Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
TBC ni Bango la Mafisadi na serikali inaongeza nguvu TBC kuwafumba macho wadanganyika, dalili zimeshaonekana na wadanganyika wameshashtuka. Asante Mola wetu kwa hili.

Wananchi wa Tarime komaeni vilivyo lakini msilete ugomvi, mlivyowafukuza viongozi wa serikali (chama tawala) mmefanya jambo la maana, wanafiki wakubwa hao watakuzuieni kufanya mtakalo.

Wapeni upinzani kama ccm muda wa kujitetea, watakuwa na mengi ya kuwaambia. Nawshukuruni mumemsikiliza Zitto Kabwe.

Hapa mnaona CCM tu?

Wkati kuna watu waliomsimamisha uongozi Bwana Chacha Wangwe baada ya kuwaambia kuwa wao wankura pesa ya Ruzuku?mambo ya ukabila na mambo mengine waliyompakazia,Rejea kauli ya Mpaka Kieleweke aliyesema kwamba Chacha aliongea na Rostam pale Kempski?mambo mengi sana yalizunguzmwa yakiwa ya Chuki,nani mwenye chuki zaidi ya hawa watu wa chama chake?Mbowe aliaanza ugombvi na Chacah wakati wa uchaguzi kwa kuwa alikuwa akimtaka alfu awe Makamau Mwenyekiti

NCCR na wao walikuja Mbele wakiwataka CHADEMA wamtimue Chacha wangwe,Yote haya Mmeshasahau?hayo yalisemwa naKaimu katibu mkuu wa NCCR,Jose.. Wanasiasa wa Bongo ni watu wa ovyo sana na ndiyo sababu upinzani huwa unashindwa.

Hapa kuna mambo mengi na magumu tuyategemeee kama ni kweli alipigwa Risasi,Je ni nani alihusika?kwani wale wataalam wa mambo hawawezi kujua ni nani alihusika?

tusubiri tuone nani alihusika
 
Kibiti,
Nimekuelewa, maana kwangu inaponishangaza yaani Tarime wakute risasi sasa huyu aliyeufanyia utafiti Dodoma yaani hakuona hizo risasi au aliziacha makusudi? na kama mchezo umefanywa yaani ashindwe kuzitoa na kumchana chana ili kuvuruga ushahidi? kazi kweli kweli

Yombayomba,

Mimi nilikuwa ni mmoja wa wale waliotaka mazishi yafanyike haraka ili watu warudi kwenye kazi zao za kujenga taifa na jimbo letu ambalo liko nyuma sana. Niliyoyasikia toka kwa ndugu wa marehemu na watu waliouona mwili wa Wangwe ni makubwa na ya kutisha hadi kufikia hatua ya kubadili mawazo yangu.

Sipendi tena kugombana na wenye nguvu (serikali) katika utendaji wao hasa ukichukulia yaliyonikuta mlimani lakini katika hili la Wangwe limeniuma kiasi kwamba hata kuandika naandika nikitetemeka na huku machozi mengi sana yakinitoka.

Chochote kile Wangwe alichofanya, hakustahili kifo cha namna hii. Haya ni mambo mabaya sana kutokea kwa jamii za kitanzania na inabidi yakemewe sana kwa nguvu zote. Tanzania tumezoea kuachia tu watu wakifa katika mazingira ya kutatanisha lakini sasa hili linaenda mbali zaidi ya uwezo wa kawaida wa kuvumilia.

Najua sina cha kufanya kwa sasa na labda Prof Wangwe atawashauri ndugu zake waachane na haya ili yaishe kama mengine lakini wakazi wa Tarime tuna uchungu sana na tumempoteza mpiganaji mkubwa sana wa haki na masuala yetu.
 
jamani.... kuna neno wanasema "to err in the side of caution". Wasipofanya au kuhurusu uchunguzi huru watakuwa wanachochea hisia zote hasi ambazo zimekuwa zikienea. Ukifiria sana utaona kuwa yawezekana ilikuwa ni ajali ya kawaida na kosa kubwa ni la kijana Malya kusema kuwa yeye hakuwa dereva na baadaye kukiri alikuwa dereva; hilo ndilo lililochanganya watu sana. Yawezekana kama walivyosema wengine hana leseni n.k

So yawezekana kuwa ni kifo cha kawaida kabisa kama Katibu Tarafa anavyosema, lakini jinsi mambo yalivyokwenda na yanavyoshughulikia yanafanya kifo hiki kisiwe cha kawaida na hivyo kulazimu uchunguzi huru ili kuwahakikishia wananchi kuwa ni kifo cha kawaida kabisa na ni ajali tu.

Kuna ubaya gani kati hilo Katibu Tarafa?
 
mkikubali hiki ni kifo cha kawaida na uchunguzi ulio huru na wa kihalifu kutofanyika; mkikubali kuwa ni "ajali tu kama zingine" na ya kuwa ni "mapenzi ya Mungu"; mkikubali kuwa hakuna haja ya kuangalia ukweli wote ule, siyo tu mtakuwa hamumtendei haki Chacha na jitihada zake za kuwa mkweli na muwazi, lakini yawezekana tutakuwa tumetoa kibali cha mambo haya kuendelea kutendeka kwa kisingizio cha "mapenzi ya Mungu" au "ajali ni ajali tu".

Sasa hivi katika Tanzania lolote linawezekana na hasa linapokuja suala la fedha na madaraka. Mkikubali kuwa hiki kifo ni mapenzi ya Mungu, basi inabidi mkubali pia kuwa yote yanayoendelea nchini ni mapenzi ya Mungu, wizi wa EPA ni mapenzi ya Mungu, ubadhirifu ni mapenzi ya Mungu n.k Kwani kimsingi kwa wale wenye imani, hakuna kitu kinachotokea ambacho si mapenzi ya Mungu. Hivyo tukubali tu yaishe kwani mafisadi nao ni mapenzi ya Mungu kwetu. Sisi ni nani hata tuwapinge?

Kaa, Mkjj hiyo ni kali! Hata hivyo kuna ukweli; yatupasa tuache kuchukluia mambo kijuujuu tu na hata kama ni ajali kweli itawahofusha Mafisadi na Wauaji wa kupanga.

Mwishowe tutasema hata kuvamiwa kwa Kubenea ni ajali; ni vibaka tu! Teh, teh!
 
Sasa ukweli ni upi , wamegundua risasi au ni maneno ya watu wanaokejeli maiti na kuwaudhi waathirika wa msiba huo.
Kwa kweli sipendi kuona watu wanaichezea maiti kwani ni vibaya kufanyia kejeli na haswa kuongezea uongo,Zito yumo humu ,na mwengine sijui nani nae yumo humu ,Je watu hawa ambao wapo ndani ya Chadema kwa nini wasiuzime uwongo na kuubakisha ukweli haswa zinapokuja dhana za kufikirika.

Waliokataa kuzika ni ndugu za marehemu na wakazi wa Tarime. Viongozi wa vyama vya siasa walienda Tarime kuzika mwili wa Chacha. Nadhani mpaka hapo umeelewa kuwa hili si jambo la wanasiasa tena bali la wakazi wa Tarime na ndugu za Wangwe.
 
Mkuu Samahani,

Naomba umuulize huyo msela hapo ofisini kwa Deus kuna print outs za Chadema peke yake au kuna print outs zingine tofauti tofauti?

Kama ni za Chadema peke yake ni utata huo...??? Yawezekana kashirikishwa ama kaziiba...??? Kazipataje...??? Kama kuna print outs zingine, hiyo ofisi ilianza lini na print outs za zamani zaidi ni za wakati gani? Je, zinahusika zaidi serikalini, NGOs, au vyama vya siasa tu? Yawezekana alizipata kwa Wangwe pia, ilikuwaje...???

Jamaa ni Printer kweli kampuni yake inaitwa Visitor Print na alikua na printout nyingine nyingi tu including some za CCM pia. According to huyu mshkaji jamaa anajua kuendesha Gari but hana uhakika kama alikua na leseni. Document hakuziiba bali alikua akiprint kazi zao. Hata Ccm alishawafanyia kazi. Jamaa anasema hata kile kitabu cha Zitto "Wajibu Wangu". jamaa alikua na Mkono wa kazi yake.
Pia dogo alikua na Ushakji na baadhi ya Vigogo wa CCM kwani kuna Kipindi alienda libya na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, Mbunge wa Iramba Magharibi CCM na Juma Killimbah.

Hizo ndo alizonipa kwa sasa. Bado nadadisi wakuu
 
Mzee Gachuma, mjumbe wa NEC ya CCCM na mtu mashuhuri Mara na MWanza, amelalamika kuondolewa katika kiti, baada ya kuonekana CCM wanataka kutumia msiba kama jukwa la kisiasa. Watu wa Mara ni wakweli na wawazi na kwamba pamoja na tofauti zao za ndani ya Chadema, wamemuita Mbowe RAIS, RAIS, RAIS!!!! amepishwa katika kiti na alitakiwa kuzungumza, viongozi wenzake wakamzuia
 
Waliokataa kuzika ni ndugu za marehemu na wakazi wa Tarime. Viongozi wa vyama vya siasa walienda Tarime kuzika mwili wa Chacha. Nadhani mpaka hapo umeelewa kuwa hili si jambo la wanasiasa tena bali la wakazi wa Tarime na ndugu za Wangwe.
haiwezekani kuwa hili ni jambo linalowahusu watu wa jamii fulani tu,hapo sikubaliani napo,na haswa jambo hili lilivyojaa magirini,na yule mzee amedai mtu wa tatu alitoweka ,pengine mtu huyo alikuwa ammalize na mshikiliwa ili kupoteza ushahidi na haswa kunapozuka hoja ya kutumika risasi,nionavyo ushahidi ulikuwa upotezwe ,kubaki kwa kijana kuna ushaidi tosha pengine baada ya risasi kutumika kwa Wangwe pistoli ilikwama na kutoweza kutumika na watu walianza kumiminika ,jamaa akatoweka.
Nirudi kuwa hapo Wangwe ni Mbunge na anawakilisha Chama Chake anawakilisha upinzani Tanzania bara na Tanzania Visiwani, Sasa tukirudi kama risasi ilitumika kummaliza uhai wake na kijana hakudai kuvamiwa na Majambazi basi ni wazi kuna jambo ambalo WaTanzania watakuwa na shauku ya kulijua.
Aidha kama wandugu walihisi ni hujuma basi kutakuwa na habari imevuja na ndio wakaitisha uchunguzi , so ni nani yupo nyuma ya mauaji haya ?
Kuna pahali niliona kuwa walimsaidia mtu wa tatu kumpa lifti ambae alitoweka muda mfupi tu baada ya ajali, Sasa kama uchunguzi umeonyesha kuna risasi mbili ambazo zilitumika,kijana anaeshiliwa na polisi atakuwa amesema uongo na maelezo yake yote yatakuwa ajuwari,na atakuwa anajua ni nani walioshiriki na kwa hivyo atakuwa ni mmoja wa washiriki wa mauaji kwa kuficha ,bila ya shaka yeyote alikuwemo ndani ya gari risasi ya mwanzo aliisikia na ya pili nayo aliisikia kama gari alikuwa akiendesha Wangwe kwa mwendo wa kasi ,bila ya shaka alipoteza control na kuelekea kwenye misingi na gari kubondeka ,alieua nae alipoteza pistol labda hakujua iliangukia wapi na wakati huo watu wameshafika alijibabaisha na kutoweka,inawezekana kijana anaeshikiliwa na polisi hakuhusika ila aliona mambo yatachukuliwa kirahisi na kwa vile mwili ulikuwa katika hatua za mwisho kupelekwa kaburini kijana alikuwa anayo siri ambayo labda angeitoa katika uzee wake,huwezi kujua.Lakini kwa nionavyo atakuwa amehusika iwapo tu risasi ni kweli zimeonekana kwani maelezo yake yote aliyoyatoa mwanzo yanaonyesha kukwepesha kila kitu na sasa itakuwa hadithi nyengine kabisa.
 
kama kuna kitu kinaitwa backfire ni hiki.... maana kampeni zilizopitishwa tangu majuzi kuhusu Mbowe, walikuwa wanatarajia kweli jamaa afukuzwe kwa mawe... Tatizo ni kuwa suala hili bado linaonekana ni la kisiasa, na hivi vyama viwili aidha vitatuletea matatizo zaidi hasa kama wameshindwa kukaa pamoja na kufanya vitu pamoja. CCM Mara isingefanya lolote pasipo kuhusiana na Chadema, na wao wangekuwa kwenye background ya uongozi wa Chadema.

Nadhani vyama hivi vilianza vizuri Dodoma mara baada ya habari za msiba, lakini somewhere along the way kuna mtu alitaka kutake advantage ya situation.
 
kijana myalla anatanua na wabunge tu mpaka nchi za nje! tena wa ccm na upinzani! siamini kama he is as innocent as he wants us to believe.....lakini ukweli lazima utadhihirika tu
 
swali kubwa ni stori gani wamtengenezee Malya ambayo itakuwa air tight? Mimi nasubiri jaribio lao la kutuzuga kama litakuwa zuri hadi tukazugika.
 
kijana myalla anatanua na wabunge tu mpaka nchi za nje! tena wa ccm na upinzani! siamini kama he is as innocent as he wants us to believe.....lakini ukweli lazima utadhihirika tu

Yawezekana akawa trainee jasusi
 
haiwezekani kuwa hili ni jambo linalowahusu watu wa jamii fulani tu,hapo sikubaliani napo,na haswa jambo hili lilivyojaa magirini,na yule mzee amedai mtu wa tatu alitoweka ,pengine mtu huyo alikuwa ammalize na mshikiliwa ili kupoteza ushahidi na haswa kunapozuka hoja ya kutumika risasi,nionavyo ushahidi ulikuwa upotezwe ,kubaki kwa kijana kuna ushaidi tosha pengine baada ya risasi kutumika kwa Wangwe pistoli ilikwama na kutoweza kutumika na watu walianza kumiminika ,jamaa akatoweka.
Nirudi kuwa hapo Wangwe ni Mbunge na anawakilisha Chama Chake anawakilisha upinzani Tanzania bara na Tanzania Visiwani, Sasa tukirudi kama risasi ilitumika kummaliza uhai wake na kijana hakudai kuvamiwa na Majambazi basi ni wazi kuna jambo ambalo WaTanzania watakuwa na shauku ya kulijua.

Aidha kama wandugu walihisi ni hujuma basi kutakuwa na habari imevuja na ndio wakaitisha uchunguzi , so ni nani yupo nyuma ya mauaji haya ?

Kuna pahali niliona kuwa walimsaidia mtu wa tatu kumpa lifti ambae alitoweka muda mfupi tu baada ya ajali, Sasa kama uchunguzi umeonyesha kuna risasi mbili ambazo zilitumika,kijana anaeshiliwa na polisi atakuwa amesema uongo na maelezo yake yote yatakuwa ajuwari,na atakuwa anajua ni nani walioshiriki na kwa hivyo atakuwa ni mmoja wa washiriki wa mauaji kwa kuficha ,bila ya shaka yeyote alikuwemo ndani ya gari risasi ya mwanzo aliisikia na ya pili nayo aliisikia kama gari alikuwa akiendesha Wangwe kwa mwendo wa kasi ,bila ya shaka alipoteza control na kuelekea kwenye misingi na gari kubondeka ,alieua nae alipoteza pistol labda hakujua iliangukia wapi na wakati huo watu wameshafika alijibabaisha na kutoweka,inawezekana kijana anaeshikiliwa na polisi hakuhusika ila aliona mambo yatachukuliwa kirahisi na kwa vile mwili ulikuwa katika hatua za mwisho kupelekwa kaburini kijana alikuwa anayo siri ambayo labda angeitoa katika uzee wake,huwezi kujua.Lakini kwa nionavyo atakuwa amehusika iwapo tu risasi ni kweli zimeonekana kwani maelezo yake yote aliyoyatoa mwanzo yanaonyesha kukwepesha kila kitu na sasa itakuwa hadithi nyengine kabisa.

Kwa kuanzia tu,

Sio kwamba Wangwe ndiye alikuwa anaendesha hilo gari, huyo "Mallya" kwa sasa ameshabadili tena story yake na kusema kuwa yeye ndiye alikuwa anaendesha hilo gari.
 
Mzee Gachuma, mjumbe wa NEC ya CCCM na mtu mashuhuri Mara na MWanza, amelalamika kuondolewa katika kiti, baada ya kuonekana CCM wanataka kutumia msiba kama jukwa la kisiasa. Watu wa Mara ni wakweli na wawazi na kwamba pamoja na tofauti zao za ndani ya Chadema, wamemuita Mbowe RAIS, RAIS, RAIS!!!! amepishwa katika kiti na alitakiwa kuzungumza, viongozi wenzake wakamzuia

Halisi,

kuna maandamano makubwa sana ya watu wa Tarime yanaendelea sasa hivi watu wakiwa wakiimba kuwa sio ajali ya gari bali risasi ndizo zimemuua Wangwe.

Huyu Gachuma watu wamemheshimu tu kwa vile huwa ni mtu fair la sivyo angekimbizwa kama wengine waliojaribu kuleta unafiki kwenye msiba. Viongozi wengine wamepewa heshima na wananchi wa Tarime watakuwa watulivu tu ili kusubiria uchunguzi huru kwenye hili.

Wasiwasi wangu ni kuwa, hekima za wazee wanaoheshimiwa kama Prof Wangwe zitashinda na wataamua kuzika hata kama ni usiku wakati watu wamelala.
 
Hapo sasa polisi inabidi waanike ukweli kabisa watu saizi wanafuatilia dot baada ya nukta wakituchuuza watakiona cha moto ni bora waweke wazi hiki kifo wamechemka kama mpirani hii ni rafu mbaya wamechemka.
 
Ina maana Mazishi yatafanyika Lini?hao ndugu zangu wakurya watakuwa wanagombania Mali tu na hizo Rambi rambi,nakujua huko..

kutakuw ana ishu nzito,nitampigia ndugu yangu mmoja ambaye yuko karibu na familia ya Wangwe na atanipa feedback na nitawahabarisha

Halafu we gembe shika adabu yako. Kwa taarifa yako kama unawajua vizuri wakurya ni watu wasiojipendekeza wala kuombaomba n the last thing you can expect from them ni kugombania rambirambi, hata kama mkurya ana shida kiasi gani hawezi kumpigia magoti mtu, remember that si washahili hao, they keep their pride. So hadi hapo nadhani umenipata, wangekuwa watu wa kujipendekeza na kufikiria rambirambi wangewakimbiza hao wabunge?
 
Kwa kuanzia tu,

Sio kwamba Wangwe ndiye alikuwa anaendesha hilo gari, huyo "Mallya" kwa sasa ameshabadili tena story yake na kusema kuwa yeye ndiye alikuwa anaendesha hilo gari.

Hapo sasa hapatakiwi tena nani aliendesha na nani aliendeshwa ,sasa gumzo ni lingine kabisa ,alipigwa risasi au hakupigwa na ninani amethibitisha hilo yaani lugha imeshageuka kabisa.
Na huyo Mallya ijulikane kuwa yumo ndani ya mikono ya Serekali so far wanatakiwa wamlinde kwa mizinga na ndege za kivita na Mheshimiwa Kikwete sasa anaingia moja kwa moja kwenye fungati hili ikiwa kijana atapotea ndani ya serikali yake.
 
Pitia thread zote mkuu, kuna mkulu kasema Mbowe amenusurika kuuwawa baada ya Dr. kutoka Kenya kufanya ukaguzi wa mwili na kugundua jamaa alikufa kwa kupigwa risasi mbili.

C kweli Habari za uhakika nlizopata kutoka Tarime ni kwamba Dr kutoka Kenya atafika leo saa 12 Jioni na atafanya uchunguzi kesho asubuhi. Hilo swala la risasi ni speculations za wa2 tu bali bado ni tetesi kwa sasa hadi hapo Dr atakapothibitisha. Ni kweli Fujo zimetokea but c kweli Mbowe kanusurika kuuawa.
 
Sasa mnaanza kukoroga ila lisemwalo lipo na kama halipo linjiani laja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom