Hapo mimi nakataa mkuu, hatujafika kuamua kama ni CHADEMA au CCM walihusika juu ya hili, lakini Bw. Mallya atakuwa na majibu yote kuhusu nani haswa amehusika na msiba huu.
Kuhusu vyama kwa ujumla CCM haina hasara kwa lililotokea ukilinganisha na hasara iliyoipata CHADEMA, kwanza CHADEMA wamepoteza jimbo ambalo sasa CCM wanapiga kambi kuliiba, pili watu wa madini ambao ni CCM watapumzika, tatu kama usemavyo wewe CHADEMA itachafuka kwakuwa itaonekana imehusika. Kwa ujumla CCM sanasana labda wamepoteza pesa ambazo sio shida kwa mafisadi...! Pia CCM ina namna, mbinu na watu wengine ambao wanaweza kutumika kuwachanganya CHADEMA...! Time will tell maana binadamu tuwaone tu usoni lakini mioyoni mwao hatuwajui wako vipi, ni hatari kuliko Simba wala watu...!
Horace Kolimba alikuwa katibu mkuu wa CCM akagongana na wenzake na muda si mrefu akafariki, uvumi ulioenezwa ni kuwa wale aliogongana nao kimawazo ndani ya chama chake wamemkolimba, haikusemwa kuwa wapinzani wamemkolimba ilitizamwa kuwa kabla ya kufa Marehemu alikuwa na ugomvi na watu gani.
mfano wa pili wa kifo cha Marehemu Amina Chifupa hakikuusishwa na Chadema wala CUF, uvumi wote ni kuwa Amina alikuwa na nia ya kugombea uenyekiti wa CCM kundi la vijana mwaka huu na baadhi ya wana CCM wenzake hawataki agombee ndio wamemfupishia maisha yake.
hakuna aliyesema kuwa CUF wamehusika na kifo cha Amina,
kama alivyopania Marehemu Wangwe kuchukua uenyekiti wa Taifa Chadema,jee wamezima azima yake? kwani Wangwe alisema kuwa uamuzi wa mwisho juu ya hatima yake wanayo wanachama wa Chadema wa nchi nzima sio kundi la wahuni wa makao makuu ya Chadema, na uzoefu unaonesha kuwa Wangwe kwenye chaguzi ni ngumu kumzuia kama alivyopita kwenye umakamu wa Mwenyekiti na kwenye uenye kiti kulikuwa hakuna cha kumzuia.
Mfano wa tatu ni wa Junior Malecela aliyekuwa kwenye sakata la uchaguzi wa vijana na akapata ajali kama WANGWE,alipokufa kifo chake kilihusishwa na chama chake si vyama tofauti.
Wangwe alikuwa na mgongano wa kimawazo na wana Chadema wengi hadi wengine wakasema kuwa afutwe uanachama, wengine wakasema apigwe risasi humu humu JF,wengine wakasema ni Pandikizi la CCM kupitia kwa Rostam na alinunuliwa akiwa Movenpick hotel.
kama CCM walimnunua kwanini wamuue? kama kipimo cha kumpimia Kolimba kilikuwa alikolimbwa na wana CCM wenzake kwa kugongana kimtazamo kama alivyogongana Wangwe na wana chadema wenzake,kwanini tusihusishe kifo chake na mgongano wa kimawazo na wenzake ndani ya chama chake?
katika vita ya ufisadi anayesema kauli hiyo ni Slaaa sio Wangwe basi wangemuua Slaa,lakini Mwanakijiji ana msemo wake kuwa kipimo kiwe kimoja nakubaliana nae,kuwa kipimo cha Kolimba aliyekuwa na mgongani wa kimtazamo na kimawazo na wanaccm,kinafaa kutumika kwenye kadhia hii ya Wangwe, alipofariki DR.OMAR ALI JUMA haiukuhusishwa CUF ni wana CCM wenzake ndio waliovumishiwa ubaya na hilo hadi kwa marehemu Sokoine. mchawi siku zote ni jirani au mtu wako wa karibu hamlijui hilo?