Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,226
- 44,395
mkikubali hiki ni kifo cha kawaida na uchunguzi ulio huru na wa kihalifu kutofanyika; mkikubali kuwa ni "ajali tu kama zingine" na ya kuwa ni "mapenzi ya Mungu"; mkikubali kuwa hakuna haja ya kuangalia ukweli wote ule, siyo tu mtakuwa hamumtendei haki Chacha na jitihada zake za kuwa mkweli na muwazi, lakini yawezekana tutakuwa tumetoa kibali cha mambo haya kuendelea kutendeka kwa kisingizio cha "mapenzi ya Mungu" au "ajali ni ajali tu".
Sasa hivi katika Tanzania lolote linawezekana na hasa linapokuja suala la fedha na madaraka. Mkikubali kuwa hiki kifo ni mapenzi ya Mungu, basi inabidi mkubali pia kuwa yote yanayoendelea nchini ni mapenzi ya Mungu, wizi wa EPA ni mapenzi ya Mungu, ubadhirifu ni mapenzi ya Mungu n.k Kwani kimsingi kwa wale wenye imani, hakuna kitu kinachotokea ambacho si mapenzi ya Mungu. Hivyo tukubali tu yaishe kwani mafisadi nao ni mapenzi ya Mungu kwetu. Sisi ni nani hata tuwapinge?