Mkuu Kubwajinga,
Hapo kwenye Slaa kuwa na uchu wa madaraka hapo nina tatizo napo. Sema yooote, mkurupukaji, hata asemwe kala ruzuku, kamuua Wangwe, si Mkatoliki mtakatifu, lolote lile, lakini sio uchu wa madaraka. Madaraka gani hayo Uwaziri, au ubunge, au katibu wa CHADEMA ? Wenye madaraka na uchu wa madaraka hawaji hapa kukosoa watoa madaraka. Na kuvumilia kupigwa madongo. Wako huko wanapiga parapandanda wakisema "Mali za nchi hazilindwi..." lakini "Rais ana nia nzuri...." What crock! Wanajibaraguza na kujishabadua kwa Kikwete. Sio Dr. Slaa.
Kikwete ndio anajibaraguza kwa Slaa. Kama juzi alivyomletea utani utani eti atamkamata akitaka. Ungefikiri Slaa ata mu entertain. No, fikiri tena. Kesho yake Slaa akakataa kuombwa undugu, akasema Spichi ya Rais ni bomu, kachemka, kateka nyara kazi za Bunge kwa kusema hela za Serikali ziende anako taka yeye Kikwete, kajitungia sheria za kusamehe Wezi ambao ilibidi washitakiwe kwa jinai, mengi mengine, so horrific a speech, mpaka leo Slaa anadai nakala yake, ambayo, as far as he knows, imefichwa.
Slaa hata mimi mara nyingi nimemkosoa nilipoona amechemsha, kama mwingine yeyote yule. Lakini jina lake halitatajwa katika orodha ya wenye uchu wa madaraka. Hana hatia hapo.