Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Inawezekana wewe unaishi dunia ya peke yako. Kwanza maswali unayouliza majibu yake ni baada ya huo uchunguzi. Kwamba ni kitu gani na siri gani, ni mpaka uchunguzi ufanyike, ambao wewe unaupinga.

Lakini pia, ujue Wangwe alikuwa mbunge na anatoka katika chama na jimbo lenye mazonge mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Ujue Wangwe ni binadamu, na sheria za Tanzania binadamu anapofariki hata katika ajali ya kawaida kabisa, ni lazima uchunguzi ufanyike tena hata kwa zaidi ya mara moja. Sasa wewe ndugu yangu fikiria mara mbili kabla ya kuandika au kujadili mada inayohusu kifo cha mtu

Mimi nipo dunia hii hii,ila watu wafuata au kuongozwa na hisia,na hasa huyu mdudu redio mbao,ndio kabisaa anatumaliza.kitu kingine tayari watu wameshakuwa na majibu yao tayari.
 
Inabidi sasa vinara wetu wawe makini,ZITO,KUBENEA,SLAA etc M.KIJIJI wapewe ulinzi hata kama utakua ni INVISIBLE lakini wasiwe tena kama wananchi wakawaida.Maana sasa wasi wasi utakua unatuingia.

niombeeni kazi ya mimi kuwalinda hawa watu,sidhani kama kuna mtu atathubutu kuwagusa.(msifikiri utani huwa kwenye ukweli siweki mzaa)

M.Kijiji wewe na ES ndiye mliyenifanya nijiunge hapa JF,uchungu mlio nao kwa nchi yetu ,umenifanya nami niwe pamoja nanyi tupigane.
 
Mzee Mwanakijiji,

Nakuhakikishia kuwa familia ya Wangwe na wananchi wa Tarime wamekataa kukubali kuwa hiki ni kifo cha kawaida. Yanayoendelea Tarime sasa hivi ni zaidi ya maelezo ya kawaida.

Uchunguzi binafsi umeanza na inaonesha kabisa kuwa inawezekana Wangwe aliuawa kwa kitu kingine (risasi?) na sio ajali kama ilivyotolewa. Kuna maelfu na maelfu ya watu wa Tarime wamekuja kumuaga Wangwe na wamesema kuwa hawatakubali longo longo na propaganda za TBC1 na magazeti ya Rostam Azizi kuhusu kifo cha Wangwe.
TBC ni Bango la Mafisadi na serikali inaongeza nguvu TBC kuwafumba macho wadanganyika, dalili zimeshaonekana na wadanganyika wameshashtuka. Asante Mola wetu kwa hili.

Wananchi wa Tarime komaeni vilivyo lakini msilete ugomvi, mlivyowafukuza viongozi wa serikali (chama tawala) mmefanya jambo la maana, wanafiki wakubwa hao watakuzuieni kufanya mtakalo.

Wapeni upinzani kama Chadema muda wa kujitetea, watakuwa na mengi ya kuwaambia. Nawshukuruni mumemsikiliza Zitto Kabwe.
 
Hizi habari za risasi ni za kweli, Wangwe hakufa kwa ajali kama inavyotaka kuelezwa hapa. VIongozi wote wa serikali na wabunge waliokuja Tarime toka Dodoma wamekimbizwa na wananchi wa Tarime.

Unafiki wa hali ya juu, kulikuwa na sababu gani kufanya haya yote.

Bado nawaomba wananchi wa Tarime wawe watulivu na wasikubali kugawanywa na wasioipenda Tarime.

Its true hajazikwa bado coz ndungu wamegoma hadi wamlete daktari wao afanye uchunguzi. Wabunge na viongozi wametolewa nduki hawana hamu. Si hua wanadharau kusolve vita huko sasa onjeni joto ya jiwe, ndo mtajua wakurya walivyo, hawapendi unafiki wenu huo. Give them hell huko hadi wajue kama mapinduzi yataanzia huko.Fuuuuuuuuuuuuuuck them killers
 
Kibiti,
Tumeelezwa daktari anakuja toka Nairobi, that mean hajafika na kuufanyia uchunguzi mwili, sasa hizi risasi mbili zinatokea wapi? Kama kauawa kwa risasi waliouona mwili wa kwanza yaani wanakijiji nafikiri hilo wangeliona kwa sababu jeraha la risasi ni tofauti saana na mkumbuke wanavijiji wengi ni wawindaji hivyo wanajua majeraha ya risasi.

Tayari kuna dakitari ambaye amefanya uchunguzi wa awali. kinachosuburiwa ni kupata confirmation zaidi. Kumbuka pia kuwa Wangwe alikuwa na marafiki zake wengi tu wakiwemo maprof na madakitari sehemu mbalimbali duniani.

Kilicholeta mshituko ni pale ambapo FFU walitaka kuwazuia wananchi wa Tarime wasiuone mwili wa mbunge wao kwenye jengo la halmashauri. Hilo tu lilipelekea watu kupelekea kwenye conclusion kuwa kuna kitu kikubwa kinafichwa.

Inawezekana hakuna conspiracy kubwa hapa lakini the way polisi na serikali ya Dodoma walivyohandle issue ya kifo cha Wangwe, ukiongezea na maelezo ya kujichanganya ya "mallya", hiyo ya kukutwa risasi ni chumvi tu kati ya mengi kwenye hili suala.
 

Source: TBC1

Mazishi ya RIP CW yameahirishwa until uchunguzi ufanywe upya na mtaaalam atakaye chaguliwa na familia pamoja na shahidi kutoka serikalini.
 
Tayari imethibitishwa kuwa ameuawa na risasi 2.hilo kwa sasa halina ubishi.
 
Hii mpya nimesoma eti huyu DEUS MALLYA alishawahi hudhuria mafunzo ya kijeshi Libya!!

Lolote linawezekana. Ni kijana makini sana. Anaweza kuwa na majina tofauti, tofauti na ameingia Chadema kwa gia kubwa na kujipendekeza, ameshindwa kuwaingia baadhi ya viongozi wengine wa Chadema kwa kuwa wengi wanapenda kufanya kila kitu wenyewe wakati mwingine hata kuendesha magari wenyewe. Ni bahati mbaya tu kwa Wangwe, maana hata yeye hana makuu na hapendi msaidizi, ila kwa kuwa mgonjwa, nadhani ndipo mambo yalipomuwia magumu na inawezekana alizugwa na ushawishi wa nguvu kwamba lazima awe Dar usiku huo huo.

Lakini taarifa za Hospitali ya mkoa ya Dodoma, karibu makachero 50 wanatajwa kufika kwa nyakati tofauti kufanya naye mazungumzo na habari zinasema, wahudumu wanafukuzwa wakifika wao. Nje kuna ulinzi wa kiaina maana eti trafiki ndiye anayelinda nje tokea jana. Watu wengine hawaruhusiwi kuzungumza naye tena. Wahudumu wanasema anapewa mazoezi ya kuzungumza kwa "ufasaha"
 
Mimi nipo dunia hii hii,ila watu wafuata au kuongozwa na hisia,na hasa huyu mdudu redio mbao,ndio kabisaa anatumaliza.kitu kingine tayari watu wameshakuwa na majibu yao tayari.

Katibu tarafa,

watu wa Tarime wana mwili wa Wangwe na wao ndio wameona hayo majeraha na wakakataa kuzika. ni vyema kuwa skeptical lakini pia ni vizuri kutodhania kuwa watu wa Tarime wote ni wajinga kiasi hiki.
 
Kifo cha Wangwe: Chadema yataka polisi wafanye uchunguzi wa kina
*Aliyekuwa na marehemu awekwa chini ya ulinzi
*Akiri kutembelea Libya, hana mafunzo ya kijeshi

*Anukuu maadiko: Kufa ni zawaidi kuishi ni Ukristo


Na Muhibu Said, Dar na Ramadhan Semtawa, Dodoma


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, kwa kujibu maswali saba yanayomhusu kijana aliyekuwa na marehemu wakati wa ajali iliyosababisha kifo chake.


Kijana huyo, Deus Mallya (27) (pichani), ambaye ni shuhuda wa kwanza wa ajali hiyo, juzi alikaririwa na gazeti hili akieleza kwa ufasaha namna ajali hiyo ilivyotokea katika eneo la Pandambili, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, Jumatatu wiki hii na kusababisha kifo cha mbunge huyo aliyekuwa machachari.


Chadema imetoa maswali hayo, kupitia barua yake Kumbukumbu namba C/HQ/ADM/SG/02/85 ya Julai 30, mwaka huu, kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, kwa madai kwamba, mazingira ya ajali hiyo, yamegubikwa na utata.


Barua hiyo, ambayo imesainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, imetaja sababu nyingine ya kutaka uchunguzi huo ufanyike kuwa ni kutokana na wabunge wa Chadema kupata taarifa za vitisho na kuzushiwa vifo kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi (sms) na ujumbe huo kusambazwa.


Mnyika, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Vijana Taifa wa chama hicho, ameeleza katika barua hiyo kuwa taarifa hizo za vitisho, ziliwahi kuripotiwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, ambaye pia, ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.


Nakala ya barua hiyo iliyotumwa kupitia mtandao wa kompyuta, imenakiliwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba.


Mnyika amedai kuwa maelezo yaliyotolewa na Mallya kuhusiana na jinsi ajali hiyo ilivyotokea na kiti ambacho alikuwa amekaa wakati ajali inatokea, yameongeza utata.


Mnyika alidai kabla ya Mallya kutoa maelezo hayo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa, katika mahojiano yake na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) kupitia kipindi cha 'Jambo Tanzania', alielezea utata huo na kutaka Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi wa kina.


Alidai taarifa ambazo zimetolewa na watoto wa marehemu walipohojiwa na vyombo vya habari, yakilinganishwa na maelezo ya Mallya, yanahitaji kupatiwa majibu ya kina.


Alisema Chadema kama mwathirika wa ajali hiyo, haiwezi kufumbia macho suala hilo, hasa baada ya kufuatilia kwa kina maelezo yaliyotolewa kwa nyakati na watu tofauti kuhusu ajali na hatimaye msiba huo na kwa vile ina maslahi ya karibu katika uchunguzi huo.


Kutokana na hali hiyo, alilitaka Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mambo mbalimbali, ikiwamo kijana huyo (Mallya) aliyekuwa na Wangwe kwenye gari lake wakati anafariki dunia, ni nani na anafanya shughuli gani.


Pia, (Mallya) alienda Dodoma kufanya shughuli gani na ana uhusiano gani na marehemu na au familia yake (marehemu).


Vilevile, (Mallya) alikuwa amekaa kwenye kiti gani wakati ajali inatokea, ni nani alikuwa anaendesha gari wakati ajali na hatimaye umauti unamkuta Wangwe na mazingira gani yaliyosababisha ajali hiyo kutokea.


"Tunataka Polisi wachukue hatua stahiki za kisheria ili Deus Mallya akaisaidie polisi na kuhojiwa kwa kina juu ya suala hili kwani maelezo yake yana utata mkubwa sana. Jeshi la polisi liitoe ripoti ya uchunguzi huo mapema na kuiweka ripoti hiyo hadharani," alisema Mnyika kupitia barua hiyo na akaongeza:


''Tunapendekeza hatua hizo zichukuliwe mara moja kwani tunaamini kuwa kifo hiki kimegubikwa na utata mkubwa sana na haswa kutokana na maelezo ambayo yamekuwa yakitolewa na aliyeshuhudia ajali (Deus Mallya) pamoja na watoto wa marehemu.''


''Tunaamini kuwa utatupatia ushirikiano wa kina ili kuhakikisha kuwa hatua za haraka na za dharura zinachukuliwa mara moja kwa ajili ya kuujua ukweli wa kifo hiki tata.


"Tunaomba wabunge wetu wapatiwe ulinzi na pia taarifa hizo zifanyiwe kazi kwa kina,'' alisema Mnyika kupitia barua hiyo.


Akizungumza na Mwananchi mjini Dodoma jana, Mallya alisema anajuana na viongozi wa Chadema na kueleza kwamba, yeye ni mfanyabiashara.


Pia alisema anajuana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na anamiliki kampuni ya uchapishaji wa majarida na vitabu, iitwayo Visitor Print, iliyoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam.


Mallya, ambaye yuko chini ya ulinzi wa polisi, mjini Dodoma, alisema mara ya mwisho alipanga kusafisha picha za Wangwe alizopiga akiwa na nywele zilizosukwa kwa mtindo wa rasta ili aziweke kwenye jarida la marehemu.


Pia alidai anafahamiana na Zitto na kwamba, mara ya mwisho alimchapishia mbunge huyo jarida linaloitwa "Wajibu Wangu".


Alipoulizwa kuhusu kupata mafunzo ya kijeshi nchini Libya, Mallya, ambaye hana makovu licha ya jicho lake kuonekana limevia kwa mbali, alikiri kufika nchini humo, lakini akasema alikwenda na akawapo huko kwa siku nne kati ya Juni na Julai, mwaka jana.


Alisema katika safari hiyo, alikuwa pamoja na Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa bin Shaaban Simba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, Mbunge wa Iramba Magharibi, Juma Killimbah na kusisitiza kuwa mbunge huyo anamfahamu.


Kuhusu kupata mafunzo ya kijeshi, alisema hajawahi hata kuwa sungusungu wala mgambo.


Alisema baada ya kutoka Libya, alikwenda Uswisi na baadaye akarejea nchini.


Mallya, alisema fani ya usanifu aliipata Nairobi, nchini Kenya katika Chuo cha Mtakatifu Hubert baada ya kumaliza sekondari kidato cha nne.


Alisema aliacha kuendesha gari tangu alipokuwa chuoni hapo baada kupata ajali kubwa kati ya mwaka 1999 hadi 2001.


Alisema amesikitishwa na taarifa za watoto wa Wangwe kwamba ndiye aliyekuwa akiendesha gari kabla ya ajali iliyosababisha kifo cha baba yao kutokea.


''Inawezekana watoto walishinikizwa, lakini mimi ni jasiri, ni mkweli, na nitaendelea kuwa mkweli,'' alisema.


Kuhusu tuhuma kwamba ametumiwa kumhujumu Wangwe, alisema anachojua yeye ni kuwa kilichotokea ni ajali na si vinginevyo.


''Mimi ni mhubiri mzuri wa injili, ninamwamini Yesu na Paulo aliwahi kusema kufa ni zawadi na kuishi ni Ukristo,'' alisema Mallya.


Hata hivyo, kwa sasa Mallya yuko chini ya ulinzi katika hospitali ya mkoa wa Dodoma daraja la kwanza na askari anayemlinda alisema wamemweka chini ya ulinzi ili kuangalia asihujumiwe na pia kusaidia taarifa nyingine kutoka kwake kama watazihitaji.

Source: Mwananchi
 
Hili linaibua mapya kabisaa,nadhani huyu mzee ni mkweli maana ni shuhuda tu kama by stander na kama kuna mtu alikuwa akimpa maelekezo na hajamtambua kama ni malya sasa huyo mtu ni nani?na huyu anathibitisha marehemu hakuwa anaendesha gari kwani yeye ndio kamfungua seat belt sasa nani aliendesha wakati malya anadai alikuwa siti ya nyuma hakugusa usukani?
mmh,it leaves many to be desired

mimi mbona nimesikia leo kuwa huyo dogo kasema yeye hajui kuendesha gari?
 
Lolote linawezekana. Ni kijana makini sana. Anaweza kuwa na majina tofauti, tofauti na ameingia Chadema kwa gia kubwa na kujipendekeza, ameshindwa kuwaingia baadhi ya viongozi wengine wa Chadema kwa kuwa wengi wanapenda kufanya kila kitu wenyewe wakati mwingine hata kuendesha magari wenyewe. Ni bahati mbaya tu kwa Wangwe, maana hata yeye hana makuu na hapendi msaidizi, ila kwa kuwa mgonjwa, nadhani ndipo mambo yalipomuwia magumu na inawezekana alizugwa na ushawishi wa nguvu kwamba lazima awe Dar usiku huo huo.

Lakini taarifa za Hospitali ya mkoa ya Dodoma, karibu makachero 50 wanatajwa kufika kwa nyakati tofauti kufanya naye mazungumzo na habari zinasema, wahudumu wanafukuzwa wakifika wao. Nje kuna ulinzi wa kiaina maana eti trafiki ndiye anayelinda nje tokea jana. Watu wengine hawaruhusiwi kuzungumza naye tena. Wahudumu wanasema anapewa mazoezi ya kuzungumza kwa "ufasaha"

Mpaka sasa ninaamini kuwa huyu kijana jina lake halisi ni tofauti na hili la Deus Mallya. Huyu kijana abanwe ili aeleze vizuri kilichotokea. Nina wasiwasi wa kutokea mambo kama kwenye kifo cha Kenedy hapa.
 
Kibiti,
Nimekuelewa, maana kwangu inaponishangaza yaani Tarime wakute risasi sasa huyu aliyeufanyia utafiti Dodoma yaani hakuona hizo risasi au aliziacha makusudi? na kama mchezo umefanywa yaani ashindwe kuzitoa na kumchana chana ili kuvuruga ushahidi? kazi kweli kweli
 
Tayari kuna dakitari ambaye amefanya uchunguzi wa awali. kinachosuburiwa ni kupata confirmation zaidi. Kumbuka pia kuwa Wangwe alikuwa na marafiki zake wengi tu wakiwemo maprof na madakitari sehemu mbalimbali duniani.

Kilicholeta mshituko ni pale ambapo FFU walitaka kuwazuia wananchi wa Tarime wasiuone mwili wa mbunge wao kwenye jengo la halmashauri. Hilo tu lilipelekea watu kupelekea kwenye conclusion kuwa kuna kitu kikubwa kinafichwa.

Inawezekana hakuna conspiracy kubwa hapa lakini the way polisi na serikali ya Dodoma walivyohandle issue ya kifo cha Wangwe, ukiongezea na maelezo ya kujichanganya ya "mallya", hiyo ya kukutwa risasi ni chumvi tu kati ya mengi kwenye hili suala.

Ni vigumu sana kwa mtu anayejaribu kupunguza makali ya UKWELI. Kwa hakika daima dama, UKWELI huwa na nguvu kubwa na UKWELI huwazodoa hata wale wanaojaribu kuupindisha. Nadhani hapa sote tufikirie kwamba lolote linawezekana, ama 1.Ajali ya kawaida, 2. Ama uzembe wa dereva 3.Uzembe wa marehemu. 4. Uhalifu ikiwa ni pamoja na ujambazi, mauaji ya kupangwa na mauaji ya kukosea (kama alikusudiwa mwingine). 5. Inawezekana pia kuwa mhusika kujiua. Lakini yote hayo, inawezekana kabisa mhusika asiwe kutoka chama chochote cha siasa kama Chadema, CCM na kadhalika. Inawezekana pia akatoka katika vyama hivyo na kwamba asiwe na baraka za vyama husika. Inawezekana akawa mtu anayetoka serukalini na asiwe na baraka na wakubwa zake (kanjanja) lakini yote hayo pia yanaweza kuwa kinyume chake. Kwa msingi huo, uchunguzi huru kabisa unapaswa kufanywa na hakika watu wa IB, wanapaswa kushirikishwa kwa haraka sana
 
TBC ni Bango la Mafisadi na serikali inaongeza nguvu TBC kuwafumba macho wadanganyika, dalili zimeshaonekana na wadanganyika wameshashtuka. Asante Mola wetu kwa hili.

Wananchi wa Tarime komaeni vilivyo lakini msilete ugomvi, mlivyowafukuza viongozi wa serikali (chama tawala) mmefanya jambo la maana, wanafiki wakubwa hao watakuzuieni kufanya mtakalo.

Wapeni upinzani kama ccm muda wa kujitetea, watakuwa na mengi ya kuwaambia. Nawshukuruni mumemsikiliza Zitto Kabwe.

Akilimtindi,

Hawa TBC1 ni wanafiki na walitaka kutumia kifo cha Wangwe ili kuleta mgogoro Tarime na kuwachonganisha wakurya na makabila mengine. Kwenye taarifa zao kila mara walikuwa wanakumbushia kuwa hivi karibuni Wangwe na viongozi wa chadema walikuwa na ugomvi. Hii ni propaganda ya kutaka hili jambo lihusishwe na kifo cha Wangwe.

Kosa moja walilofanya ni kudhania kuwa wananchi wa Tarime (in this case wakurya) ni wajinga na watakubali mambo ya uongo kama haya. Magazeti ya Rostam Aziz - majira na mtanzania nao - walianza kuleta mambo mengine ikiwemo ya mgogoro wa kikoo kule Tarime na kutaka kuwagawa wananchi wa Tarime.

Wananchi hawataki uzandiki na unafiki wa vyombo vya habari kwenye mambo kama haya. Nimesikia uchungu sana kwenye yaliyomkuta Wangwe. Uliza watu walioko Tarime wakuambie namna watu wa Tarime wanavyolia kwa uchungu mkubwa sana.

Wangwe amepigania haki ya wananchi wa Tarime kwa miaka mingi sana toka siku akiwa diwani hadi leo. Anayehusika na hiki kifo amefanya makosa makubwa sana. Kama ana dini aombe msamaha kwa MUNGU wake.
 
Utata mtupu, sijui nishike lipi. Anyway nipo tayari kwa mwenye maelezo yasiyohitaji ufafanuzi
 
Sasa ukweli ni upi , wamegundua risasi au ni maneno ya watu wanaokejeli maiti na kuwaudhi waathirika wa msiba huo.
Kwa kweli sipendi kuona watu wanaichezea maiti kwani ni vibaya kufanyia kejeli na haswa kuongezea uongo,Zito yumo humu ,na mwengine sijui nani nae yumo humu ,Je watu hawa ambao wapo ndani ya Chadema kwa nini wasiuzime uwongo na kuubakisha ukweli haswa zinapokuja dhana za kufikirika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom