Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
.taarifa nilizonazo mjj...ni kuwa hii hoja ya wangwe ilikuwa na madai mazito ya ardhi na fidia kwa wana tarime ..kutokana na ardhi yao kuchukuliwa na wawekezaji..ilhali wao wana shida ya ardhi kwa kilimo na uchimbaji mdogo...habari zinazidi kusema kuwa madai ya chacha kwa hawa watu wa madini na serikali yalikuwa yanafikia dola milioni 800...

katika siku za karobuni baada ya serikali kufanikiwa kupata nakala za hiyo hoja[labda kwa kumtumia mallya]...juhudi kubwa zilikuwa ziikifanyika kumbembeleza asilete hoja au apunguze ukali wa hoja...najuwa hakukubali kuitupa hoja yake...ila sijui kama alikubali kupunguza ukali......

NI KWELI INAWEZEKANA KABISA CHADEMA WAKAWA HAWANA COPY YA HIYO HOJA KWANI .....HATA MKUU WA UPINZANI BUNGENI ALISHAWEKA WAZI KUWA CHACHA ALIKUWA AMEANZA TABIA YA KUTOWASHIRIKISHA WAPINZANI WENZAKE KWENYE HOJA ZAKE BUNGENI.....NAKUBALI KUWA UWEZEKANO MKUBWA UPO KWA CCM KUWA NA HIYO HOJA AU SPIKA ....

KILIO CHA SPIKA BUNGENI....kuna wabunge wengi wamepata kufa ..na spika wetu ni jasiri..sijapata kumuona akidondosha japo chozi...zaidi ya kwa wangwe...sijui haya machozi ya spika tunayachambuaje???.....je kuna jambo la hatari ambalo spika angeweza kumuepusha wangwe na akashindwa,,,au kuna nini hapa>..kumbuka alikuwa amemuahidi ruhusa ya kuwasilisha hoja baada ya kutoka dar es salaam..kuzika...spika ndio pekee alijua anasafiri.

KUIBIWA KWA LAPTOP YA MAREHEMU ...kunaweza kuwa kumepoteza nyaraka zote za kuwasilisha hiiyo hoja..kwa nini haijapatikana hadi leo...kama ingekuwa imeibiwa na mwanakijiji ..angeshindwa kuiuza ,itakuwa imechukuliwa na waelewa......

UKIANGALIA YOTE HAPO JUU na kitendo cha KATIBU MKUU WA CCM kutuma nyaraka za mgogoro wa CHADEMA mikoa yote ..masaa machache kabla ya msiba as if walikuwa wakitegemea BIG NEWS..inazidi kukita mawazo yetu kufikiria zaidi..katibu mkuu alijuaje kuwa hoja ya wangwe dhidi ya wana chadema wenzake..ilikuwa inakaribia kuwa mtaji wa kisiasa???

bado tunahitaji kuchunguza...

Mkuu hizo points hapo juu nilizitowa siku ya kwanza kabisa ya mjadala wa kuhusu kifo cha Wangwe.
Licha ya kwamba ni experience theories nyingi...Lakini hii pia niliitowa kama part of speculation...Kuwa naona tatizo lilikuwa kwenye hoja yake aliyotaka kuiwakilisha.
Na hata mkuu MKJJ nilionelea nimpigie simu na kumweleza wazi kuwa tunatakiwa tujiulize kuwa hiyo hoja ni hoja gani hiyo.
Na aliniambia kuwa hakuna mtu anayo labda ni spika Six mwenyewe...Hapo hata mimi nguvu ziliniishia na ndio maana nikatoa ujumbe kuwa ni muhimu kuja pamoja na kujadili namna ya ku move forward kwani mikataba ilishainiwa na hao wawekezaji wana nguvu sana.

NB:Hapo kwenye spika kulia nadhani ni dalili kuwa alihofia maisha yake na labda pia alimkanya asisafiri!

Inaelekea mpango wa kumwua marehemu ulikuwa leaked miongoni mwa ccm na wakawa hawana njia ya kumuokoa tena...Huyo kijana alindwe ndiye shahidi mkuu...Huyo Mallya ndiye Marley mwenyewe...Ukweli auweke wazi...Tunajuwa alitumwa...Lakini kuna wanausalama ambao hawataki na hawajapenda kitendo hicho cha kumuondoa wangwe na ndio maana walilikisha habari kwa baadhi ya wana ccm...Sasa wana ccm wengine wakaamuwa kuchukuwa uamuzi wa ku ipoliticize issue hiyo....The fact kwamba kijana amebaki mzima ndio ukweli kuwa kesi hii haitaweza kufa na kama familia imechukuwa hatuwa hiyo...Basi usishangae MAPINDUZI YAKIANZIA HUKO KWA KINA WANGWE...Maana nahisi harufu ya damu damu tu.

Sijui JK kwanini amefumba macho na pamba masikioni...Yani kama hayupo kabisa.

Sasa atueleze kama ni mapenzi ya Mungu wanausalama kuchemsha kiasi hiki na kutaka kuleta BALAA!

KWASABABU ISSUE ZA USALAMA ZIKIINGIZIWA SIASA NI HATARI SANA...NA NDIO MAANA NAMUUNGA MKONI PROFESSA WANGWE KWA ASILIMIA ZOTE!
 
Safi sana Yebo Yebo...Hapa ndio kwenye mzizi wa FITNA HAPA...Hoja nani anayo kati ya chadema na ccm?
HAPO.....
Ila kumbuka Marehemu chacha Wangwe alikuwa amesimamishwa na CHADEMA ,unadhani alikuwa na ushirikiano wa karibu na viongozi wa juu wa Chama?Nadhani alikuwa na mkakati wa kuwaeleza wananchi wajue na waamue ni nani mchochezi na mwenye kiburi ndani ya CHADEMA.
 
Question of the Year: Nani alimpa Wangwe fedha siku ya safari, fedha ambazo baadaye ilirudishwa ilikotoka? - That is the breaking news!
 
Question of the Year: Nani alimpa Wangwe fedha siku ya safari, fedha ambazo baadaye ilirudishwa ilikotoka? - That is the breaking news!


Taratibu wataumbuka tu. Tunasubiri habari motomoto si unaona hata hao ndugu zake wanaanza kugeuza kauli.
 
Haya mambo kina Professa Wangwe tuwaachie...Hao ni watu smart na wata handle situation inavyotakiwa....Cha muhimu ni yeye awe akizungumza na sisi hapa kwa namna moja ama nyingine ili tupate direction ya namna ya kuendelea na mjadala huu...Nadhani MKJJ amekuwa msaada mkubwa sana kwenye hilo...MKJJ Mungu aendelee kukubariki kwa moyo huo...Na kweli tuombeane Mungu tu kwani mafanikio yangu ni mafaikio yetu...Tunatakiwa tuzingatie positiveness ili kulikomboa Taifa...Kwani amani ya Afrika ni amani ya DUNIA!
 
Chadema yamshtaki Makamba polisi kuhusu waraka wa Wangwe Na Kizitto Noya

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema, kumhoji Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, kuhusu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.


Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema jana kuwa, chama chake kina wasiwasi na jinsi CCM ilivyopata waraka wa marehemu kuhusu mgogoro wake na Chadema na kuanza kuusambaza siku moja kabla ya kifo chake.


Alisema, Makamba anapaswa kuhojiwa ili aeleze uhusiano wake na marehemu ambaye alikuwa Mbunge Chadema, hata akapata nyaraka hizo za siri katika kipindi kifupi kabla ya kifo chake na kuzisambaza.


''Hatutaki kuhitimisha kwa sababu sisi ni wanademokrasia, ila tunataka IGP sambamba na maombi yangu ya awali ya kumhoji Mkurugenzi wa TBC1, amhoji Makamba ili tujue uhusiano wake na marehemu na jinsi alivyopata waraka huo na kuusambaza siku moja kabla ya kifo chake,'' alisema Kabwe na kuongeza:


''Waraka huo ulipotolewa kwa mara ya kwanza na TBC1, mimi (Kabwe) nilikuwa na mashaka na Jumamosi iliyopita, niliwasiliana na IGP na Mkuu wa Usalama wa Taifa kuwataka wamhoji Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya umma. Lakini leo (jana) tumefumbuliwa macho kwamba waraka huo ulianzia CCM na ikabidi niwasiliane naye (IGP), tena ili zoezi hilo limguse pia Makamba,'' alisema.


Alisema Makamba anapaswa kueleza alikopata waraka huo na sababu za kutumwa kwake muda mfupi kabla ya kifo cha marehemu ikiwa ni pamoja na msukumo uliomfanya ausambaze kwa viongozi wa CCM.


Kwa mujibu wa Kabwe, sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1996 inatambua ndugu wa marehemu kuwa wamiliki wa mali na taarifa muhimu zinazomhusu marehemu, hivyo ni ajabu CCM kumiliki waraka huo wakati haina uhusiano wa kindugu wala kiitikadi na marehemu Wangwe.


''Hivi CCM ina uhusiano gani na mbunge wa Chadema au ndugu wa marehemu hata ikahalalisha kumiliki waraka huo na kuusambaza bila woga?'' alihoji Kabwe na kusisitiza kuwa Chadema haijauona waraka huo na wala kuambiwa na ndugu wa marehemu.


Akizungumzia suala hilo, Makamba alikanusha kuhusika na waraka huo na kueleza kuwa, CCM haina haja wala sababu ya kuwa nao na kuusambaza.


Alisema CCM haihusiki na waraka huo na kubainisha kuwa wanaofanya hivyo ni watu wanaomwunga mkono marehemu Wangwe katika migogoro yake na chama chake.


''Mimi sijauona waraka wenyewe na sina taarifa nao, lakini kwa nini CCM iusambaze, ina shida gani na Chadema?'' alihoji na kuongeza:


"Chadema sisi hatuiogopi, tuliishinda Jimbo la Kiteto na tutaishinda mwaka 2010, hatuna haja nayo wala haitusumbui."


Kauli za Makamba na Zitto zimefuatia taarifa kwamba, CCM imekuwa ikisambaza waraka wa marehemu Wangwe wenye kurasa sita unaoelezea jaribio la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kutaka kumvua wadhifa wake na uanachama.


Waraka huo unadaiwa kusambazwa kwa viongozi wa CCM kwa lengo la kuwafahamisha mgogoro wa Chadema ambao umekuwa ukihusishwa na chanzo cha kifo cha mbunge huyo.


Ukurasa wa nne wa nakala ya waraka huo unaonyesha kwamba, kwa mara ya kwanza ulitumwa kutoka Dodoma Julai 27 mwaka huu majira ya saa 9:42 alasiri toka namba (026) 2322965 ambayo imeonyesha kusajili kwa jina la ‘KATIBU MKUU CCM DOM’ tarehe ambayo ni siku moja kabla ya kifo cha Wangwe.


Uchunguzi umebaini kuwa waraka huo ulianza kusambazwa kutoka Dar es Salaam kwa namba za faksi 2667457 iliyotanguliwa na kodi namba ya mkoa (022) ikimaanisha kutumwa kutoka Dar es Salaam Julai 31, mwaka huu saa 5:50 asubuhi na mmiliki wa namba hiyo akitambuliwa kama SIGMA ICT.


Waraka huo, umetumwa kwa baadhi ya viongozi wa CCM mikoani, wakiwemo Makatibu wa Mikoa na Wilaya na wengine ukiwa ni mahususi kwa ajili ya kuwaonyesha kwa kina mgogoro wa Chadema ulivyo.


''Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa 2005, Mbowe alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama dola za Kimarekani 181,949.00, sawa na Sh 218,338,546 na mpaka sasa chama kimemlipa Sh175 milioni.


''Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha wilayani na makao makuu, niliamua kumshauri Mbowe asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku, kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa pesa za ruzuku kwa vyama vya siasa kutoka serikali.


''Mbowe alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo, basi atuthibitishie pesa hizo anazodai alikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya Chadema kupitia hundi ipi na lini?'' ilieleza sehemu ya waraka huo.

Source: Mwananchi.

Maoni yangu: Inaonekana SISIEMU ilikuwa imeshajua nini kilikuwa kinafuata kabla ya kutoa/ kusambaza huo waraka. Nafikiri Makamba awe part ya mashahidi katika kesi ya Mallya.
 
Question of the Year: Nani alimpa Wangwe fedha siku ya safari, fedha ambazo baadaye ilirudishwa ilikotoka? - That is the breaking news!

Inaelekea pesa alipewa kijana azipeleke na Wangwe alizikataa na ndio kijana akapinduwa gari...Na labda Wangwe alitaka achukuwe pesa na bado afikishe hoja...Na inaonyesha alitaka kufanya vyote...Kwani inaelekea huko Dar alikuwa na miadi ya kukutana kuzungumzia namna ya kuongezewa dau ama something that bado hatujajuwa...Kwani ni muhimu pia kujuwa alikuwa akutane na nani huko Dar..Na ndio maana kijana akapiga simu kusema ni ajali...Akimaanisha pesa zimekataliwa ama jamaa bado ana msimamo wa kufikisha hoja yake kama mtoto wa marehemu alipoweka wazi pamoja na spika six...Pesa yule mtu wa tatu aliyetowa order zitolewe mfukoni alikuwa kwenye gari nyingine na hakutaka kumgusa marehemu labda kwa kuhofia fingerprints nk.
Hilo linawekana kabisa...Haya...Jibu la aliyetowa pesa ndio litamaliza machezo hapa.
 
Question of the Year: Nani alimpa Wangwe fedha siku ya safari, fedha ambazo baadaye ilirudishwa ilikotoka? - That is the breaking news!

Mkjj, hiyo ni njemba ya CCM. Baada ya Makamba kununua siri za CHADEMA kwa bei mbaya inaelekea njemba hiyo labda ndiyo ilikabidhi bulungutu hilo hivyo ikashuhudia bulungutu limewekwa maeneo yapi. Alichokifanya baada ya ajali tu ni kuomba bulungutu litolewe katika mfuko wa koti na akatimka haraka sana. Makamba atakuwa anamjua huyu ni nani maana inaelekea yeye ndiye aliyemkabidhi pesa hizo za manunuzi. Duh! Kweli bongo kuna mafioso!!
 
Mkjj, hiyo ni njemba ya CCM. Baada ya Makamba kununua siri za CHADEMA kwa bei mbaya inaelekea njemba hiyo labda ndiyo ilikabidhi bulungutu hilo hivyo ikashuhudia bulungutu limewekwa maeneo yapi. Alichokifanya baada ya ajali tu ni kuomba bulungutu litolewe katika mfuko wa koti na akatimka haraka sana. Makamba atakuwa anamjua huyu ni nani maana inaelekea yeye ndiye aliyemkabidhi pesa hizo za manunuzi. Duh! Kweli bongo kuna mafioso!!

Nakumbuka sana alishasema NEC INAONGOZA BUNGE!
 
mimi nafikiri,watu wa kununuliwa walikuwa ni wale wa kamati ya mwakyembe.hakuna hoja ya wapinzani ambayo inaweza kuwasumbua ccm.
hapa tutafute mchawi mwingine tu.
leo mkjj umenikumbusha mbali sana kwenye huo mdundo wa moris nyanyusa sijausikia yapa miaka mingi sana.
 
Inaelekea pesa alipewa kijana azipeleke na Wangwe alizikataa na ndio kijana akapinduwa gari...Na labda Wangwe alitaka achukuwe pesa na bado afikishe hoja...Na inaonyesha alitaka kufanya vyote...Na ndio maana kijana akapiga simu kusema ni ajali...Akimaanisha pesa zimekataliwa ama jamaa bado ana msimamo wa kufikisha hoja yake kama mtoto wa marehemu alipoweka wazi...Pesa yule mtu wa tatu aliyetowa order zitolewe mfukoni alikuwa kwenye gari nyingine na hakutaka kumgusa marehemu labda kwa kuhofia fingerprints nk.
Hilo linawekana kabisa...Haya...Jibu la aliyetowa pesa ndio litamaliza machezo hapa.

naamini kuwa aliyempa/waliompa fedha ndio wanahusika na kifo hicho na ni hao ndio walizilitrieve na ni wao pekee wana access ya laptop na nyaraka zote za wakati wa safari. Kuna uwezekano kuwa Wangwe hakuzikataa, lakini hakukubali masharti yake.

Swali: Marehemu Wangwe alikutwa na kiasi gani cha fedha mwilini? I'm really interested. I'll bet you that they never found any money on him.
 
Kwahiyo inawezekana kabisa ugomvi kati ya Wangwe na Mbowe ni kuhusu UKALI WA HOJA.....Na pia tunasubiria kusikia kutoka kwa six kwani hiyo hoja imegeuzwa na kufanywa kuwa ni mgogoro wa chdema...Sidhani kama marehemu alitaka kulifikisha suala la mgogoro wa chama bungeni.
Spika Six awe makini sana na anahitaji maombi ya hali yajuu!
Huyo mtu aliyesema Bunge linaongozwa na chama ndiye aliyeibadili hiyo hoja na kuisambaza kwa kutumia cheo cha ukatibu mkuu..Sasa labda Six ndiye wanayembana ili na yeye akubali kuwa hoja ilikuwa ni waraka wa ugomvi.
Duh...Tunakoelekea sijuwi.
 
Mkiwasoma hawa vizuri yani wanaobishana baada ya uchungunzi kufanyika utajua tu wanataka nini ktk siasa zao ? Usipoamini vipimo vya kitaalumu asilimia kubwa unaamini ushirikina.Na ukiamini ushirikina hii inamaana kamwe hupiganii haki.

Nakama hawaamini ushirikana basi watakua wanalazimisha kutafuta umaarufu kwa vile unahofia kupakwa matope na mtu wanamna hii si mkombozi wa kweli.

Mfano kama YESU naye zile shutuma angepoteza mda mwingi kujisafisha angepoteza uelekeo na kuonekana siye yule .LAKINI majibu yake yaliwashitua nakuona ndiye mfano WEWE WASEMA,MIMI NDIYE,KAMWAMBIENI YOHANA MLICHOONA,MTU HAISHI KWA MKATE TU,
 
Mkiongea na Google kwa kushirikiana na controllers wa USA (au wanaomiliki satellite zinazo-monitor haka kadunia ketu) wanaweza kuwapatieni satellite pictures za ule usiku kwenye tukio mtawafunga goli safi sana maana hizo zipo na walio karibu wanaweza kuzipata ingawa inaweza kuchukua muda ili kujua kama ilikuwa ni ajali au la. Lakini mnavyojua tena Kichaka ........Just thinking....
 
It seems kuwa CCM wana nyaraka za Wangwe.

Off course, si nilisema juzi kuwa anayo Spika tayari, ila alikuwa anamzuga zuga kumpa nafasi ya kuisema bungeni, ndio maana Spika ndiye the only person aliyejua kuhusu safari ya Wangwe, kwenda Dar, kwa sababu alikwenda kumuaga akiwa na nia ya kufuatilia mawasilisho ya hii hoja yake,

So far mstari wa uchunguzi wa kifo cha Wangwe bado upo huko Barrick, sio siri tena!
 
Kwahiyo inawezekana kabisa ugomvi kati ya Wangwe na Mbowe ni kuhusu UKALI WA HOJA.....Na pia tunasubiria kusikia kutoka kwa six kwani hiyo hoja imegeuzwa na kufanywa kuwa ni mgogoro wa chadema...Sidhani kama marehemu alitaka kulifikisha suala la mgogoro wa chama bungeni.

Spika Six awe makini sana na anahitaji maombi ya hali yajuu!
Huyo mtu aliyesema Bunge linaongozwa na chama ndiye aliyeibadili hiyo hoja na kuisambaza kwa kutumia cheo cha ukatibu mkuu..Sasa labda Six ndiye wanayembana ili na yeye akubali kuwa hoja ilikuwa ni waraka wa ugomvi.
Duh...Tunakoelekea sijuwi.
 
mwanakijiji naomba kama kuna uwezekano ufanye mahojiano ya live na pro. Wangwe na yarushwe moja kwa moja hewani ili tuweze kuona ni kwa haraka kiasi tunahitaji kuomba msaada toka Scotland Yard.
 
MKJJ,

How much are we talking about here to cause a us a concern?

MKJJ,

How Much time does it takes for a man to speak what he knows it is true?I think it is a time to say what you have and stop to speculate..

I wanna know all about it.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom