Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
kwanza R.i.p Wangwe!

Unajua Wewe Ni Mtu Mzima Haujui Watu Tunauchungu Kiasi Gani... Unaleta Bifu Lako Na Mbowe Humu Kwanini Usifungue Thrd Yako Na Mbowe? Huu Ni Ujinga Hapa Tunaitaji Kujua Wangwe Kafa Kwa Ajari Au Kwa Risasi? Sasa Wewe Sijui Umetumwa Kutuondoa Kwenye Mada.umeniuzi Sana Sikutegemea Kama Kwenye Swala Zito Namna Hii Unaweza Kujaribu Kuvuruga Mada.

Chacha Rasta Alitumwa Na Watu Wa Tarime.
 
Kama kuna risasi polisi wetu itabidi watupe majibu ,na wao watakuwa wanajua dili kamili ni nani na nani walihusika na hivyo walitumiliwa kuficha ukweli wa matundu ya risasi ,tusubiri tume watakayoundiwa.Ndivyo tulivyozoea lakini hawa itabidi wahukumiwe azabu kali sana .

Ni hawa polisi wetu ambao kila siku wanatudai ushahidi wa tuhuma mbali mbali badala ya wao wenyewe kuutafuta?

Ikitokea kwamba uchunguzi wa pili wa mwili wa marehemu ukaonyesha kwamba kuna jeraha la risasi, labda sasa itabidi watafutwe wachunguzi kutoka nje lakini siyo hili Jeshi letu la Polisi.

Si ni hawa hawa ambao walipelekewa tape juzi juzi wakakaa mwezi mzima bila kutoa majibu, na baadaye wakasema camera hazijawahi kuzimwa na pia hata tape waliyopewa haikuwa na picha yoyote, yaani ilikuwa tupu. Hao ndio tuwategemee wafanye huu uchunguzi? Au ile tape ilipopelekwa Polisi ina maana aliyeipeleka (Spika na Katibu wa Bunge Msaidizi) hawakuangalia huo mkanda kabla ya kupeleka? Hao wote ni lawyers, sidhani kama wanaweza kupeleka ushihidi bila wao wenywe kujiridhisha kwanza.

Labda kama waliohusika na mauaji siyo wanachama wa genge fulani. Lakini kama ni wanachama wa genge hilo basi kesi itakuwa imekwisha. Sana sana Deusi anaweza kuwekwa ndani kwa kipindi fulani na baadaye kesi ikafa kibudu au Deusi mwenyewe akapotea.

IGP Mwema alishatuambia nchi imetekwa mafisadi (tunaposema mafisadi ni pamoja na wawekezaji ambao wameiweka serikali yetu kwenye mikono yao na maamuzi wanajifanyia wenyewe au wanafanya yale wanayotaka kufanya bila woga wowote). Pinda akaongezea kwa kusema kwamba mafisadi wa EPA ni hatari inabidi kwenda nao taratibu. Sasa bado hapo utakuwa na imani serikali ambayo inawaogopa mafisadi? Utakuwa na imani na Jeshi la Polisi ambalo IGP alishakiri kwamba nchi imetekwa na mafisadi?
 
Kuondoshwa kwa Wangwe ni kutaka kuisambaratisha Chadema

Wangwe hakuwa tishio kubwa wa kuifanya serikali ya CCM itake kumuua. Wapo vinara wengine wa CHADEMA walioitingisha Serikali kuliko Marehemu.

Una suspect au nadharia nyingine ?
 
Wangwe hakuwa tishio kubwa wa kuifanya serikali ya CCM itake kumuua. Wapo vinara wengine wa CHADEMA walioitingisha Serikali kuliko Marehemu.
Una suspect mwingine ?
Kuhani umenielewa sivyo kabsaa ! Hakuna sehemu nimeandika kama marehemu alikuwa tishio ! naona umekurupuka.taratibu kaka.
 
Wana humu humu,hiyo thread ya Mallya wapi?Hatuioni vp mmeitoa?Plz tuambiane why imetolewa,kuna vitisho au?INVISIBLE fanya mambo irudi tuijadili
 
Wangwe hakuwa tishio kubwa wa kuifanya serikali ya CCM itake kumuua. Wapo vinara wengine wa CHADEMA walioitingisha Serikali kuliko Marehemu.

Una suspect au nadharia nyingine ?

Chacha alikuwa ana role gani ndani ya Chadema? Mi sizungumzii umakamu mwenyekiti. Nazungumzia role, Dr Slaa ni attack dog, zitto is the charismatic leader, etc. Labda Chadema members wanaweza kutueleza, maana mi ninavyojua Wangwe was information collector.
 
Hakuna sehemu nimeandika kama marehemu alikuwa tishio ! naona umekurupuka.taratibu kaka.

Kumuua Wangwe ili kuisambaratisha CHADEMA - kama ulivyodai - maana yake CHADEMA ni tishio au Wangwe ni tishio. Unakubali Wangwe hakuwa tishio. Kwa hiyo tunabaki na CHADEMA. Ukitaka kuuwa watu CHADEMA ili kuisambaratisha CHADEMA unatafuta wale vinara ambao ni tishio na sio Marehemu.

Nadharia yako bado ina matatizo.
 
Nadharia tatu kama kweli mwili wa marehemu wangwe umekutwa na matundu ya risasi:

(a) Muuaji alitaka kumwondoa Wangwe ili kusababisha mgogoro zaidi ndani ya CHADEMA na hivyo kuisambaratisha zaidi CHADEMA na pia kuliondoa jimbo la Tarime mikononi mwa CHADEMA. Kwa nadharia hii, mtu huyu atakuwa siyo wa CHADEMA, anaweza kuwa ametoka CCM au NCCR-Mageuzi au kwa mbali sana TLP ambao wana potential ya kulichukua jimbo hilo la Tarime

(b) Muuaji alikuwa anataka kumzima Wangwe kwa vile alikuwa anapata umaarufu sana na hivyo kutishia nafasi za viongozi wengine ndani ya CHADEMA. Muuaji wa aina hii lazima awe ametoka CHADEMA na kwa vyoyote ama nafasi yake mwenyewe au ya rafiki yake wa karibu sana ilikuwa inatishiwa na Wangwe. Kwa vyovyote vile muuaji huyu hakushirikiana na kiongozi mwingine yeyote ndani ya CHADEMA, ndiyo maana viongozi wengine wa CHADEMA wamefumaniwa unprepared.

(c) Muuaji hakuwa na motive yoyote ya kisiasa, bali alikuwa na kinyongo na Wangwe kwa sababu za kibinafsi kabisa, kwa mfano sababu za kibiashara au za kijamii. Mtu wa aina hii anaweza kuwa yeyote yule, mwanasiasa au raia wa kawaida asiyekuwa na madaraka yoyote, lakini lazima ni mtu mwenye pesa nyingi.
 
Huu mjadala wa kama Wangwe ameuwawa au la nafikiri tuache daktari wa familia aseme then tuache polisi au serikali itafute watu wa uchunguzi, otherwise kuna watu humu watapotosha kabisa siasa za bongo.

Ina maana mtu asionywe au wasitofautiane kuwa kuwa hatujui atakufaje? Jamani tunaelekea wapi? Sioni sababu ya wanatarime kufukuza waombolezaji kabisaaa. haiingii akilini hata kidogo. Kufa kwingine na bado unaweza kufa na ukakosolewa e.g. Idi Amini na unaweza kufa na bado ukaheshimiwa e.g. Mwalimu Nyerere.

RIP Wangwe anaheshima yake na naamini tofauti zote zimezikwa na sasa mawazo yake yafanyiwe kazi. Chanzo cha kifo chake ni lazima kiwekwe bayana bila kuhitaji ufafanuzi wa ziada.
Mengi yanaandikwa na kusemwa lakini tifike mahala tuache wataalamu watuambie ila tofauti zetu zisubiri kwanza.

ASANTENI SANA
 
Maswali ya makuu 3 kuhusu kifo tete:

1. Je, ni kifo cha kawaida?
2. Je, ni kifo cha kisiasa?
3. Je, ni kifo cha kibiashara?
 
Nadharia tatu kama kweli mwili wa marehemu wangwe umekutwa na matundu ya risasi:

(c) Muuaji hakuwa na motive yoyote ya kisiasa, bali alikuwa na kinyongo na Wangwe kwa sababu za kibinafsi kabisa, kwa mfano sababu za kibiashara au za kijamii. Mtu wa aina hii anaweza kuwa yeyote yule, mwanasiasa au raia wa kawaida asiyekuwa na madaraka yoyote, lakini lazima ni mtu mwenye pesa nyingi.

Hiyo nadharia ina ahueni kidogo. Lakini sio nadharia ya kuitwa nadharia kwa sababu mauaji karibu yote ya binadamu huwa ni ya sababu za kijamii au kikambazi jambazi. Ni nadharia nyepesi nyepesi.

Zingine hizo za kusema TLP na NCCR waue Wangwe ili kupata kiti cha Tarime, well, aaaah, sio nadharia. I'll leave it at that.

Kuna nyingine ?
 
Huu mjadala wa kama Wangwe ameuwawa au la nafikiri tuache daktari wa familia aseme then tuache polisi au serikali itafute watu wa uchunguzi, otherwise kuna watu humu watapotosha kabisa siasa za bongo.

Ina maana mtu asionywe au wasitofautiane kuwa kuwa hatujui atakufaje? Jamani tunaelekea wapi? Sioni sababu ya wanatarime kufukuza waombolezaji kabisaaa. haiingii akilini hata kidogo. Kufa kwingine na bado unaweza kufa na ukakosolewa e.g. Idi Amini na unaweza kufa na bado ukaheshimiwa e.g. Mwalimu Nyerere.

RIP Wangwe anaheshima yake na naamini tofauti zote zimezikwa na sasa mawazo yake yafanyiwe kazi. Chanzo cha kifo chake ni lazima kiwekwe bayana bila kuhitaji ufafanuzi wa ziada.
Mengi yanaandikwa na kusemwa lakini tifike mahala tuache wataalamu watuambie ila tofauti zetu zisubiri kwanza.

ASANTENI SANA

Nadhani umeshasoma habari ifuatayo:

Ndugu mwingine wa marehemu, Kefa Wangwe, aliutangazia umati wa waombolezaji waliojitokeza kwa ajili ya maziko ambayo yalipangwa kufanyika jana kijijini kwao kwamba yameahirishwa ili kuruhu uchunguzi wa sababu za kifo cha marehemu.

Kefa alisema familia yao imeamua kuwa Marehemu Chacha hatazikwa hadi hapo madaktari watakapo uchunguza mwili wake na kubaini kifo cha mwanasiasa huyo kimesababishwa na nini.

Keba alisema familia ya marehemu akiwamo kaka yake Prof. Wangwe, waliamua kuufunua jeneza na kudai kuwa kulikuwa na alama za kupigwa risasi shingoni iliyotokea mdomoni nyingine tumboni na kusababisha kifo chake.
Kifo cha Wangwe kimegusa hisia za watu wengi sana hapa ukumbini. Habari kama hiyo hapo juu ndiyo inayotufanya tuanze kuangalia mbali zaidi ya kusubiri hiyo taarifa ya uchunguzi.
 
Hiyo nadharia ina ahueni kidogo. Lakini sio nadharia ya kuitwa nadharia kwa sababu mauaji karibu yote ya binadamu huwa ni ya sababu za kijamii au kikambazi jambazi. Ni nadharia nyepesi nyepesi.

Zingine hizo za kusema TLP na NCCR waue Wangwe ili kupata kiti cha Tarime, well, aaaah, sio nadharia. I'll leave it at that.

Kuna nyingine ?

Hasa hasa nilikuwa na maana ya possibilities. Hizo mbili za kwanza zikiwa zinasukumwa na sababu za kisiasa wakati ile ya tatu ikiwa inasukumwa nsa sababu zisizo za kisiasa. Huwezi ku-rule out sababu za kisiasa kwa vile marehemu alikuwa ni mwanasiasa
 
I was flabbergasted by the bereavement of Late Chacha wangwe, I appreciated the steps taken by his family of having investigation before his entombment, this is real good and we enthusiastically waiting for the results and whoever will be identified to be involved, she/he must taken before the law as soon as possible.
I hope nothing will be concealed in this investigation.
 
Sasa nyie watu wa mkoa wa Mara sijui wakurya au wajita mkimaliza kulumbana na kujionyesha mlivyo na misimamo mjibu ama mkubali hoja yangu kuwa watu wa mara wana fujo au la!!!!

Halafu wewe Magabe Kibiti usijifanye kuwa wewe ndo mkurya peke yako hapa mtandaoni na kuwaona wakurya wengine siyo wakurya.Kwani Tarime nzima unakaa wewe???Araaaaaaaa!!wewe mkurya wa wapi?? Ulitahiriwa wapi??Yani unajiona wewe ndo mkurya tuu,mkiambiwa mmezoea mifujo mnakuja juu.Wewe ukoo wa nani wewe magabe wewe???,na usijifanye una uchungu sana na tarime.Umesikia???
 
Taarifa ya Habari ya TBC1 ya leo ambapo dogo Mnyika alihojiwa imeibua mambo kadhaa:

1. Kuwa TBC wana nyaraka toka kwa Chacha Wangwe, za kesi aliyotaka kufungua(hapa TBC1 hawajui kabisa kuwa kesi alishafungua tayari), tamko la Chacha kuhusu CHADEMA na mambo mbalimbali (hapa TBC lazima waeleze umma wamepataje nyaraka toka kwa marehemu kabla hazijatoka wakati ambapo inaelezwa kuwa nyaraka zote za marehemu ziliibiwa garini pamoja na laptop).

2. TBC1 wanaelekea kuwa na mkakati wa dhati wa kufanya propaganda za kuhusisha CHADEMA na hiki kifo.

3. Taarifa nilizonazo ni kuwa Chacha alishafungua kesi ya kuzuia CHADEMA isimvue uanachama na si kesi ya kutaka fidia ya kuchafuliwa kama alivyodai angefungua baada ya siku kumi na nne. Na tamko lake ambalo alikuwa afanye press conference DSM baada ya kuaga mwili wa Bhoke Munanka lilikuwa ni kueleza kwamba CHADEMA inataka kumtimua uanachama. Alikuwa aelekee kufanya reconcilliation kwa kuwa mikakati yake mingi iligonga mwamba ikiwemo kikao na Makamba Dodoma.

Nasubiri kwamba mpambanaji huyu azikwe ndio niseme kwa uwazi zaidi.

PM
PM huwa unanifanya nicheke sometimes. Unajua kuibua mambo ambayo wengi wanayachukulia 'simpo' na yakiwa na ukweli ndani yake. Anyway, credit to you brother!
 
RIP Chacha Wangwe. Poleni wana familia pamoja na WaTanzania kwa ujumla. Yaani Bongo imefikia kuanza mauaji kwa sababu ya siasa!? its a shame! Lakini naamini Roho ya mtu haiendi hivihivi na walioanzisha haya yatawarudi tuu na watauona Mkono wa MUNGU. yaani kama watu wako desperate hivi maana yake wanauona mwisho wao unakaribia ndio maana wanatapatapa. Eee Mwenyenzi Mungu naomba uwapige kwa kutumia mkono wako waliofanya maovu hayaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom