawazo yataelekezwa kwa wenziwe aliokuwa na ugonvi nao.
Sasa hebu niambie kwa nini akina Zitto na wenziwe ilibidi wahifadhiwe na habari nyengine zinasema wameondoshwa na kupelekwa Musoma ? Nataka sababu ya hayo ili niendelee kukufafanulia.
 
Kwani ripoti ya awali iliyo fanywa na serikali inasemaje? ama huwa haitolewi mpaka.... mi nilidhani inatolewa kabla ya kuzika ama...?

Nimemsikia jana huyu Kamanda wa upelelezi anadai eti uchunguzi bado unaendelea sasa sijui kwenye gari au wapi huu ndo usanii wa polisi angezikwa ndo basi tena walikuwa wanadai ajali ya kawaida.
 
Nimemsikia jana huyu Kamanda wa upelelezi anadai eti uchunguzi bado unaendelea sasa sijui kwenye gari au wapi huu ndo usanii wa polisi angezikwa ndo basi tena walikuwa wanadai ajali ya kawaida.

Hao wachunguzi wetu wameshanasa na uhalifu huu ni yale yale ya Zombe.Hawa akina dizaini za Zombe bado wamo ndani ya jeshi letu la polisi.
 
Mzee aliye msaidia Chacha eneo la tukio
1.JPG
Mzee Mwiguni George
 
Mura maghabe kana nke obhaye, tatigha abhalisya bhano bhatemwe kemakorere hala neho bhalaighwe!

RIP CHACHA ZAKAYO WANGWE aka MZEE WA MWONGOZO WA SPIKA.

Heshima yako Chacha wa Mwita,

naomba unisaidie kutafsiri maneno yako, maana hapa naamini tunatumia lugha kuu mbili ambazo ni Kiswahili na Kiingereza, naomba msaada wako.
 
Huyo Dr. atakaye fanya uchunguzi atakuwa peke yake?bila mwakilishi kutoka serikalini au serikali ilisha fanya uchunguzi wake?na je report hizi mbili za familia na serikali zikitofautiana si inaweza ikazusha mambo mengine tena?

Wakurya ni wakorofi wa asilia. Hawaambiliki na wakiamua kitu wameamua si rahisi kubadili msimamo labda kwa bakora. Wana amini Mbowe kahusika na kifo cha Chacha na kama Mbowe hatapewa ulinzi wanaweza kabisa kumlima mapanga na mikuki.
 
Huyu ndiye Deus Mallya
3.JPG
Mallya msanii kwelikweli, I can't even mention. Akibanwa zaidi anaweza kutoa maelezo mazuri na ya msaada kukamilisha investigation dhidi ya kifo hiki.

Itakuwaje itakapogundulika marehemu hakufa kwa ajali bali alipigwa risasi?
 
Hao wachunguzi wetu wameshanasa na uhalifu huu ni yale yale ya Zombe.Hawa akina dizaini za Zombe bado wamo ndani ya jeshi letu la polisi.

Kwa mfano huyu jamaa alikuwa hapendi kabisa kutoa maelezo ya kina kuhusu kijana waliye kuwa naye na mazingira ya tukio yeye alisisitiza kuwa uchunguzi bado unaendelea na kwa sasa ni mapema mno kuzungumzia swala hili.Wao bado wanaendelea na uchunguzi sasa kama ndo hivyo kwa nini waliruhusu mwili wa marehemu uzikwe huku wangalia wanaendelea na uchunguzi???Polisi wetu ndo walivyo kizombe zombe tu.
 
Itakuwaje itakapogundulika marehemu hakufa kwa ajali bali alipigwa risasi?

Mkuu inawezekana Kibaka aibe computer na doc. alafu aache vitu vya mhimu kwake kibaka kama simu za kubebeka kiurahisi.
 
Mallya msanii kwelikweli, I can't even mention. Akibanwa zaidi anaweza kutoa maelezo mazuri na ya msaada kukamilisha investigation dhidi ya kifo hiki.

Itakuwaje itakapogundulika marehemu hakufa kwa ajali bali alipigwa risasi?

Kuna mahali nimesoma kuwa Mallya aliwahi kupitia mafunzo ya kijeshi na alikuwa anamiliki kihalali bastola ambayo alikuwa anatembea nayo. Vile vile alishahudhuria mafunzo ya kijeshi katika nchi mbalimbali ikiwamo Libya na Misri.

Je maelezo hayo ni kweli au ndiyo ya kutuvuruga vichwa tena? Najua sasa hivi kuna kila aina ya porojo inaweza kuandikwa hapa.
 
Uchunguzi tayari mlioko Tarime ? Tunasubiri kwa hamu ili tupange au tupangue yale yaliopitishwa katika majadiliano na kufungua ukarasa mpya.Ila kama polisi wanasema wanaendela na uchunguzi baada ya kusikia jamaa wamelifungua jeneza na kukuta madudu ambayo yalikuwa yazikwe basi ipo kazi mpya,Kikwete omba isiwepo risasi lakini polisi wako naona wanaingia tena matatani.uliambiwa uwasimamishe makamishna wote na kuunda vijana wepya wewe ukajidai ukocha na kupangua position ,sasa jinamizi bado linafanya vitu vyake.
 
Mkuu inawezekana Kibaka aibe computer na doc. alafu aache vitu vya mhimu kwake kibaka kama simu za kubebeka kiurahisi.
Hahaha, Bongo ni 'full usanii' halafu unaambiwa doc hizo zishafika TBC. Hapo nachoka zaidi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom