Nilichoona mpaka sasa ni hichi
something is very wrong....who has his phone?
Mallya alisema, baada ya ajali alipoteza fahamu, alipozinduka wanakijiji alikuwa tayari wameshafika katika eneo la tukio. Wakaanza kumsarch marehemu, alichukua laptop na mabegi yao pamoja na makorokoro mengine.
TVT na ITV alifika kwenye tukio, walionyesha mpaka Mallya alivyofika hospitali, wakati mallya anapelekwa huko, yani kitandani, Nesi alichukuwa Simu mbili, moja ni blackberry zile pana na ingine ni nokia zile za torchi kama sikosei, battery ilikuwa imetoka na pesa kama 50,000 hivyi zikiwa na damu.
Kuhusu simu ya Marehemu, sijui.............
Kitila.. tangu jana mara tu baada ya ajali nimekuwa nikiuliza maswali fulani na nimewauliza watu wengi kweli; na kati ya majibu ambayo hayakupatikana ni suala la muda. Sisemi nini chaweza kuwa kimetokea, lakini suala la muda ni muhimu sana kwani ndilo litaweza kujibu mara moja na daima kuwa hii ni ajali tu. Wasipojibu suala la muda, wamejichimbia shimo kubwa tu la maelezo. Ninaposema "wamejichimbia" sijui ni kina nani. Nitaanza kuyauliza maswali hayo hapa, na mwenye majibu anisaidie kutuliza udadisi wangu.
a. Nani alikuwa wa kwanza kufika eneo la ajali?
Kutokana na maelezo, wanakijiji ndio walikuwa wakwanza kufika, wakamtoa marehemu na kuanza kumsarchi.
Wanakijiji ndiyo walikuwa wa Kwanza Kufika Katika eneo la ajali.Hawa wanakijiji wa Pandambili.
b.Nani alikuwa akiendesha Gari?
Marehemu ndio alikuwa anaendesha gari
very good. hivyo aliweza kuwa na simu karibu baada ya ajali, usiku, katika eneo baada gari kurushwa "mita chache" na kusababisha kifo papo hapo... na aliweza kutolewa ndani ya hilo gari baada ya vibaka kufika kwanza ndani ya muda mfupi... kuna muda gani kati ajali na Polisi kufika?
Sijui, ila naona ni baada ya Mallya kupata fahamu
Waliiba nini hasa? Mbona abiria alipokea simu ya marehemu ilipopigwa? Au simu haikuibwa?
Mallya ametamka kwamba wameiba laptop mbili na mabegi yao, na vitu vingine vilivyokuwa kwenye gari.
so kama saa moja baadaye... Polisi walifika baada ya Mkuu wa Polisi kupata taarifa au kabla ya mkuu wa Polisi kupata taarifa?
Mkuu wa Mkoa amesema kwamba mkuu wa polisi alituma askari wa barabarani waliokuwa karibu na tukio, baadaye yeye ndio akaenda majira ya saa nne.