Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Sidhani kama hao wengine uliwapigia magoti. Au hao akina Mtikila, Ms. Malecela n.k., uliwapataje? Hii ya kwako ya kuendelea kumtafuta Mbowe naona karibu tutaifanyia birthday, maana na sababu za yeye kutoshikika sasa huwa zinabadilika. Kama kweli na wewe una mengi ya kuuliza, nafikiri yeye angekuwa priority kuliko kuleta wababaishaji kama Mtikila n.k. Tufahamishe ulikokwama ili tutafute dawa.

Kubwajinga

Unampigia mbuzi gita, nimekuuliza toka lini mtu akakata tawi alilokalia?
 
Poti
Lakini hili swali lako sijui msingi wake ni nini?

Mda utafika tu siku hili swali litakapokugeukia na kukuuliza mfano wewe ni msemaji wa SLAA ,ZITO,MBOWE ama chadema.

Haya mkuu .

Poti,

Mimi ninachoongelea hapa ni masuala ya Tarime. Niulize chochote kuhusu Tarime na wanatarime au niulize kama mimi ni msemaji wa Tarime. Mtu ambaye anasimamia hoja za Chadema au CCM au Mtikila ataulizwa haya maswali kama yeye ni msemaji wa hao watu na sera zao.

Kufikia wakati umeona nimeanza kuelezea masuala ya Chadema, nitakuwa na furaha kujibu swali lako kama mimi ni msemaji wa Chadema.

Kwa sasa kubwajinga anaonekana anajua undani wa maneno ya Mtikila na anaonekana kuelewa nia na maelezo ya Mtikila. Swali langu ni rahisi tu hapa,
je yeye ni msemaji wa Mtikila?
 
Huu ndio ninaoita u-pr school. Ustaadhi anapokosa hoja, huamua kuropokwa.

The bottom line ni kuwa hata kipenzi cha watu akichemsha ni lazima na yeye afahamishwe.

Dharau hazitasimama badala ya jibu la swali langu. Kujiona wewe ni wa chuo kikuu na mimi ni wa pr school haijengi hoja zako kuwa na nguvu kuliko za watu wengine hapa.

Kama huna jibu ni sawa tu ila pia itakuwa vizuri ukiweka wazi masilahi yako au kuhusika kwako katika hii issue ya Mtikila. Watu wa Tarime sasa hivi wako chini ya ulinzi wa mamia ya polisi eti kwa vile "wanataka kuleta fujo" huo unafiki wenu mwingine muupeleke huko huko na sio kwenye uchaguzi wa Tarime.
 
Mkuu Kuhani,

Hili nafikiri ni suala linaloanza kujitokeza hivi sasa ambalo linatufanya wengine tuanze kukagua sana mienendo ya Dr. Slaa et al.

Mimi bado ninajiuliza ni kwa nini wapiganaji kama Dr. Slaa na Zitto hawakuona hata 1% ya aliyokuwa anapigania marehemu Wangwe kuwa yana umuhimu? Kwa nini walishiriki kumpiga mawe badala ya kutafuta njia ya ku-accomodate maoni yake?

Hapa ndio ninapobakia na conclusion moja tu, madaraka. Hawa mabwana hakuna atakayewaelewa endapo wataondoka CHADEMA na kuingia CCM. Hivi sasa sio kuwa wanasota ndani ya CHADEMA, wako Ok tu ingawa sio kama akina Lowassa ndani ya CCM.

Kwa hiyo, uchu wao wa madaraka sio serikalini kwa hivi sasa, bali ni ndani ya mtandao wao waliojijengea ambapo Mbowe ndie supreme being ingawa na wao wanaelewa kuwa hana the best qualities za kuongoza chama.

Wote wameamua kufungia macho matumizi mabaya ya pesa ndani ya chama, ukabila, nepotism n.k. ili tu wasiwe against Mbowe. As long as hapigi kelele kama marehemu Wangwe basi yuko Ok. Hiki ndio kigezo changu cha uchu wa madaraka. I might be wrong, but time is a good story teller, and we will have the story well told in a short while.

Ndio maana ni vibaya kuhukumu wakati bado tunasubiri muda ndio utusimulie hadithi.

Kile kisanga cha Wangwe na viongozi wenzake hatujui nani alikuwa mkosi. Mimi nadhani wote CHADEMA na Wangwe walikuwa wanavuruga. Hivi Kubwajinga unaamini kweli Chacha alikuwa sawa wakati wote? Kingine, hujui kama kina Slaa hawakujali au kujaribu "ku accomodate maoni yake." Unless ulikuwemo kwenye vikao vyao humo. Iliundwa mpaka kamati ya uchunguzi kuhusu ukabila. Na kuhusu shutuma za matumizi ya ruzuku, tatizo pale sio Wangwe au Slaa au Mbowe peke yake. Ni li aibu la chama kizima kinaendesha organization bila daftari la ankra. Kungekuwa na daftari tusingeulizana nani kachukua hela. Hawana daftari wale, hilo ndio tatizo.

Kuhusu Slaa kumfagilia Mbowe, nadhani hawezi na hatakiwi leo hii aruke kutaka kupinga u supremacy wa Mwenyekiti wake eti kwa vile sio bora kuliko yeye Slaa. Mbowe ndio amechaguliwa. Na wapinzani wanajua kwamba upheavals ndani ya vyama vyao ndio nyoka anaewaua kila siku. Sio busara leo hii Slaa alianzishe ndani ya chama. Litakuwa valangati kama la Wangwe, na Mrema, na Marando, na Kaburu, au yule wakili the pitiful guy yule aliyerudi CCM. Na hakuna kizuri kitakachopatikana kwa bifu za uongozi ndani ya chama. Internal politics za CHADEMA na dynamics zake nadhani kwa kweli hazitoshi kum judge Katibu Mkuu wao.
 
Naona mkuu umeanza kashfa sasa,

Mambo ya Pr School?
Kuzidiwa hoja? hoja gani uliyonizidi hiyo?
Kubatiza wewe msemaji wa Rev?

Nimekuuliza swali rahisi tu lililohitaji jibu rahisi,
Bado swali langu linasubiri jibu ndugu yangu, wewe ni msemaji wa Mtikila?

Asante.

Poti
Lakini hili swali lako sijui msingi wake ni nini?

Mda utafika tu siku hili swali litakapokugeukia na kukuuliza mfano wewe ni msemaji wa SLAA ,ZITO,MBOWE ama chadema.

Haya mkuu .

mkamap,
Kuelimishana ni jambo jema. Shukrani kwa busara zako.
 
Dharau hazitasimama badala ya jibu la swali langu. Kujiona wewe ni wa chuo kikuu na mimi ni wa pr school haijengi hoja zako kuwa na nguvu kuliko za watu wengine hapa.

Kama huna jibu ni sawa tu ila pia itakuwa vizuri ukiweka wazi masilahi yako au kuhusika kwako katika hii issue ya Mtikila. Watu wa Tarime sasa hivi wako chini ya ulinzi wa mamia ya polisi eti kwa vile "wanataka kuleta fujo" huo unafiki wenu mwingine muupeleke huko huko na sio kwenye uchaguzi wa Tarime.

Magabe Kibiti,
Kama unafanya mambo ya pr-school lazima tuyaite kama yalivyo, ndio maana hata h/poti wako mkamap akaguna juu ya maswali yako. Sijaona humu JF mtu ambaye ni mshabiki wa Mtikila blindly, lakini hatuwezi ku-ignore anayosema kwa vile tu ni kinywa chake kilichobwabwaja.

Tujadili issues kama zinavyokuja na tuachane na ushabiki au maswali yasiyo na msingi. Tukumbuke kuwa historia imeonyesha mara nyingi kuwa Mtakatifu wa leo kesho anaweza akawa fisadi mkubwa sana. Kumbuka Chiluba na Bakili Muluzi pia walikuwa wakombozi.
 
Sidhani kama hili linasimama badala ya jibu la swali langu. Nimeuliza swali langu kujua masilahi na kuhusika kwako kuhusu madai ya Mtikila. Hilo likiwa wazi hapa, itakuwa wazi kwenye nini unaweza kuulizwa na kwa ukubwa gani maandishi yako yachukuliwe hapa. Kwa vile wewe unakuwa na umuhimu na ulazima wa kuuliza maswali ambayo watu wa Tarime tuliyauliza siku kibao zilizopita wakati ambapo Mtikila (na wewe?) akiwa kimya, ni vyema ukawa tayari kupokea maswali ya wana Tarime hapa mtandaoni pia.

Hili swali lilihitaji jibu rahisi tu - ndiyo au hapana. Kwa vile ulivyohangaika sana kulikwepa na kutolea maelezo uamuzi wako wa kutolijibu, inaonesha unafiki na usiri (ajenda mtoto ndani ya ajenda kuu) kwenye maandishi yako hapa.

Kama hauko tayari kujibu maswali toka kwa wachangiaji hapa, unategemea vipi kupata majibu toka kwa wachangiaji hapa au watanzania wengine?

Tujadili issues kama zinavyokuja na tuachane na ushabiki au maswali yasiyo na msingi. Tukumbuke kuwa historia imeonyesha mara nyingi kuwa Mtakatifu wa leo kesho anaweza akawa fisadi mkubwa sana. Kumbuka Chiluba na Bakili Muluzi pia walikuwa wakombozi.

Ohh,

Sasa unataka kujadili issue?

Kwa sababu hii ajenda inahusiana na mbunge wa Tarime, je uko tayari kuwa na issue hizi kwenye mabandiko yako hapa kabla ya kuleta udaku na umbea ambao Mtikila anaamua kuumwaga sasa hivi kwenye vyombo vya habari vya Rostam Azizi?

1. Nani yuko responsible kuzuia makampuni ya madini Tarime yasimwage sumu kwenye vyanzo vya maji ya Tarime?

2. Nani yuko tayari kuhakikisha raia wa Tarime wanapata share yao kamili na wanayostahili toka kwa makampuni ya madini?

3. Nini nafasi ya serikali (na wabunge au bunge) kuhakikishisha kuwa wana Tarime ambao walipisha makampuni ya kigeni kuchimba madini wanaendelea kunufaika na mapato ya madini?

4. Mamia ya polisi walioko Tarime sasa hivi "kuzuia fujo" wameziona leo hii "hizo fujo" za wana Tarime?

5. Ingawa wana Tarime wanajaribu kusahau mazingira tata ya kifo cha mbunge wao ili waendelee kujenga jimbo lao, je serikali sasa itabadili uamuzi wake na kuleta wachunguzi huru kwenye swala hili (kwa kuanzia na ushahidi wa Mtikila)?

Nakupa tu muda wa kutosha kuongelea "issue" za Tarime hapa na sina sababu ya kuandika kabla hujatoa majibu hayo. Nitategemea pia utakapoendelea kuongelea habari za Mtikila, uweke wazi hapa masilahi au nafasi yako kwenye matamko ya Mtikila (ambaye anasubiriwa Tarime ili ayaseme yote anayojua kuhusu kifo cha Wangwe).
 
Kubwajinga

Unampigia mbuzi gita, nimekuuliza toka lini mtu akakata tawi alilokalia?

Hivi hapa tunashindanisha Fikra au tunashindana kusema na kubwabwaja kwa kila tunalodhani ni kweli?
 
Ndio maana ni vibaya kuhukumu wakati bado tunasubiri muda ndio utusimulie hadithi.

Mkuu kuhani,
Sina nia ya kumhukumu mtu, bali kama ilivyosema misahafu, utawajua kwa metendo yao. Kama nilivyoeleza hapo awali kuna dalili kubwa za kuonyesha kuwa kuna mtandao ndani ya CHADEMA ambao lao ni moja. Sasa ni juu ya kila mtu kuwa na conclusion yake ya kitovu cha huo mtandao kama ni madaraka au ni urafiki tu. Mimi napata hisia za uchu wa madaraka.

Kile kisanga cha Wangwe na viongozi wenzake hatujui nani alikuwa mkosi. Mimi nadhani wote CHADEMA na Wangwe walikuwa wanavuruga. Hivi Kubwajinga unaamini kweli Chacha alikuwa sawa wakati wote?

Kama ni kweli wote walikuwa wanavuruga, sasa ilikuwaje akaadhibiwa Wangwe peke yake? Ugomvi ulikuwa kati ya Mbowe na Wangwe, sasa ilikuwaje Dr. Slaa, Zitto n.k., wakaamua kuwa upande mmoja tu kama kweli Wangwe naye alikuwa ana point? Kama tulivyojadili hili hapo awali, mengi ya aliyopigania Wangwe yalikuwa ya kweli lakini hayakukubalika na Mbowe (Mtandao) na hicho ndio chanzo cha Wangwe kuitwa fisadi.

Kingine, hujui kama kina Slaa hawakujali au kujaribu "ku accomodate maoni yake." Unless ulikuwemo kwenye vikao vyao humo. Iliundwa mpaka kamati ya uchunguzi kuhusu ukabila. Na kuhusu shutuma za matumizi ya ruzuku, tatizo pale sio Wangwe au Slaa au Mbowe peke yake. Ni li aibu la chama kizima kinaendesha organization bila daftari la ankra. Kungekuwa na daftari tusingeulizana nani kachukua hela. Hawana daftari wale, hilo ndio tatizo.

Sidhani kama walijaribu ku-accomodate maoni ya Wangwe. Walipojaribu kufanya hivyo kwa kuunda kamati, ripoti yake ilikataliwa na mwenyekiti wa hiyo kamati (Mziray) pamoja na Wangwe wote wakabambikiziwa sifa za kuwa vibaraka wa RA. Mtandao wa CHADEMA ukikukataa tu basi wewe unabatizwa kuwa fisadi.

Kuhusu Slaa kumfagilia Mbowe, nadhani hawezi na hatakiwi leo hii aruke kutaka kupinga u supremacy wa Mwenyekiti wake eti kwa vile sio bora kuliko yeye Slaa. Mbowe ndio amechaguliwa. Na wapinzani wanajua kwamba upheavals ndani ya vyama vyao ndio nyoka anaewaua kila siku. Sio busara leo hii Slaa alianzishe ndani ya chama. Litakuwa valangati kama la Wangwe, na Mrema, na Marando, na Kaburu, au yule wakili the pitiful guy yule aliyerudi CCM. Na hakuna kizuri kitakachopatikana kwa bifu za uongozi ndani ya chama. Internal politics za CHADEMA na dynamics zake nadhani kwa kweli hazitoshi kum judge Katibu Mkuu wao.

Dissent ni sehemu muhimu sana ya Demokrasia, kama alivyofanya bwana mdogo Nape huko UVCCM. Haya ya zidumu fikra za mwenyekiti ndio yaliyotufikisha hapa tulipo. Dr. Slaa nafikiri amejitahidi kuwa mkali dhidi ya CCM lakini amefeli sana ndani ya CHADEMA. Tusimuonee aibu kama tunataka awe kiongozi bora.
 
Nakupa tu muda wa kutosha kuongelea "issue" za Tarime hapa na sina sababu ya kuandika kabla hujatoa majibu hayo. Nitategemea pia utakapoendelea kuongelea habari za Mtikila, uweke wazi hapa masilahi au nafasi yako kwenye matamko ya Mtikila (ambaye anasubiriwa Tarime ili ayaseme yote anayojua kuhusu kifo cha Wangwe).

Mkuu Magabe,
Nafikiri labda umekosea thread maana hapa tulikuwa tunaongelea kifo cha mpiganaji Wangwe kama kilivyoshutumiwa na Mtikila, pamoja na matamko ya Dr. Slaa kuhusiana na hizo shutuma.

Sasa kama wewe lako ni la Tarime, FFU, Polisi n.k., basi inawezekana tuko kwenye frequencies tofauti au threads zimeingiliana.
 
Hivi hapa tunashindanisha Fikra au tunashindana kusema na kubwabwaja kwa kila tunalodhani ni kweli?

Mtazamo wa Masatu inaelekea ni wa kweli kwani Fikra tulizotaka kupata toka kwa Mbowe kupitia kwa MMJJ - KLHNews, zinaelekea kukwama kila wakati. Itabidi tutafiti kuwa pengine ni kweli MMJJ amekalia tawi.
 
Wenyewe wanasema huwezi kuzuia ndege wasiruke juu ya kichwa chako, lakini unaweza kuzuia wasijenge kiota!
 
Wenyewe wanasema huwezi kuzuia ndege wasiruke juu ya kichwa chako, lakini unaweza kuzuia wasijenge kiota!

Mkuu MMJJ, nafikiri hizi ndio Fikra alizokuwa anasubiri kigarama 'tubwabwaje'. Lakini usisahau kutufahamisha progress ya mahojiano ya Mbowe.
 
Mkuu Magabe,
Nafikiri labda umekosea thread maana hapa tulikuwa tunaongelea kifo cha mpiganaji Wangwe kama kilivyoshutumiwa na Mtikila, pamoja na matamko ya Dr. Slaa kuhusiana na hizo shutuma.

Sasa kama wewe lako ni la Tarime, FFU, Polisi n.k., basi inawezekana tuko kwenye frequencies tofauti au threads zimeingiliana.

Ukiongelea kifo cha Wangwe - mbunge wa Tarime, basi utaongelea mambo ya Tarime (jimbo ambalo Wangwe aliliwakilisha bungeni).

Kama kwako mambo ya Tarime sio issue hapa basi sijui issue lazima iwe na nini ili kwako i-qualify kuwa issue.

So far nasubiria jibu la swali langu, wewe ni msemaji wa Mtikila?
 
Mkuu kuhani,
Sina nia ya kumhukumu mtu, bali kama ilivyosema misahafu, utawajua kwa metendo yao. Kama nilivyoeleza hapo awali kuna dalili kubwa za kuonyesha kuwa kuna mtandao ndani ya CHADEMA ambao lao ni moja. Sasa ni juu ya kila mtu kuwa na conclusion yake ya kitovu cha huo mtandao kama ni madaraka au ni urafiki tu. Mimi napata hisia za uchu wa madaraka.

Kama ni kweli wote walikuwa wanavuruga, sasa ilikuwaje akaadhibiwa Wangwe peke yake? Ugomvi ulikuwa kati ya Mbowe na Wangwe, sasa ilikuwaje Dr. Slaa, Zitto n.k., wakaamua kuwa upande mmoja tu kama kweli Wangwe naye alikuwa ana point? Kama tulivyojadili hili hapo awali, mengi ya aliyopigania Wangwe yalikuwa ya kweli lakini hayakukubalika na Mbowe (Mtandao) na hicho ndio chanzo cha Wangwe kuitwa fisadi.

Sidhani kama walijaribu ku-accomodate maoni ya Wangwe. Walipojaribu kufanya hivyo kwa kuunda kamati, ripoti yake ilikataliwa na mwenyekiti wa hiyo kamati (Mziray) pamoja na Wangwe wote wakabambikiziwa sifa za kuwa vibaraka wa RA. Mtandao wa CHADEMA ukikukataa tu basi wewe unabatizwa kuwa fisadi.

Dissent ni sehemu muhimu sana ya Demokrasia, kama alivyofanya bwana mdogo Nape huko UVCCM. Haya ya zidumu fikra za mwenyekiti ndio yaliyotufikisha hapa tulipo. Dr. Slaa nafikiri amejitahidi kuwa mkali dhidi ya CCM lakini amefeli sana ndani ya CHADEMA. Tusimuonee aibu kama tunataka awe kiongozi bora.

Naona kwako hizi ndizo unazoita issue (ambazo sio za Pr school level) kuhusu kifo cha Wangwe na mambo ya jimbo la Tarime. Katika hili ndugu yangu una lako ila limepotea njia maana wana Tarime hawana umbea na udaku kama huu wako.
 
isayamwita!
Wa Tarime nawapenda sana kwa misimamo yao na sio watu wa kudanganywa kwa Tshirt wala kanga/vitenge na hawamung'unyi maneno kama waoga na ndivyo alivyokuwa Marehemu Wangwe (mbunge kupitia Chadema). Sasa Mtikila na wenzake wabwabwaje wakiwa huko Dsm kwa wamesahau yule aliyeleta hayahaya jukwaani majuzi alipatwa na nini? alisahau hata usafiri. Mwageni sera na sio upupu Tarime na watawakaribisha.Acheni njaa za kuendekeza.

Mkuu,

Leo nasema tena, kama kuna kitu CCM watakosea ni pale watakapoendelea kuwazuia chama cha CHADEMA wasihutubie hapa mjini Tarime, kwa kisingizio eti chadema wana fujo, nadhani wanaendelea kujichimbia kabuli bila kujijua, pia ni vema wakajua hakuna kitakachoibiwa,
 
Mura mwita hapo umenikosha,
kama walizoea kuwatisha wengine na kuiba mabox ya kura mura hapo lazima kieleweke! Huwezi tumia vitisho kuminya haki ya walio wengi. wamezoea hao kuwatisha wa karatu wasijitokeze piga kura, yego mura jitokezeni muonyeshe ukomavu wenu. Tunawaombea mura mpate haki yenu na sikuyumbishwa na kutishwiwa nyau!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom