Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Pole kwa wafiwa.
wandugu, hii ni ajali na mimi ninaamini ni ajali kama zilivyo ajali nyingine.
Ingeweza kutokea hata kama Chacha angekuwa anaedneshwa na dereva kwa sababu huyo dereva naye ni binadamu kama marehemu alivyokuwa.
Corlla zinapata ajali kama yanavyopata ajali mashangingi, treni, ndege na meli.
So far as hakuna authority iliyoeleza sababu za ajali hiyo conclusively, speculations hazitatusaidia kujua chanzo cha ajali.
La msingi ni kujiuliza; kwa nini ajali zinaendelea kumaliza maisha ya watanzania kila kukicha?
 
Hizi politics za elimination Tanzania zitatumaliza, we need to know huyo "Nchimbi" wa huko ni nani?
Masatu najua yaweza kuwa una imani kubwa sana juu ya nguvu za giza ambazo watu mbalimbali wanazo pia..lakini imani yako inapokuwa ni potofu kimsingi inaumiza watu wengine wasio na hatia...mimi sio kati ya ninaoamini juu ya nguvu za giza..siamini binadamu anaweza kujipa uwezo wa mamlaka ya kulifanya gari lipinduke au roho itoke.matokeo ya imani za nguvu hizo tumeshuhudia ndugu zetu zeruzeru wakiuwawa na kukatwa viungo vyao....wao ni wahanga wa imani za kishirikina...kwa kweli tutoe pole kwa familia ya Wangwe.Bwana alitoa na Bwana ametoa.
 
Warudishe Bunge Dar safari kila siku na barabara zetu hizi za mashimo tutakwisha

Kwa nini usingesema ya kwamba makao makuu yawe Dodoma? maana hata kama ni Dar bado kila Mbunge atawakilisha Jimbo lake. Ama unataka kuleta ajenda za kwamba wabunge watakuwa wanarudi majimboni kwao nyakati za uchaguzi tu?
 
Jamani wana jamii mnapaswa kujenga tabia ya kukubali kile kichotea kwa upande wa kifo, si vyema kuanza kuhusisha kifo cha ndugu yetu kaka yetu mpiganaji Chacha Wangwe na mambo ya ushirikina, ni vyema tukaungana kuwafariri wana familia pamoja na wanandugu wa huyu mwenzetu aliyetangulia mbele za haki kuliko kuhoji juu ya kifo chake.
kumbuka:-

KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.
R.I.P Brother
 
Sasa inaonyesha kuna squad maalum ya kutekeleza mapambano kwa ajali ,inaonyesha walinzi walale ndani ya magari.La si hivyo wata,alizana.
 
Wametunyima nafasi ya kumuaga hapa Dar. Sijui kama ni ndugu zake akina Profesa Wangwe au ni mwajiri wake Bunge la Jamhuri?
 
Pole kwa familia ya Wangwe, Chadema na wanachi wa jimbo lake. Kwa kumsikia na kusoma anavyoelezewa, bila shaka ameacha pengo kubwa hasa kwa Chadema licha ya mgogoro uliokuwapo. Ni watu wa aina ya Wangwe ambao huleta msisimko na mabadiliko katika vyama vya siasa. Pamoja na mapungufu, Chadema wafanyie kazi baadhi ya hoja za marehemu. Mungu amlaze pema peponi
 
ambao mnaweza kuangalia ITV wako live sasa na kulikuwa na mahojiano na mtoto wa marehemu, Hakika kifo cha Chacha Wangwe kinasikitisha sana.
 
Kitila.. tangu jana mara tu baada ya ajali nimekuwa nikiuliza maswali fulani na nimewauliza watu wengi kweli; na kati ya majibu ambayo hayakupatikana ni suala la muda. Sisemi nini chaweza kuwa kimetokea, lakini suala la muda ni muhimu sana kwani ndilo litaweza kujibu mara moja na daima kuwa hii ni ajali tu. Wasipojibu suala la muda, wamejichimbia shimo kubwa tu la maelezo. Ninaposema "wamejichimbia" sijui ni kina nani. Nitaanza kuyauliza maswali hayo hapa, na mwenye majibu anisaidie kutuliza udadisi wangu.

a. Nani alikuwa wa kwanza kufika eneo la ajali?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom