Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
....kama mna chochote cha kusema semeni la sivyo hii inafaa kule kwenye udaku!
 
fikra zangu kuna huwezekano kwamba walikuwa wa3,lakini kulikuwa na gari ambayo ilikuwa inawafuatilia nyuma,kama kuna lolote walifanya kwa marehemu basi ulikuwa ni ushirikiano wa watu,ajali ilifuata baada ya kitendo.
Mhh! You mean He was Mur....before the 'Accident' was staged??
 
Hii hali inatisha usalama wa wananchi. kwa mwendo huu, one need to think twice before becming a politician.

Malima, kolimba, kombe, and the list is growing
 
mzee ajazungumzia lolote la vibaka,hayo yalikuwa maelezo mallya,kutokana na maelezo ya shahidi wa kwanza ambaye ni mallya ni kwamba walikombwa vitu vyote na vibaka,lakini wakamuachia simu na bastola. mzee hata kama kutakuwa na kesi yeye atakuwa ni shahidi wa pili.

fikra zangu kuna huwezekano kwamba walikuwa wa3,lakini kulikuwa na gari ambayo ilikuwa inawafuatilia nyuma,kama kuna lolote walifanya kwa marehemu basi ulikuwa ni ushirikiano wa watu,ajali ilifuata baada ya kitendo.


Yawezekana CHACHA alikua peke yake ,ila walimteka na kumfanyia unyama huo.
Pamoja ajali ni ajali lakini Mzee anasema yeye ndio amemvua mkanda RIP CHACHA na mtu kama amefunga mkanda ni vigumu sana kichwa kubanwa na mlango wa nyuma.

Mfano kama gari limegonga mti linge m sequeze kifuani .
 
Mhh! You mean He was Mur....before the 'Accident' was staged??

yes,ni fikra zangu lakini,usije ukaniuliza ushahidi mie sina. nchi yetu inatisha sana sasa hivi,yani hali ya taifa inatisha,kama mengi yanayotokea na ayapatiwi ufumbuzi, inatisha sana tanzania yetu.
 
sijawahi kudai kuwa kila ninachokijua nakiweka JF. Uhuru wa habari huendana na kuwajibika kwa habari hizo. So, vinavyoweza kusemwa hadharani vinasemwa vingine vinakuwa ni kuchombeza tu kuwa tunavijua. So, nadhani kutwa nzima ya leo tumemwaga mtama mwingi tu.

Tunachosubiri ni jinsi gani wataamua kutuzuga.

Ni kweli kabisa. Lakini kama hauko tayari kukisema, nadhani sio vyema ukachombeza kwamba unakijua. Manake hapo sasa inakuwa kama chekechea wanadodeshewa na baba na peremende zake.
 
Is it still to early to call for an independent investigation from the Scotland Yard..?
 
Tarime kuna madini na Chacha Wangwe asingekubali uchuro utokee jimboni kwake.
 
naungana Na Mkuu Mwingine Hapa, Tunaomba mwenye Picha Ya Huyu Deus Mallya Aiweke Hapa Tuione Tafadhali, Ama Kama Kuna Ambaye Anaweza Kuipata Kwa Namna Yeyote Aibandike Hapa Tafadhali
 
Hivi polisi wamesema kuhusu hiyo bastola aliyokuwanayo huyo Mallya? Je, wameifanyia forensic analysis kuona kama haikutumika? Je aliipata kihalali na anajulikana kuwa nayo?

Hii ndio Tanzania nchi ya amani lakini kila uchwao Viongozi wanakufa kwa njia zisizo julikana. Si walisema Bungeni yule Chenge sijui hakukuwa na uchawi au Pollonium 210.



Jamani hivi picha za gari lililopata ajali ziko wapi?
 
Kazi ipo kweli kweli, kwa mwendo huu, hata polisi wachunguze vipi, watu wameshakuwa na majibu yao.

Sasa si isaidieni polisi ili wafanye uchunguzi wa maana?

Hata kama huyo kijana amesema mambo tofauti sitashangaa, baada ya kupata ajali kubwa kama hiyo, mtu yeyote anaweza kuchanganyikiwa hivyo.

Muhimu ni ukweli kamili utoke kwa faida ya familia yake, lakini kwa jinsi rumours zilivyo nyingi, ukweli wowote utageuka kuwa uwongo.
 
Sijui unaongelewa watu wapi wa Tarime maana mimi ni mtu wa Tarime na sijaona kama watu wa Tarime ni wapenda zari. Tafadhali ondoa generalization kwenye statement zako.

Kama wewe unapenda zari basi si wote. Kama wewe unasuluhisha mambo yako kwa silaha basi ujue kuwa si wote Tarime tunapenda fujo. Umeelewa?

Magabe,

Tafadhali ndugu yangu achana na watu kama hao -huyo ni mfano mzuri sana ukitaka kuwajua watu ambao wako tayari kuuza hata utu wao mradi wanatupiwa makombo na status quo. Watatetea lolote lile, watazua yote yale na watalamba miguu ya mafisadi mradi wanatupiwa mabaki kutoka meza kuu liyoandaliwa kwa wenye meno. Watu wa aina hii wako wengi na matendo yao yamewaziba macho - hawajui maadui zao wala marafiki zao - na wanabakia wa kuhurumiwa. Ole wao siku ya ukombozi watajikuta wanatafutana wenyewe kama manyang'au kwa kuwa hiyo mirija yao itakuwa imekatwa na wazalendo wenye uchungu wa kweili na nchi yao. Naandika haya kwa uchungu kama mwenyeji wa Tarime ambaye anaona mbinu chafu za kujaribu kutugawa zikianza kupamba moto kwa nguvu, kasi na ari mpya. Mungu atuepushe na hizi njama na amlaze mahala pema peponi kamanda wetu Wangwe, amina.
 
Pundit.. usifikirie CCM (of course inaweza kunufaika zaidi) fikiria nini kilichoko Tarime that is worthy killing for.

MKJJ Huyu jamaa alikuwa akipambana kuwatetea wachimbaji wadogo wadogo dhidi ya BARRICK...Sasa hiyo hoja aliyokuwa aiwasilishe na akawa anazungushwa iwekwe hapa.

Nilishasema wazi kuwa BARRICK ni kampuni kubwa na kuwapinga hawa watu ni sawa na kutangaza vita mbaya sana!

Kazi ipo!

Na mnavyoendelea kuvuta muda...Wataendelea kutumia vita ya kisaikolojia na watu wataendelea kumung'unyuliwa tuu!

YANI NI HARUFU YA DAMU KILA MAHALI.

Hata mimi mwenyewe huko face book mara naanza kupata marafiki wa CANADA...Nasema ala..!

Cha muhimu nataka nitumie nafasi hii kuwaeleza hao BARRICK kwa kupitia wajumbe wao ambao wako hapa...WAPENI WANYONGE CHOCHOTE JAMANI...CHONDE CHONDE NA UBINADAMU JAMANI.
 
Paparazi.. hili la Wangwe litaangusha watu; NIngekuwa mimi nisingetaka Polisi hawa kuendelea na uchunguzi kwa kudai sina imani nao; ningeomba hata wapelelezi toka Afrika ya Kusini kama NSY hatuwataki. Lakini hili ni kubwa; nina breaking news ambayo hata kuweka leo naogopa. People can't handle this much twist and turns... kama wewe na miye ngoja nisiseme mengi.
Mkuu MMJJ na PM, tunaomba msifiche kitu hapa maana ndio kitovu cha ujanja wetu. Hatuwezi kubeba mapanga moja kwa moja lakini tutajua wazi nyoka, kondoo na simba wala watu wako wapi na wanaendesha harakati za kutufanyia mambo gani. Itatupa akili ya tukae pande gani tukijipanga kutenganisha simba na kondoo kisha kuwagonga nyoka vichwa. Bwana Asifiwe maana kasi ya maovu inahatarisha nchi yetu lakini inafumua uovu mwingi na kuwaweka simba pagumu kila tuendako, ushindi unaelekea kujileta karibu zaidi ingawa naona sadaka zikiongezeka. Mungu awaweke pema peponi wale wote watakaokumbwa na haya kwa bahati mbaya wakipambana. Sisi tuko pamoja nao.
 
1217400841_ajaliyawangwewen.jpg
 
Asante kwa picha lakini tunaomba za kutoka kila angle please kama zipo.

Nafikiri kuna haja ya kuwa na private investigators ambao kama watawahi kwenda kule ilikotokea ajali na kutoa donge nono kwa taarifa za waliokuwepo usiku ule.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom